Q-Net na Forever Living zimenipotezea marafiki zangu wa karibu

Hahahaha kuna siku niliitwa sinza aisee kuna wadada wanajua kuongea kuna jamaa mmoja alinunua dawa ya meno kwa 50k wakamwambia akienda kuiuza atauza 200k mpaka akaamua kutumia mwenywew tu
Hii Dawa ya meno ina sifa gani?
 
KijanaHuru soma majuto haya,,🤣🤣🤣🤣
 
Hahaa nakumbuka ilikiwa mwaka 2016/2017 hivi nlipata mwaliko kutoka kwa binti mmoja hivi niende makumbusho kuna seminar, kufika nikapanda kule juu kwenye jengo la uchumi supermarket nikakuta vijana wengi wapo, seminar ikaanza nkaona mara wanaimbishwa nyimbo za diamond , mara wiii waaa..nikaona wananipotezea muda ,nilisepa bila kumuaga
 
Jamaa umenikumbusha mbali sana mapindi ya kwa muddy physics na mihogo ya mgosi....mchikichini hiyo way back. Allah amrehemu mwalimu Muddy physics ameen
 
Kunayo hio mama ya chuga imesimama kinoma inapiga IFM nlikutana nayo mtandaoni nkashangaa inajaa ovyo ovyo nkasema au huyu sio yeye....
piga video call mtoto ni yeye

Ananambia anataka kuonana na mimi si akanpa namba sasa...
Status ni C9 mara detoxify mara sun screen nkamvungia sasa nataka nmchane tuweke issue za global pemben tubonge kiutu uzima nione atafanyaje yule mrembo wa kimasai
 
Kuna jamaa yangu mmoja, alinikwaza sana, ilikuwa 2011, nimemaliza 6 niko kitaa nahangaika na tuition nipate sh 2 3. Siku hyo kanipigia simu eti nenda pale mwenge Karibu na ITV kuna bonge la mishe, dah si nikatoka chalinze mpka Dar, then naenda pale kumbe GNLD....dah! Wanaongea hao......nilijutw sana kutumia 3k yangu kwa kwenda kusikiliza ule upuuz
 
Juzi kati watu wamepigwa na kitu kizito uncle Kalynda😂😂😂
 
Kuna rafiki yangu nae wa kitambo sana aliniomba sana tuonane ili tuongee jambo. Nikadhani labda anataka ushauri. Ile nafika nakutana na timu ya watu wanne na stories zao za Q-NET.

Baada ya kuwasikiliza kwa utulivu, niliwauliza kama wao washaonja mafaniko na wapo vizuri? Wakajibu yees. Then nikawaambia aliye tayari sasa hivi anikope Million 5 nijiunge chini yake harafu yeye atakuwa analamba faida yangu na riba juu mpaka deni liishe

Kikao kiliishia palepale na rafiki yangu yule ni kama aliniblock
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…