TrueNakuambia Prado sio gari ni takataka bin uchafu....hata bila kukata mguu Hua zinakata na kiuno[emoji3][emoji3]hasa kwenye njia za changarawe...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
TrueNakuambia Prado sio gari ni takataka bin uchafu....hata bila kukata mguu Hua zinakata na kiuno[emoji3][emoji3]hasa kwenye njia za changarawe...
DuhMAMA ALIYEPOTEZA WANAWE WANNE NI UCHUNGU MTUPU.
Pichani ni Liliani Msuya, Mama mzazi wa watoto wanne waliofariki katika ajali ya gari, Mbwewe Chalinze mkoani Pwani walipokuwa wanaenda msibani Kilimanjaro, akionekana ni mwenye majonzi na uchungu nyumbani kwake kijiji cha Kisangeni, Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro.View attachment 2708846
Sent using Jamii Forums mobile app
Exactly [emoji817]Unaongea kweli nina ndugu yangu kapata kazi mwaka jana tu huyu alikuwa hajui hata kushika usukani wa gari mienzi mitatu mbele kanunua gari week 3 nying kashapata leseni ...kwa kifupi anjifunza kuendesha gari yake huku ana leseni.....
Ukitaka kujua mtu ni dereva wewe mpe gari ya kirungu.
View attachment 2707159View attachment 2707160
Watu wanne wamefariki dunia baada ya gari aina ya Toyota Prado walilokuwa wamepanda kugongana uso kwa uso na gari ya mzigo aina ya Scania majira ya saa nane usiku katika eneo la Mapatano, Kata ya Mbwewe, Halmashauri ya Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Waliofariki katika ajali hiyo ni dereva wa Toyota Prado, pamoja na abiria watatu waliokuwa kwenye gari hilo.
Kamanda ya Polisi Mkoa wa Pwani, Piusi Lutumo, amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Toyota Prado ambaye alihama upande wake na kugongana uso kwa uso na gari hilo la mizigo.
Miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika Zahanati ya Lugoba mkoani Pwani kwa ajili ya uchunguzi na kutambuliwa na ndugu wa marehemu.
CHANZO: AZAM TV
===
Ajali ya gari, iliyotokea jana Jumatano usiku katika kijiji cha Mapatano, Kata ya Mbwewe, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani, imepoteza maisha ya Mkurugenzi wa Benki ya ABSA na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Tawi la Dar es Salaam.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo kupitia taarifa yake iliyotolewa leo Alhamisi Agosti 3, 2023 na kusainiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutuma.
Katika taarifa hiyo, imesema kuwa ajali hiyo ilitokea jana Agosti 2, saa 2:30 usiku, ikihusisha gari aina ya Toyota Prado na Scania. Taarifa hiyo imebainisha kuwa gari ya Toyota Prado ilikuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, na kwamba ilikuwa ikiendeshwa na Nechi Msuya, huku Scania ilikuwa ikitokea Arusha na kwamba iliendeshwa na Philipo Mtisi.
Taarifa hiyo iliwataja waliofariki kwenye jali hiyo kuwa ni Nechi Msuya anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 45 hadi 50, Dayana Mageta, mfanyabishara na makazi wa Dar es Slaam anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 hadi 45, Nora Msuya anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 hadi 45 ambaye ni mwalimu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Tawi la Dar es Salaam, na abiria wa kike ambaye jina lake halikufahamika na anakadiriwa kuwa na miaka 30 hadi 35. Polisi imeeleza chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Toyota Prado kuhama kutoka upande wa kushoto wa barabara kwenda upande wa kulia kisha kogongana uso kwa suo na lori hilo. (Imeandikwa na Nasra Abdallah)
Huku njema ndugu yanguni uzma bwawa.. sjui kpande hiko...?
Nipo na Kontawa hapa anakupa hi!!ni uzma bwawa.. sjui kpande hiko...?
Siwezi kabisa kulisahau hili tukio na hua namtanguliza mungu kila ninapo safiriHii utakaaa usahau kabisa, ulitumia nguvu na akili nyingi sana mkuu hongera sana.
Aisee good choice.Siwezi kabisa kulisahau hili tukio na hua namtanguliza mungu kila ninapo safiri
HakikaKila siku tunapiga kelele suala la upanuzi wa barabara ya Morogoro road, line mbili za kupishana zitaendelea kusababisha ajali kila siku
Kuna haja ya upanuzi wa hivi barabara serikali iangalie hili ni muhimu sana maana hizi barabara inatumiwa sana na magari mengi na ndio inayofungua nchi.
Kwanini usiandike kiswahili kizuri ukaeleweka! Au unataka kuonyesha kiwango cha uhuni ulichonacho?inaonekana suka wa prado alikua mwendo wa ngiri mkia juu
AiseeeYes mkuu,ujue watu wana-base kusema mama/bana hata awe kichaa ni baba/mama tu,No ni uongo,binafsi sipatani na mama mzazi kabisa,kaniacha mikononi mwa baba nikiwa na mwaka mmoja na miezi minne,baada ya mwaka mmoja kabeba mimba na kuzaa na mwanamme mwingine,bila ya kuja hata kuniona,I was to die,ila mungu akawa upande wangu.
Hadi sasa nikisikia mtu anasema nani kama mama huwa nakasirika sana,nafarijika sana nikisikia nani kama baba,
Chuga boys hao hawajifichi kabisa!!Kwanini usiandike kiswahili kizuri ukaeleweka! Au unataka kuonyesha kiwango cha uhuni ulichonacho?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hawa jamaa wa chuga me nawasifu kwa kuweza kutengeneza Identity yaoChuga boys hao hawajifichi kabisa!!
Duh 🙄 !! Maneno gani hiyo tena. ???!!!Umejenga majumba makubwa Tabata, kisirisiri ili mumewe asijue, sasa sijui itakuaje? Kamq nakiona vile kibenten chake kikiwa tajiri[emoji23].
Mumewe alikua haongei chochote kwake cz pesa hana[emoji2955]
Natoka muda wowote saa yeyeto, naenda nchi za njee nakaa miezi hadi mwaka, sitaki mume unipangie pesa ni zangu elimu ni yangu[emoji2955]
Heeh !!!Ndo akina msuya hawa??
Hujawaho kwenda kwenu..miaka na miaka..baba yenu anawaita njoo nyumbana niongee nanyi..mnajifanya busy..mnachofanya ni kumchukua mama yenu na kukaa nae mjin na baba anabaki kijijin akiwa hana msaada wowote huku AMEINAMISHA nafsi yake kwa sababu ya matendo yenu...linakuja kutokea tatizo kubwa pasipo kureconcile na baba yenu mnajibeba mnaenda.........
Waliotengeneza pamoja na hizi kampuni zinauza hawana utaalamu wa ugunduzi wa matatizo kama haya na kufanya kitu kinaitwa Recall ili kufanya marekebisho ambayo ni Free. Kwa jinsi hii na nchi zetu za uchakachuaji mengi yatajitokeza.Toyota Prado, 'The Most Dangerous Vehicle' Seen
Hivi kwa nini haya Ma Prado yanaongoza kuchomoka tairi la mbele? Nimeshakutana na jamaa kama wanne hivi katika nyakati tofauti tofauti wakiwa wamechomokewa na tairi za mbele. Nikawaza kama wangepatwa na maswahibu hayo katika speed kubwa, si ingekuwa ni balaaa? Jamani mnaomiliki haya magari...www.jamiiforums.com
MBONA TUNAFOKEANA MZEE KWANI SHIDA NI NINI..?Kwanini usiandike kiswahili kizuri ukaeleweka! Au unataka kuonyesha kiwango cha uhuni ulichonacho?
Mkuu usimzibe mdomo, acha tujifunze kuishi vema ktk dunia hii yenye kupita, kupitia mafunzo ya wengine.kuna elimu wala usimzibe mdomo.Mchepuko naye atakufa ataziacha. Ni kawaida hamna jipya.
Masuala binafsi haya.
Kifo hakichagui boss, hata angempa mumewe zote angekufa. Usione kama ni malipo ya alichokifanya.
Sawa bossMkuu usimzibe mdomo, acha tujifunze kuishi vema ktk dunia hii yenye kupita, kupitia mafunzo ya wengine.kuna elimu wala usimzibe mdomo.