Sehemu ya 37
Wakiwa na nyuso zenye furaha,
Job na Dr Marcelo walilizunguka gari la
Amarachi ambalo ndani yake alikuwemo Amarachi na Austin waliowasili wakitokea hospitali.Job
akaufungua mlango wa upande aliokaa
Austin.
“ karibu nyumbani Austin”
“ Ahsante Job” akajibu Austin
“ Hallow Austin” akasema Dr
Marcelo
“ Hallo Marcelo” akasema Austin
“ Pole sana Austin”akasema
Marcelo akionekana kuwa na hofu
“ Ahsante” akajibu Austin.Job akamshusha Austin akamtegemeza na kumpeleka sebuleni.
“ Pole sana Austin.Vipi maendeleo yako,unajisikiaje? Akauliza Job
“ Ahsnate sana Job.Naendelea vizuri.maumivu ni ya kawaida sehemu zile zilizofanyiwa upasuaji .habari za hapa? Akawaza Austin
“ habari nzuri.hakuna tatizo.Usalama umedhibitiwa hapa na ndiyo maana hujaniona
hospitali.Nilimuachia Amarachi
majukumu yote ya hospitali”
“ Good.Ahsante sana nyote kwa juhudi mlizofanya kuokoa maisha yangu.Nipe ripoti ya operesheni yetu tumefikia wapi? Nini tayari kumefanyika hadi hivi sasa? Akauliza Austin .Kabla Job hajajibu Marcelo akasimama
“ Samahani jamani.Kuna jambo nataka niseme kabla maongezi hayajaendelea” akanyamaza na kumuelekezea macho Austin
“ Austin napenda nichukue nafasi hii kukuomba msamaha sana kwa
jambo la kijinga nililolifanya
lililopelekea haya yote yakatokea.Umenusurika kifo kwa sababu ya ujinga wangu.Maria aliniambia nimfungue akajisaidie na
mimi nikashikwa na huruma nikadhani
ninatenda wema.Nisamehe sana Austin”
akasema Marcelo na kupiga magoti
“ Inuka Marcelo” akasema Austin
“ Siwezi kukulaumu kwa ulichokifanya kwani hukutegemea kama jambo lile lingetokea.Hakuna kati yetu aliyetegemea kama Maria angeweza
kuwa mtu hatari.Naamini kwa
kilichotokea kuna funzo umelipata .Sina tatizo nawe Dr Marcelo tuungane sote katika mapambano haya.Wewe ndiye uliyenifumbua macho kuhusu Maria
kwa hiyo napaswa mimi kusema ahsante sana” akasema Austin .Dr
Marcelo akainuka na kumfuata Marcelo akampa mkono
“Ahsante Marcelo.Ahsante sana
.Mapema leo nilizungumza na Job nikamueleza kwamba mimi pia ni mwenzenu japokuwa sina utaalamu wowote wa mambo ya upelelezi lakini
bado naweza kuwa na msaada hata
mdogo.Mimi ni daktari nitawahudumia pale mtakapohitaji matibabu kwa mfano kwa sasa Austin yuko hapa nyumbani ni jukumu langu kumuhudumia.Naombeni msinibague .Nioneni ni mwenzenu mnitumie kila pale mtakapohitaji
msaada wangu” akasema Dr Marcelo
“ Marcelo wewe ni mwenzetu na usihisi kutengwa.Tunahitaji sana msaada wako japokuwa kuna wakati unaweza kuona kama hatukushirikishi
ni kutokana na mambo yetu haya kuwa ya hatari ,lakini fahamu kuwa una msaada mkubwa kwetu” akasema
Austin na kuwatazama akina Job
“ Job na Amarachi naomba mtambue rasmi kuwa huyu anaitwa Dr Marcelo Yuko chini ya ulinzi wangu .Ni mtu ambaye tunapaswa kumlinda kwa
kila namna .Suala lake ni kubwa na
mtalifahamu hapo baadae”
“ Karibu sana Marcelo”akasema
Amarachi
“Ahsanteni sana nyote.Naomba sasa nielekee jikoni kuandaa chakula” akasema Marcelo na kuelekea jikoni
“ Job nilikuuliza awali kuhusu ni
wapi tumefikia katika operesheni yetu? Akauliza Austin
“Tulipofikia mpaka sasa ni kwamba Maria tunaye hapa ndani na leo hii tumempata pia baba yake Boaz.Pongezi kubwa kwa Amarachi
kwani ndiye aliyefanikisha kumdhibiti Maria na leo hii ndiye aliyemleta Boaz” “Ahsante Amarachi kwa yote
uliyoyafanya.Mungu alikuleta kwa wakati muafaka.Umefanya kazi kubwa ambayo sikuwa nimeitegemea kabisa”
“Ahsante Austin kwa kuniamini”
akasema Amarachi
“ Now let’s get back to work.Tunatakiwa kwanza kufahamu huyu Maria ni nani.Sote tumeshuhudia kitu alichokifanya ambacho hakuna aliyekitegemea kwa hiyo ni mtu hatari zaidi ya tunavyodhani .Lengo la
kumpata Boaz lilikuwa ni kupata taarifa za kumuhusu Mukasha ambaye rais alikuwa amefikiria kumteua kuwa
waziri mkuu.Jana usiku Job ulimueleza
rais kuhusiana na uchunguzi tunaoufanya juu ya Mukasha.Kwa bahati nzuri hatuna tena haja ya kuendelea na uchunguzi huo kwani
tayari rais ametuamini kwa hiyo ombi letu limejibiwa na amebadili mawazo ya kumteua Mukasha kuwa waziri mkuu.”akasema Austin
“ Oh thank you Lord” akasema Job
“ Boaz tutamuhoji kuhusu suala la
Marcelo kwani ndiye anayemtafuta kwa gharama kubwa na alinipa mimi kazi ya kumtafuta.Tunapaswa kufahamu kwa
nini anamtafuta Marcelo? Pamoja na rais kutuamini kuhusu Mukasha lakini bado tutaendelea kumfuatilia hadi tufahamu mtandao wake wote.Tutamfikia hadi huyu bilionea anayejita dogo Bill na tutahakikisha tunampata mtoto Millen ”
Sura ya Job ikabadilika baada ya
Austin kumtaja mwanae Millen.Austin akamtazama kwa muda na kusema
“ Jambo lingine ni kwamba rais alinipa kazi ya kutafuta sampuli toka kwa Monica kwa ajili ya kipimo cha vinasaba .Kazi hiyo tayari imekamilika na tunayo sampuli ya nywele toka kwa Monica na rais.Kinachofuata ni
kuziwasilisha sampuli hizo maabara nje
ya nchi kwa ajiliya kipimo hicho na
Amarachi utasimamia zoezi hilo.Rais ameahidi kutupa ushirikiano mkubwa.Nitazungumza naye baadae ikiwezekana iwepo ndege maalum kwa ajili ya kupeleka sampuli hizo nje ya
nchi kwa vipimo.Kwa umuhimu wa suala hili rais hataweza kukataa” akasema Austin
“Austin samahani kidogo.Umesema kwamba tayari
tumepata sampuli ya nywele ya Monica
na rais kwa ajili ya kipimo cha vinasaba.Monica ana husiana na rais? Akauliza Amarachi
“Amarachi kuna mambo kadhaa
unahitaji kuyafahamu kuhusiana na operesheni hii inayoendelea na moja wapo ya mambo unayopaswa kufahamu ni hili la kuhusiana na hiki kipimo cha vinasaba tunachotaka kukifanya.Kwa
ufupi ni kwamba rais Ernest
amefahamishwa hivi karibuni na mwanamke ambaye aliwahi kuwa na mahusiano naye enzi za ujana wake kwamba wakati wa mahusiano yao waliwahi kupata mtoto ambaye ndiye Monica.Rais anataka kufanya kipimo cha vinasaba ili kupata uhakika kama kweli Monica ni mwanae”
“ Mpaka hapo nimekuelewa Austin lakini Monica anafahamu chochote
kuwa rais ni baba yake mzazi?
“ hapana bado hafahamu chochote.Rais anataka kwanza afanye kipimo kwa siri na akihakikisha kuwa kweli ni mwanae basi atamueleza ukweli wote.” Akasema Austin
“ Nashukuru Austin kwa kunielewesha lakini kuna kitu na mimi nataka kuchangia katika suala hili.Uliponiambia nichukue nywele ya
Monica sikuelewa kama ulihitaji kwa
ajili ya kipimo hiki cha vinasaba.Kwa kawaida unapohitaji sampuli ya nywele kwa ajili ya kufanya kipimo cha
vinasaba unatakiwa kuipata nywele ambayo imeanzia katika mzizi wake.Hii tuliyonayo haifai kutumika kama
sampuli kwa sababu niliikata tu bila
kuchukua na mzizi wake.Kwa mujibu wa wataalamu usahihi wa kipimo cha vinasaba kwa kutumia sampuli ya
nywele ni asilimia 80.Sampuli nyingine
ambayo inaweza kuwa nzuri zaidi ni kucha halisi,usahihi wake ni asilimia
95.Tunaweza pia kutumia sampuli nyingine kama vile mswaki lakini unahitajika mswahi uliotumika kwa muda huo huo kwani hewa hukausha mswaki ndani ya dakika thelathini.” Akasema Amarachi na kuwatazama Austin na Job
“Ahsante sana Amarachi kwa
darasa hilo zuri.Mimi sikuwa na
ufahamu wowote kuhusiana na mambo haya ya kipimo cha vinasaba.Kwa maelezo hayo uliyoyatoa ni wazi kwamba hatuna sampuli hapa.”
Akasema Austin
“ Ndiyo hatuna sampuli
.Tunatakiwa kutafuta sampuli zinazofaa na si hizi tulizo nazo” akasema Amarachi.Austin akafumba macho akazama mawazoni halafu akasema
“ This is what we’re going to do” akasema na kunyamaza kidogo halafu akaendelea
“ Monica aliniambia nimsaidie
kuonana na rais ana maongezi naye binafsi.Nitaongea na rais na lazima atakubali kuonana naye .Nataka iwe ni usiku wa leo.Tutakutana pale katika nyumba ya rais aliyonipa niishi kwa
chakula cha usiku.Tutamuwekea
Monica dawa ya usingizi katika kinywaji na halafu tutachukua sampuli tunazozitaka” akasema Austin
Job na Amarachi wakabaki kimya wakimtazama
“Nafahamu mmeshangaa lakini hatuna namna nyingine ya kufanya ili kuzipata sampuli hizo labda kwa kumueleza ukweli Monica kitu ambacho hatuwezi kukifanya.Kazi yetu ni kupata sampuli na kushughulikia kipimo na matokeo kumpa rais.Kwa hiyo usiku wa leo tutafanya zoezi hilo na tutachukua sampuli.Nitakwenda na Amarachi
katika zoezi hilo .Job wewe utabaki hapa
nyumbani ukiimarisha usalama hadi hapo tutakaporejea” akasema Austin
“Hakuna neno Austin tunakusikiliza wewe na neno lako ni
mwongozo kwetu.Tutafanya kama
ulivyoelekeza”
“Kuna jambo nataka nilishauri ndugu zangu” akasema Amarachi
“Kama mtakubaliana nami hakuna haja ya kupeleka sampuli nje ya nchi
kwa ajili ya kufanya kipimo cha vinasaba.Hapa hapa nchini kuna maabara nzuri za kisasa zenye uwezo mkubwa wa kufanya kipimo hicho na
kutoa majibu ndani ya muda mfupi.Pale Bernadetha hospital kuna maabara kubwa na nzuri sana .Kati ya siku moja
au mbili tutakuwa tumepata majibu.Kama hakuna sababu za msingi za kupeleka sampuli nje ya nchi
nashauri tufanyie kipimo hapa hapa nchini .Ninafahamiana na daktari mkuu wa maabara ile kwa hiyo nitawasiliana naye na baada tu ya kuzipata sampuli
nitaziwasilisha kwake kwa ajili ya
vipimo.”
“Wazo lako ni zuri sana na hata mimi nakubaliana nalo.Kuna ulazima gani wa kupeleka sampuli nje ya nchi? Akauliza Job
“Lengo la rais kutaka kipimo hicho kikafanyike nje ya nchi ni ili kuepuka uchakachuaji lakini ushauri wa
Amarachi ni mzuri na hata mimi nakubaliana nao kwa hiyo kipimo hicho tutakifanyia hapa hapa nchini katika maabara aliyoipendekeza Amarachi.Ahsante sana Amarachi kwa mara nyingine tena umekuwa ni
msaada mkubwa kwetu” akasema
Austin na wote wakatabasamu
“ Hilo la sampuli nadhani tumelimaliza .Kuna jambo lingine ambalo sikuwa nimewajulisha” akasema Job
“ Boaz na Maria wamefikia katika
hoteli moja.Nililifahamu hilo baada ya kuwapekua na kuwakuta wote na kadi za kufungulia milango ya hoteli
.Nilikwenda katika hoteli hiyo
nikachukua chumba nikalipia siku mbili halafu nikaingia katika chumba cha Monica .Nilichukua kompyuta yake iliyokuwa kitandani,pia nikachukua
pochi yake iliyokuwa na pesa na kadi
tatu za benki.Sikuweza kuingia kupekua katika chumba cha Boaz kwani tayari wahudumu walikuwa wameingia wakifanya usafi.Nilichofanikiwa
kukipata kwa Boaz ni simu yake tu.Nina uhakika tukiipekua kwa makini
tunaweza kupata kitu chochote cha kutusaidia katika uchunguzi wetu” akasema Job
“kazi nzuri Job.Vipi hali zao
zinaendeleaje? Akauliza Austin
“Wote wanaendelea vizuri
.Marcelo anawaandalia chakula.”akajibu
Austin
“Good” akasema Austin
“Nenda kavilete hivyo vifaa vyao tuanze kuvifanyia uchunguzi mara moja” akasema Austin
“Austin kwa nini usipumzike
kwanza halafu baada e ndipo tuifanye kazi hiyo ? Amarachi pia anahitaji kupumzika hajapumzika toka jana”akasema Job\
“Job hatuna muda wa kupumzika.Tuna kazi nyingi zinazotukabili kwa hiyo hatupaswi kupumzika.Kila dakika tunayoipata tunapaswa kuitumia vyema.Watu tunaowawinda nao pia wanatuwinda
.Tutapumzika tutakapokamilisha kazi” akasema Austin na Job akapanda ghorofani.Marcelo akaingia sebuleni
akiwa na sinia lenye mchanganyiko wa
vyakula Austin akatabasamu
“ Ahsante marcelo” akasema Amarachi akachukua bakuli la supu na kumnywesha Austin.Job akarejea akatabasamu,akaweka pembeni vifaa alivyokuja navyo naye akajipakulia chakula .Wakati wakiendelea kula akaja tena Dr Marcelo na sinia lingine lenye chakula
“ Chakula cha wageni wetu kiko tayari” akasema na Job akaacha kula wakaongozana na Marcelo hadi katika chumba alimofungwa Maria
,akaufungua mlango.Marcelo akamlisha chakula.Job hakutaka kumfungua .Maria alionekana kulemewa na njaa alimaliza chakula chote .Alipomaliza kula Job akamfungua akapelekwa chooni huku bastora ikiwa nyuma yake.Alionekana kudhoofika sana.Alijisaidia huku Job
akimtazama,hakutaka kumpa hata
sekunde moja akiwa peke yake.Alipomaliza akarejeshwa katika kile chumba akafungiwa katika kiti.Job akageuka na kupiga hatua kuondoka Maria akamuita
“ hey !! Job akageuka
“ How’s Austin? Is he dead? Akauliza Maria.Job akamsogelea.Marcelo aliyekuwa amesimama mlangoni akamuita
“ Job !!
Job akamtazama Maria kwa hasira na bila kusema chochote akageuka na kuondoka
“ Jaribu kupunguza hasira
Job.Nimekuona kila unapomuona Maria unakuwa na hasira kali.” Akasema Marcelo
“ Kila nikimtazama yule
mwanamke napatwa na hasira
kali.Alitaka kumuua Austin ambaye ni
mtu muhimu sana kwangu”
“ Austin ni mtu muhimu kwetu sote.Ameniokoa toka kwa watu
waliokuwa wananitafuta waniue na kwa bahati nzuri mtu ambaye ananitafuta
yuko humu humu ndani leo.” Akasema Marcelo Job akachukua chakula kilichobaki akamtaka Marcelo arejee sebuleni ,akaufungua mlango wa chumba alimo Boaz na bila
kumsemesha akamfungua mikono
akampa chakula ale.Boaz akamtazama
Job aliyekuwa amemsimamia na bastora akauliza
“ Whats the meaning of this? Nani
kawatuma mnifanyie hivi? Ni rais? Akauliza Boaz.Job hakujibu kitu
“Kijana unanifahamu mimi ni nani? Waliokutuma unifanyie hivi wamekudanghanya kijana wangu na
wamekuingiza katika moto.Mimi si mtu
wa kufanyiwa hivi.Mimi ni mtu mbaya sana lakini ninaweza kukusaidia.Ninzao pesa nyingi na ninaweza nikakupa kiasi kikubwa cha pesa ukaniachia huru na ninaweza kukusaidia hata ukaenda
mbali nje ya nchi ukayaanza maisha yako mapya.Ninakupa ofa hii kijana wangu uchague mwenyewe.” Akasema
Boaz
“ Eat !! akasema kwa ukali Austin na kumzuia Boaz asiendelee.Boaz akaonekana kukasirika na kulisukuma lile sinia la chakula chote kikamwagika.Job hakumsemesha akamfunga tena mikono
“Umemwaga chakula changu?Unajua ni pesa na muda gani vimetumika kuandaa chakula hiki? Ahsante tutaonana baadae” akasema
Job na kutoka mle chumbani akarejea
chini
“Wanaendeleaje Maria na Boaz? Akauliza Austin
“Wanaendelea vizuri.Maria alitaka kufahamu maendeleo yako lakini sikumjibu kitu” akasema Job
“ Good.Atafahamu baadae
ninaendeleaje” akasema Austin
“ I loved her with all my heart.Sikuwahi kufikiri kama Maria anaweza kuwa namna hii.Tuachane na hayo na tuendelee na zoezi letu” akasema Austin
“ Simu ya Boaz haikuzimwa na amepigiwa na watu kadhaa,wa kwanza ni Mukasha”
Wote wakatazamana .Job akaendelea
“Pili amepigiwa na mtu anaitwa
Peter chui.Ninamfahamu mtu mwenye
jina hili ambaye ni muuzaji mkubwa wa
magari hapa Dar es salaam.Sijui kama ni huyu aliyempigia Boaz au kuna Peter
chui mwingine.Tutafuatilia.Simu ya tatu
imetoka kwa Julieth”
Dr Marcelo aliyekuwepo pale sebuleni akastuka jina lile lilipotajwa.
“ Samahani Job unaweza kunitajia
namba za huyo Julieth? Akauliza Marcelo na Job akamtajia namba hizo.Mstuko mkubwa ukaonekana katika sura ya Marcelo.
“ Vipi Marcelo mbona umestuka? Unamfahamu Julieth?
“ namba hizo ni za Julieth dada yangu” akasema Marcelo na wote wakabaki na mshangao.Austin aliyekuwa amelala sofani akataka
kuinuka ili aketi lakini akagugumia kwa maumivu.
“Easy Austin…easy..” akasema Job
na kumsaidia Austin kuketi
“Nimestuka sana .Sikujua kama Julieth na Boaz wana mawasiliano” akasema Marcelo
“ Nilishangazwa awali imewezekanaje Boaz akawa na taarifa zote za Marcelo.Tayari jibu limepatikana kumbe Julieth ndiye
anayempa taarifa zako zote.We need to get her as quick as possible.Tukimpata huyu kuna mambo mengi tutayafahamu kuhusu Boaz.Marcelo unaweza
kutusaidia kumpata Julieth? Akauliza
Austin
“ Bado siamini jambo hili lakini nitawasaidia kumpata.” Akasema Marcelo
“ Kitu kingine tayari tunao uthibitisho kuwa Boaz na Mukasha wanawasiliana kwa hiyo lazima kuna
mambo Boaz anayafahamu kuhusu
Mukasha na mtandao wake,atatusaidia sana kuyajua” akasema Austin.
“ Kweli Austin,ulikuwa sahihi
kuhusu Boaz na Mukasha.Hawa ni watu wa karibu na tunatakiwa kuwachimba hadi mzizi wao” akasema Job
“Washa hiyo kompyuta ya
Maria.Tunatakiwa kuichunguza kwa makini na kuona kama kuna chochote tunaweza kukipata kinachoweza kutusaidia katika kumchunguza Maria.Hakutegemea kama angeweza kugundulika kwa hiyo naamini
hakupata muda wa kufuta mambo yake aliyohifadhi katika kompyuta yake.” Akasema Austin.Amarachi akaiwasha kompyuta ile lakini ilihitaji namba za
siri kufunguka.
“ Kunahitajika namba za siri kuifungua” akasema Amarachi
“ sawa tutashughulika naye baadae
kwa sasa tushughulikie kwanza kumpata Julieth.Marcelo chukua simu ya Amarachi mpigie simu Julieth mueleze kuwa unahitaji kumuona.Mwambie uko sehemu umejificha na utamtuma mtu aende
kumchukua.” Akasema Austin.Amarachi
akaziandika zile namba za Julieth katika simu yake akapiga na kumpa Marcelo simu
“hallow” Ikasema sauti ya mwanamke upande wa pili
“ hallow Julieth” akasema Marcelo
“ Marcelo ??!! akasema Julieth kwa mshangao baada ya kuitambua sauti ya mtu aliyempigia simu
“ Julieth tafadhali naomba usilitaje jina langu wala usiongee kwa nguvu kama uko karibu na watu wengi sogea pembeni tafadhali” akasema Marcelo
“ Marcelo unaendeleaje? Uko
wapi? Akauliza Julieth
“ Ninaendelea vizuri .Kwa sasa nimejificha sehemu Fulani kwa rafiki yangu.Vipi wewe unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri.Hofu kubwa ni kwako.Hatulali tunakuombea Mungu huko uliko uwe salama.Una hakika uko salama? Tafadhali nieleze mahali ulipo nahitaji sana kuonana nawe” akasema
Julieth
“Hata mimi nina hamu sana ya kuonana nawe lakini kwa sasa hali ya usalama si nzuri.Kuna watu wananitafuta waniue kwa hiyo
ninaweza kukuweka hata wewe katika
hatari”
“Hapana Marcelo nahitaji sana kukuona.Mimi ni ndugu yako na siogopi hata kama kuna hatari.Kuna jambo la
muhimu sana nataka kuzungumza
nawe” akasema Julieth
“Sawa Julieth.Namtuma rafiki yangu anakuja kukuchukua .Nielekeze mahala ulipo.Lakini naomba tafadhali usimueleze mtu yeyote kama
nimekupigia simu na hakikisha hakuna mtu anayejua unakwenda wapi”
“ Nimekulewa Marcelo nitakuwa makini sana.Muelekeze huyo rafiki yako hapa katika saluni yangu .Akifika
aegeshe gari na anipigie simu
anielekeze aina ya gari alimo na mimi nitatoka na kuingia moja kwa moja
katika gari hilo na kuondoka.” Akasema
Julieth
“ Ahsante Julieth.Ninamtuma rafiki yangu sasa hivi” akasema Marcelo na kukata simu .Jasho lilikuwa linamtoka usoni.
“ You did great” akasema Austin
“Job jiandae uende kumchukua
Julieth.Tahadhari kubwa inatakiwa katika zoezi hili” Akasema Austin na kabla Job hajajibu kitu simu ya Boaz ikaita.Mpigaji alikuwa Julieth
“ Julieth anampigia Boaz” akasema
Job
“ lazima lengo lake ni kumtaarifu
kuwa ameongea na Marcelo.Amarachi utaongozana na Job kwa nyuma ili kuimarisha ulinzi.Ninahisi kunaweza kuwa na hatari akienda Job peke yake.Huu ni matandao mkubwa” akasema Austin na mara ukaingia ujumbe katika simu ya Boaz
“Darling uko wapi leo? Mbona
nakupigia hupokei simu? Kuna jambo nataka kukueleza la muhimu mno naomba unipigie mara uupatapo ujumbe huu”
“Mhh !! Job akaguna
“ Ina maana Boaz na Julieth ni
wapenzi? !! akauliza Marcelo kwa mshangao
“ Mjibu huo ujumbe mwambie
kwamba uko katika kikao na huwezi kumpigia mwambie akwambae ana jambo gani anataka kukueleza?
Akasema Austin.Job akaandika ujumbe
na kumjibu Julieth na baada ya muda mfupi ukaingia ujumbe katika simu ya Boaz ulitoka kwa Julieth
“Pole sana darling.Nimepigiwa
simu na Marcelo sasa hivi yuko sehemu amejificha.Ninaelekea huko kwenda kuonana naye.Nitakupa taarifa zote nitakaporejea.”
Dr Marcelo alihisi kuchanganyikiwa.Uso wake ulionyesha hasira za wazi na machozi yakamlenga
“ Ndugu yangu wa damu kumbe
ndiye anayeniuza!!! Akasema kwa hasira
“ Pole sana Marcelo.Sasa
tumekwisha pata jibu la uhakika kwamba Julieth na Boaz ni washirika.Job na Amarachi tusipoteze muda nendeni mkamchukue Julieth mara moja.Umakini unatakiwa sana katika zoezi hili” akasema
Austin.Jobakapanda ghorofani akarejea na bastora mbili akampa moja Amarachi
“ Huko tuendako yanaweza yakatokea mapambano ,lazima tujiandae vya kutosha” akasema Job
“ Job please make sure you bring
Julieth here” akasisitiza Austin
“ usihofu Austin.Julieth atafika hapa ndani ya muda mfupi ujao” akasema Job na kuingia katika gari
lake.Amarachi naye akaingia katika gari
lake wakaondoka.
“ Nimeumia sana Austin.Kwa nini ndugu yangu wa damu anifanyie hivi? Kwa nini? Akauliza Marcelo
“ Marcelo maisha ya sasa yamebadilika sana .Ubinadamu hakuna
na watu wamekuwa wanajijali mno wao
wenyewe kuliko wenzao.Waliobobea katika maandiko wanasema kwamba haya yote yalitabiriwa yatatokea na tunashuhudia yanatokea kwa hiyo yasikuumize sana.Jipe moyo tuendelee na mapambano.Julieth analetwa hapa
na atatueleza kwa nini amefanya haya aliyoyafanya? Akasema Austin
“Austin inaniumiza mno dada yangu kunifanyia hivi.Analipwa kiasi gani na Boaz? Ngoja tumsubiri aje atueleze kila kitu” akasema
Marcelo.Austin akamtazama na kusema
“ Nilimuamini Maria kwa asilimia
mia moja kuwa ndiye mwanamke wa maisha yangu.Nilikuwa tayari kuachana na kila kitu kwa ajili yake.Sikuwahi kupenda kama nilivyompeda
.Alinionyesha upendo wa hali ya juu kiasi kwamba nilijiona mwanaume mwenye bahati kuliko wanaume wote duniani.Lakini kumbe nilikuwa najidanganya na Yule Yule ambaye
nilikuwa tayari kufanya lolote kwa ajili yake ndiye aliyetaka kunitoa uhai wangu.Kwa hiyo usiumie sana Marcelo.Si wewe peke yako
uliyeumizwa na mtu uliyemuamini.Matukio haya ya
kusalitiwa na wapendwa wetu yanatupa somo kuwa tusiwaamini sana watu
.Muda wowote wanaweza badilika na kutujeruhi.Muamini Mungu pekee yeye hawezi kubadilika .Yeye ni muaminifu
daima ,Mweleze siri zako atakutunzia”
akasema Austin na kwa mbali Marcelo akatabasamu
“ Umeongea maneno mazito hapa
mwisho Austin.Sikutegemea kama nawe kuna nyakati huwa unatafakari kuhusu Mungu” akasema Marcelo huku akitabasasmu
“ Who do you think I am? A devil? Akauliza Austin huku akicheka kidogo
“ Hapana simaanishi hivyo ila kwa namna ulivyo ukiwa kazini hakuna atakayeamini kuwa kuna wakati huwa unamkumbuka Mungu.Ukiwa kazini unakuwa mtu mwingine tofauti kabisa”
“Nakubaliana nawe Marcelo,kazi
hizi wakati mwingine hutufanya tutoke katika ubinadamu .Hata hivyo mimi ni msomaji mzuri wa maandiko na ninaamini katika Mungu.Nilipokuwa
Afrika ya kusini nilitaka kubadili maisha
yangu na kuanza maisha
mapya.Sikufikiria tena kufanya kazi hizi” akasema Austin na kunyamaza akafikiri kidogo kisha akamuomba Marcelo ampatie simu yake iliyokuwa mezani.Akazitafuta namba za rais akampigia
“ hallow Austin” akasema rais
“ Mheshimiwa rais,nimekupigia kukutaarifu kuwa tayari nimetoka hospitali na sasa niko nyumbani “
“ Nafurahi kusikia hivyo
Austin.JItahidi upate mapumziko ya kutosha.Kama kutatokea mabadiliko yoyote unitaarifu mara moja” akasema
rais
“ Ahsante mzee.Kuna jambo lingine nataka nikujulishe”
“ Sema Austin”
“ Ni kuhusu zile sampuli za nywele”
“ Ndiyo nakusikia”akasema rais
“ Baada ya kupata ufafanuzi toka kwa mtaalamu wa masuala haya ya vinasaba tumegundua kwamba zile sampuli hazitaweza kufaa kwani
inatakiwa nywele iliyong’olewa na mzizi wake.”
“Oh my God ! so what are we going
to do?
“Tutafanya hivi.Monica aliniomba nimuombee nafasi ya kuonana nawe kuna mambo ya msingi anataka
kuzungumza nawe.Hii ni nafasi nzuri ya kuweza kulifanya zoezi la kuchukua sampuli zinazotakiwa kwa
usahihi.Usiku wa leo nitaandaa chakula
kule katika ile nyumba uliyonipa
.Nitakuomba uhudhuria na Monica pia atahudhuria.Tutamuwekea dawa za usingizi katika kinywaji na akisha lala tutachukua sampuli tunazozihitaji
mbele yako na kisha tutamchoma
sindano ya kumzindua .Sampuli tunazozihitaji ni nywele ,damu kidogo,na kucha kama hatakuwa
ameweka kucha za bandia.Jambo lingine tumeona hakuna ulazima wowote wa kupeleka sampuli nje ya nchi kwa
kipimo wakati hata hapa Dar es salaam
kuna maabara kubwa zenye uwezo wa kufanya kipimo hicho na kutoa majibu ndani ya muda mfupi.Kwa hiyo mheshimiwa rais baada ya kuchukua sampuli hizo kipimo kitafanyika hapa hapa nchini.Hatutapeleka tena nje ya nchi” akasema Austin na kukaa kimya
“ Mheshimiwa rais !!..akaita Austin
“ Samahani Austin,nilikuwa natafakari kidogo haya uliyonieleza.Hata hivyo siwezi
kukukatalia jambo lolote ambalo wewe
unaona lina manufaa kwetu.Jioni ya leo
nitafika kwa ajili ya chakula kama
ulivyopanga.Hata mimi nina hamu sana ya kuonana na Monica” akasema rais
“ Ahsante sana mheshimiwa
rais.Nakushukuru kwa kukubali ombi langu.Tutaonana hiyo usiku”
“ Ahsante Austin” akasema rais na kukata simu
“ Rais amenielewa sasa ni zamu ya Monica.Naamini naye atanielewa pia” akawaza Austin na kuzitafuta namba za Monica akampigia
“ hallow my ghost” akasema Monica huku akicheka baada ya kupokea simu
“ Am I a ghost? Akauliza Austin
huku naye akicheka kidogo
“ Ofcourse you are.Only ghost can survive four bullets” akasema Monica kwa utani
“ Vipi maendeleo yako
Austin?Nimefurahi kusikia tena sauti yako”
“Ninaendelea vizuri .Tayari
nimetoka hospitali .Niko nyumbani napumzika”
“ King’ang’anizi sana wewe.Umeshinikiza hadi umeruhusiwa kutoka.Jitahidi upate mapumziko ya kutosha” akasema Monica
“ Nitajitahidi Monica” akasema Austin na kimya cha sekunde kadhaa kikapita.
“Monica nimekupigia simu kukujulisha kwamba nimezungumza na rais na ameomba kuonana nawe kama ulivyoomba.”
“ Austin tafadhali acha utani”
“ Sikutanii Monica.Kweli rais amekubali”
“ Oh my gosh.!.Thank you so much
Austin.Lini nitaonana naye?
“ leo usiku”
“ Tonight?!! Monica akashangaa
“ yes tonight” akasema Austin
“ Oh my gosh !! I can’t believe it.Nitaonana naye wapi?
“ At my place”
“Your place ?Monica akaonyesha mshangao kidogo
“ Yes at my place”
Monica akafikiri kidogo na kusema
“Sipafahamu nyumbani kwako”
“ Nitamtuma Amarachi atakuja kukuchukua.Anza kujiandaa kwa ajili ya chakula cha usiku na rais”
“ Ahsante Austin.Tutaonana hiyo jioni” akasema Monica na kukata simu na kuruka ruka kwa furaha
“ Sijui nitamlipa nini Austin kwa
hili alilonifanya kunikutanisha na rais.Ni
jambo kubwa ambalo sikuwa
nimelitegemea kabisa.Hatimaye baada ya kuonana na rais nitaonana pia na Marcelo.Nahitaji sana kufahamu maendeleo yake.Vile vile nataka afahamu kuwa mimi ndiye
niliyemsaidia na kwa pamoja tuone namna ya kuweza kumtoa hapa alipo ili aendelee na maisha yake.” Akawaza Monica
Dr Marcelo alipatwa na mshangao mkubwa aliposikia Austin akizungumza na Monica simuni
“Austin nimesikia unazungumza na Monica.Ni Monica yupi huyo? Akauliza.Austin akamtazama kwa sekunde kadhaa na kusema
“ Your friend.Monica Benedict mwamsole”
Uso wa Marcelo ukaonyesha
mshangao mkubwa
“ Do you know her? Akauliza
“ Yes I know her”
“ Oh ! Austin kwa nini hukunieleza awali kama unamfahamu Monica? I’ve been dying to see her.She’s the only friend I asked her to help me escape
from hospital.Toka hapo sijawahi kuonana naye tena .Austin tafadhali naomba unisaidie nionanae naye.Nakuomba sana Austin” akasema Marcelo.Austin akamtazama kwa muda na kusema
“UsijaliMarcelo utaonana naye lakini si sasa hivi”
“Tafadhali Austin nisaidie sana.” Akaendelea kuomba Marcelo
“ Marcelo kwa kuwa wewe ni mtu wetu wa karibu kuna jambo nataka nikuweke wazi.Monica ni mtoto wa
rais”
“ Mtoto wa rais? Marcelo
akashangaa
“ ndiyo.Ni mtoto wa rais.Hata rais mwenyewe amelijua hilo siku chache zilizopita na amenipa mimi kazi ya kutafuta sampuli toka kwa Monica kwa ajili ya kipimo cha vinasaba ili kuthibitisha kama kweli ni
mwanae.Kwa hiyo Marcelo zoezi hilo litakapokamilika nitakukutanisha na Monica”
“ Ahsante Austin kwa taarifa
hizo.Sampuli tayari mmezipata?
“ Bado hatujazipata ila tuko mbioni kuzipata”
“Austin naomba pale utakapopata
majibu ya kipimo unijulishe na mimi tafadhali.Monica ni mtu wangu wa muhimu sana”
“Nitakujulisha usijali” akasema
Austin na kumuomba Marcelo amuache apumzike”
********************