Putin kuifuta Wagner group

Putin kuifuta Wagner group

Marikani akawapata Wagner 500 tuu !!! Puttin atajua hajui!! Watoe TU position ya jeshi la urusi huko Ukraine!!! Inatosha
 
Baada ya Wagner group kufanya maandamano yao ya kijeshi kitendo hicho kimeonekana kama ni tishio kwa usalama Russia, Putin kwenye kikao cha Leo amekuja uamuzi wa kuifuta Wagner Group kwa kuwapa options tatu Askari wa warger

1: kurudi nyumbani Yani kuachana kabisa na shughuli za kijeshi
2: Kujiunga na jeshi (Russian Army)
3:kwenda Belarus

Makundi haya matatu yameahidiwa kutokuchukuliwa hatua za kinidhamu iwapo watakubali offer hizo

Kuvunjwa vunjwa huku kwa Wagner itawaathili uwepo wapo barani Africa na sehemu zingine(Syria...etc) kwasababu Wagner ambayo inayofanya kazi barani Afrika na kwengine ipo chini ya MOD(Ministry of Defence).

Belarus haina ushawishi barani Afrika, kandarasi za Wagner za kuwa Afrika na Syria zilitolewa na MoD kwa hivyo mkataba utakuwa wa Wagner Russia(Russian Army) sio Belarusi.

Pia katika Hotuba hio yake Putin aliwashukuru Warusi kwa uvumilivu, mshikamano na uzalendo wao wa aina yoyote ya usaliti, majaribio ya kuleta machafuko ya ndani yatashindwa,Uasi wa kutumia silaha ungezuiliwa hata hivyo.

Pia kasema

Maadui wa Urusi walitaka nchi hiyo iingie katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yenye umwagaji damu, imeshindikana

Putin ameahidi kwamba ahadi kwa Wagner itatekelezwa.

Vladimir Putin ameshukuru Lukashenka kwa mchango wake katika kukomesha uasi huo.

Putin anaamini kwamba roho za kizalendo za Warusi, ilichukua nafasi kubwa katika kukomesha uasi hio.
Kumbe hii issue ilikuwa serious?? Me nilijua ni Planned na wao wenyewe lkn sasa kwa hatua hizi inaonyesha kabisa hata Putina hakuhusika, Aloo!!! ???
 
Mwisho wa Urais wa Putin haupo mbali sana, unaweza kuwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwakani. Warusi hawapendi Rais dhaifu.
Sure Aisee. Kwanza me nilihisi yaliyotekea ni Tricky tu na kwamba walikuwa na dhamira fulani hivi labda ya kuwakung'uta Ukraine kisawasawa kwa kuwahadaa na hayo mapinduzi uchwara lakini lahasha naona PUTIN maji yalimzidi Unga. Ni muda sasa apigwe chini tu
 
Wagner ilikuwa iiharibu Moscow maana silaha zote zilielekezwa urusi , russia awalipe haki zao haraka sana.
 
hujawahi kuona bongo movie wakiigiza kulala ktk jeneza na kufa

Prigozhin in one of the only hotels in Minsk without a window, says US official​

Yevgeny Prigozhin has landed in Belarus and is staying in one of the few hotels in the capital that does not have any windows, a US official has suggested.

The Wagner leader was told to flee to Belarus as part of a deal to end his group's armed rebellion on Saturday.

He was last seen in public leaving the southern Russian city of Rostov-on-Don after calling off his troops, and there has been speculation about his whereabouts since then.

US Senate Intelligence chair Mark Warner told NBC News Prigozhin is in Minsk, and he believes he is in a hotel with no windows.

"I understand, literally as I was coming on air, that he says he's in Minsk and he actually is," he said.

"And get this – this is just reports – that he is in one of the only hotels in Minsk that does not have any windows."

Mr Warner suggested this could be to protect him against assassination attempts.
=========================

Usalama wa Prigozhin ni kukimbilia nchi za EU au hata Poland ili wamkabidhi kwa FBI wanaomtafuta maana huko Belarus sio salama kwake.
 
Russia mambo yao kama Sudan alafu anatokea mtu kijiji cha Chita anakwambia ni superpower.
Naona leo kasema kama Wagner wangesonga hadi Moscow basi kila kilichotokea Ukraine kinge reset, wangepoteza kila kitu.

Kasema pia Wagner ndiye alikuwa analisha jeshi.

Wagner walilipwa zaidi ya 1bil usd kwa wanajeshi tu, huku chakula nacho kikibeba kiwango cha Dollar Milioni 900
 
Russia mambo yao kama Sudan alafu anatokea mtu kijiji cha Chita anakwambia ni superpower.
Leadership is not about size(power) , it's about knowledge and wisdom Kuwa superpower haimaanishi kutumia nguvu kila wakati, Putin alikuwa na uwezo wa kuwafuta Wagner kwa mizinga na airstrike kadhaa ,

Lakini hakufanya hivyo bali kachagua kutumia hekima na akili ukubwa kupooza mambo . Sasa Urusi ina wanajeshi 25k wa Wagner waliojisajili.

Putin ni rais ambaye anaona pande mbili za bodi ya za mchezo sio upande mmoja. Alizuia umwagaji wa damu na sasa kawafanya Wagner wajisalimishe kwake na wengine kupelekwa Belarusi.

Akili kubwa
 
Wagner ndo ishapotea milele, tayari hatari imenuswa.

Swala ni je Russia ataweza peleka watu ka wagner wafe?
Putin amesha bonyeza unfriend button kwa Prigozhin sasa ataanza kuishi kama mkimbizi kitendo alichokifanya kilihatarisha usalama wa Russia

Tayari katangaza kuwa fungulia mashtaka viongozi wa Wagner

It's wagnover
 
Yote hiyo inaonyesha udhaifu wa keshi la Urusi; halitakiwi kujulikana kama jeshi namba mbili duniani. Special Military operation imewashinda mpaka wakasaidiwa na jeshi la mamluki. Jeshi hilo la mamluki lilipowageuka wakaingia kwenye TV za taifa zinazomilikiwa na serikali ili kupiga filimbi za serikali yao .
Hiyo US wapi ilishaenda kwenye vita bila washirika wake
 
Leadership is not about size(power) , it's about knowledge and wisdom Kuwa superpower haimaanishi kutumia nguvu kila wakati, Putin alikuwa na uwezo wa kuwafuta Wagner kwa mizinga na airstrike kadhaa ,

Lakini hakufanya hivyo bali kachagua kutumia hekima na akili ukubwa kupooza mambo . Sasa Urusi ina wanajeshi 25k wa Wagner waliojisajili.

Putin ni rais ambaye anaona pande mbili za bodi ya za mchezo sio upande mmoja. Alizuia umwagaji wa damu na sasa kawafanya Wagner wajisalimishe kwake na wengine kupelekwa Belarusi.

Akili kubwa
Achana na leadership, hakuna nchi superpower ambayo kundi la wanamgambo sijui kampuni binafsi ya ulinzi inaweza asi na kutembea 24hrs zaidi ya kilomita 600 na ikabakiza kilomita kama 200 kufika mji mkuu.
Wagner wamepita HQ za vikosi kadhaa vya Urusi bila kupingwa. Hakuna superpower mzembe hivi. Ingekuwa ni nchi hata Uturuki tu hao Wagner hata 100km wasingefika. Yani Russian Army ni kama ilipotea mpaka Airforce ikaja okoa jahazi kwa gharama kubwa, mjini Moscow walishaanza kuchimba barabara na kuzitia mashimo, walishaweka vizuizi barabarani, walishalipua maghala ya mafuta njiani. Sasa hiyo ni kampuni binafsi, assume ingekuwa nchi imevamia.
 
Pia hili tukio linaonyesha civic maturity kubwa ya warusi kama jamii pia utiifu wa kiraia na approval ya warusi kwa mamlaka ni kubwa.

Jamii asi huwa tayari kukiwasha wanachosubiri tu ni fursa.

Mf Egypt wakani Hosni Mubarak, kulikuwa na watu mf muslim brotherhood na factions za kijeshi nyingi zilizokuwa zinasubiri fursa ijitokeze, wamng'oe HM.

Ni dhahiri jamaa amedhibiti jeshi lake.
Egypt hafikirii wala hatajwi kuwa superpower, Russia inatajwa kama miongoni mwa superpowers ila inafanya mambo ya nchi radicals. 1991 walikuwa na coup attempt, 1993 wakawa na constitutional crisis jeshi likashambulia bunge na bunge likachagua Rais wa mpito, 2023 imetokea mutiny ya kampuni ya mercenaries.
Hakuna superpower wa hivi
 
Achana na leadership, hakuna nchi superpower ambayo kundi la wanamgambo sijui kampuni binafsi ya ulinzi inaweza asi na kutembea 24hrs zaidi ya kilomita 600 na ikabakiza kilomita kama 200 kufika mji mkuu.
Wagner wamepita HQ za vikosi kadhaa vya Urusi bila kupingwa. Hakuna superpower mzembe hivi. Ingekuwa ni nchi hata Uturuki tu hao Wagner hata 100km wasingefika. Yani Russian Army ni kama ilipotea mpaka Airforce ikaja okoa jahazi kwa gharama kubwa, mjini Moscow walishaanza kuchimba barabara na kuzitia mashimo, walishaweka vizuizi barabarani, walishalipua maghala ya mafuta njiani. Sasa hiyo ni kampuni binafsi, assume ingekuwa nchi imevamia.
Ina maana jeshi lao asilimia 90 wapo Ukraine ?.....ndio maana waliobaki Urusi walishindwa kuzuia uasi ?
 
Huu ndio muda muafaka wa kuivunja Wagner maana huko mbeleni watafanya kweli.
Kundi linaongozwa na mpishi linatishia nchi inayoitwa superpower. Russia alishapiteza sifa za kuwa superpower basi tu kenge hawasikii mpaka damu itoke puani.
Wagner inapigana vizuri kuliko jeshi la Urusi lenye ukiritimba, leadership mbovu, logistics za hovyo na low morale. Hao Wagner wengine wao ni wanajeshi walioachishwa, na Wagnerites wanajua ubovu wa jeshi lao na wengine wana kesi kule hivyo option ya kujisalimisha jeshini hadi tarehe 1 July iliyotolewa na Shoigu ilikuwa haitekelezeki.

Wagner ni wapiganaji kutoka moyoni hakuna aliyejiunga kisa baba yake ni Sajenti au Kanali, organization structure yao iko very fast kwenye maamuzi kama kuna uhitaji wa artillery au retreat ni muda mfupi tu kamanda wa chini kwenye tukio husika anafanya maamuzi wakati jeshi la Urusi lina process kibao mpaka kamanda ambaye hayupo uwanja wa vita idhinishe. Wagner hakuna rushwa na ubadhirifu kama jeshini, makamanda wa Urusi kuiba bulletproof vests mwanzoni mwa vita na kuziuza online ilikuwa kawaida so unakuta Wagner wana gears nzuri kuliko jeshi ila tu hawapewi heavy weapons.

Walipokuwa Syria walipigana vizuri na iligundulika baada ya waandishi wa Urusi kutembelea hospitali na kukuta majeruhi wengi ni Wagner wakati ratio ya wanajeshi waliopo Syria ni kubwa kuliko Wagners. Wagner wanakuwa na casualties nyingi sababu wanapigana kwenye sehemu ngumu kama Bakhmut, na hawasiti kiholela.

Options tatu walizopewa na Putin kwenye hotuba yake ndio za akili, ile ya kujiandikisha ya Shoigu haiingii akilini ila naye hakuwa na namna maana hakuianzisha Wagner yeye ilianzishwa na Putin. Hakuna jeshi la nchi yoyote duniani huwapenda mamluki. Ya Russia ni sawa na ya Sudan, huku Janjaweed/RSF kule Wagner.
 
Tuone kama Urusi wataweza kuivunja hii offensive ya Ukraine bila uwepo wa Wagner (hasa fighting spirit yao )
 
Ina maana jeshi lao asilimia 90 wapo Ukraine ?.....ndio maana waliobaki Urusi walishindwa kuzuia uasi ?
Jeshi la Urusi lililopo Ukraine hata nusu haifiki, ni kwamba jeshi hasa Army ilionyesha mgomo baridi. Inaonekana kuna discontent kwamba Waziri wa Ulinzi na Mkuu wa majeshi hawakubaliki kivile baina ya makamanda hasa wadogo na wanajeshi. Maamuzi yao yamekaa kisiasa zaidi kuliko kijeshi, mfano kwanini walimtoa General Sergey Surovikin kuongoza vita ya Ukraine kama sio wivu.

Wagner walipita makao makuu ya vikosi kadhaa vya kijeshi hawakupata upinzani. Zikatumwa ndege zikadondoshwa saba, kule Chechnya mbali sana Kadyrov akaandaa jeshi lake waje Moscow kuongeza ulinzi wa mji mkuu sababu ni kama kina Putin walianza kuwa na wasiwasi na vikosi vyao vya ulinzi. Imani ilikataa ndio maana wakalipua storages za mafuta njiani Wagner wanakopita, barabara ya kuingia Moscow ikachimbwa mashimo.
Vikosi vilikuwepo kina OMON na Rosvdaglia sijui nimepatia spelling ila haikujulikana ni nani atamuunga mkono Prigozhin. Prigozhin mwenyewe alijua waziwazi hawezi, ila hakuwa na cha kupoteza, alijua wamepanga kumuua so bora ajaribu kutafuta makubaliano au ajaribu bahati yake anaweza ungwa mkono na makamanda kadhaa na vikosi vyao jambo ambalo halikutokea akaishiwa pumzi.

Kitendo cha Putin kumuomba msaada Rais wa Belarus ni aibu kubwa sana kwake, Putin sio mtu wa kukubali kushindwa na kusaidiwa kirahisi. Kwenye Kursk disaster Waingereza walipaki eneo la tukio na meli yao yenye uwezo ila wakakataliwa na Russian navy ambayo uwezo wa kuokoa haikuwa nao hadi wahanga wakafa. Siku ya tukio Putin anahutubia kwamba wanaofanya uhaini watachukuliwa hatua, Surovikin anatuma video kuomba Wagner waheshimu mamlaka alafu ndani ya saa 24 Prigozhin na Wagner wanasamehewa na kufutiwa mashtaka, na Prigozhin kupewa asylum Belarus. Kuna mtu hiyo hali inamuuma sana
 
Egypt hafikirii wala hatajwi kuwa superpower, Russia inatajwa kama miongoni mwa superpowers ila inafanya mambo ya nchi radicals. 1991 walikuwa na coup attempt, 1993 wakawa na constitutional crisis jeshi likashambulia bunge na bunge likachagua Rais wa mpito, 2023 imetokea mutiny ya kampuni ya mercenaries.
Hakuna superpower wa hivi
Uko vizuri sana kwenye takwimu na matukio ya kihistoria, lakini ,respectfully, unauelewa mdogo sana wa Uongozi na Utawala.

Dunia kote, huwezi zuia watu kuact, lakini uongozi unareact vipi na hiyo reaction ina acha impact zipi ndio kipimo cha umahiri wa kiongozi. Kama unadhani superpower ni kufyatua tu mabomu, jielimishe zaidi.
 
Back
Top Bottom