Putin na Kim Jong UN wamekubaliana kusaidiana endapo mmojawapo atashambuliwa

Waneshambulia wapi tangu waruhusiwe kushambulia ndani ya Urusi!!!
Ukraine imeharibu safu za wanajeshi wa Urusi waliokuwa wamejipanga kwa kutumia HIMARS, kamanda wa Ukraine alisema.

Alisema walilengwa mara tu Ukraine ilipopata kibali cha kutumia silaha za washirika kuvuka mpaka.

Wataalamu wanasema uwezo wa Ukraine wa kutumia silaha zinazotolewa na nchi za Magharibi katika ardhi ya Urusi unasaidia katika mapambano yake.

Ukraine imeweza kuharibu safu za wanajeshi wa Urusi baada ya kupata ruhusa kutoka kwa washirika wake kutumia silaha zao kushambulia maeneo ya kijeshi kuvuka mpaka na kuingia Urusi, kamanda wa Ukraine alisema.

Kamanda wa mizinga, aliye na ishara ya simu Hefastus, aliiambia Associated Press kwamba HIMARS ya Ukraine ilianza kufyatua risasi katika eneo la kaskazini la Kharkiv mara tu Ukraine ilipopata kibali.

Ukraine ilipata kibali kutoka kwa washirika wake mwezi uliopita kushambulia maeneo ya kijeshi nchini Urusi kwa silaha walizokuwa wametoa, hivyo basi kubatilisha kizuizi cha muda mrefu.

"Tangu siku za kwanza, vikosi vya Ukraine viliweza kuharibu safu zote za wanajeshi kwenye mpaka wakisubiri amri ya kuingia Ukraine," Hefastus alisema, kulingana na AP.

Alisema Ukraine isingeweza kuafiki hili bila ruhusa yake mpya, kwani risasi za kawaida haziwezi kufika mbali hivyo.

Hefastus aliongeza kuwa Ukraine sasa inaweza kuharibu vituo vya amri vya Urusi.

Urusi pia imekuwa ikiweka wanajeshi karibu na mpaka na Ukraine, tayari kuitwa kupigana.Naibu waziri wa ulinzi wa Ukraine, Ivan Havryliuk, aliliambia shirika la habari la AP kwamba takriban wanajeshi 90,000 wa Urusi walioko ndani ya ardhi ya Urusi walikuwa wakijiandaa kwa shambulio jipya vizuizi vitakapoondolewa.Haijabainika ikiwa yoyote kati ya hawa walikuwa wanajeshi wanaodaiwa kushambuliwa na HIMARS.

 
Unawezaje kudhoofisha jeshi la adui yako na hatimaye kuondoa huo "unazi" bila ya kuondoa utawala wa hiyo nchi?
Sasa bila jeshi kiongozi atafanya nini? Tatizo siyo Zelensky bali ideology ya hao neo nazi.
 
Sasa bila jeshi kiongozi atafanya nini? Tatizo siyo Zelensky bali ideology ya hao neo nazi.
Ngoja FRANC THE GREAT atakuja kukupatia jibu stahiki mkuu.

Yani ideology ya jeshi analoongoza Zelenskyy ni tofauti na ideology yake? Mbona hawamuondoi ama kumpindua?

Huwezi kuongoza jeshi lenye ideology tofauti na wewe na ukaendelea kuliamrisha na likatii hiyo amri.

So your point is Oxymoronic.

Kuna point gani kumuacha Zelensky ambaye ndo jemedari mkuu na rafiki wa west?
 
Jana urussi imeshambuliwa kwake na ukraine. Na wameua watu 150+ plus maeneo ya kimkakat. Mheshimiwa North korea majibu tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…