Putin amechoka na Vita na Ukraine. Apongeza wazo la kumaliza vita yake na Ukraine

Wewe ni mpuuzi, nimekwmbia nitajie hizo nchi 37 zinazoisaidia Ukraine, kwahyo hadi Eritrea inaisaidia Ukraine sio?
 
Nilichogundua humu, wengi wanaoegemea upande wa nchi za Magharibi ni weupe kichwani na hoja za maana hawana zaidi ya matusi na kuzungumzia udini...

Kiukweli ukisoma maoni kuhusu wadau wanaoegemea upande wa Russia wanatoa hoja za kueleweka na wanaonekana wana uelewa sana katika uchambuzi wa siasa za kimataifa.

Mtu hajui kitu anakomaa kubisha tu...
 
Wewe ni mpuuzi, nimekwmbia nitajie hizo nchi 37 zinazoisaidia Ukraine, kwahyo hadi Eritrea inaisaidia Ukraine sio?
We nae utakuwa umelewa....
Nani alikuambia Ukraine Ukraine anasaidiwa na nchi 37?

Nilisema Russia anapambana na nchi 32 za NATO, au huelewi NATO ni umoja wa nchi 32?

Rudi kasome tena, nlikuambia Iraq ilivamiwa na nchi zingine 37 baada ya USA, UK, Poland na Australia, halafu zikafuatia nchi zingine tena hadi zikatimia nchi 48 jumla...

Sasa usikimbie swali, narudia tena, je USA alizidiwa na Iraq hadi hizo nchi zingine kuingia na kutuma vikosi Iraq?
 
Yeah anasasitiza Vita iishe kwa sababu ashapata advantage tayari. Anashikiria 27% ya eneo la Ukrain. Eneo hili pia ni eneo lenye rasilimali nyingi mno. So, Jamaa ana akili kubwa anajifanya neutral lkn mkienda mezani mashart yake yako wazi.
Mimi nashangaa wanaodhani Russia amekuwa mwoga kwa kuitaka amani na Ukreni. Lakini wanasahau kwamba huo ndio ulikuwa msimamo wake hata kabla hawajaivamia Ukrene.

Isingekuwa Boris Johnson kumjaza upepo Zelensky na kumwahidi ushindi wa mapema kwa njia ya bao la mkono, leo hii dunia haingekuwa na adha kubwa kiasi hicho kutokana na athari za vita hivi.

Maelfu ya watu wasio na hatia wamekufa. Tusisahau hilo kamwe.
 
Huo ushahidi wa nchi 32 ndio tunautaka, usijifiche kwenye kichaka cha iraq
 
Hivi wakuu mnamuongelea putini yule jamaa alikuwaga namba sita ya Simba inacheza rafu sana Ile jamaa, sadio kanoute, wakuu nawaelewa sana
 
Yericko Nyerere anasemaje?
 
Russia hata akisimama vita leo, tayari kafanikiwa mission yake...
Kachukua sehemu kubwa ya Ukraine, Zelensky alisema moja ya mbinu ya ushindi wanayotaka kuitumia dhidi ya Russia ni pamoja na kuiunganisha Ukraine na NATO...

Sasa Russia hizo sio shida zake tena kwa sasa as kong as tayari kachukua ardhi ya kutosha uchaguzi utakuwa juu ya Ukraine either akajiunge NATO au arudishe ardhi yake iliyomegwa.

Ukraine ninaamini ataomba kipande chabardhi yake, hii vita mwisho unajulikana utakuwa Russia kuondoka na kipande cha Ukraine...


Sasa nashangaa humu nyumbu wanavyopiga kelele kusema Putin kashindwa vita ..

Na hilo jeshi la Korea linaloingia ni kwenda kufanya usafi na kufagia takataka zote kuelekea uchaguzi wa USA ambapo tunaweza kushuhudia negotiations kati ya Russia na Ukraine...

Hao askari waliopo Russia wataondoka tu wenyewe...

Russia sio Libya...
Viongozi wengi wa West wanajuta sasa, kwa maana hakuna walichofanya..
 
Huo ushahidi wa nchi 32 ndio tunautaka, usijifiche kwenye kichaka cha iraq
Hujanijibu swali langu kwanza, nchi mi nitakutajia...

Nimekuuliza US kuingia na zile nchi zote Iraq ni kwa sababu alikuwa amezidiwa, alikuwa kaishiwa askari? Au alimuogopa Iraq?

Ndio maana nikasema kama huna jawabu kaa kimya, kama hoja huna kaa kimya, sasa baada ya maswali magumu umeanza kuongea pumba za mahindi...
 
Iraq ilivamiwa kwa azimio la umoja wa mataifa, marekani ilienda na nchi washirika, ni tofauti na Urusi inavyopigana na Ukraine alienda peke yake na ameishiwa wanajeshi akaomba msaada kwa north Korea sasa utalinganisha na USA, ebu sema lini USA aliishiwa wanajeshi akaomba msaada wa wanajeshi?
 
Mama yangu 😂😂
Ndio maana nasema kama hujui kitu ni bora ukae kimya...

Wengi wenu ni weupe mnabisha na hamjui chochote...

UN haikuhusika na uvamizi nchini Iraq, US ndiye aliongoza hio operation wakiita jina la operation Iraq freedom, tena US akitumia azimio la baraza la umoja wa mataifa namba 678 kuidhinisha uvamizi huo ambao hata katibu mkuu umoja wa mataifa Kofi Annan alisema uvamizi huo haukuwa halali....

Mkuu fuatilia vitu...
 
We upo dunia ipi?
 
hoja mchungu lakini haina budi kuwa hivyo.
 
Kinachokufanya uamini US na washirika wape wameshuka kiuchumi kutokana na kuathirika vita nchini Ukraine ni uhuru wa vyombo vya habari kwao.

Ikiwa tajiri kama US, UK, German, France n.k wametikisika basi Russia inaweza ikawa mara 7 yake.

Russia Putin alipiga stop chombo chochote cha habari kuripoti hiyo vita pasipo ridhaa ya serikali yake.
 
Kuna Putin, Utawala wa Iran na North Korea.

Mwenzao China alishastaarabika.
 
Hajui hata kama Ukraine haruhusiwi kupiga ndani ya Urusi kwa kutumia silaha anazopewa
Halafu mtu anasema eti NATO haiwezi kumuangusha Russia. Ukraine tu asiyekuwa na nguvu ya Jeshi la anga, Navy na anaipasua Russia ndani ya ardhi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…