Pwani: Wafanyakazi wa kampuni ya mikopo ya OYA, mbaroni kwa tuhuma za mauaji

Pwani: Wafanyakazi wa kampuni ya mikopo ya OYA, mbaroni kwa tuhuma za mauaji

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za mauaji ya Juma Mfaume (40), Mfanyabiashara na mkazi wa Mbagala Mlandizi.

Tarehe 07-10-2024 katika Kitongoji cha Mbagala, Wilaya ya Kipolisi Mlandizi, Mkoa wa Pwani, watu wanne ambao ni wafanyakazi wa kampuni ya mikopo ya OYA, walifika nyumbani hapo kwa lengo la kudai fedha za marejesho ya mkopo kwa mke wa Juma Said Mfaume aitwaye Khadija Ramadhan.

Baada ya kufika nyumbani kwa Juma Mfaume, ailiwaelekeza kuwa mkewe hayupo lakini watuhumiwa hao walilazimisha kuingia ndani kwa nguvu huku wakimshambulia sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia fimbo na baadae Bw. Mfaume, alianguka na kupoteza fahamu.

Kutokana na hali hiyo watuhumiwa walimbeba, Juma Mfaume kwa kutumia gari lao ili wampeleke hospitali na alifariki akiwa anapatiwa matibabu katika kituo cha Afya cha Mlandizi. Mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na daktari kisha kukabidhiwa kwa taratibu za mazishi.
Linawashikilia watu wasio na majina?.
 
Back
Top Bottom