Mara ya kwanza nasikia kuhusu Forever Living ilikuwa mwaka 2005 kipindi hicho imepamba moto sana. Kulikuwa na mtoto mmoja mkali sana chuo nlikuwa namfukuzia.
Naye akaona atumie nafasi hiyo kuniunganisha firever living.nikamkubalia ili kwanza nimle halafu tutajuana mbele kwa mbele.kweli nikaenda kwenye semina elekezi moja wapo siku hiyo nikaonesha utayari sana wa kujiunga naye akafurah maan ningekuwa mteja wake wa kwanza.
Tulipotoka kwenye semina jioni nikampitisha sehemu tukala ,tukanywa nikamla kwa mara ya kwanza. Chuo nikamrudisha kesho yake. Sikujiunga forever living.nlijiunga kwake yeye kama yeye.
Miaka 8 baadaye dada mmoja mrembo sana alianza nitafuta akitaka tuonane.ana maongezi mazito sana.kila nlipomuuliza maongezi yanahusu nini hakutaka kunambia.kwa dada mwenyewe mashallah nikawaza "pengine huyu dada anataka nyanjo" maana mara ya mwisho tulionana udsm nikiwa namfukuzia.akagundua namtumia rafiki yake.tukaachana hapo.
Miaka nane baadaye ndo ananitafuta kwa udi na uvumba.siku moja akanibembeleza sana kuwa Ijumaa nisikose kuonana naye sehemu ya kuonana naye ni pale Sinza kilipo Chuo cha Kilimanjaro.
Nikatoka mapema kazini Town nikisema mtu hakati wito anakataa aliloitiwa. Ingawa kila nikimuuliza huyu dada mada ya kutaniko letu ni nini....anasema we njoo tu bwana.usiniangushe
Siku hiyo Ijumaa nikatoroka kazin nikiwa na shauku mrembo ananiitia nini week tatu zote anataka tuonane.
Kufika akanielekeza nipande juu.kwenda ndani nikamkuta huyo dada na watu wengine kama wamemaliza issue flan sasa wanaconclude kwenye tuvikundi.akanambia nikae sehemu pembeni.nikakaa nachezea chezea simu.
Baada ya muda akavuta kiti akawaita na wenzie wawili warembo waje kukaa ile meza.akanisalimia na kutambulisha wenzie.na kutaka kuanza kunambia habari za forever living.
Kwa mwaka ule hamna siku ambayo nilikasirika kama ile.nlianza kutetemeka kwa hasira na kumuuliza "ndo siku zote nakuuliza unaniitia nini kumbe unaniitia huu upuuzi? Kwa nini umenipotezea muda?…" Nliamka na kuondoka. Toka siku hiyo hatukuwasiliana tena. Nlikuwa namuona tu kwenye mitandao picha zake akionekana alivyochange toka kuwa mnene hadi kuwa mwembamba.
Mwaka huu mwanzo tena dada mmoja tumefahamiana kwa ajili ya mambo ya kazi.tukawa marafiki wa penzi sana.na huyu dada naye ni mashallah hasa kwa umbo.naye akaanza kunambia anahitaj tuonane.nikawa najiuliza ana nini analotaka tuonane "sehemu tulivu" maana hofu yangu ilikuwa nisije nikamtokea bure na wakati tunaheshimiana.
Jumatano moja nikamwambia nipo tayari kupata naye lunch. Tukatafuta hotel moja tulivu tule tuongee...baada ya maongezi ndo ananambia habari za Qnet. Nikagundua yeye wameshampiga anatafuta pa kulipizia.ana saa ya milions of money.
Nikamsikiliza...akanisimulia jinsi watu wanavyotajirika n.k akasimulia kwa shauku na bashasha.akiniasa hayo anayombia ni siri sana.hakupaswa niambia ila kuna sehemu itabidi anipeleke mikocheni kwa maelezo zaidi jumamosi.
Sikutaka muumiza. Nlimsikiliza na mwishowe nikamwambia ntamtaarifu.alipoona sina uelekeo kwa sasa hata nikipiga simu hapokei.ni kama ameshanichukia.nawaza why anichukie kwa pesa zangu mwenyewe?
Binafsi sitak na sipend kufanya kazi yoyote ambayo inaonekana ni rahis kunipatia pesa.utapeli huanzia hapo.sijawah tapeliwa na sitak kuanza sasa. Hakuna maisha rahisi. Kuna mtu anakuja anakwambia nliacha kazi bank,chuo,udaktar,sijui kampuni gan ili nifanye hii Forever,Qnet and the like.
Ukimtizama anavyokubembeleza mpaka anataka kulia ili ujiunge unagundua alishapigwa naye anataka akupige.mmoja alikuja ofisini akanambia aliacha upolisi ili afanye forever living.nlimtizama alivyochoka viatu vina vumbi,vimeisha upande, ameloana na jasho,midomo imemkauka.
Nikamwambia alifanya kitendo cha kipumbavu sana.maana sasa anapata taaabu yoote hiyo kwa kuwa hana kazi ya maana.jamaa aliondoka mnyonge sana. Ashakum si matusi dont let yourself fucked by these people and their fascinating stories.maisha si rahisi hivyo.