Pwani: Mtambo wa kuvuna maji lita milioni moja kwa Saa, wakamatwa katika chanzo cha maji cha mto Ruvu

Pwani: Mtambo wa kuvuna maji lita milioni moja kwa Saa, wakamatwa katika chanzo cha maji cha mto Ruvu

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
#HABARI BODI ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imemkamata mkulima mkubwa raia wa China anayefanya kilimo cha umwagiliaji Kijiji cha Kidogozelo Kitongoji cha Migudeni wilayani Chalinze akivuta Maji katika Mto Ruvu kwa kutumia mashine yenye uwezo wa kuvuta maji Lita milioni moja kwa saa.

=====

Mwandishi Wetu

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imekamata mtambo wa kuvuna maji kwa ajili ya umwagiliaji shamba la Hekta 50 katika kitogoji cha Kidozero ,Chalinze

Mtambo huo unaweza kuvuna maji lita milioni moja kwa saa hali ambayo inafanya maji mengi kushindwa kufika katika kidakio cha Ruvu Chini.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa kuangalia chanzo cha maji cha Mto Ruvu Afisa Maji Bonde la Wami/Ruvu Dar es Salaam Halima Faraji amesema katika mazingira hayo wiki moja ya Novemba 12 walifika hapo na kukuta mtambo wakauchukua na kulipa faini lakini wameweza kufunga mtambo mwingine.

Faraji amesema juhudi zinazofanyika ni kwa ajili ya kuhakikisha maji hayapotei katika mikono ya watu ili sehemu za vidakio vinapata maji ili kupunguza makali ya mgao hasa kidakio cha Ruvu Chini inayolisha Bagamoyo na sehemu ya Dar es salaam.

Faraji amesema kuwa mwenye shamba hilo hana kibali cha bonde pamoja na kuchukua maji hayo ndani ya mita 60 kutoka kingo za mto Ruvu.

Aidha amesema katika uvunaji wa maji hayo anavuna masaa nane kwa nyakati za Asubuhi na Jioni huku mafuta yanayosukuma mtambo huo yakitiririka kwenye mto ambao unatumiwa na watu wengine kabla hayatiwa dawa.

Aliongeza kuwa kwa kipindi hiki wananchi waache kuvuta maji wakikutwa wakiwa na mashine na wao wenyewe wanaowakamata ili sheria ishike mkondo wak

Hatuweza kuwaacha wananchi ambao wanapata elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na kuendelea kufanya kwa kijificha katika kichaka ya kuwa elimu hayatolewa.

Kwa upande Afisa Maendeleo wa Bodi hiyo Hhau Sarwatt amesema kuwa wamefanya ukaguzi katika shamba hilo na kuweza kuona makosa yanajirudia.

Amesema kuwa kwa hali ya sasa ukaguzi utakuwa endelevu na atakayekutwa hatakuwa salama kwao na mashine au mitambo yao.
WhatsApp-Image-2021-11-19-at-7.14.21-PM-768x576.jpeg
WhatsApp-Image-2021-11-19-at-7.14.22-PM-768x576.jpeg

Afisa Maji wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu Dar es Salaam Halima Faraji akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana mtambo walioukuta katika shmaba wenye uwezo wa kuvuna lita milioni moja kwa saaa.
 
#HABARI BODI ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imemkamata mkulima mkubwa raia wa China anayefanya kilimo cha umwagiliaji Kijiji cha Kidogozelo Kitongoji cha Migudeni wilayani Chalinze akivuta Maji katika Mto Ruvu kwa kutumia mashine yenye uwezo wa kuvuta maji Lita milioni moja kwa saa. https://t.co/sdJ6JzZ2Ck
View attachment 2016510
kuna sheria aliyoikiuka????
 
Mashine inauwezo wa kuvuta maji lita milioni 1 kwa siku, halafu unasema anavuta lita milioni 1 kwa siku. Kwahiyo kama mimi ninauwezo wa kuoa wake 10, utaenda kusema nimeoa wake 10? Utaahira wa wapi huu?!
 
#HABARI BODI ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imemkamata mkulima mkubwa raia wa China anayefanya kilimo cha umwagiliaji Kijiji cha Kidogozelo Kitongoji cha Migudeni wilayani Chalinze akivuta Maji katika Mto Ruvu kwa kutumia mashine yenye uwezo wa kuvuta maji Lita milioni moja kwa saa. https://t.co/sdJ6JzZ2Ck
View attachment 2016510
Huyo mwekezaji wa mbogamboga angekuwa awamu ya Mobutu kule Zaire angepewa kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji wa fedha😂😂
 
Back
Top Bottom