Pwani: Magari yagongana uso kwa uso, wanne wafariki

Pwani: Magari yagongana uso kwa uso, wanne wafariki

Ila alikua haringii, alikua mtu wawatu, full story kwa watu,alikua mshauri,

Japo ukuta wa nyumba yake alisogeza hadi barabarani/alivuka mpaka akatupa shida kugeuza na magari yetu hadi leo(barabarani ikawa nyembamba)[emoji23]

Kwa mafundi ujenzi ndio aliniacha HOI na mimi hii staili aliekua anaitumia lazima niitumiee aisee[emoji23]
@ Akikuuliza hii nyumba inahitaji matofali mangapi? Mbao ngapi?? Bati ngapi?? Cement ngapi?? Rangi ndoo ngapi? Nondo ngapi?? ALAFU akaja kuvinunuaa THEN wewe fundi uje KUVIBAKISHAAAA[emoji119][emoji119] iwe vyotee au kimoja wapo?? Lazima akukate kwenye malipo atakayo kulipa( yani ana kuuzia kwa Bei ile ile alienda kununua iko ulicho bakisha[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

HANA BAYAA r.I.p Dada yetuu[emoji25][emoji25]
Huyo dada umemuamulia
Nyumba 6 tu unamuandikia kurasa kuna watu wana nyumba 40
 
Yes mkuu,ujue watu wana-base kusema mama/bana hata awe kichaa ni baba/mama tu,No ni uongo,binafsi sipatani na mama mzazi kabisa,kaniacha mikononi mwa baba nikiwa na mwaka mmoja na miezi minne,baada ya mwaka mmoja kabeba mimba na kuzaa na mwanamme mwingine,bila ya kuja hata kuniona,I was to die,ila mungu akawa upande wangu.

Hadi sasa nikisikia mtu anasema nani kama mama huwa nakasirika sana,nafarijika sana nikisikia nani kama baba,
Mama ni mama wewe......muda wa kukaa tumboni kwake miezi tisa bila ya kukudhuru na akakuzaa kwa uchungu bila ya kukudhuru hilo ni bora kuliko hilo unalo lifikiria.....

Mama anauchungu na mwanae kuliko baba....ila kuna muda kama binadamu wamama wanavurugwa tu.

Nawamiss sana wazazi wangu hasa mama,Allah awape nuru uko walipo...Amiin
 
Barabara zetu zinatakiwa zote ziwe na mfumo wa Kimara-Kibaha vile. Wa kwenda waende na wa kurudi warudi upande wao. Hutakaa ukasikia ajali ya uso kwa uso ile njia. Labda watu mkwanguane.
Labda tukiwa Jimbo la US au tujiuze Kwa DP world maana Steve Nyerere hawezi kupanga Mipango ya muda mrefu
 
Dereva daladala aliyekunywa viroba anaweza kuwa anaendesha vizuri gari kuliko madereva wengi sana wa maofisini ambao wamenunua leseni. Nina ndugu zangu wa SADC wakija Tanzania ndio wananunua leseni wakazitumie nchi zao, wana uzoefu wa kuendesha magari ila wakifanya test chances za kufeli kule kwao ni kubwa.

Kuna maelfu ya waendesha daladala jiji la Dar ila nadra kusikia daladala limeua watu wanne kwa ajari. Na yanakimbia kila usiku na kila alfajiri, na madereva wanakunywa wengine mida trafiki hamna, na wana fatigue kila siku, wanakuwa na usingizi kila siku. Uzoefu wao usiuchukulie kawaida.
Unaongea kweli nina ndugu yangu kapata kazi mwaka jana tu huyu alikuwa hajui hata kushika usukani wa gari mienzi mitatu mbele kanunua gari week 3 nying kashapata leseni ...kwa kifupi anjifunza kuendesha gari yake huku ana leseni.....

Ukitaka kujua mtu ni dereva wewe mpe gari ya kirungu.
 
Kauli ya mwisho ya Sia kabla kutokea ajali iliyoua wanafamilia wanne

Mmoja wa wafanyakazi wenzie na Sia Msuya amemuelezea marehemu huyo kama miongoni mwa watu wengu upendo na alipenda watu wawe na furaha.

"Lile tabasamu ambalo tumekuwa tumezoea kumuona nalo dada Sia ndiyo hilo nililomuona nalo jana akiwa kwenye usingizi wa mauti"

Hiyo ni kauli ya Aminata Juma mfanyakazi wa Shirika la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) aliyekuwa akifanya kazi na Sia Msuya aliyefariki na ndugu zake watatu katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa Agosti 2.

Aminata anamuelezea Sia kama mtu mkarimu na mwenye upendo aliyetaka kuona siku zote watu wana furaha.

Kitaifa
Kauli ya mwisho ya Sia kabla kutokea ajali iliyoua wanafamilia wanne
Ijumaa, Agosti 04, 2023

Aminata Juma mfanyakazi wa Shirika la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Agosti 4, 2023 akiwa nyumbani kwa Dk Norah Msuya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

By Waandishi Wetu
Muktasari:
Mmoja wa wafanyakazi wenzie na Sia Msuya amemuelezea marehemu huyo kama miongoni mwa watu wengu upendo na alipenda watu wawe na furaha.
Dar es Salaam. ‘‘Lile tabasamu ambalo tumekuwa tumezoea kumuona nalo dada Sia ndiyo hilo nililomuona nalo jana akiwa kwenye usingizi wa mauti’’.

Hiyo ni kauli ya Aminata Juma mfanyakazi wa Shirika la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) aliyekuwa akifanya kazi na Sia Msuya aliyefariki na ndugu zake watatu katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa Agosti 2.

Aminata anamuelezea Sia kama mtu mkarimu na mwenye upendo aliyetaka kuona siku zote watu wana furaha.

RELATED
Simanzi nyumbani kwa ndugu wanne waliofariki ajalini
Kitaifa 20 hours ago
Bosi wa benki, mhadhiri wa Mzumbe wafariki dunia ajali Bagamoyo
Kitaifa 20 hours ago
“Mimi nafanya kazi idara ya rasilimali watu yeye alikuwa kurugenzi ya utekelezaji oparesheni, Ijumaa alikuja ofisini kwetu na tukazungumza.

“Muda wote wa mazungumzo yetu alikuwa akinieleza mimi ni nani na anavyofurahia mafanikio yangu, akaniambia Aminata simama nikukumbatie basi tukakumbatiana,” amesema Aminata.

Bado Sia aliendelea kuzungumza na Aminata akimueleza anatamani kufanyike shughuli yoyote itakayowakutanisha wanawake wachache wafurahie maisha.

“Aliniambia kama tunaweza kuandaa jambo lolote zuri la kuwakutanisha wanawake wachache, nikamwambia Agosti 8 nitakuwa na tukio langu la kuchangia damu akasema lazima atakuwepo.”

“Aliniambia anaenda msibani akirudi tutakuwa pamoja. Tukiwa pale bado tunazungumza akapita dada mmoja bila kutusalimia akamwita akamuuliza wewe kwanini unakuta watu halafu husalimii unajuaje kama huyu kesho utamuona?”

Sia ambaye ni mtoto wa kwanza kwenye familia hiyo ya ndugu wanne waliopoteza maisha, hakubahatika kupata mtoto.
 
Mama ni mama wewe......muda wa kukaa tumboni kwake miezi tisa bila ya kukudhuru na akakuzaa kwa uchungu bila ya kukudhuru hilo ni bora kuliko hilo unalo lifikiria.....

Mama anauchungu na mwanae kuliko baba....ila kuna muda kama binadamu wamama wanavurugwa tu.

Nawamiss sana wazazi wangu hasa mama,Allah awape nuru uko walipo...Amiin
Kila mtu na mtazamo wake,wamama wanazaa na kutupa watoto nao tuseme mama ni mama!?,kukaa tumboni ni majukumu ambayo nature ilimpa mwanamke, ulitaka ukae tumboni kwa baba!?
 
Kila mtu na mtazamo wake,wamama wanazaa na kutupa watoto nao tuseme mama ni mama!?,kukaa tumboni ni majukumu ambayo nature ilimpa mwanamke, ulitaka ukae tumboni kwa baba!?
Ulishawahi kusikia mwanaume yeyote ameshtaki mwanamke aliyetupa mtoto wake? Wanaume wanatupa watoto waliozaliwa na wanakataa watoto ambao hawajazaliwa.
 
Mkuu usingizi unakukuta popote pale kama unaendesha gari usiku ukiona macho yameanza kuwa mazito ni Bora upaki pembeni.
Sahihi na ndo mmegundua ajali nyingi usiku ni uchovu na usingizi
Iliwahi Nikuta hii yaani Mungu tu km kungekua na gari mbele Inakuja tungekufa
Tulijikuta upande wa kulia wa Barabara karibu tuzame bondeni huko
Tukalala pale Bungu
Nikajua kumbe usiku hakuna Nini Wala shetani ni usingizi tu
 
Hatari sana hiyo aisee
 
Back
Top Bottom