Putin atoa masharti yake ya kumaliza vita yake na Ukraine, na hivyo kuondoa majeshi yake kwenye nchi hiyo

Katika press zake, sikuwahi sikia akisema ndani ya masaa hayo kyiv itakua chini yake, bali ni maneno ya wachambuzi na taarifa za wana usalama wa USA. Hata hivyo, kwa marekani yenyewe katika operation zoote za kutoa utawala madarakani hakuweza kufanya hilo...sana sana ni mwezi mmoja.
 
Wewe ushawahi kuwepo kwenye hizo Nchi mpaka ukaweza kujua vita ya wamarekani ipo vip na Warusi ipo vip mbona unaandika vitu vya kusadikika Mkuu yaani Nchi ambayo muda wote tunazungumzia mafuta ya kupikia na sukari bei imeongezeka tuzungumzie Vita za wenzetu...
 
Kuwa shoga ni uamuzi wa mtu man na ni dhambi kama dhambi zingine utajuana na muumba wako....

Kwahiyo mbali na ushoga,, suala la mauwaji dhidi ya nchi za kiarabu/kiafrika ni sawa kuwasapoti hawa wamagharibi?? mamilioni ya raia/civilians wamepoteza maisha, mwafrika mwenzio Gadaffi ameuawa kinyama mlikaa kimya. Leo hii kwa ukreine kelele nyiingi 😁 saddam kauawa kinyama mlikaa kimya.


Suala la vikwazo,, urusi anawekewa vikwazo😁, why??? Amefungiwa kushiriki michezo ya kuwania kucheza w/cup nchini Qatar n.k 😁 marekani na washirika wake wameuwa mamilioni ya watu waco na hatia nchi za kiarabu n.k, why hawakuwekewa vikwazo? Israel ameuwa maelfu ya wapalestina na bado anaendeleza unyama huo lakini hakuwekewa vikwazo vya aina yoyote ile au kufungiwa dah 😁 hii dhulma acha tu yani. watoto, wajane n.k wamepoteza maisha, very sad
 
Wewe unawataja wafadhili wa makundi ya kigaidi! Gadaffi mtu aliye kuwa anauwa watu kilinda wadhifa anaongoza nchi kidini alistahili kufa.. Saddam nae anae uwa watu kwasababu ni jamii tofauti nae alistahili hakuna mtu mzuri hata mmoja kati ya wote uliyo wataja umelishwa mataputapu na hao watu wanaoishi jagwani...
 
Kidume.cha shoka kimekwisha zungumza bila kumung'unya maneno. USA na NATO kazi wanayo, waendelee kubweka kama mbwakoko au wafanye kitu shaul yao. Huyu jamaa ninazidi kumkubali kila siku
 
Hawa maraisi wawili wangekua wanasoma maoni ya wana JF angalau mmoja wao, angesha shinda vita ndani ya masaa sita tu, sijui wana kwama wapi, maana du....!! Mimi naendelea kuchimba tu handaki na familia yangu hapa hapa visig.. ili
 
Kama ulikua hujui kuwa URUSI ni Nchi nzuri sana na viongozi wake ni wastaarabu sana wacha nikufahamishe;-
Huo Ndio ukweli URUSI Ndio Nchi Kubwa Kuliko zote duniani,
Urusi ni nchi namba mbili kwa ukubwa wa Jeshi duniani,
Ni Nchi ya kwanza Kwa kuzalisha gesi Duniani,
Na ni Nchi ya pili Kwa kuzalisha mafuta Duniani,
URUSI ndio nchi pekee Duniani inayopakana na mabara mawili yaani upande mmoja wa nchi ipo Barani ASIA na upande mwengine wa nchi ipo Barani ULAYA,
Lakini pia Watu wake wengi wamesoma na wanauwezo Mkubwa kiuchumi, kiteknolojia, na kijeshi,
Lakini Pamoja na sifa zote hizo hawajawahi kuwafanyia ubaya wowote wa AFRIKA,
Sasa wewe muafrika unaanzaje kuichukia URUSI na kuwapenda NATO wakati wao wamefanya mambo ya hovyo mengi AFRIKA,
Waafrika inabidi tuamke na kuipenda URUSI kwasababu zifuatazo;-

1) URUSI Hajawahi kuchukua watumwa Afrika

2)Urusi haijawahi kuitawala Afrika kiukoloni.

3) URUSI haijawahi kushiriki Berlin conference, mkutano wa kuigawa Afrika.

4) URUSI hawajahi kupora rasilimali za Afrika.

5) URUSI haijawahi kuweka mikataba ya kilaghai na Machifu wa Afrika.

6) URUSI haijawahi Kupora Ardhi ya Afrika au kuwa mlowezi wa Afrika Kama wale waliopo south Afrika, Kenya na wale walionyang'anywa ardhi na Mugabe kule Zimbabwe.

7) URUSI haijawahi kuivamia kijeshi Afrika Kama Yale majeshi ya NATO inchini Libya.

Makala hii imeletka kwenu na Dhulkad Madara Kutoka Morogoro
 
Kidume.cha shoka kimekwisha zungumza bila kumung'unya maneno. USA na NATO kazi wanayo, waendelee kubweka kama mbwakoko au wafanye kitu shaul yao. Huyu jamaa ninazidi kumkubali kila siku
Na Leo bendela za USSR zimeanza peperushwa hivyo wakichelewa Ukraine itakuwa jimbo kama majimbo mengine ndani ya Russia
 
BBC, CNN and the like, wameshindwa kabisa kushawishi dunia. Sanctions childish propaganda zao zimezimwa. Russia is very Serious wenyewe wanaleta mbwembwe. Ni wakati wa kujua sasa mbabe ni nani.
Kuwa serious siyo kushinda, usiwe mshabiki sana badala ya kusimamia uhalisia
 
Hatahivyo ni wavamizi.. hawapori maeneo Africa sababu wanapora hapo hapo Europe tena sio kwa mikataba kwa mtutu kabisa kuuwa watu na kuharibu miundo mbinu....
 
Pro-Russia ni wajuaji mno na kumbe hakunaga wanalojua, Russia haitashinda hii vita [emoji16][emoji1][emoji16][emoji16]
 
Unajua hile vita ya kumuondoa Sadam Hussein ilichukua almost Mwezi Mmoja, Ukraine ni moja ya nchi ya pili Kwa ukubwa Ulaya unadhani itakuwa Rahisi kuichukua yote?
 
Marekani na Urussi hawana tofauti. Wote ni mabeberu watafuta ukoloni. Madai kuwa USA siyo wakoloni siyo kweli. USA ni wakoloni wa uchumi. Madai eti USA ina nguvu na imefanya kweli Iraq na Afghanistan siyo kweli.Ilichoweza USA ni kuwaua viongozi lakini mabadiliko yaliyotegemewa hayakutpokea. Technically speaking, USA imeshindwa vita ya Iraq, Afghanistan, Libya, Vietnam, Korea, na kwingineko. Walienda huko kwa ubabe na kukimbia kama kuku aliyenyeshewa maana lengo lao halikutimia.
 
Unajua hile vita ya kumuondoa Sadam Hussein ilichukua almost Mwezi Mmoja, Ukraine ni moja ya nchi ya pili Kwa ukubwa Ulaya unadhani itakuwa Rahisi kuichukua yote?
Lakini matokeo yalikuwa yapi? Mbona USA ilikimbia bila kupata waliyotaka.
 
Unapoandika hapo sasa hivi ujue kuwa Marekani yupo Syria na hakuna wa kumtoa na mafuta anafyonza vibaya.
 

Tatizo lako upo kishabiki. Unatetea ujinga badala kukemea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…