Putin asema operesheni ya Urusi nchini Ukraine imefanikiwa

Putin anahamisha magoli na kusema sizitaki mbichi hizi, alifikiri vita inajua Super Power.

Wananchi wa Russia uchumi wao unarudi kule kule kwa USSR, kupanga foleni hata kwa kununua mkate 🍞 na kuvaa mitumba kutoka nchi za magharibi.
 
Rais wa Urusi, Vladmir Putin amesema kuwa operesheni yake ya kijeshi nchini Ukraine imefanikiwa na kuwa hatoiruhusu nchi hiyo kutumika kama uwanja wa kuitishia Urusi.

Akizungumza katika mkutano wa serikali uliorushwa moja kwa moja kwenye televisheni, Putin amesema operesheni yake inaendelea vizuri kwa kufuata kikamilifu mipango waliyoiweka.

Rais huyo ameongeza kuwa Benki Kuu ya Urusi haina haja ya kuchapisha pesa kwa kuwa nchi hiyo ina rasilimali za kutosha za kifedha za kukabiliana na changamoto za sasa za vikwazo.

Mazungumzo kati ya pande hizo mbili za kivita yanaendelea kwa sasa huku kila mmoja akielezea matumaini ya kupatikana suluhu.

Source: DW
Kama ni hivyo kwanini sasa Russia wanaingia na meli za kivita ukrain? Ngomba bado mbichi

japan.jpg
 
Rais wa Urusi, Vladmir Putin amesema kuwa operesheni yake ya kijeshi nchini Ukraine imefanikiwa na kuwa hatoiruhusu nchi hiyo kutumika kama uwanja wa kuitishia Urusi.

Akizungumza katika mkutano wa serikali uliorushwa moja kwa moja kwenye televisheni, Putin amesema operesheni yake inaendelea vizuri kwa kufuata kikamilifu mipango waliyoiweka.

Rais huyo ameongeza kuwa Benki Kuu ya Urusi haina haja ya kuchapisha pesa kwa kuwa nchi hiyo ina rasilimali za kutosha za kifedha za kukabiliana na changamoto za sasa za vikwazo.

Mazungumzo kati ya pande hizo mbili za kivita yanaendelea kwa sasa huku kila mmoja akielezea matumaini ya kupatikana suluhu.

Source:
Kumbe yupo Kigoma
 
Back
Top Bottom