Putin ni shahidi, Mtume na Nabii wa Zama zetu. Namuunga Mkono

Tatizo mkiambiwa mtu Fulani ni Nabii mnafikiri nabii sio binadamu.
Manabii wote waliokuja Duniani walikuwa na madhaifu Yao mengi tuu kuliko huyo Putin.
Hata ukinitajia Nabii unayemuamini zaidi ninaweza kukuorodheshea madhaifu yake Kama mwanadamu WA kawaida tuu.

Putin mpaka ujue ni nabii ni mpaka umuangalie Kwa jicho la kinabii
Mimi Putin ninamkubali.

Embu nitajie Madhaifu ya Nabii Yesu
 
Nchi za kikomunisti hawanaga dini.. Kiongozi wao ndio Mungu wao. Kama ambavyo Urusi wamegoma kumzika Lenin ili wawe wanaabudu.
Acha kuandika vitu visivyo na ukweli wowote.

: Russia ni Orthodox na Putin ni muorthodox.
 
PUTIN NI SHAHIDI, MTUME NA NABII WA ZAMA ZETU. NAMUUNGA MKONO.

Na, Robert Heriel
Shahidi.

Tunaojua Dunia ilipotoka, ilipo na wapi inaenda, tutabaki kuwa Wafuasi watiifu wa falsafa za Ki-putin.

Putin ni mtakatifu, Shahidi na shujaa ambaye anaitumia nafasi na Cheo chake vizuri kutekeleza utume alioagizwa na Mungu wetu Mkuu.

Tunajua wengi wasiompenda ni Wale waliodanganywa na hila za Yule adui, hata hivyo Sisi hatuna chuki nao Kama wao walivyo na chuki nasi.

Sisi tupo kwaajili ya kuilinda dunia wao wapo kwaajili ya kuiharibu.
Tunajua Adui yetu Kama ilivyo asili yake ya uongo hutumia mbinu ya kuwapa watu Uhuru ambao tayari walikuwa nao huo Uhuru wenyewe lakini yeye akaupoka na kuwapa Uhuru bandia. Wakajiharibu Kwa mambo yenye aibu, Fedheha, na dhulma.

Sisi hatutakubali kivyovyote huyu adui awe sehemu yetu. Kama alivyoshindwa ndivyo tutakavyomshinda.
Vita hii ilianzia Rohoni na itaishia rohoni.

Falsafa zetu ni Kama ifuatavyo;

1. Tunaheshimu Asili na sheria zake.
2. Hatutaki kuingilia watu wengine na wala Sisi hatutaki mtu yeyote kutuingilia.
Tunaheshimu mipaka ya kiutamaduni, kimila, kidesturi, Kidini, lugha, miiko, mavazi, mipaka n.k.

3. Tunaamini kila jamii ni Bora Kwa nafasi yake. Na wala hakuna jamii Bora kuliko jamii nyingine.

4. Hatutaki unyonyaji, ukoloni wala Aina yoyote ya ubepari.

5. Tunaongozwa na mfumo Dume Kwa maana anayeongoza dunia ni Mungu Baba mwenye Mfumo dume.

6. Tupo tayari kupigana kufa kupona ili kulinda sheria na mipaka yetu.
7. Kamwe hatutaweza kujisalamisha Kwa mashetani. Ni akheri dunia itoweke lakini Sisi hatutokubali.

8. Tunafahamu Shetani ameungana na adui zetu wa Magharibi kupenyeza agenda zake za uongo Kwa kisingizio cha Uhuru na demokrasia. Ili kuvuruga asili ya heshima na utu wa binadamu.

10. Sisi ni matajiri halisi Kwa maana hatumdhulumu yeyote, Ila adui zetu ni masikini wakutupa na huo wanaouita Utajiri ni Utajiri bandia kwani ni wadhuluma na unyonyaji Kwa mataifa mengine.

Kundi lililonyuma ya Putin ni kubwa ingawaje wengi wao wanashindwa kuonyesha hisia na upande wao kutokana na kumhofia adui yetu aliyeungana na Shetani hivyo Hana huruma.

Putin hata afe Leo lakini ameonyesha utakatifu mkubwa na ushujaa katika ulimwengu huu.

Putin ni Shahidi, shujaa, Mtakatifu wa Zama zetu ambaye tunamshukuru MUNGU Kwa kumleta nyakati hizi tukiwa hai.

Tunapenda demokrasia lakini sio Ile demokrasia ya kishetani. Tunataka demokrasia ya Mungu Mkuu na tupo tayari kuipigania.

Tunataka demokrasia inayoonyesha ramani ya mpaka baina ya Mwanaume na mwanamke.

Hatutaki demokrasia ya kutaka wanaume wawe Kama wanawake, au wanawake wawe Kama wanaume.
Hilo tutapigana nalo kufa kupona Kwa nyakati nyakati pasipo kuchoka.

Tunataka demokrasia itakayolinda Rasilimali za dunia na kuwafanya walimwengu na viumbe kila mmoja ale Kwa urefu wa kamba yake, kadiri ya akili zake, elimu yake, jinsia yake, uwezo na kazi azifanyazo. Na sio demokrasia ya kunyonya wengine na kuwazuia wanyonge wasipate hata kile kidogo kilicho halali yao.

Tunataka demokrasia ya usiku ubaki kuwa usiku na mchana ubaki kuwa mchana. Hakuna haki sawa baina ya Magharibi na mashariki, usiku na Mchana.

Adui yupo kuvuruga hayo, na vibaraka wake wanashabikia Kama nzi wafuatao Mavi yanukayo.

Putin ndiye Nabii na mtume wa Karne ya ishirini na moja wa Zama zetu. Yeye ndiye anaweza kutuambia nini chakufanya.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Ni mtu mbinafsi na asiyejali wengine na aishiye kama wanyama pori ndio anaweza kumwona Putin kuwa mtakatifu. Unajua mateso na vifo vitokanavyo na vita isiyokuwa ya lazima ya Putin huko Ukraine?!
 
Waafrika bana tunajifanyaga kujua meeengii. Tufanyeni kazi kwa bidii ili tuwe na uwezo wa milo mitatu kwa siku ili tufurahie ngono na umbea vitu tunavyopenda kuliko chochote tukisubiria kufa.
We jamaa umemdumisha saaana mama Africa
 
Acha kuandika vitu visivyo na ukweli wowote.

: Russia ni Orthodox na Putin ni muorthodox.
Nyie mna ufinyu sana wa kuelewa, tofautisha dini rasmi ya serikali na dini za watu binafsi mmoja mmoja, mnanichosha sana nyie watu..
 
Iraq= mafuta
Iran=mafuta
Syria=mafuta
Sudan=Mafuta
Pakistan =mafuta & unga
Afghanistan =mafuta & unga
Ukraine= gas & mafuta

Marekan sio mjinga na urusi sio mjinga tusiwe mashabiki wa ovyo historia haidanganyi

Marekani ana miliki visiwa vya Hawaii na haiti hamna anaye ongea
Urusi naye anataka kumiliki Ukraine
China naye anaitaka Taiwani
[emoji2363]
Tanzania ??????
 
PUTIN NI SHAHIDI, MTUME NA NABII WA ZAMA ZETU. NAMUUNGA MKONO.

Na, Robert Heriel
Shahidi.

Tunaojua Dunia ilipotoka, ilipo na wapi inaenda, tutabaki kuwa Wafuasi watiifu wa falsafa za Ki-putin.

Putin ni mtakatifu, Shahidi na shujaa ambaye anaitumia nafasi na Cheo chake vizuri kutekeleza utume alioagizwa na Mungu wetu Mkuu.

Tunajua wengi wasiompenda ni Wale waliodanganywa na hila za Yule adui, hata hivyo Sisi hatuna chuki nao Kama wao walivyo na chuki nasi.

Sisi tupo kwaajili ya kuilinda dunia wao wapo kwaajili ya kuiharibu.
Tunajua Adui yetu Kama ilivyo asili yake ya uongo hutumia mbinu ya kuwapa watu Uhuru ambao tayari walikuwa nao huo Uhuru wenyewe lakini yeye akaupoka na kuwapa Uhuru bandia. Wakajiharibu Kwa mambo yenye aibu, Fedheha, na dhulma.

Sisi hatutakubali kivyovyote huyu adui awe sehemu yetu. Kama alivyoshindwa ndivyo tutakavyomshinda.
Vita hii ilianzia Rohoni na itaishia rohoni.

Falsafa zetu ni Kama ifuatavyo;

1. Tunaheshimu Asili na sheria zake.
2. Hatutaki kuingilia watu wengine na wala Sisi hatutaki mtu yeyote kutuingilia.
Tunaheshimu mipaka ya kiutamaduni, kimila, kidesturi, Kidini, lugha, miiko, mavazi, mipaka n.k.

3. Tunaamini kila jamii ni Bora Kwa nafasi yake. Na wala hakuna jamii Bora kuliko jamii nyingine.

4. Hatutaki unyonyaji, ukoloni wala Aina yoyote ya ubepari.

5. Tunaongozwa na mfumo Dume Kwa maana anayeongoza dunia ni Mungu Baba mwenye Mfumo dume.

6. Tupo tayari kupigana kufa kupona ili kulinda sheria na mipaka yetu.
7. Kamwe hatutaweza kujisalamisha Kwa mashetani. Ni akheri dunia itoweke lakini Sisi hatutokubali.

8. Tunafahamu Shetani ameungana na adui zetu wa Magharibi kupenyeza agenda zake za uongo Kwa kisingizio cha Uhuru na demokrasia. Ili kuvuruga asili ya heshima na utu wa binadamu.

10. Sisi ni matajiri halisi Kwa maana hatumdhulumu yeyote, Ila adui zetu ni masikini wakutupa na huo wanaouita Utajiri ni Utajiri bandia kwani ni wadhuluma na unyonyaji Kwa mataifa mengine.

Kundi lililonyuma ya Putin ni kubwa ingawaje wengi wao wanashindwa kuonyesha hisia na upande wao kutokana na kumhofia adui yetu aliyeungana na Shetani hivyo Hana huruma.

Putin hata afe Leo lakini ameonyesha utakatifu mkubwa na ushujaa katika ulimwengu huu.

Putin ni Shahidi, shujaa, Mtakatifu wa Zama zetu ambaye tunamshukuru MUNGU Kwa kumleta nyakati hizi tukiwa hai.

Tunapenda demokrasia lakini sio Ile demokrasia ya kishetani. Tunataka demokrasia ya Mungu Mkuu na tupo tayari kuipigania.

Tunataka demokrasia inayoonyesha ramani ya mpaka baina ya Mwanaume na mwanamke.

Hatutaki demokrasia ya kutaka wanaume wawe Kama wanawake, au wanawake wawe Kama wanaume.
Hilo tutapigana nalo kufa kupona Kwa nyakati nyakati pasipo kuchoka.

Tunataka demokrasia itakayolinda Rasilimali za dunia na kuwafanya walimwengu na viumbe kila mmoja ale Kwa urefu wa kamba yake, kadiri ya akili zake, elimu yake, jinsia yake, uwezo na kazi azifanyazo. Na sio demokrasia ya kunyonya wengine na kuwazuia wanyonge wasipate hata kile kidogo kilicho halali yao.

Tunataka demokrasia ya usiku ubaki kuwa usiku na mchana ubaki kuwa mchana. Hakuna haki sawa baina ya Magharibi na mashariki, usiku na Mchana.

Adui yupo kuvuruga hayo, na vibaraka wake wanashabikia Kama nzi wafuatao Mavi yanukayo.

Putin ndiye Nabii na mtume wa Karne ya ishirini na moja wa Zama zetu. Yeye ndiye anaweza kutuambia nini chakufanya.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mashoga wa western ya matombo na nyakanazi watakuja kukukashifu hapa
 
Kwani serikali za kikomunisti peke yake ndizo hazina dini ?
Hapana, kuna serikali zisizo za kikomunisti pia hazina dini, lakini serikali ikishakuwa ya kikomunisti, maana yake dini yake ndio huo ukomunisti, kumbuka, ujamaa ni imani.

Lakini Urusi siku hizi wamekuwa kama wabepari, wameacha kufuata sera za ukomunisti walizoachiwa na Mungu wao Lenin!
 
Jambo la msingi ni kuwa Lenin, Mao hawa sio miungu wa China, Russia bali wana pewa heshima ya uasisi wa mataifa yao na sio kuabudiwa.
 
Mashoga wa western ya matombo na nyakanazi watakuja kukukashifu hapa
Kuita watu wataomchalenji ni mashoga ni uoga, ni kutaka kuwafrustrate chalengers ili waogope kuja kujibu hoja. Infact, mtu anaeleta hoja za ushoga kwenye huu mgogoro ni mtu mwenye akili finyu..

Putin na westerners wanapambania maslahi mapana ya nchi zao, sisi waafrika tunachoona ni ushoga tu.
 
Jambo la msingi ni kuwa Lenin, Mao hawa sio miungu wa China, Russia bali wana pewa heshima ya uasisi wa mataifa yao na sio kuabudiwa.
Kukataa kumzika mtu aliyekwisha kufariki, mtu kumuweka kama maonyesho miaka nenda rudi, Ni kumuabudu. Mbona sisi Nyerere tumemzika, kwani hatumpi heshima ya uasisi?

Kule North Korea, hata mtu akioa, anaenda na mchumba wake kwenye maiti ya Kim Il Sung ili kupata baraka, hiyo ni kumuabudu.
 
Unajichanganya sana.
Putin anapigania sana kuhusu huu mgogoro.
Putin alianza kuivamia Georgia akaja Crimea. Je kawamaiza hao mashetani huko kote? Kama bado hapo Ukraine atawamaliza?

West ni mashetani na wewe ni msabato dini iliyoanzishwa na mama wa kimarekani ambako mashetani wapo.
Kwanini usifuate dini ya mtume ambaye unampigia chapuo hapa?

Putin anapigania interest zake yeye binafsi na ma Oligarc kadhaa hapo Urusi hata warusi wenyewe hii vita hawaitaki. Acha kuleta upuuzi wa dini.
I see, I see, I see! Umemaliza.

Nilikuwa sijampata vizuri, kumbe Msabato!
Wasabato wanafundishwa kwamba Marekani ni shetani, kwamba kwenye 666, sita Moja ni Papa, sita ta pili ni Umoja wa mataifa na sita ya maisho ni Marekani.

Kwa hiyo hapa ndiyo anakamilika shetani ambaye ni 666., na kwa hiyo yeyote anayepingana na UN na marekani anapingana na shetani. Lakini umemkumbusha vizuri, mwenezaji wa Usabato Ellen G White ni mmarekani.

Ooops! Wasabato hawahawa walitukalia tako wazi kutuambia kwamba mwaka 2000 ndiyo mwisho wa dunia!

Ni jambo la kusikitisha kwa kijana mwenye IQ kama ya ROBERT HERIEL kuamini mambo ya kipuuzi kama haya.
Alaaniwe aliyeleta hizi dini za hovyo.
 
Mkuu, naunga hoja. Japo inasikitisha, kwakuwa hakuna sababu yoyoye inayo halalisha vifo, majeruhi, ukimbizi na mtafaruku unaosababisha watu kukimbia makazi yao.

WAUNGWANA WANASEMA, UKITAKA KUTAWALA JAMII YOYOTE, HAKIKISHA JAMII HUSIKA INASAHAU/INAPOTEZA ASILI YAKE, KUTOJALI MILA, TAMADUNI, DESTURI, MIIKO NA MAADILI YA WALIOWATANGULIA (MABABU ZAO).

ZELENSKY kwa kuungwa mkono na Magharibi, alianza jukumu hilo kwa Jamii ya Warusi waliopo Ukraine. Lengo kumsogeza NATO mpakani na URUSI.

Kosa kubwa la Waukraine ni kushawishika kukubali NATO/EU na URUSI kupambana katika ardhi yao. Na mwisho wa vita haijulikani itakuwaje.

Mwenyezi MUNGU awanusuru
.
 
Back
Top Bottom