Putin sio tu ni tishio kwa usalama wa nchi za Ulaya na Marekani, bail sasa ni tishio kwa uchumi wa hizi nchi, hivyo ikibidi wataungana kumuondoa

Putin sio tu ni tishio kwa usalama wa nchi za Ulaya na Marekani, bail sasa ni tishio kwa uchumi wa hizi nchi, hivyo ikibidi wataungana kumuondoa

Uko sahihi utakuta mtu ana sema Russia kashindwa wakati lengo kuu ni kutokuwa na mpaka na ukraine na kafanikiwa
Hawa wanatumia akili ya kisiasa kuchanganua mambo ya kiusalama. Akili ya namna hii wanayo viongozi wa sasa wa magharibi na mchambuzi mmoja wa Marekani alisema hii inatokana na viongozi wengi wa sasa hawajui historia ya miaka ya nyuma, wanachofahamu wao ni kulewa ule ukubwa wa nchi zao zilipofikia. Hii imesababisha wanafanya maamuzi yenye kuleta hatari kubwa kwa usalama wa nchi zao na hata dunia kwa ujumla.

Japan ni nchi ambayo iliyopiga hatua kiteknolojia tangu karne za nyuma. Karne zilizopita waliongoza hata kwa uuzaji wa bunduki bora duniani. Sababu kuu iliyopelekea Japan kuingia ww2 ni vita ya kiuchumi waliyopigwa kuwekewa vikwazo. Hii ilimfanya Japan awe upande wa Hitler na kuingia vitani.

Hivi ndivyo historia inavyotueleza. Vita ya vikwazo vya kiuchumi huzalisha vita halisi vya kutoana damu. Kwa sababu watu wataona hawana cha kupoteza.

Kipindi cha Cold war baada ya ww2 Marekani kupiga mabomu ya nuclear Japan wanasayansi wa Kisovieti wakishirikiana na wengine wa Kijerumani walikuwa tayari wameshaingia kwenye program ya kupata nao bomu la nuclear. Russia ilitumia mpaka majasusi nchini Marekani ili kupata siri za nuclear yaani formula yake.

Wengi wanadhani ni majasusi ndiyo waliyofanikisha Soviet kupata formula ya mabomu ya nuclear. Lakini ukweli ni kuwa si wao! Ni wanasayansi wa Marekani ndiyo waliyotoa siri kwa wanasayansi wa Kisovieti. Kwa sababu tayari walishaiona hatari ya dunia inapoelekea kwa mmoja kumiliki mabomu hatari na tayari hakusita na hakuonyesha kusita kuyatumia. Lengo la wanasayansi ni kuifanya dunia iwe na balance.

Sasa hii balance ndiyo wanasiasa wanajaribu kuiharibu kwa kasi ya ajabu. Hawafahamu vita wanachojua ni kutuma wanajeshi waende vitani. Hawafahamu athari ya mabomu. Kwa vile nchi zao wamezikuta zimeshakuwa kubwa wanajiona nyundo kila tatizo mbele yao ni msumari.

Mgogoro wa Cuba kipindi cha cold war kwa Amerika hauna tofauti na mgogoro wa Ukraine kwa Russia. Lakini haya yote kwa dunia ya sasa yanafanyika kwa nini? Ili kuifuta Russia? Hivyo watu inawabidi wafahamu: Falsafa ya kusema nchi huru ni uhuru uliyo ndani ya mipaka yako ya nchi, ukishatoka nje huko kuna sera za wabwana wakubwa. Chezea maslahi yao watakuchezea vizuri tu. Kinachotakiwa nchi ni kuifahamu nafasi yake.

Na matokeo ya kushinda ama kushindwa kwa Russia yatatokana na makusudio yao waliyoyaweka. Ninachofahamu mimi alichokisema Putin ni kwamba: Kinachofanyika Ukraine ni special military operation. Russia haina malengo ya kuikalia maeneo ya Ukraine bali ni kama sio kuondoa ni kupunguza nguvu za kijeshi za Ukraine kwa kupiga kambi za jeshi na miundombinu yake. Pia, kuwaondoa Nazi nchini Ukraine. Kwa haya naona amefanikiwa.

Kingine ninachokiona ni bora Zelensky akubali mapema majimbo yaliyojitenga nchini mwake yawe nchi mapema. Kwa sababu kinachonekana yale majimbo kwa sasa hivi yanazidi kuongeza kilometer za mraba siku baada ya siku. Nahofia wasije wakapata eneo kubwa sana la ardhi kwani litakuwa pigo kubwa sana kwa Ukraine kwa ujinga wa Rais wao Zelensky.
 
Baada ya mambo kuwa magumu, hii sasa wanaiita ni military operation na sio vita!

Only fools will understand this.
 
mkishashiba munajisikia tu kuandika ugoro
hongera muandishi kwakunipotezea muda wangu ila ujue tu yakwambaa
RUSSIA sio ZIMBABWE
 
Mwanzoni Putin alionekana ni tishio zaidi kwa usalama wa nchi za Magharibi na Marekani, ila sasa anaonekana ni tishio pia kwa ustawi wa maisha ya watu katika mataifa haya(kiuchumi na kijamii) kupitia swala la gesi na hili halitomuacha salama.

Hili swala la gesi linaongeza sababu za mataifa haya kumuona Putin ni tishio kwa ustwai wa watu wao na pia kwa ustawi wa kiuchumi katika mataifa haya, hivyo lazima watafute namna ya kumshughulikia na ikibidi kumuondoa madarakani.

Unapoona Marekani kajiingiza mahal kijeshia au vinginevyo, basi ujue hapo kuna masilahi ya kiuchumi au sababu za kiusalama na hizi ndio sababu za Marekani kujiingiza katika mataifa ya Kiarabu na ikibidi hata kupigana vita waweke watawala ambao watakuwa vibaraka wao.

Kwa msingi huo, Putin kwa sasa lazima aondolewe kwa kutengenezewa fitina za kisiasa nchi mwake au kugombanishwa na wananchi wake kwa uchumi wa nchi yake kuvurugwa kupitia vikwazo, n.k.

Akiendelea kuwa kiburi huku akiendelea kutishia usalama na ustawi wa watu katika nchi hizi, basi atatafutiwa sababu kama zile za Saddam Hussein kuhalalisha uvamizi wa NATO na Marekani kumuondoa madarakani kwa gharama yoyote.

Kwa sasa mataifa haya yanaweza kuwa na mipango ya siri kumkabili Putin katika vita ya nyuklia ili kupunguza au kuondoa kabisa uwezekano wa Russia kutumia nyuklia au hata akizitumia, madhara yasiwe makubwa (wanawwza kumuwahi na kumvuruga kabisa au vinginevyo).

Wacha tusubiri.
Wewe uko dunia ipi, unaaambiwa russia sasaiv ata miezi 4 bado wanapanga foleni kununua 2kgs za sukari kwa mteja mmoja na si zaidi ya hapo

Huo uchumi unaoporoja hapa ataupata wapi?
 
Wewe uko dunia ipi, unaaambiwa russia sasaiv ata miezi 4 bado wanapanga foleni kununua 2kgs za sukari kwa mteja mmoja na si zaidi ya hapo

Huo uchumi unaoporoja hapa ataupata wapi?
Read between lines.
 
Mwanzoni Putin alionekana ni tishio zaidi kwa usalama wa nchi za Magharibi na Marekani, ila sasa anaonekana ni tishio pia kwa ustawi wa maisha ya watu katika mataifa haya(kiuchumi na kijamii) kupitia swala la gesi na hili halitomuacha salama.

Hili swala la gesi linaongeza sababu za mataifa haya kumuona Putin ni tishio kwa ustwai wa watu wao na pia kwa ustawi wa kiuchumi katika mataifa haya, hivyo lazima watafute namna ya kumshughulikia na ikibidi kumuondoa madarakani.

Unapoona Marekani kajiingiza mahal kijeshia au vinginevyo, basi ujue hapo kuna masilahi ya kiuchumi au sababu za kiusalama na hizi ndio sababu za Marekani kujiingiza katika mataifa ya Kiarabu na ikibidi hata kupigana vita waweke watawala ambao watakuwa vibaraka wao.

Kwa msingi huo, Putin kwa sasa lazima aondolewe kwa kutengenezewa fitina za kisiasa nchi mwake au kugombanishwa na wananchi wake kwa uchumi wa nchi yake kuvurugwa kupitia vikwazo, n.k.

Akiendelea kuwa kiburi huku akiendelea kutishia usalama na ustawi wa watu katika nchi hizi, basi atatafutiwa sababu kama zile za Saddam Hussein kuhalalisha uvamizi wa NATO na Marekani kumuondoa madarakani kwa gharama yoyote.

Kwa sasa mataifa haya yanaweza kuwa na mipango ya siri kumkabili Putin katika vita ya nyuklia ili kupunguza au kuondoa kabisa uwezekano wa Russia kutumia nyuklia au hata akizitumia, madhara yasiwe makubwa (wanawwza kumuwahi na kumvuruga kabisa au vinginevyo).

Wacha tusubiri.
Sio rahisi Putin kuondolewa kama unavyofikiri
 
Tanzania tuna shida sana ujuaji umetuzidi sana hata kama wakiungana haiwezi kuwa rahisi kama unavyofikili Russia sio sio dhaifu kama unavyofikili wewe, hatua moja ya West wakikosea tu wamepoteza kumbuka mbinu hizi zinazoendelea ndo sababu ya kuibuka WW2 nakukumbusha mifumo iliyopo inaumiza nchi nyingi endapo Russia ikiwa mbele zidi ya West wengi watakua Russia ili kuangusha western block
 
Back
Top Bottom