Putin asema operesheni ya Urusi nchini Ukraine imefanikiwa

Putin asema operesheni ya Urusi nchini Ukraine imefanikiwa

Rais wa Urusi, Vladmir Putin amesema kuwa operesheni yake ya kijeshi nchini Ukraine imefanikiwa na kuwa hatoiruhusu nchi hiyo kutumika kama uwanja wa kuitishia Urusi.

Akizungumza katika mkutano wa serikali uliorushwa moja kwa moja kwenye televisheni, Putin amesema operesheni yake inaendelea vizuri kwa kufuata kikamilifu mipango waliyoiweka.

Rais huyo ameongeza kuwa Benki Kuu ya Urusi haina haja ya kuchapisha pesa kwa kuwa nchi hiyo ina rasilimali za kutosha za kifedha za kukabiliana na changamoto za sasa za vikwazo.

Mazungumzo kati ya pande hizo mbili za kivita yanaendelea kwa sasa huku kila mmoja akielezea matumaini ya kupatikana suluhu.

Source: DW
What happened to Stalin's Invision of Finland in 1939/1940 will happen to Putin's Invasion of Ukraine.
 
operesheni yake ya kijeshi nchini Ukraine imefanikiwa na kuwa hatoiruhusu nchi hiyo kutumika kama uwanja wa kuitishia Urusi.
Kama lengo la vita limetimia maana yake vita itakuwa imeisha.

Kama ataendelea na vita maana yake bado hajafanikiwa lengo lake.

Tunatarajia kuwa vita imeishaa
 
Kama ni hivyo kwanini sasa Russia wanaingia na meli za kivita ukrain? Ngomba bado mbichi

View attachment 2154009
Br hiyo pichA ya hizo meli Vita ilipigws mwaka 2017 kwenye mazoezi ya kivita yaliyoitwa zapad na sio hivyo BBC imetukaririsha..
Nb. Hiyo headline ya BBC ukiifungua Haina maelezo kabisa ndani yake zaidi ya update za Vita Ukraine.
N
 
Operesheni "imefanikiwa" ama "inaendelea vizuri"? Lipi hasa?

Operesheni "imefanikiwa" kuendana na malengo yote tuliyotangaziwa? Doubtful!

Operesheni "inaendelea vizuri" kuelekea katika malengo yao yote tuliyotangaziwa? Also, doubtful!
wewe endelea na doubtful
ila mwenye operation yake anasema imefanikiwa
nb:~haijakamilika ila imefanikiwa kwahio kaeni kwakutulia
 
Kama lengo la vita limetimia maana yake vita itakuwa imeisha.

Kama ataendelea na vita maana yake bado hajafanikiwa lengo lake.

Tunatarajia kuwa vita imeishaa
hakuna sehem kasema lengo limetimia na kukamilika nimamambo yanayofanana ila yanatofautiana
lengo limetimia ila bado halijakamilika ila limetimia
nandio maana hta US lengo lakumuua SADAM lilitimia ila halikukamilika lengo lao ndio maana baada yakumuua wakakaa sana zaidi ya miaka 10s
kwahio RUSSIA bado wapo wapo sana UKRAINE tena sanaaaa
 
general wa nchi gani akaenda vitani (front line)?
Hawa hapa
JamiiForums1365511732.jpg
 
Back
Top Bottom