Mkuu mimi namwona Putin kama mtu ambaye anajiona yeye ni zaidi ya wengine, yeye anajua na ana uelewa mkubwa, anaona bila yeye bara la Asia na Asia ya Mbali itahodhiwa na Ulaya au Amerika. Yeye aliomba kujiunga na NATO, Ukraine hakupinga wala kulalamika. Leo Ukraine anaomba kujiunga na NATO imekuwa nongwa kwake na vita juu.
NATO walimkataa kujiunga nao kwa sababu wanajua nia na matamanio yake: > apate nguvu za kuzinyanyasa nchi ambazo zilikuwa majimbo USSR. > apate mwanya wa kujua nini kipo ndani ya NATO na hatimaye kuisambaratisha. > Apate mwanya wa ushawishi wa yeye kuwa RAIS wa Urusi wa kudumu kwa mbinu yake ya kujiongezea muda wa kukaa madarakani Rais ama kuwa Waziri Mkuu. Hii vita itamgharimu sana.