Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 17,251
- 22,929
Hatimaye Putin ameshinda Vita ya kiuchumi kati yake na Ulaya.C.E.O wa kampuni kubwa kabisa ya mambo ya uchumi Ulaya asema,"Ulaya hatimaye inaelekea katika mgogoro wa kibenki, kuanguka kwa viwanda, kaya na uchumi.Hii ni katika "wiki chache tu zijazo" amesema.
07 SEPTEMBA 2022 
Tuomas Malinen ni Afisa Mkuu Mtendaji (CEO) wa GnS Economics huko Helsinki, Finland. Leo Jumatano, Septemba 7, 2022, amesema hadharani kwamba Ulaya inaelekea katika anguko kamili la biashara, na sarafu yake, ndani ya wiki chache zijazo, kulingana na tovuti yake ya GnS Economics.GnS Economics ni washauri huru, wenye makao yao makuu mjini Helsinki.Kampuni hii imebobea katika kutabiri na kuchambua habari za uchumi wa dunia na masoko ya fedha.
Mkurugenzi Mtendaji Tuomas Malinen( PhD), ni Mkurugenzi Mtendaji na Mchumi Mkuu wa GnS Economics. Yeye pia ni Profesa Mshiriki wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Helsinki. Amesomea uchumi katika Chuo Kikuu cha Helsinki na Chuo Kikuu cha New York. Amebobea katika ukuaji wa uchumi, migogoro ya kiuchumi, Benki Kuu na mzunguko wa biashara.
Katika msururu wa jumbe zake hadharani kwenye akaunti yake ya Twitter, Malinen ameonya leo na kusema, "utabiri wangu (wetu) wa kila mwezi umetoka, na jamani unatisha! Ni kwamba,Ulaya inazama na inavuta dunia nzima pamoja nayo. "
Kinacho-ambatana na ujumbe huo ni chati(chini) inayoonyesha matatizo makubwa. 
Alikwenda mbali zaidi na kuonya "ninawaambia watu kwamba hali ya Ulaya ni mbaya zaidi kuliko watu wengi wanavyo-dhani na wanavyoelewa. Kimsingi tuko ukingoni kabisa mwa mgogoro mwingine wa kibenki, kuporomoka kwa msingi wa viwanda na kaya zetu, na hivyo kuwa kwenye ukingo wa kuporomoka kwa biashara yetu" Aliendelea kuuambia umma, "kasi ya kuzorota ni kubwa sasa, na ni suala la muda tu." Nasema hivi kwamba,bado tuna wiki chache kabla ya "matatizo makubwa" Ulaya kuanza. Kwa hiyo watu wa Ulaya wachukue hatua za tahadhari haraka,kama kuwa na fedha cash nyumbani kwa kuwa haku-takuwa na riba ya maana tena Bank,chakula, maji na kuni.
Huu ni ushauri mzito kutoka kwa mshauri mkubwa wa Kampuni kubwa ya mambo ya uchumi Ulaya kama GnS,kwa hiyo ni vizuri ukapewa umuhimu unao-stahili.Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni kubwa namna hii kusema mambo mazito kama hayo hadharani si kawaida,kwa hiyo ni kweli hali itakuwa ni mbaya sana Ulaya kwa hiyo watu Ulaya wanapaswa kuchukia tahadhari stahiki.
EURO KUANGUKA?
Msomaji mmoja alimuuliza Malinen "Je, Euro kuanguka kwa kasi ni dhahiri unafikiri?" Alijibu kwa uwazi "Ndiyo." Jibu hili linatoka kwa mtaalamu mbobezi wa masuala ya uchumi Ulaya mwenye PhD katika uchumi,kwa hiyo ni wazi kwamba Euro(€ ) itashuka thamani sana ikilinganishwa na US Dola(US$),tena kwa haraka sana.
Mnamo Agosti 22, Euro(€) ambayo hapo awali ilikuwa na thamani ya takriban US$1.25, ilishuka chini
hadi takriban US$0.99. Hii ni kwa sababu wawekezaji wamepoteza imani kwa Ulaya kwa haraka kutokana na matatizo ya nishati yanayo-ikumba Ulaya kwa sasa,yaliyoletwa na vikwazo dhidi ya Urusi kwa sababu ya "special operation" ya Urusi inayo-endelea huko Ukraine. Vikwazo hivyo,badala ya kuidhuru Urusi kiuchumi,sasa vinaidhuru sana Ulaya yenyewe. Ulaya haina gesi asilia ya kutosha kuendesha mitambo yake ya umeme, na kutokana na vikwazo walivyo-iwekea Urusi vya kiuchumi, wanakataa kununua gesi kutoka Urusi!Hii inamaanisha kuwa Ulaya lazima iende kwenye masoko mengine ya Dunia kununua gesi asilia na katika masoko hayo bei imeongezeka sana huku mahitaji yakiongezeka sana pia.
Sio tu kwamba biashara za Ulaya zinaona gharama ya juu ya gesi asilia, pia sasa wanapata bili za umeme kubwa zaidi,ambapo thamani ni mara kumi zaidi (au hata zaidi) kuliko kawaida,kwa sababu mitambo ya kuzalisha umeme pia sasa inalipa zaidi kwa gesi asilia.Hali hii imesababisha gharama za uzalishaji kupanda sana na hivyo bishara kufungwa kwa sababu ya gharama za juu za nishati.Hii imefanya watu wengi sana kukosa kazi wakati ambapo bili zao kibinafsi za nishati majumbani pia zinaongezeka. Kwa kuwa watumiaji wanalazimika kulipia zaidi gesi asilia na umeme na biashara zimedorora,hakuna tena fedha. Jambo hili limesababisha watu wengi kuachishwa kazi na makampuni mbali mbali vikiwepo viwanda.
Wawekezaji barani Ulaya wakiona jinsi mambo yanavyo-poromoka Ulaya, sasa wanatuma fedha nyingi Marekani ili kuweka vitega uchumi huko.Marekani kwa sasa kuna riba kubwa kulinganisha na Ulaya na kwa hiyo kuna viwango bora zaidi pia vya mapato. Kadiri pesa nyingi zaidi zinavyoondoka Ulaya kwenda Marekani, ndivyo Euro(€) inavyozidi kupoteza thamani yake haraka. Hii itasababisha pesa zaidi kwenda Marekani,kwani wawekezaji wanatambua kuwa wanahitaji kuondoka kwenye Euro zone sasa wakati bado Euro(€ )ina thamani fulani.
Inaonekana Mkurugenzi Mtendaji Tuomas Malinen anaona maandishi ukutani, na sasa anawaonya hadharani Wazungu kuweka akiba ya chakula, maji na vitu vingine muhimu,kwa kuwa hakutakuw na bidhaa zozote kwenye
maduka za kununua. Maafisa wa serikali ya Ulaya wamejimajiza wenyewe kwa vikwazo vyao vya kijinga visivyo-zingatia maslahi ya watu kiuchumi na kijamii.
Shida ni kwamba, kile kinachotokea huko Ulaya kitaathiri maeneo mengine pia,hususan Afrika. Ikiwa Ulaya itaanguka rasmi kiuchumi, jambo hilo hilo litafanyika nchini Marekani takriban wiki mbili baadaye, na Afrika baadaye,kutokana na kwamba biashara zetu zimefungamana. Wamarekani na hata Waafrika wanashauriwa kuzingatia sana kile kinachoendelea Ulaya.
Source:C.E.O. in Europe Sounds the Alarm: Heading into Banking Crisis, Collapse of Industry, Households, Economy -- "weeks away"