TANZIA Pwani: Polisi wawili wagongwa kwa mkupuo na kufariki

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Askari wawili wa Jeshi la Polisi, Izdory George Michael na Rehema Juma Magawa, wamefariki dunia baada ya kugongwa na gari aina ya Toyota Noah katika barabara kuu ya Dar es salaam - Morogoro kwenye eneo la Maili Moja, Kibaha Mkoani Pwani.

Jeshi la Polisi mkoani Pwani limesema baada ya ajali, gari hilo namba T 804 ERM lilikimbia, na baada ya msako kufanyika lilikutwa likiwa limefichwa maeneo ya Kwa Mfipa.

MY TAKE

Wameanza kupungua.. Au tuanzishe thread ya vifo vya mapolisi?
 
Makamu? Naam Boss ongeza moto
Wameanza kutoana maini ongeza moto
 

Askari wawili wa Jeshi la Polisi ambao ni Izdory George Michael na Rehema Juma Magawa, wamefariki dunia baada ya kugongwa na gari aina ya Toyota Noah katika barabara kuu ya Dar es salaam - Morogoro kwenye eneo la Maili Moja, Kibaha Mkoani Pwani.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani imeeleza kuwa ajali hiyo ilitokea jana Agosti 25, 2026 saa 1 usiku ikihusisha gari aina ya Toyota Noah lenye namba T 804 ERM lililokuwa likitokea Dar es salaam kuelekea Mlandizi ambapo lilipofika katika kivuko cha Watembea kwa miguu (zebra), lilipita magari mengine yaliyokuwa yamesimama kupisha Watu na kwenda kuwagonga Askari hao.

Askari Izdory George Michael alifariki dunia katika eneo la ajali huku Askari Rehema Juma Magawa akijeruhiwa kichwani na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi kwa matibabu ambako hata hivyo alifariki dunia asubuhi ya leo Agosti 26, 2026.

Imeelezwa kuwa gari hilo lilikimbia baada ya ajali lakini baada ya msako kwa kushirikiana na Wananchi, lilikutwa likiwa limefichwa maeneo ya Kwa Mfipa.
 
Taarifa ya polisi inasema gari iliohusika ni T804ERM ni Noah Nyeusi na waandishi wetu wanatuambia hivo...

Ila ukicheki number plate T804ERM kwenye usajili wa magari inatambulika kama Subaru Forester ya Grey.

Au ukiamua kucheki kwenye malipo ya Parking still ni Subaru Forester.
Kuna uwezekano jamaa alikua anatumia namba fake au kuna tatizo la kusoma izo namba.

Madogo wanaonekana watoto sana. Wapumzike kwa amani.
 
Wanazikwa lini? Kifo ni kifo tu
 
 

Attachments

  • 3fb40fd9-db27-4c86-8a72-ae4ef0758deb.jpeg
    114.4 KB · Views: 23
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…