Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
Rais wa Urusi, Vladmir Putin ameahidi kuzisaidia Nchi Washirika wake Barani Afrika katika Sekta mbalimbali za kuleta maendeleo na amesema ataisaidia pia Afrika kupambana na ugaidi.
Rais Putin ameahidi kutoa msaada kamili kwa Bara la Afrika ahadi ambayo ameitoa leo Jumapili katika mkutano kati ya Maafisa wa Bara la Afrika na Urusi huko Sochi, Kusini Magharibi mwa Nchi hiyo.
Mtandao wa DW Kiswahili umeripoti kuwa katika hotuba ya Putin iliyotolewa na Waziri wake wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov mbele ya Mawaziri ya Mambo ya Nje wa Mataifa mengine pamoja na Maafisa wengine wa ngazi za juu, Kiongozi huyo amesema Nchi yake itaendelea kuzisaidia kikamilifu Nchi Washirika wake Afrika katika Sekta mbalimbali.
Amesema Urusi inaweza kuyasaidia Mataifa hayo ya Afrika katika maendeleo endelevu, kupambana na ugaidi na itikadi kali pamoja na kupambana na majanga, matatizo ya chakula na athari zizanosababishwa na majanga ya kiasili.
Mkutano huu pia ni fursa nyingine kwa Urusi kutangaza malengo yake ya kutaka kuona ulimwengu usioendeshwa na Taifa au upande mmoja tu wa Dinia, ikiwa ni baada ya Taifa hilo kuaandaa mkutano wa kilele wa mataifa yanayokuwa kiuchumi ya BRICS, Urusi inataka kuuonesha Ulimwengu wa Nchi za Magharibi kwamba vikwazo vyake vilivyolenga kuifanya itengwe kutokana na kuivamia Ukraine vimeshindwa kufanya kazi.
SASA MAGAIDI NA IMANI YAO YAKAE CHONJO. PUTIN HANA MASIKHARA LINAPOKUJA SUALA LA MAGAIDI.
Ritz Webabu Adiosamigo FaizaFoxy Tuendeleeni kunywa mtori nyama tutazikuta chini.
#MillardAyoUPDATES