Punguzo la PAYE kwa asilimia 1 ni dhihaka kwa wafanyakazi!

Punguzo la PAYE kwa asilimia 1 ni dhihaka kwa wafanyakazi!

Kodi ni kwa ajili ya wanyonge tu? raisi, makamu wa raisi, waziri mkuu, mawaziri, wabunge na wakuu wa Mikoa na wilaya hawakatwi payee! Hii ni haki? kweli inauma sana sana jamani.:frusty:
 
Kulipa kodi ni wajibu wa kila raia bila kujali ana wadhifa gani ktk serikali. Mbona Marekani na nchi zingine hadi rais analipa kodi? Tatizo la Tz walipa kodi ni sehemu ndogo sana ya wananchi wanaoingiza kipato matokeo yake serikali inawang'ang'ania hao wachache kugharamia matumizi yote ya serikali. Kuna haja ya kupanua aina ya walipa kodi/vipato vinavyopaswa kulipa kodi. Kila anayeingiza kipato na alipe kodi. Hii itapunguza mzigo wa kodi kwa walipaji wa sasa kwani kila mmoja atalipa kidogo bila maumivu makubwa lakini zitapatikana hela za kutosha kuendesha serikali. Kodi anayolipa mfanyakazi iangaliwe upya pia, either ipunguzwe au alipe baada ya kutoa gharama za msingi za maisha yake na familia kwa mwezi( Inaweza tafutwa standard ya matumizi ya mtu na familia yake- 4 kids kwa mwezi). Mfano-hela ya chakula, matibabu, kodi ya nyumba, usafiri etc. Mbona wafanyabiashara hulipa kodi out of their profit ili asilipe kodi toka hela ya mtaji? Kwanini mfanyakazi asitoe kwanza matumizi ya mwezi ili kinachobaki ndicho kitozwe kodi?
 
Mkuu serikali kandamiz ndivyo zilivyo , bado wameona kodi hizo bado hazitoshi wameamua kufuta increment ya mwaka katika mishahara ambayo ipo kisheria, mfano siku hizi watu wote wa tgs D wameachwa D1 hakuna kwenda D2 hatA kwa miaka zaidi ya 5. huu ni ukandamizaji wa waziwazi

Sikuhizi kuanzia lini!na upo idara gani?
 
Hesabu za haraka haraka, kama ongezeko hilo la mshahara limesababisha ongezeko hilo la kodi basi mshahara wako wa mwanzo ulikuwa ama ni TZS 800,000 kamili au zaidi ya apo.

Kumbuka kiwango cha chini elekezi kutoka serikalini ni TZS 170,000.
Unapaswa kumshukuru Mungu kwa kipato hiki badala ya kuanza kulalamika, kuna watanzania mamilioni ambao hawapati hata shilingi kwa mwezi, si wafanyakazi, si wakulima, si wajasiriamali, si lolote, wako kama vile wanasindikiza wenzao (katika ulimwengu huu wa fedha na tamaa).

Nachokushauri, kwa ongezeko hili, na Mabenki outomatically yameongeza kiwango yaliyotayari kukukopesha, usiwasikilize, hao ni wabaya kuliko hata serikali.usiingie tamaa ya kufanya biashara kwa sababu unaweza kukopa pesa nyingi, wala usiwatenge wenzako uliowapita kipato na usijiunge na wale uliowafikia kipato katika matumizi.

Ongeza bidii kazini, inshalah, labda Mshahara utaongezeka tena muda si mrefu.

Kwani mshahara ni nini? Mbona una mwambia amshukuru Mungu? Yes anamshukuru lakini hayo ni malipo halali kwa kazi anayofanya pengine kazi anayofanya ni kubwa zaidi ya malipo sasa hapa amshukuru Mungu kwakutopewa haki yake au achukue hatua ya kumponda huyo shetani anayeiba haki yake?

Haya mambo ya kuwafanya watu kutokuwajibika kwa kichaka cha Mungu ni baya mno kwa attitude za raia.....

Kila mtu afanye kazi na akishafanya ni wajibu wa serikali toa malipo sahihi kwa kila mfanya kazi pengine niwajibu wa serikali pia kulipa hata wasiofanya kazi kama haijawapatia kazi ya kufanya. Ni wajibu wa serikali ku coordinate raia kufanya kazi kama kuna failure in coordination aka bad governance ndiyo tunaishia kudanganya watu kumshukuru Mungu kwa kunyonywa..... Ushindwe kabisa katikajinavla Yesu aliye hai!
 
Naunga mkono hoja huu wizi wa serikali. Mfano anayepokea zaidi ya laki saba analipa kodi asilimia 30 ya fedha inayozidi. Hatukatai kulipa kodi lakini basi kuwe na usawa. Wafanyabiashara na viongozi wa juu serikalini pia walipe kodi. Sio wananyonywa tu wanaofanya sekta binafsi.

Huu ujambazi kwenye mishahara yetu nimeuchoka!
 
kwa nini wanifanyie dhihaka?
1%? Kweli?
Watoze PAYE sawa sikatai, lakini mbona sioni dhati yoyote ya kupunguza mfumuko wa bei ili niyamudu maishi? Unadhani mfumuko wa bei ungedhibiwa ningelalamika kuwa PAYE ipunguzwe?
Consigliere, si hiyo tu, Kwa nini mimi nilipe kodi na wengine hawalipi na wao wana kipato kikubwa kuliko mimi?
Kwa nini kikwete na Pinda hawalipi kodi??

Kwa nini wabunge hawalipi kodi kwenye gratuity yao wanayopata kila baada ya bunge kuvunjwa ?

Wao hawalipi kodi lakini wanaona shida kutupunguzia mzigo wa kodi..... !!
 
Kwenye uchaguzi 2015 lazima mgombea urais aseme wazi kwamba atapunguza paye kutoka 14% hadi 3% mbona migodi wanachajiwa 3% tena kwenye net profit iweje sie tunalambwa kwenye gross? Hilo neno paye lifute iwe tax tu.

Nakuunga mkono aise! Wafanyakazi kwanza wana determine fate ya mwanasiasa yeyote maana ndiyo bread earners nchi hii! Tumenyonywa vyakutosha this time mm nitaongoza campaign kwenye kada ya wenye ajira rasmi waache kututania kabisa ss ndiyo tubebe garama za masikini wote huko vijijini then na serikali tuibebe? Enough is enough!
 
Punguzo la 1% (kutoka 15% hadi 14%) kwenye kodi ya mishahara (PAYE) ni dhihaka kwa wafanyakazi wa Tanzania kwani gharama za maisha ziko juu sana kufuatia mfumuko mkubwa wa bei. Ifike wakati sasa serikali iwaonee huruma wafanyakazi kwa kuwapunguzia mzigo wa kodi badala ya kufawafanyia mzaha kama huu. Wafanyabiashara wakubwa na mafisadi kibao wanasamehewa kodi lakini mfanyakazi masikini anazidi kukandamizwa tu kila kukicha. Hii haikubaliki hata kidogo.

Kwa jinsi serikali ilipokuwa inatamba kwa mbwembwe kwamba itapunguza kodi ya mishahra, sikutegemea kwamba mwisho wa siku wangekuja kupunguza kiasi kidogo kama hiki cha kodi. Ni aibu kwa kweli. Wafanayakazi mnanapaswa kutambua kwamba seriklali ya CCM haina nia njema katika kuwapunguzia ukali wa maisha, hivyo basi fanyeni uamuzi sahihi hapo mwaka 2015 ili kurejesha nidhamu kwa serikali hii isiyokuwa na mwelekeo.

Kana kwamba hili halitoshi, bado wafanyakazi hao hao watakamuliwa Tsh 2500 kama kodi ya kumiliki simu kwa kila mwezi! Wananchi mmnatakiwa kuacha uzezeta—amkeni tukawafundishe adabu hawa mafisadi mwaka 2015. Saa ya ukombozi ni sasa. Bila kufanya hivyo, tutaendelea kukandamizwa hadi mwisho wa dahari.

Tafakari, chukua hatua!

-------
Mwananchi (Juni 14)
kama kweli wamepunguza asilimia 1 wafanyakazi kwa pamoja kuna haja ya kuitoa serikali hii madarakani kwa kuinyima kura ccm
 
Kwani mshahara ni nini? Mbona una mwambia amshukuru Mungu? Yes anamshukuru lakini hayo ni malipo halali kwa kazi anayofanya pengine kazi anayofanya ni kubwa zaidi ya malipo sasa hapa amshukuru Mungu kwakutopewa haki yake au achukue hatua ya kumponda huyo shetani anayeiba haki yake?

Haya mambo ya kuwafanya watu kutokuwajibika kwa kichaka cha Mungu ni baya mno kwa attitude za raia.....

Kila mtu afanye kazi na akishafanya ni wajibu wa serikali toa malipo sahihi kwa kila mfanya kazi pengine niwajibu wa serikali pia kulipa hata wasiofanya kazi kama haijawapatia kazi ya kufanya. Ni wajibu wa serikali ku coordinate raia kufanya kazi kama kuna failure in coordination aka bad governance ndiyo tunaishia kudanganya watu kumshukuru Mungu kwa kunyonywa..... Ushindwe kabisa katikajinavla Yesu aliye hai!

AME twende taratibu. Unataka kuniambia katika nchi yetu, na karibia zote katika dunia ya tatu, swala la kupata fursa ya kufanya kazi sio la kumshukuru Mungu, achilia mbali mshahara wote huo??
 
Hili janga la kodi kandamizi litapata ufumbuzi pale tu mishahara minono ya wanasiasa itakapoanza kukatwa kodi. Vinginevyo...tutakaa sana. Hawa walafi hawawezi kumpunguzia mfanyakazi kodi ya mshahara kwa kuwa hawajui uchungu wake. Wataonja uchungu wa kodi mara watakapoanza kukatwa kodi. Ni bahati mbaya kwamba hili wazo halimo kwenye katiba mpya.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
AME twende taratibu. Unataka kuniambia katika nchi yetu, na karibia zote katika dunia ya tatu, swala la kupata fursa ya kufanya kazi sio la kumshukuru Mungu, achilia mbali mshahara wote huo??

Haitakiwi kuwa hivi kama kwa wengine si hivyo kwanini na ss tusiikatae hii hali ya kidunia ya tatu? Mbona korea wametoka, Singapore, Malasiya na kwingine?

Ss tunaanza lini kuondokana na haya mawazo? Swala la ajira ni la serikali ikikubali jukumu lake basi hiyo pekee ni hatua kubwa kuliko kuendelea kukusanya kodi huku wakiacha kuturatibisha kwenye kazi na malipo!

Hata kama uchumi ni ndogo katika udogo huo kila mtu apate kidogo kidogo na kila mtu apatiwe kazi yakufanya!

Ili nisiwe mlalamikaji bali mchangiaji chanya basi wizara ta TAMISEMI, wizara ya viwanda na buashara na hii ya Uwezeshaji hazija onyesha ni vipi kila raia ame wezeshwa!

Naiona dhamura ya Rais katika kutaka kuwasaidia raia lakini patronage inamfanya asifikie malengo yake. Mtu kama ni rafiki yako akashindwa kukusaidia kutimiza wajibu wako kwa raia ww ndiye mkosaji maana uwezo wa kuchagua na kuondoa umo mabegani mwako. Kama unalalamika pamoja ba walio kupa huo uwezo na mamlaja ya kitendaji basi ww ni msaliti na dhamura hiyo njema inaonekana kuwa si njema tena!

Hajachelewa, akubali kuondoa patronage na atimize wajibu wake!
 
PAYE ni kodi wanayokatwa wafanyakazi na Muajiriwa wao kutoka kwenye kipato walichokubariana katika Mkataba wa Kazi, sasa wabunge wanamkataba na nani? Bunge?Serikali? Mkataba wa kufanya nini?

Kama hivi ndivyo sasa kwanini wanalipwa mshahara na kiinua mgongo? Si wapewe tu posho ya vikao na mafuta ya kusafiria basi?

Tatizo la hao wabunge ni wao kujigeuza taasisi badala ya wao kuwa ndani ya taasisi. Serikali nayo kwakua haiwajibiki inaogopa kugusa maslahi ya wabunge! Hii yote inapelekea sote tuishi kwakuviziana na kuongeza uncertainty katika maisha.

We need to get out of this kwakukubali ushauri wa Obama kwamba we need strong institutions and not strong people. Njia pekee ni kuinstitutionalize things na individual walipwe kila mtu kwa stahiki yake kiasi kwamba kuwepo kwake au kutokwepo kusibadili sana maisha kwa ujumla la kila raia.

Ilivyo ni kuwa kuna individual wengi sana wana operate privately na hii inaongeza transaction costs kwakukiasi kikubwa.... Maana hao wamejigeuza taasisi isiyo rasmi!
 
Haitakiwi kuwa hivi kama kwa wengine si hivyo kwanini na ss tusiikatae hii hali ya kidunia ya tatu? Mbona korea wametoka, Singapore, Malasiya na kwingine?

Ss tunaanza lini kuondokana na haya mawazo? Swala la ajira ni la serikali ikikubali jukumu lake basi hiyo pekee ni hatua kubwa kuliko kuendelea kukusanya kodi huku wakiacha kuturatibisha kwenye kazi na malipo!

Hata kama uchumi ni ndogo katika udogo huo kila mtu apate kidogo kidogo na kila mtu apatiwe kazi yakufanya!

Ili nisiwe mlalamikaji bali mchangiaji chanya basi wizara ta TAMISEMI, wizara ya viwanda na buashara na hii ya Uwezeshaji hazija onyesha ni vipi kila raia ame wezeshwa!

Naiona dhamura ya Rais katika kutaka kuwasaidia raia lakini patronage inamfanya asifikie malengo yake. Mtu kama ni rafiki yako akashindwa kukusaidia kutimiza wajibu wako kwa raia ww ndiye mkosaji maana uwezo wa kuchagua na kuondoa umo mabegani mwako. Kama unalalamika pamoja ba walio kupa huo uwezo na mamlaja ya kitendaji basi ww ni msaliti na dhamura hiyo njema inaonekana kuwa si njema tena!

Hajachelewa, akubali kuondoa patronage na atimize wajibu wake!

Sidhani kama kikwete ana dhamira ya kuliweka swala hili sawa, na kama anayo basi hana maarifa ya kufanikisha, na nina shauri tuache kumjadiri huyu mtu, huyu ni tatizo kubwa sana kwa sasa katika taifa letu zaidi ya ccm yake.
 
Katika bajeti ya mwaka jana (2013/2014) serikali ilipunguza kodi ya PAYE kwa 1%, kiwango ambacho hakikukidhi haja, na mwaka huu tena wamerudia ujinga ule ule wa kupunguza kwa 1%!!! Na kibaya zaidi, Rais aliahidi kuongeza mishahara kumbe ilikuwa danganya toto. Wafanyakazi wa umma mnatakiwa kuwa makini na serikali yenu ‘sikivu'. Ni lini mtaamka kutoka usingizini na kukataa kutumikishwa na seikali kama punda huku mishahara yenu ikiwa haikidhi? Kada ya wafanyakazi inayonyonyeka zaidi ni WALIMU lakini, kwa bahati mbaya sana, hao hao walimu ndio wanaotumiwa na CCM kuiba kura na hatimaye kuirejesha madarakani. Acheni kulalamika, tafuteni njia mbadala ya kujiongezea vipato.

SULUHISHO
1. Wafanyakai wa umma, hasa sisi walimu, tunatakiwa tusitishe kazi. Cha kufanya ni kuwahi asubuhi kazini, ukifika unasaini kwenye kitabu cha mahudhurio na kuondoka mashuleni. Kama kuna shule za binafsi karibu na maeneo yenu ya kazi, jisajilini kufundisha huko. Kwa wale wa vijijini tafuteni mashamba ya kulima na waliopo mjini fungueni magenge au biashara ya naina yoyote ya kuwaingizia vipato. Muda wa kutumikishwa kama punda huku mafisadi pekee wakifaidi keki ya taifa, umekwisha.

2. Jiandikisheni kupiga kura na jitokezeni siku ya kupiga kura mkiwa na ndugu zenu, lengo likiwa moja tu-kuiondoa serikali hii dhalimu madarakani. Badala ya kushirikiana na CCM kuiba kura, shirikianeni na wananchi kuiba kura za CCM na kuzihamishia UKAWA ili kuwang'oa hawa mchwa madarakani katika uchaguzi wa mwaka ujao (2015). Bila kujitetea kwa namna hii tutaendelea kuumia mpaka Yesu atakaporudi.
 
tunasema toka kwa sababu uneshindwa kazi bajeti inesomwa leo hakuna jipya ujinga ule ule nakato ya kodi kwa mtumishi wa umma bado mzigo

wanasiasa wamegeuza mtumishi wa umma zezeta unamwambia umeongezewa mshahara pasipo kumtajia kuwango kipi

walimu wetu wameendelewa dharaulika baada waongezewe posho serikali inaongeza majengo na madawati si ujinfa huu hayo majengo na vifaaa vya kufundishia atavitumia nani ikiwa mwalimu hana moyo wakufundisha

tunasema mgaya toka kwa sababu matatizo haya unayajua na umekuwa unakaaa vikao na serikali sasa umeshindwa toka huna msaada kwa watumishi wa umma.
 
Atatokaje wakati ni mchumia tumbo no. 1 Anarizika na kupeana mikono na Jk siku ya mai day ya wanaoigiza kufanya kazi.
 
tunasema toka kwa sababu uneshindwa kazi bajeti inesomwa leo hakuna jipya ujinga ule ule nakato ya kodi kwa mtumishi wa umma bado mzigo

wanasiasa wamegeuza mtumishi wa umma zezeta unamwambia umeongezewa mshahara pasipo kumtajia kuwango kipi

walimu wetu wameendelewa dharaulika baada waongezewe posho serikali inaongeza majengo na madawati si ujinfa huu hayo majengo na vifaaa vya kufundishia atavitumia nani ikiwa mwalimu hana moyo wakufundisha

tunasema mgaya toka kwa sababu matatizo haya unayajua na umekuwa unakaaa vikao na serikali sasa umeshindwa toka huna msaada kwa watumishi wa umma.
akiitisha mgomo utam-support au ndo ule woga wa mtanzania unaoambatana na "fikra za hayanihusu!" Mgomo wa Barrick Gold ulitufundisha hulka ya Mtanzania kwamba ni mwoga! Pia mgomo wa madaktari Muhimbili, Mwambepande tu iliwanyamazisha! Usiwatupie lawama viongozi tu, jiulize kama upo tayari kwa mkong'oto kutokaa wenye nchi?
 
Back
Top Bottom