RTI
JF-Expert Member
- Dec 20, 2018
- 2,423
- 7,155
Kwa hiyo ww hoja yako ni ipi?Kwahiyo nchi kuundiwa tume ni dalili za uimara? Mnapenda sifa za kijinga, kina Somalia na Rwanda wanaundiwa tume wakati wamejaaa utapiamlo nyinyi mnaona kuundiwa tume ni ushujaa.
Huwezi itenga Russian Federation na USSR au Russian empire. Hatuwezi kuwa tunazungumzia nchi iliyoanzishwa 1991 hapo eti ndio unaita iko stable. Lazima turudi nyuma kuihusisha ilivyokuwa, huwezi taka tusizungumzie uhuru wa Tanganyika au mapinduzi ya Zanzibar kisa hizi nchi ziliungana kwahiyo tufute kila kitu tuanzie 1964.
Unajua Russia inaadhimisha siku ya VDV lini? August 2 kuadhimisha siku ya kuanzisha first paratrooper division mwaka 1930. Hapo Russia Federation hii ilikuwepo?
Victory Day parade huwa ni May 9 kuadhimisha ushindi dhidi ya Nazi Germany mwaka 1945. Huo mwaka 1945 hii Federation ilikuwepo? Then why nchi ina matukio yote na maadhimisho, na wimbo wa taifa, na silaha na mikataba ambavyo vyote ni legacy ya USSR alafu kirahisi tu unasema tuachane na USSR. Kwamba wewe ni mjanja na wao wajinga kuitambua.
Unataka tuzungumzie kuanzia 1991 eti nchi ni stable alafu unaiita superpower. Kina Sweden ambao Freedom of Speech na Press kwenye katiba yao waliweka mwaka 1766 si tutasema wametoka nje ya dunia
Kuwa Putin akifa au akiondoka madarakani Urusi itasambaratika au itaingia kwenye machafuko? Ebu weka mambo wazi unacho taka kumaanisha maana kuna kitu una taka kukimaanisha ila unazunguka mkuu.