Pwani: Ajali ya Magari imeua Watu 21 na wengine 15 kujeruhiwa. Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi

Pwani: Ajali ya Magari imeua Watu 21 na wengine 15 kujeruhiwa. Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi

Kuna tetesi kuwa kuna ajali imetokea huko mkoani Pwani wilaya ya Mkuranga, Gari ya kampuni ya Dangote imegongana uso kwa uso na gari aina ya Costa.

Sent from my itel S32 using Tapatalk

=====

Watu 18 wamefariki na wengine 15 kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana katika kijiji cha Kilimahewa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Aprili 15, 2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amesema ajali hiyo imehusisha lori na gari la abiria aina ya Toyota Coaster.

“Ni Kweli tuko kwenye eneo la tukio, ajali imetokea na imesababisha vifo vya watu 18 na majeruhi 15,” amesema Lyanga.

Amesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi baada ya Coaster hiyo iliyokuwa ikitokea mikoa ya Kusini kwenda Dar es Salaam iligongana na lori hilo lililokuwa likitokea Kimanzichana.

Kamanda Lyanga amesema majeruhi katika ajali hiyo wamepelekwa katika kituo cha afya cha Kilimahewa.
Subhana'Allaah, Allah awafanyie tahfifu majeruhi wa ajali na awarehemu marehemu wote
 
Barabara ina mashimo sana japo ni lami..kwa wale waliopita njia hiyo hivi karibuni ni mashahidi,ni kugombea nani apite sehemu nzuri..japo mwendo kasi pia ni tatizo,hizo Coaster za Ikwiriri zinamwagika sana..
 
Mbona kila wakati ni Dangote, Dangote, amewekeza Sana kwenye damu nini! Mbona kampuni zingine hatusikii Sana kuhusu ajali!!? Hapana buana!! Ndo kusema kwamba anamagari mengi Sana yanayotembea barabarani Kwa siku!! Mmmmh,!
 
Kuna nini madereva wa gari za Dangote? mbona matukio ya ajali za haya magari ni mengi? Nashauri kitengo kinachohusika Traffic kikawafanyie usahili hao madereva wa Dangote kuthibitisha kama wana weledi wa kuitwa madereva
Lakini ukiangalia hii picha si gari ya dangote angawa mtoa taarifa ametaja gari ya dangote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habarini za Asubuhi wana pwani yetu.

Naomba kuwajuza kuwa Mkuranga kumetokea ajali mbaya sana ambayo imepoteza maisha ya ndugu zetu zaidi ya ishirini Asubuhi hii.

Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom