Puuzeni taarifa ya Nipashe, hakuna uchotaji fedha BoT

Puuzeni taarifa ya Nipashe, hakuna uchotaji fedha BoT

Kila siku uko mbio kuleta maelezo marefu hapa lakini ukiulizwa maswali hutoi majibu, unakuja na maelezo ya kisiasa kudanganya wajinga ukidhani hili ni jukwaa la robots, kama unajiamini kweli tulia hapo utoe majibu ya maswali unayoulizwa.

Kaa chini ujiulize kwanini ni wizara yako ndio inayohusishwa na mambo ya hovyo zaidi badala ya wizara nyingine? usitake kutuaminisha hao wanaosema mabaya yanayohusu wizara yako wanakuchukia personally, ukweli una tatizo bahati yako unalindwa na your incompetent boss.

Mpina amekuwa akitoa mapungufu mengi kukuhusu kule bungeni, ukaishia kumjibu hovyo badala ya kumjibu kwa weledi, baadae ukashangilia sana kwa kugonga meza siku ile aliyoadhibiwa na yule spika mbovu anayewatumikia mafisadi.

Leo Mpina yuko nje ya buinge, ajabu bado wizara yako inahusishwa na madudu kila siku, umekuwa wa kujitokeza na kukanusha kama ndio mtindo mpya wa maisha yako huku ukiogopa kujibu maswali yetu, ukijidanganya huo ndio utendaji, utendaji gani wa kiuoga!, acha usanii.

Naamini kesho tena utakuja kukanusha kingine, waziri wa fedha unayeona sifa kujiita unakuposheka!.
Nasikita tumepata bahati mbaya kuwa na viongozi wapigaji awamu hii.
 
PUUZENI TAARIFA YA NIPASHE, HAKUNA UCHOTAJI FEDHA BOT, HUU NI MWENDELEZO WA KUZUA TAHARUKI KWA MAKUSUDI, BOT INASIMAMIA KWA UMAKINI SANA SHERIA ZA NCHI NA MIIKO YA BENKI KUU ZOTE DUNIANI.

Nimesoma taarifa hiyo ambayo inatokana na uchambuzi wa NGO iitwayo WAJIBU inayoongozwa na Mzee Ludovic Uttoh, CAG Mstaafu. Kwa ujumla maelezo ya taarifa hiyo yanaeleweka na hayana utata wowote, hivyo sijui kwa nini mwandishi wa Nipashe ameeleza kuwa KUNA UTATA BoT.

Taarifa imeelezea suala ambalo ni la kawaida na huwa linafanyika kila mwaka kutokana na Sheria ya BoT inayoruhusu kutoa advances or Short Term Loans kwa Serikali ili kukidhi mahitaji ya matumizi ambayo yanakuwa hayajapata mapato. Kwa mujibu wa kifungu cha 34 hadi 37 cha BoT Act, Serikali inaruhusiwa kukopa hadi 18% ya makusanyo halisi ya ndani ya mwaka uliopita. HILI LIMEKUWA LIKIFANYIKA HIVYO TANGU BOT IANZISHWE, BOT NI BENKI YA SERIKALI, SERIKALI UCHUKUA ADVANCE KWA MUJIBU WA SHERIA BADALA YA KUKOPA KWA RIBA KUBWA KUTOKA BENKI ZA KIBIASHARA.

Hivyo, kwa mwaka 2022/23, Serikali ilikuwa inaweza kukopa BoT kiasi kinachofikia TZS. 4.5 trillion. Hivyo, taarifa ya kuwepo kwa mkopo wa TZS. 1.7 trilioni ni suala ambalo liko ndani ya wigo unaokubalika kisheria. Kiasi hicho kilipofika mwisho wa Mwaka kilijumuishwa kwenye Treasury Bonds za Mwaka husika ambazo zinaendelea kulipia riba kama sehemu ya mikopo ya ndani.

Utaratibu huo ni wa kawaida na ufanyika kwa Benki Kuu za nchi nyingi duniani, pindi Serikali inapohitaji Fedha za kugharamia Bajeti wakati bado inaendelea kujipanga na kukusanya mapato kutoka katika vyanzo mbalimbali. Ndio maana hata IMF waliridhika kuwa BoT na Serikali wamezingatia Sheria na taratibu za kimataifa kama inavyotakiwa. Kutokana na uzingatiwaji wa Sheria hizo, Bodi ya IMF waliridhia kutoa USD. 300 milioni kwa mwaka 2023/24 na Benki ya Dunia waliridhia kutoa USD. 750 milioni kwa mwaka 2023/24 kwa kuwa tathmini ya Pili ya program ya IMF iliyofanyika Desemba 2023 iliangalia masuala mbalimbali yakiwemo ya mapato, matumizi, madeni, uzingatiwaji wa Sheria ya BoT, ukuaji wa uchumi, mfumuko wa bei, urari wa biashara, thamani ya shilingi na usimamizi wa masoko ya fedha nchini.

Kutokana na maelezo haya, nadhani mwandishi wa gazeti la Nipashe hakupaswa kusema kuwa kuna utata BOT tena bila hata kuulizia au kuomba ufafanuzi kutoka BoT. Inawezekana aliandika kwa nia ovu ya kuupotosha umma, kuidhalilisha BoT na kusababisha taharuki kwa jamii. Aidha, inawezekana mwandishi ameandika kwa kutojua Sheria suala ambalo angeuliza angepewa ufafanuzi unaotakiwa.

Kutokana na maelezo hayo, BoT itaandaa taarifa kwa umma na kukanusha na kutoa elimu kuwa hakuna utata wowote uliopo kutokana na taarifa hizo bali ni suala la kawaida ambalo Serikali inaruhusiwa kukopa kwa kuzingatia ukomo wa 18% ya mapato halisi ya mwaka uliopita, kama ilivyo kwa Sheria za nchi nyingine duniani. Hata ukomo huu upo kwenye viwango karibiana kati ya Nchi zote za EAC.

View attachment 3047891
Mtuhumiwa anasema tupuuze taarifa ambazo yeye ndiye muhusika. Zile za EPA walificha mwishowe wakampeleka Balali uhamishoni na kudai amekufa.
 
Ukoo wa panya huu, hizi tabia za uizi hazianzi ukubwani..udokozi ulianza utotoni..haya ni matokeo ya kuulea ujinga. Msubiri ulimwengu uwafunze kuna siku mtapata akili uzeeni mwenu. kwanini mnaiba aisee!!?...mmeapa kwa Biblia na Quran mkiwa mmezinyenyua juu....why mna dharau na imani zenu?...inamaana Biblia na Quran zimewabariki ninyi tu kuiba mali??
 
Tumshukuru kwa uwepo wake jf, Waziri kuingia jf na kujibu hoja sii miongoni mwa wajibu wake!, Waziri hawajibiki jf, hivyo uwepo wake humu ni ametuheshimu sana, turudishe heshima, Mawaziri zaidi waingie, juzi nimemuona Gerson Msigwa , hii ni heshima kubwa kwa jf.
P
Kuna wakati hata mmoja aliwahi kuombwa kuingia hapa jf, kwanza si yupo hapa jf kabla ya huo uwaziri wake.
Ameleta hoja ijadiliwe nae awepo kwenye hoja, ameleta taarifa, awepo kwenye mjadala wa taarifa, ameleta ufafanuzu awepo kwenye kufafanua kwa kina.
 
Tumshukuru kwa uwepo wake jf, Waziri kuingia jf na kujibu hoja sii miongoni mwa wajibu wake!, Waziri hawajibiki jf, hivyo uwepo wake humu ni ametuheshimu sana, turudishe heshima, Mawaziri zaidi waingie, juzi nimemuona Gerson Msigwa , hii ni heshima kubwa kwa jf, lets be appreciative.
P
Hawajibiki kwa jf kivipi we mzee! Anawajibika kwa wananchi, na jf tupo wananchi. Sasa tumshukuru vipi kwa kutimiza wajibu wake!! Yeye ndio anapaswa aishukuru jf kwakuwa ni platform iliyompa wasaa wa kuweza kuwajibika kwa wananchi.
 
PUUZENI TAARIFA YA NIPASHE, HAKUNA UCHOTAJI FEDHA BOT, HUU NI MWENDELEZO WA KUZUA TAHARUKI KWA MAKUSUDI, BOT INASIMAMIA KWA UMAKINI SANA SHERIA ZA NCHI NA MIIKO YA BENKI KUU ZOTE DUNIANI.

Nimesoma taarifa hiyo ambayo inatokana na uchambuzi wa NGO iitwayo WAJIBU inayoongozwa na Mzee Ludovic Uttoh, CAG Mstaafu. Kwa ujumla maelezo ya taarifa hiyo yanaeleweka na hayana utata wowote, hivyo sijui kwa nini mwandishi wa Nipashe ameeleza kuwa KUNA UTATA BoT.

Taarifa imeelezea suala ambalo ni la kawaida na huwa linafanyika kila mwaka kutokana na Sheria ya BoT inayoruhusu kutoa advances or Short Term Loans kwa Serikali ili kukidhi mahitaji ya matumizi ambayo yanakuwa hayajapata mapato. Kwa mujibu wa kifungu cha 34 hadi 37 cha BoT Act, Serikali inaruhusiwa kukopa hadi 18% ya makusanyo halisi ya ndani ya mwaka uliopita. HILI LIMEKUWA LIKIFANYIKA HIVYO TANGU BOT IANZISHWE, BOT NI BENKI YA SERIKALI, SERIKALI UCHUKUA ADVANCE KWA MUJIBU WA SHERIA BADALA YA KUKOPA KWA RIBA KUBWA KUTOKA BENKI ZA KIBIASHARA.

Hivyo, kwa mwaka 2022/23, Serikali ilikuwa inaweza kukopa BoT kiasi kinachofikia TZS. 4.5 trillion. Hivyo, taarifa ya kuwepo kwa mkopo wa TZS. 1.7 trilioni ni suala ambalo liko ndani ya wigo unaokubalika kisheria. Kiasi hicho kilipofika mwisho wa Mwaka kilijumuishwa kwenye Treasury Bonds za Mwaka husika ambazo zinaendelea kulipia riba kama sehemu ya mikopo ya ndani.

Utaratibu huo ni wa kawaida na ufanyika kwa Benki Kuu za nchi nyingi duniani, pindi Serikali inapohitaji Fedha za kugharamia Bajeti wakati bado inaendelea kujipanga na kukusanya mapato kutoka katika vyanzo mbalimbali. Ndio maana hata IMF waliridhika kuwa BoT na Serikali wamezingatia Sheria na taratibu za kimataifa kama inavyotakiwa. Kutokana na uzingatiwaji wa Sheria hizo, Bodi ya IMF waliridhia kutoa USD. 300 milioni kwa mwaka 2023/24 na Benki ya Dunia waliridhia kutoa USD. 750 milioni kwa mwaka 2023/24 kwa kuwa tathmini ya Pili ya program ya IMF iliyofanyika Desemba 2023 iliangalia masuala mbalimbali yakiwemo ya mapato, matumizi, madeni, uzingatiwaji wa Sheria ya BoT, ukuaji wa uchumi, mfumuko wa bei, urari wa biashara, thamani ya shilingi na usimamizi wa masoko ya fedha nchini.

Kutokana na maelezo haya, nadhani mwandishi wa gazeti la Nipashe hakupaswa kusema kuwa kuna utata BOT tena bila hata kuulizia au kuomba ufafanuzi kutoka BoT. Inawezekana aliandika kwa nia ovu ya kuupotosha umma, kuidhalilisha BoT na kusababisha taharuki kwa jamii. Aidha, inawezekana mwandishi ameandika kwa kutojua Sheria suala ambalo angeuliza angepewa ufafanuzi unaotakiwa.

Kutokana na maelezo hayo, BoT itaandaa taarifa kwa umma na kukanusha na kutoa elimu kuwa hakuna utata wowote uliopo kutokana na taarifa hizo bali ni suala la kawaida ambalo Serikali inaruhusiwa kukopa kwa kuzingatia ukomo wa 18% ya mapato halisi ya mwaka uliopita, kama ilivyo kwa Sheria za nchi nyingine duniani. Hata ukomo huu upo kwenye viwango karibiana kati ya Nchi zote za EAC.

View attachment 3047891
Tunajua yote kuwa fedha ya umma unachukua unaenda kuwapa ihefu kununua timu na kuwalipa mishahara wachezaji.
Muda utafika tu mwigulu
 
mtuhumiwa anasema tupuuze taarifa ambazo yeye ndiye muhusika. Zile za EPA walificha mwishowe wakampeleka Balali uhamishoni na kudai amekufa.
Hii nchi ngumu sana siku hizi wamekuwa malaika watoa roho yaani hivi hivi wanamficha DEA BALALI governor na kusema amekufa kuepuka fedheha

Huyu mzee skendo ni nyingi ni bora tu ajiuzulu nafasi yake
 
ila we mzee naamini kabisa utaanza kuchomwa hapa hapa duniani yaani utaanza kuteseka hapa hapa duniani halafu kuzimu ni muendelezo tu
Hivi hizo hela mnazoiba hamuwaonei huruma watanzania?
Mamilioni ya watoto wa kitanzania wanasoma shule chakavu hapa nchini, huduma za afya ni ghali sana kwa mwananchi wa kawaida, mfumuko wa bei ni mkubwa sana kwa maisha ya Sasa, miradi lukuki inasuasua na kama inatekelezwa basi sio kwa wakati kwa sababu ya ufisadi, WIZI, uhujumu na ubadhirifu uliopitiliza uovu, lakini nyie mnaona sawa tu mateso ya watanzania kunufaisha matumbo

MUNGU ninayemuani ni mkuu sana hakika hataacha haya yapite katika JINA LA YESU KRISTU ALIYE HAI

kila kilichofichwa kitafunuliwa na hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe
Mbona kuvuga mambo sasa...
 
Back
Top Bottom