Putin ni shahidi, Mtume na Nabii wa Zama zetu. Namuunga Mkono

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
PUTIN NI SHAHIDI, MTUME NA NABII WA ZAMA ZETU. NAMUUNGA MKONO.

Na, Robert Heriel
Shahidi.

Tunaojua Dunia ilipotoka, ilipo na wapi inaenda, tutabaki kuwa Wafuasi watiifu wa falsafa za Ki-putin.

Putin ni mtakatifu, Shahidi na shujaa ambaye anaitumia nafasi na Cheo chake vizuri kutekeleza utume alioagizwa na Mungu wetu Mkuu.

Tunajua wengi wasiompenda ni Wale waliodanganywa na hila za Yule adui, hata hivyo Sisi hatuna chuki nao Kama wao walivyo na chuki nasi.

Sisi tupo kwaajili ya kuilinda dunia wao wapo kwaajili ya kuiharibu.
Tunajua Adui yetu Kama ilivyo asili yake ya uongo hutumia mbinu ya kuwapa watu Uhuru ambao tayari walikuwa nao huo Uhuru wenyewe lakini yeye akaupoka na kuwapa Uhuru bandia. Wakajiharibu Kwa mambo yenye aibu, Fedheha, na dhulma.

Sisi hatutakubali kivyovyote huyu adui awe sehemu yetu. Kama alivyoshindwa ndivyo tutakavyomshinda.
Vita hii ilianzia Rohoni na itaishia rohoni.

Falsafa zetu ni Kama ifuatavyo;

1. Tunaheshimu Asili na sheria zake.
2. Hatutaki kuingilia watu wengine na wala Sisi hatutaki mtu yeyote kutuingilia.
Tunaheshimu mipaka ya kiutamaduni, kimila, kidesturi, Kidini, lugha, miiko, mavazi, mipaka n.k.

3. Tunaamini kila jamii ni Bora Kwa nafasi yake. Na wala hakuna jamii Bora kuliko jamii nyingine.

4. Hatutaki unyonyaji, ukoloni wala Aina yoyote ya ubepari.

5. Tunaongozwa na mfumo Dume Kwa maana anayeongoza dunia ni Mungu Baba mwenye Mfumo dume.

6. Tupo tayari kupigana kufa kupona ili kulinda sheria na mipaka yetu.
7. Kamwe hatutaweza kujisalamisha Kwa mashetani. Ni akheri dunia itoweke lakini Sisi hatutokubali.

8. Tunafahamu Shetani ameungana na adui zetu wa Magharibi kupenyeza agenda zake za uongo Kwa kisingizio cha Uhuru na demokrasia. Ili kuvuruga asili ya heshima na utu wa binadamu.

10. Sisi ni matajiri halisi Kwa maana hatumdhulumu yeyote, Ila adui zetu ni masikini wakutupa na huo wanaouita Utajiri ni Utajiri bandia kwani ni wadhuluma na unyonyaji Kwa mataifa mengine.

Kundi lililonyuma ya Putin ni kubwa ingawaje wengi wao wanashindwa kuonyesha hisia na upande wao kutokana na kumhofia adui yetu aliyeungana na Shetani hivyo Hana huruma.

Putin hata afe Leo lakini ameonyesha utakatifu mkubwa na ushujaa katika ulimwengu huu.

Putin ni Shahidi, shujaa, Mtakatifu wa Zama zetu ambaye tunamshukuru MUNGU Kwa kumleta nyakati hizi tukiwa hai.

Tunapenda demokrasia lakini sio Ile demokrasia ya kishetani. Tunataka demokrasia ya Mungu Mkuu na tupo tayari kuipigania.

Tunataka demokrasia inayoonyesha ramani ya mpaka baina ya Mwanaume na mwanamke.

Hatutaki demokrasia ya kutaka wanaume wawe Kama wanawake, au wanawake wawe Kama wanaume.
Hilo tutapigana nalo kufa kupona Kwa nyakati nyakati pasipo kuchoka.

Tunataka demokrasia itakayolinda Rasilimali za dunia na kuwafanya walimwengu na viumbe kila mmoja ale Kwa urefu wa kamba yake, kadiri ya akili zake, elimu yake, jinsia yake, uwezo na kazi azifanyazo. Na sio demokrasia ya kunyonya wengine na kuwazuia wanyonge wasipate hata kile kidogo kilicho halali yao.

Tunataka demokrasia ya usiku ubaki kuwa usiku na mchana ubaki kuwa mchana. Hakuna haki sawa baina ya Magharibi na mashariki, usiku na Mchana.

Adui yupo kuvuruga hayo, na vibaraka wake wanashabikia Kama nzi wafuatao Mavi yanukayo.

Putin ndiye Nabii na mtume wa Karne ya ishirini na moja wa Zama zetu. Yeye ndiye anaweza kutuambia nini chakufanya.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Unaposema Putin ni Nabii unajua maana ya Nabii na Role yake?? Unajua Era za Manabii na Unabii ni zipi??
Unabii ulikoma baada ya Kristo tu kuzaliwa!

Heads-up.
Mimi ni team Russia

Putin ni Nabii, Mtume na Shahidi.
Na nafasi yake anaifanya vizuri Sawa na watangulizi waliomtangulia.
Putin ni Nabii ngazi za kidunia.

Aliyekuambia unabii ulikoma Enzi za Yesu ni Nani?
 
Putin ni Nabii, Mtume na Shahidi.
Na nafasi yake anaifanya vizuri Sawa na watangulizi waliomtangulia.
Putin ni Nabii ngazi za kidunia.

Aliyekuambia unabii ulikoma Enzi za Yesu ni Nani?
Umechanganya sana mambo..

Umehusisha dini, imani kwa Mungu mkuu, kuna wanaotumiwa na shetani nk nk.
Kiufupi tu, huu ni mgogoro wa kimaslahi, Purely interests. Putin anapigana kuzuia wamagharibi wasinufaike na Ukraine ili anufaike yeye.

Hayo mambo ya sijui ya wanawake kuwa wanaume Putin hana ishu nayo, huwa ana insinuate ili kupata wafuasi tu, akina nyinyi..

Ukihusisha huu mgogoro na mambo hayo ya imani, na ni kipi ni dhambi na kipi siyo dhambi, unakuwa umepuyanga mno, Putin anajirafikisha na waarabu siyo kwa sababu ya imani zao za kidini, bali ni kwa sababu ni maadui wa magharibi..

Hili andiko ndugu yangu umepuyanga sana, total rubbish!
 

Unajua kile marekani anachokitafuta Urusi au Irani au mataifa yote yenye msimamo ya kiungu?
Hakuna dini hakuna Siasa?
Huwezi itenga dini na Siasa hata ungefanyaje.

Chanzo cha Siasa ni Dini.
 
Unajua kile marekani anachokitafuta Urusi au Irani au mataifa yote yenye msimamo ya kiungu?
Hakuna dini hakuna Siasa?
Huwezi itenga dini na Siasa hata ungefanyaje.

Chanzo cha Siasa ni Dini.
Urusi nchi ya kikomunisti ina uungu gani?, Kwa nini huwezi tenga dini na siasa?
 
[emoji1666] [emoji1666] [emoji1666] Well said..
 
Urusi nchi ya kikomunisti ina uungu gani?, Kwa nini huwezi tenga dini na siasa?
Mkuu hata history wanaijua basi?? Mzee wetu Kingunge Ngombale Mwiru, ambaye taaluma yake aliipata huko Urusi alikuwa hana dini kabisa.
 
Mkuu hata history wanaijua basi?? Mzee wetu Kingunge Ngombale Mwiru, ambaye taaluma yake aliipata huko Urusi alikuwa hana dini kabisa.
Nchi za kikomunisti hawanaga dini.. Kiongozi wao ndio Mungu wao. Kama ambavyo Urusi wamegoma kumzika Lenin ili wawe wanaabudu.
 
Wanaompinga Putin ni mashabiki wa ushoga na usagaji
Too low for a legend like you!

Kwa hiyo wewe tatizo lako kubwa kabisa hapa duniani ni ushoga na usagaji, na unaamini kwamba Putin ndio mtatuzi wa tatizo hili?
 
Putin ni zaidi ya nabii, kwasababu ata hapa Tanzania kuna mijitu inajiita manabii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…