Pwani: Wafanyakazi wa kampuni ya mikopo ya OYA, mbaroni kwa tuhuma za mauaji

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za mauaji ya Juma Mfaume (40), Mfanyabiashara na mkazi wa Mbagala Mlandizi.

Tarehe 07-10-2024 katika Kitongoji cha Mbagala, Wilaya ya Kipolisi Mlandizi, Mkoa wa Pwani, watu wanne ambao ni wafanyakazi wa kampuni ya mikopo ya OYA, walifika nyumbani hapo kwa lengo la kudai fedha za marejesho ya mkopo kwa mke wa Juma Said Mfaume aitwaye Khadija Ramadhan.

Baada ya kufika nyumbani kwa Juma Mfaume, ailiwaelekeza kuwa mkewe hayupo lakini watuhumiwa hao walilazimisha kuingia ndani kwa nguvu huku wakimshambulia sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia fimbo na baadae Bw. Mfaume, alianguka na kupoteza fahamu.

Kutokana na hali hiyo watuhumiwa walimbeba, Juma Mfaume kwa kutumia gari lao ili wampeleke hospitali na alifariki akiwa anapatiwa matibabu katika kituo cha Afya cha Mlandizi. Mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na daktari kisha kukabidhiwa kwa taratibu za mazishi.
Alafu unakuta kazi ni ya mhindi masikini mshahara wenyewe ulikuwa unalipwa laki 3 ukataka kuonyesha juhudi ili boss akuone wewe jembe kwelikweli.

unaweza kujihisi unamikosi ya ukoo mzima.
 
Selikari ya TANZANIA ipo haja ya kuingilia kati
Kusitisha mikopo holela na wao wenyewe kutoa mikopo yenye mashart nafuu

Hao oya ukiwa na I'd na mdhamini mmoja kwisha

Ila ukijumba kiuchumi kama umeiba kanisani au msikitini
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za mauaji ya Juma Mfaume (40), Mfanyabiashara na mkazi wa Mbagala Mlandizi.

Tarehe 07-10-2024 katika Kitongoji cha Mbagala, Wilaya ya Kipolisi Mlandizi, Mkoa wa Pwani, watu wanne ambao ni wafanyakazi wa kampuni ya mikopo ya OYA, walifika nyumbani hapo kwa lengo la kudai fedha za marejesho ya mkopo kwa mke wa Juma Said Mfaume aitwaye Khadija Ramadhan.

Baada ya kufika nyumbani kwa Juma Mfaume, ailiwaelekeza kuwa mkewe hayupo lakini watuhumiwa hao walilazimisha kuingia ndani kwa nguvu huku wakimshambulia sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia fimbo na baadae Bw. Mfaume, alianguka na kupoteza fahamu.

Kutokana na hali hiyo watuhumiwa walimbeba, Juma Mfaume kwa kutumia gari lao ili wampeleke hospitali na alifariki akiwa anapatiwa matibabu katika kituo cha Afya cha Mlandizi. Mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na daktari kisha kukabidhiwa kwa taratibu za mazishi.
Sijui mpaka wafe wangapi ndo bi chura astuke kuwa kuna jambo halipo sawa?
 
Hizi taasisi uchwara za mikopo ni janga. Zinaibuka mitaani kila kukicha kama uyoga. Mamlaka ichukue hatua hizi taasisi zipigwe marufuku. Zimesababisha watu wengi zama hizi wakose utulivu wa moyo. Ni bora ubaki na shida zako kuliko kudaiwa kausha damu.
 
Back
Top Bottom