pye Chang shen
JF-Expert Member
- Jul 11, 2016
- 11,422
- 6,108
Poleni sana wote
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pale kilimahewa mbona pako vizuri tu tena Hakuna kona wala mashimo
Sent using Jamii Forums mobile app
Hio ni Rosa, huwa ina cabin ndefu zaidi na viti vingi zaidi.Coaster ina uwezo wa kubeba abiria 22-25, sasa hiyo number ya majeruhi + marehemu unapata thelathini na ushehe plus ambao hawajajeruhiwa unapata ngapi?
Huwa nashindwa kabisa kuelewa mambo haya.yanapopamba moto kila uchaguzi mkuu.unapokaribiaTulikuwa tumesha sahau haya mambo ya ajali ila naona yameanza kurudi kwa kasi ya 5g
Duuu!!! Poleni Sana.Hii ajali nimempoteza kaka yangu na binamu wa huyo kaka.
Kaka yangu(best ya kaka wa kuzaliwa tumbo moja) alikua dereva wa hiyo Rosa na binamu yangu kondakta..
Pia tumewapoteza matajiri wa kijiji cha magawa BM na Mfaume binadamu wabaya sana wamechukua pesa zote 1.6 alizokua nazo marehemu Kaka,BM awamemchukulia pesa zote 2.8M na Mfaume 6M walizokua wanafuata bidhaa mjini, watu wameanza kuchukua hela kabla ya kutoa msaada Mungu awalaani wote.
Msiba ulikua mkubwa sana kijiji kilizizima watu ilibidi tujigawe katika kuzika wengine walienda huku wengine kule gari ya maiti ilikua inashusha maiti hapa wengine wanabaki wengine wanaenda hivyo hivyo mpaka mwisho.
Chanzo cha ajali
Kuliko na gari mbili moja Rosa maarufu kwa jina la Mchilu(iliyokua inaendeshwa na marehemu) na nyingine Coaster(box maarufu kwa jina la Mama Peter) hizi gari zilikua zinafukuzana Mama Peter Mbele na Mchilu nyuma.Walipofika kilima hewa Mama Peter alisimama njiani bila kutoka kwenye barabara kuchukua abiria,Mchilu ilipoona hivyo ikabidi itanue lakini alikua spidi hamadi anakutana na Scania iliyokua inafuata tiles Mkiu na pale kulikua na kona pembeni kuna hospital..Rosa ikabidi itoke nje ya barabara kuikwepa ile Scania na ile Scania nae alikua na akili hiyo hiyo hivyo zikakutana uso kwa uso nje ya barabara na kila gari kugeuka kule ilipotokea..wengine walikufa kutokana na uzembe wa watu kujali mali kuliko uhai wa watu.
kuona maiti ya mtu unaemfahamu akiwa imeharibika kiasi kile ni jambo gumu sana sikuwahi kuwaza kama Bro angekufa kifo kile alivunjika kiuno,miguu,mikono,kichwa kimepasuka la haula kifo kibaya sana.Marehemu ameacha wake wawili na watoto watano na gari aliyokua akiendesha ni ya kaka ake ambayo tarehe 18 mwezi huu inatimiza mwezi.
Nimejaribu kueleza tu yale ninayoyafahamu jana tumewazika wote,tunamshukuru mbunge wa mkuranga Mh Abdallah Ulega kutoa sanda na gari ya maiti ,,, Mungu azilaze roho za marehemu panapostahili.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna nini madereva wa gari za Dangote? mbona matukio ya ajali za haya magari ni mengi? Nashauri kitengo kinachohusika Traffic kikawafanyie usahili hao madereva wa Dangote kuthibitisha kama wana weledi wa kuitwa madereva
Zilikuwa coaster 2 zinafukuzana ndio tyte likabast na kuhama njia kulifuata Lori
Hiyo ndio sababu ya ajali
Coaster ina uwezo wa kubeba abiria 22-25, sasa hiyo number ya majeruhi + marehemu unapata thelathini na ushehe plus ambao hawajajeruhiwa unapata ngapi?
Utakuta chanzo ni mwendo kasi halafu abiria wapo kimya hawaongei chochote Kama mizigo.
Ni kweli ilikuwa ni overtaking tu, aliyeniambia alikurupuka
Yeye ndiye mtu gani huyo mbona mpenda kurahisisha mambo hivyo kama huna data kaa kimya wenye data za uhakika walete sio majungu na umbea tu kila saa.Yeye mwenyewe ndio chanzo,
unataka nini tena
R I P
Yeah ndo hivyo ndugu niko na huzuni sana dereva alikua mtu poa sana japo kuhusu mwendo kwake ilikua kama chakula...siku moja aliwahi kusema "Mimi sitaki nipate ajali afu niwe kilema niteseke ,nikipata ajali nataka waokote vipande sitaki mambo ya kuuguzwa..kweli kimetokea kile alichoomba japo ajali kwa asilimia 90 ajali imesababishwa na hiyo coaster nyingine maarufu kama Mama Peter kwa kusimama ghafla barabarani ili achukue abiria bila kuingia kituoni"
Sent using Jamii Forums mobile app
Aiseee pole sana mkuuYeye ndiye mtu gani huyo mbona mpenda kurahisisha mambo hivyo kama huna data kaa kimya wenye data za uhakika walete sio majungu na umbea tu kila saa.