View attachment 2707159View attachment 2707160
Watu wanne wamefariki dunia baada ya gari aina ya Toyota Prado walilokuwa wamepanda kugongana uso kwa uso na gari ya mzigo aina ya Scania majira ya saa nane usiku katika eneo la Mapatano, Kata ya Mbwewe, Halmashauri ya Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Waliofariki katika ajali hiyo ni dereva wa Toyota Prado, pamoja na abiria watatu waliokuwa kwenye gari hilo.
Kamanda ya Polisi Mkoa wa Pwani, Piusi Lutumo, amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Toyota Prado ambaye alihama upande wake na kugongana uso kwa uso na gari hilo la mizigo.
Miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika Zahanati ya Lugoba mkoani Pwani kwa ajili ya uchunguzi na kutambuliwa na ndugu wa marehemu.
CHANZO: AZAM TV