Nilishakujibu huko juu sio rahisi kuvunja utawala wa mtu mwingine ndani ya taifa lingine.Putin hataki tena kuondoa utawala wa Zelensky. Anataka kuachiwa majimbo tu ambayo wamechukimuwa kwa nguvu mfano Crimea na Donbas ndo vita iishe.
Ukraine anataka Russia arudi kwenye mipaka inayotambulika kimataifa. Hataki kuachia ardhi.
Kama Putin anataka kumaliza hii issue. Ashambulie Kyiv na kumuondoa Zelensky na kufutilia mbali utawala wake na aichukue Ukraine yote ambayo ilikuwa USSR wakati yeye akiwa KGB.
Shida iko wapi?
Just think bila mihemko.
Hapo inapigana nchi na nchi,we unadhani ni rahisi kitu alichokitaja Russia!?
Mbali na hapo NATO wako nyuma ya Ukraine unadhani jambo ni jepesi!?
Crimea itoe maana toka 2014 ilishanyakuliwa na Russia,Donbas,Donetsk na Kharkiv kote huko kumemegwa.
Na Russia alisema kama Ukraine iko tayari kukaa mezani kwaajili ya kuongelea amani basi sharti moja wapo itambue maeneo yaliyochukuliwa na Russia ni ya Russia sio ya Ukraine tena.
Na Putin kusisitiza tofauti na hapo hakuna majadiliano ya amani.
Kwa haya maelezo we unapata picha gani hapo!?