Putin atafanya nini baada ya kuiangusha Serikali ya Ukraine? Au alikurupuka kwa hasira?

Mbona hujajibu swali la Mleta maada badala yake unaeleza sababu zilizoifanya Russia Kuivamia Ukraine ambazo bila Shaka Kila mmoja anazijua make Putin amekuwa akiziimba Kila Mara.

Marekani japo ana uchumi Mkubwa,aliisimika Serikali kibaraka wake wa Afghanistan na kutoa mafunzo ya Kijeshi kwa miaka 20 lakini Alivyoondoa Majeshi yake tu Basi Serikali Kibaraka ya Afghanistan ilidondoshwa chini ya Wiki moja tu.


Sasa Mleta maada anauliza hivi?

Kama Urusi ataiangusha Serikali ya Ukraine na Kuweka Serikali Kibaraka wake,Hiyo Serikali itawezaje kudumu Madarakani ikiwa Raia walio wengi wa Ukraine wanapinga Uvamizi wa Urusi Plus Uchumi wa Urusi ambao unakwenda kuporomoka kwa vikwazo vilivyowekwa?

Tatizo wengi mnajibu kishabiki TU. Mtu akisema against your Wishes mnaanza kutukana badala ya kutoa Facts,na hii ni asili ya Ngozi nyeusi(Cancer ya vizazi vya Ngozi nyeusi Milele). Mnaishia kusema TU eti Putin anajua na hajakurupuka,mkiulizwa anaweza kufanya Nini Kuisimika hiyo Serikali yake Kibaraka mnashusha matusi.


MAONI YANGU.

Russia ananjia Nyingi ambazo anaweza kusimika utawala pale Ukraine hata Kama Raia wa Ukraine hawatapenda lakini watalazimika kupenda. Njia moja ambayo naona ataitumia ni hii hapa.

Kuliacha Jeshi la Urusi ndani ya Ukraine na Kulinda Usalama hata kwa miaka 5 mpaka pale ambapo Jeshi Kibaraka la Ukraine litakapopatikana ili kuilinda Serikali hiyo ya Kibaraka wa Russia. Hapo ndipo Russia inaweza kuondoa Wanajeshi wake. Hii njia ni raihisi kwa Urusi kwasababu inapakana na Ukraine. Endapo Zisingelikuwa zinapakana Basi ni wazi hata Uvamizi Urusi ingelishindwa vibaya Sana. Kupeleka Wanajeshi 200,000 umbali wa 6,800Km Kama alivyofanya Marekani kule Iraq ni Gharama kubwa kitu ambacho Urusi asingeliweza kutokana na MATOKEO ya vikwazo hivi hapo baadae.*

Nchi Nyingi za Africa kunaserikali Nyingi ambazo haziungwi mkono na Raia lakini maisha yanakwenda make Jeshi Liko upande wa Utawala. Hata ukiangalia BELARUS Raia wengi hawaitaki Serikali ya Lukashenko,na walipojaribu kuandamana,Urusi ilituma Wanajeshi kwenda kuzima maandamano.

MTz 255Dar.
 
Mkuu kwanza nikupongeze kwa kuwa na uelewa mkubwa na pia kuwa na kichwa sober

Lakini vipi huo mpango wa hao wanaomuwekea vikwazo vikali si watakuwa wanafadhili vikundi vya waasi kwa nguvu sana? je hii haitapelekea Urusi kuanza vita na NATO?
au unaona ana uwezekano wa kufanikiwa kwa asimilia ngapi?
 
Kilaza huyo
 
Kuna raia wanawatizama wanajeshi wa urusI kama ngoma ya mchiriku, huku wakiwatukana f*****k U, tena wamejipanga kando ya barabara,
 
Siku hizi JF inapoteza hadhi yake. Mbumbumbu kama huyu naye karuhusiwa kuwa na account!? Nawashauri mods. Kwa sasa mtu akitaka kujiunga JF alete barua ya maombi toka serikali za mitaa.
Una uhalali gani wa kumwita mwenzako mbumbumbu kwa sababu tu ametoa maoni yake ambayo yanakinzana na mtazamo wako?
Umekosea sana mkuu.
 
Putin hana lengo la kuchukua Ukraine yote, yeye ataka Kyiv tu na miji mingine ambayo anaidhibiti kwa sasa kuelekea kule chini Donbass na Crimea.

Hizi ni sehemu zake na hataki Russia isogelewe na NATO.

Putin ataka serikali ambayo haitasikiliza upande wa nchi za magharibi na itamsikiliza yeye yaani ataka nchi kama Belarus na kisha kutiliana saini za suluhu pamoja na mahusiano ya kibiashara yaani bilateral relations.

Akimaliza hiyo atataka NATO wamsikilize masharti yake mapya kuhusu usalama katika eneo hilo.
 
Mi nawaza kuwa anataka kuigawa nchi. Labda anaigawa kwenye mto Dnipier, Ukraine Magharibi na mashariki, halafu anaweka DMZ mpakani. Nchi zikifanyiwa hivyo huwa zinapoa kabisa, tena kwa miaka mingi.
 
Mkiambiwa Dictators sio wazuri muwe mnaelewa. Russian federation watapata tabi sana na hii vita italitesa hilo taifa kiasi watachapana wenyewe kwa wenyewe nakugawana vipande. Hakuna nchi ulaya inafurahia kile kinaendelea Ukraine na kwa taarifa za siri idara za usalama zinajuwa why Russian wameanza hii vita na ili kumuonyesha ni mpumbavu wamesema hawatoenda kuipigania Ukraine ila putin will pay high price... Kiufupi Putin watamuondoa na kwa data zipo kufika July2022 Russian watakuwa na hali mbaya ya uchumi..
 
Atakua na kazi mbili. Kwanza kusimamisha uchumi wa ukraine [emoji1255] ambao utakua umeharibiwa kutokana na vita, pili kupambana na vikwazo vya magharibi ili kunusuru uchumi wake.
Huyu mzee alikurupuka sana na ubabe wake wa mwaka 47
unataka kuniambia wewe unazijua mishemishe za NATO kuliko Putin!?,au unaijua Ukraine kuliko Putin !!! the man is fighting for his concrete reason ,like wise marekani alimtumia Ukraine kufanikisha lengo lake for her concrete reason !! so wengine let's keep watching the game
 
Hujui uchumi wewe bora ukae kimya. Mpaka sasa wanaoteseka ni wao kuliko Russia, angalia bei ya fuel USA, bei ya coal pale Germany, bei ya ges ulaya yote.

Ungekua na akili ungejiuliza kwanini mpaka sasa wameshindwa ku ban ges ya Russia kuingia Ulaya. Kwanini mpaka sasa wameshindwa kuzifungia benk zote za Russia kwenye mfumo wa SWIFT.

Kwa taarifa yako tu, mafuta ni kama dhahabu ukisusa wewe wenzio watanunua, Nato nzima hawafiki idadi iliyopo China, hapo sijazungumza asia yote, africa na south America.
 
Tukishamalizana na Ukraine, tutawachimbia mkwara mzito vile vinchi tunavyopakana navyo vijitoe NATO la sivyo tutavikatia supply ya gesi na mafuta vikanunue huko kwenye NATO yao kwa bei ya kuruka.
Vikiendelea na ubishi tunavipelekea Moto kwa mpigo kuliko wa Ukraine
 
Siku hizi JF inapoteza hadhi yake. Mbumbumbu kama huyu naye karuhusiwa kuwa na account!? Nawashauri mods. Kwa sasa mtu akitaka kujiunga JF alete barua ya maombi toka serikali za mitaa.
Jamaa ana swali zuri Sana lakini we'we Ni much know
 
Siku hizi JF inapoteza hadhi yake. Mbumbumbu kama huyu naye karuhusiwa kuwa na account!? Nawashauri mods. Kwa sasa mtu akitaka kujiunga JF alete barua ya maombi toka serikali za mitaa.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mnachekesha sana , wewe una akili nyingi kumshinda Trump , ambye anaona kuwa vikwazo havitosaidia kuishusha RUSSIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…