QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

Niwatakie usiku mwemwa mliopo nyumbani TZ. Mwanzo umekuwa wa kusuimbua kidogo, hata mwandiko na mpangilio haujawa mzuri, lakini mtapata vitu bora kadri siku zinavyoenda. karibuni
Ahsante sana Mkuu. Japo imekua fupi lakini hakuna namna. Je, hutaweza kushusha yote ili tubakie na arosto ya kusubiria sehemu ya 5?
 
Ahsante sana Mkuu. Japo imekua fupi lakini hakuna namna. Je, hutaweza kushusha yote ili tubakie na arosto ya kusubiria sehemu ya 5?
Sehemu ya 4 bado kabisa, kesho nitaweka tena. Pia nimeweka sehemu mbili, usije ukawa umeruka page ya nyuma.
 
Mkuu hilo ni jambo jema sana.ukitaka kununua bei yake ni.sh elfu 3000 tuu kwa seaeon moja. Hivyo kwa seaeon zote tano ni elfu 15 .

Uachane na usumbufu wa kusubilia hapa jf.lakini ukinunua huko kimya kimya.usije ukapeleka ya hapa ooooh mwanzo nilikuwa nasoma buleee jf pyee pyee pyee pyeeee.usije ukatuharibia kama wenzio walivyofanya na kusababisha kuwe na arosto ya mda mrefu sana.


Si muuuze tu hii huduma kuliko kila kukicha mnakuja na uwongo mwingine tutanunua tu kwan sh ngapi [emoji57]
 
Mkuu hilo ni jambo jema sana.ukitaka kununua bei yake ni.sh elfu 3000 tuu kwa seaeon moja. Hivyo kwa seaeon zote tano ni elfu 15 .

Uachane na usumbufu wa kusubilia hapa jf.lakini ukinunua huko kimya kimya.usije ukapeleka ya hapa ooooh mwanzo nilikuwa nasoma buleee jf pyee pyee pyee pyeeee.usije ukatuharibia kama wenzio walivyofanya na kusababisha kuwe na arosto ya mda mrefu sana.
Shida nikuwa hamuwi wakweli lege unajua kuongea ukweli huondoa utata wote
 
Sehemu ya 36

Job alirejea nyumbani kwake akaingia sebuleni na kumkuta Marcelo akiwa amekaa na bastora mkononi
“ habari za hapa marcelo? Kuna
tatizo lolote? Akauliza Job
“ Hapa ni salama hakuna tatizo
lolote” akajibu Marcelo .Job akapakua mizigo yote aliyokuja nayo akaipeleka jikoni akaihifadhi
“ Ulinieleza kuwa wewe ni mpishi mzu…” Job akanyamza baada ya simu yake kuita.Alikuwa ni Amarachi
“ hallo Amarachi.Vipi hali ya huko?
Nimeshindwa kuwasiliana nawe nilikuwa na mambo kadhaa ya kushughulikia asubuhi hii.Vipi hali ya Austin? Akauliza Job
“ Austin anaendelea vyema.Nimekupigia kukujulisha kuwa Austin anarejea nyumbani leo tayari madaktari wamethibitisha kuwa hakutakuwa na tatizo lolote.Hivi sasa tunajiandaa kurejea nyumbani hivyo anza kufanya maandalizi ya chumba atakamolala.” Akasema Amarachi
“ Dah ! Ahsante Amarachi kwa
taarifa.Nitalifanyia kazi hilo suala” akasema Job wakaagana ,akamtazama Marcelo kwa furaha
“ Austin ameruhusiwa kurejea nyumbani na hivi wanajiandaa kurejea.Bado atahitaji uangalizi kwa
hiyo hilo ni j ukumu lako kama daktari
kumuhudumia.Anza kuandaa chakula kwa ajili yake.Mimi ninakwenda
kuandaa chumba atakamolala” akasema Job na kupanda ghorofani akaihifadhi kompyuta aliyoitoa chumbani kwa
Maria halafu akakifungua chumba alimo
Maria
“Water please !!..akasema Maria kwa sauti ya chini .Job akamfuata na kumshika kichwani akamtazama kwa macho makali
“Sintakupa chochote.You are going
to die very slowly you devil !! akasema
na kumnasa kibao cha mgongo halafu
akatoka nje
“ Sijui kwa nini kila ninapomuona
Maria hubadilika ghafla na kupandwa na hasira za ghafla.Nitampa chakula apate nguvu,anaonekana kuanza
kudhoofika.Huyu ni mtu muhimu sana kwetu” akawaza na kuelekea katika chumba alimofungwa Boaz.Akawasha taa na kumtazama
“ Kijana naomba unifungue haraka sana.kwa nini unanifanyia hivi? Unataka nini toka kwangu? Pesa? Sema unataka kiasi gani? Nifungue haraka sana
niende zangu” akafoka Boaz
“ Halow Mr Boaz.Welcome to the hell and I’m your devil incharge here!! Akasema Job huku akitabasamu .Boaz akaogopa
“ Who are you? What do you want
from me? Akauliza
“ Endelea kupumzika
Boaz.Tutaonana baadae” akasema Job na kupiga hatua kutoka nje
“ You ‘ll pay for this I swear !!
akapiga ukelele Boaz,Job akaufunga mlango
“ Natamani muda ufike niwashughulikie hawa jamaa.Ni muda mrefu umepita sijafanya kazi.Boaz na mwanae wana bahati mbaya sana kukutana nami.Nitamuomba Austin aniruhusu niwafanyie mahojiano hawa watu na watajuta.Ni heri wakutane na shetani kuliko kukutana na mimi” akawaza akielekea chumbani kwake

****************
Monica akiwa bado chumbani
alimolazwa Austin ,simu yake ikaita alikuwa ni mama yake ,akatoka nje akaipokea
“ hallow mama” akasema
“Monica unafanya nini hapo? Lini umefahamiana na huyo Austin?
Akauliza Janet
“Mama Austin ni rafiki yangu.Sijafahamu naye muda mrefu ila kuna miradi tunataka kufanya kwa mashirikiano.Do you know him?
“ Hapana simfahamu ila Ernest ameniambia kuwa anaishi afrika kusini.Kuwa makini na hao vijana wanaotoka nje ya nchi.Angalia usije poteza mwelekeo”
“Ouh mama usiwe na hofu yoyote.Mimi na Austin ni marafiki wa kawaida na hakuna chochote kinachoendelea kati yetu zaidi ya
kushirikiana naye katika miradi .By the
way nataka kuonana nanyi mchana huu wewe na baba kuna jambo la muhimu sana nataka kuwaeleza”
“jambo gani tena? Kuna tatizo lolote?
“ Usiogope mama hakuna tatizo lolote.Ni jambo zuri na la muhimu sana
.Naomba umtaarifu baba kuwa tukutane pale Amboni city centre hotel mchana huu tupate chakula na niwaeleze hicho ninachotaka kuwaeleza.”
“ Sawa nitamtaarifu baba yako na ikiwezekana nitampitia kazini kwake nikamchukue ili asichelewe .Lakini Monica kuna jambo nataka nikuombe”
“ Omba mama.”
“ Naomba usimueleze baba yako chochote kuwa umeniona na rais.Naomba sana iwe siri yako”
akasema Janet na kumshangaza Monica
“Naweza kufahamu kwa nini
mama? Akauliza Monica
“ Monica mbona unaanza maswali mengi? Nakwambia usimueleze
chochote baba yako kuhusu kuniona pale hospitali na rais.Umenielewa? “Nimekuelewa mama”
“Good.Nampitia baba yako
tunatangulia utatukuta kule city centre.” Akasema Janet na kukata simu
“ Mhh !! Mbona simuelewi mama
.Kwa nini hataki baba afahamu kuhusu kuwaona yeye na rais? Mbona rais aliniambia kuwa yeye ni rafiki yao? Ngoja niachane na masuala yao yanawahusu wao wenyewe wazee.” Akawaza Monica akaingia chumbani kwa Austin wakaagana akaondoka
“Naamini niko karibu sana kuonana tena na Marcelo.Austin ameahidi kunikutanisha na rais na
lengo langu ni moja tu kumuomba
anieleze mahala alipo Marcelo.Naamini hataweza kukataa kutokana na mahusiano mazuri kati yake na mama
.Hata hivyo rais anaonekana ni mtu muungwana sana .Sifahamu Marcelo atakuwa katika hali gani hivi sasa,ila nataka afahamu kuwa mimi ndiye niliyemsaidia akatolewa pale hospitali.Naamini atakuwa anajiuliza maswali ni nani aliyemsaidia hadi akatoka hospitali? Akawaza Monica akiwa garini akielekea city centre kuonana na wazazi wake
“Nikipata nafasi ya kuonana na rais nitamuomba pia amsadie sana Marcelo dhidi ya watu wanaotaka kumuua.Yeye ni rais wa nchi anao uwezo mkubwa sana wa kumsaidia
.Sitakiwi kumuogopa.Natakiwa kuanza
kujenga mazoea na hawa wakubwa
kwani siku si nyingi nitaingia katika
ikulu ya Kinshasa” Monica akatabasamu Aliwasili Amboni City centre hotel akashuka garini akampigia simu mama
yake akamuuliza kama tayari wamefika.Mzee benedict mwamsole na mkewe bi Janet tayari walikwisha wasili pale hotelini ,wakamuelekeza Monica mahala walipokaa akawafuata
“Samahani kwa kuchelewa.Foleni ilikuwa ndefu sana”akasema Monica huku akiketi.Chakula kikaletwa wakaanza kula huku wakiendelea na maongezi mengine na utani.Baada ya chakula maongezi rasmi yakaanza.
“Haya Monica uwanja ni wako sasa
kutueleza kile ulichotuitia hapa” akasema mzee Benedict .Monica akatabasamu na kusema
“ Nilichowaitia hapa ni kuwapa
taarifa kuhusiana na suala langu na
David.Amenipigia simu mapema leo na
kunieleza kwamba hali ya mkewe Pauline imebadilika ghafla usiku na amekimbizwa Ufaransa kwa ajili ya upasuaji wa kichwa.Tumuombee sana kwani kwa mujibu wa David lolote linaweza kutokea.Jambo hili linaniumiza sana hasa nikikumbuka ukarimu wa Pauline namna alivyonipokea nilipokwenda Congo.Ni mwanamke mwenye roho nzuri sana.Natamani mngepata nafasi ya kukutana naye” akasema Monica na kulengwa na machozi.
“ Pole sana Monica.Jipe moyo mwanangu.Tutasimama nawe katika maombi na lolote litakalotokea basi tuwe tayari kulipokea kwani ndiyo mapenzi yake Mungu” akasema Mzee benedict
“Ahsante sana baba” akasema
Monica
“ Tukiachana na hilo kuna suala la pili nililoongea na David.Ameniambia kwamba tayari amekwisha andaa ujumbe mzito wa kuja kuonana nanyi kwa ajili ya kuanza mchakato wa uchumba.Ujumbe huo utaondoka Kinshasa leo alasiri na tutakutana nao kesho”
Uso wa Benedict mwamsole ukapambwa na tabasamu kubwa kwa taarifa ile ya Monica
“ Hizo ni habari njema sana .Rais
David ana nia ya dhati ya kutaka
kufunga nawe ndoa Monica.Una bahati kubwa sana kumpata mwanaume kama huyu” akasema Ben kwa furaha
“ Lakini mbona imekuwa ghafla sana? Kwa nini asingetupa nafasi ya kujiandaa kwanza? Ndugu wengine wa
muhimu wako mbali wanatakiwa
wawepo katika kikaoo hicho.Halafu sidhani kama itakuwa vizuri kukaa na kuzungumzia masuala ya uchumba wakati mkewe Pauline yuko mahututi hospitali.This is totaly unfair” akasema
Janet
“Nilimweleza hilo David lakini akagoma na akasema hawezi kuahirisha” akajibu Monica
“ David yuko sahihi kabisa.Mambo yamebadilika zama hizi.Kila kitu kinakwenda kwa mpangilio.Mke wake kulazwa hospitali si kigezo cha kuzuia mambo mengine yasiendelee.Yeye mwenyewe anafahamu kuwa mke wake hawezi kupona na ndiyo maana akaruhusu mchakato huu uendelee.Kwa hiyo kikao kitakuwepo na haijalishi
kama ndugu watakuwepo au
vipi.Watakaokuwa karibu watahudhuria
na wale watakaokuwa mbali watapewa
taarifa.Monica usihofu mama ujume huo tutaupokea na kujadiliana
nao.Tunaanza maandalizi ya suala hilo
kuanzia sasa” akasema Ben
********************

Baada ya kutoka hospitali Ernest Mkasa alirejea Ikulu .Hakwenda ofisini kwake bali alipitiliza chumbani kwake akaketi kitandani na kutafakari kwa muda halafu akachukua simu na
kumpigia mke wake.Simu ikaita mara ya kwanza bila kupokewa akapiga tena ikapokewa
“Una shida gani? Akauliza Agatha baada ya kupokea simu
“Hello Agatha” akasema Ernest
kwa sauti ya upole
“Niambie una shida gani” akauliza
Agatha kwa ukali
“I need to see you.Uko wapi? “Unataka kuonana nami? Umekwishaandaa karatasi za talaka?
Akauliza Agatha
“Agatha please stop that. I need to see you. I want to talk to you” akasema Ernest kwa sauti ya ukali
“ Niko katika hiki chumba ulichonipa niishi” akasema Agatha.Ernest akamfuata.Akaufungua mlango na kuingia ndani akaketi
sofani.Wakatazamana kwa muda Ernest akasema
“ How’re you?
“ You real want to know how I’m doing? Gosh ! Ernest why are you so cruel? Ninaumwa toka jana na hujathubutu hata kunijulia hali.What kind of a man are you? What a
devil,what a cruel husband !!! akasema
Agatha
“Stop calling me devil.Nimekwisha kukanya kuniita hivyo.kwa nini kila wakati unataka tulumbane? What kind
of a woman are you? Akasema Ernest kwa ukali
“ I hate you Ernest.Nikikuona
natamani hata kutapika.Sema haraka shida yako iliyokuleta utoke humu ndani.Najuta kwa nini nilikupenda mwanaume kama wewe usiye na hata chembe ya huruma.” Akasema Agatha
“ You never loved me.There was no love between us,it was all lies!!
Akasema Ernest kwa ukali na kusimama
akamtazama Agatha
“ Kama ungekuwa na hata chembe moja ya mapenzi kwangu
usingenifanyia haya
uliyonifanyia.Usingenifikisha hapa
uliniponifikisha. Usingewatoa kafara
watoto wangu kwa shetani wako unayemuabudu.Tena naomba ukae kimya kabisa usiendelee kunitibua na kunipandisha hasira” akasema Ernest.Agatha akakaa kimya na macho yake yakaonekana kulengwa na
machozi alipokumbushwa kuhusu
watoto wake.
“Kwa hiyo Ernest nini kimekuleta hapa chumbani kwangu? Sit and tell
me” akasema Agatha.Ernest akaketi
sofani
“Nataka kuzungumza nanyi”
“ Kuzungumza nasi? Mimi na nani?
“ Ninyi Alberto’s.Nataka uwaambie wakuu wako kwamba nataka tukutane kesho kutwa na asikose hata mmoja”
Agatha akamtazama kwa makini na kusema
gani?
“ Unataka kuzungumza nasi jambo
“ Nataka kuweka makubaliano kati
yetu.Kuna mambo ambayo nataka tukubaliane ili niwape nafasi ya kufanikisha mambo yenu.I don’t want to fight with you.Nafahamu athari zitakazoipata nchi endapo tutaendelea kupambana kwa hiyo nataka tuwe na makubaliano maalum ili kila upande ufaidike.Ninyi mfanye mambo yenu na mimi nibaki huru kama rais.Sitaki kuwekwa kama kivuli .Nataka mniachie madaraka yangu kama mkuu wa nchi.Kama tutakubaliana katika mambo hayo basi mtapata nafasi ya kuendelea
na mambo yenu bila matatizo”
“ Kwa hiyo ni hilo tu la kutakakuwa huru ndilo limekufanya uikafanya haya mambo yote uliyoyafanya? Kwa nini usingesema
mapema shida yako hadi ukaturudisha
nyuma kiasi hiki? Akauliza Agatha
“ Agatha fikisha ujumbe huo kwa wenzako wakubali tuzungumze tuyamalize mambo haya kwani malumbano hayatatufikisha kokote.Kesho jioni nahitaji jibu kama wako tayari tukae mezani kwa mazungumzo” akasema Ernest na kuinuka akajiandaa kuondoka
“Sawa nitawaeleza lakini naomba uwe na nia ya dhati na si kutupotezea wakati wetu” akasema Agatha na kumtazama Ernest
“ Loot at youErnest.Kitu gani kilikuingia na kukudanganya .Siku zote huwezi wewe peke yako ukapambana
na Alberto’s.Wewe kwa Alberto’s ni sawa na mchanga ambao unaweza ukapeperushwa sekunde yoyote na upepo. Nitalifikisha ombi lako kwa
wenzangu na kesho nitakupa jibu”
akasema Agatha
“ Thank you” akajibu Ernest akaanza kuondoka
“ You are not going to ask? Akauliza Agatha.Ernest akageuka
“ Ask what? Akauliza
“ Nilikwambia ninaumwa.Hutaki kujua ninaumwa nini?
“ Hapana sihitaji kujua” akajibu
Ernest
“ Why Ernest? Why are you doing this to me? Kwa nini umetengeneza tabaka hili kubwa kati yetu?
“ Stop Agatha .There is no us.Me and you we’re over.Kilichobaki ni makaratasi tu lakini katika mioyo yetu
hakuna ndoa tena.Ukomo wa penzi letu ni pale ulipowatoa kafara watoto wangu
kwa shetani wako” akasema Ernest
huku akimtazama Agatha kwa hasira
kisha akatoka
“ Natamani nikuweke upofu Ernest lakini siruhusiwi kufanya hivyo
japokuwa uwezo huo ninao.Nani lakini kambadilisha Ernest namna hii? Aliyemshauri awageuke Alberto’s alimdanganya sana na sasa mambo yameanza kumuendeea kombo hadi anataka makubaliano na sisi. Kitu pekee ambacho nitawashauri wenzangu tukifanye kama anataka makubaliano
na sisi ni kumshauri aachie madaraka
kwa hiari yake mwenyewe ili tuteue rais mwingine.Endapo akikataa basi hatutakubali kuwa na majadiliano naye tena” akawaza Agatha
Baada ya kutoka chumbani kwa Agatha,Ernest akarejea chumbani kwake na kumpigia simu mkuu wa magereza wakaongea kwa takribani
dakika tano halafu akaagiza helkopta ya
rais iwekwe tayari alihitaji kuitumia.Ilipokuwa tayari akataarifiwa akapanda na helkopta ikapaa kuelekea katika gereza kuu la Uwangwa.
Ilimchukua dakika kumi na mbili kuwasili katika gereza hili kubwa lililojengwa katika kisiwa cha Uwangwa kilichopo ndani ya bahari ya hindi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.Gereza
hili kubwa lilikuwa maalum kwa ajili ya wafungwa wale waliohukumuwa
vifungo virefu,vifo au wale wahalifu
sugu kama majambazi na magaidi.Ulinzi wake ulikuwa mkali mno.
Helkopta ya rais ikatua katika eneo
maalum kwa helkopta kutua rais akashuka akalakiwa na mkuu wa gereza ambaye alimtambulisha kwa baadhi ya maafisa wa gereza lile kisha
wakaelekea ofisini
“ karibu sana mheshimiwa rais
hapa gereza la uwangwa.” Akasema mkuu wa gereza walipoingia ofisini kwake
“ Ahsante sana.Nadhani maagizo yangu yamefanyiwa kazi” akasema rais
“ Ndiyo mheshimiwa rais.Maagizo yako tayari yamefanyiwa kazi .Kila kitu kiko tayari” akasema mkuu wa gareza wakatoka mle ofisini wakaelekea katika chumba Fulani.Rais akawaomba walinzi wake wabaki nje akafunguliwa mlango akaingia ndani.Mtu mmoja mwenye nywele ndefu na ndevu nyingi aliyefungwa mikono na miguu kwa minyororo alikuwemo mle
chumbani.Rais akamtazama kwa sekunde kadhaa halafu akavuta kiti akaketi
“ Tariq Abdulkarim!! Akasema Rais
“ Who are you? Akauliza Yule
jamaa kwa sauti kavu ya kukwaruza
“ Ernest Mkasa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.”
Tariq akastuka sana kusikia Yule aliyesimama mbele yake ni rais wa Tanzania.Akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Nimefungwa katika chumba cha chini kabisa ya gereza hili kwa zaidi ya miaka saba sasa na sina habari kama Tanzania kuna rais mpya.Namfahamu rais aliyekuwepo madarakani wakati nafungwa alikuwa ni rais Ferdinand”
Ernest akameza mate na kusema
“ Ferdinand alifariki dunia na mimi ndiye rais kwa sasa”
“Mungu amesikia na kujibu maombi yangu ya kumuondoa Ferdinand duniani.Alikuwa ni adui
yangu mkubwa na kama nisingefungwa
hapa gerezani ningemuua mimi”
akasema Tariq
“ Tariq ulikuwa mratibu mkuu wa mashambulio yote yanayofanywa na Alshabaa hasa yale makubwa yaliyofanyika Kenya na Somalia.Serikali ya Kenya inakutafuta kwa udi na
uvumba kwa kosa la kupanga
shambulio katika chuo kikuu cha
Nairobi lililoua wanafunzi zaidi ya mia mbili .Unatafutwa na serikali ya Somalia kwa kupanga shambulio lililosababisha vifo vya watu mia tatu katika uwanja wa michezo.Serikali za Kenya na Somalia
zote hazina taarifa kama unashikiliwa nchini Tanzania.Nilipochukua madaraka nilishauriwa nikukabidhi kwa serikali
ya Somalia lakini sikufanya hivyo” akanyamaza akamtazama Tariq halafu aakendelea
“ Nimekuja mimi mwenyewe
kukutaarifu kuwa pamoja na hayo yote uliyoyafanya nataka nikuachie huru nikurejeshe kwa kundi lako la Alshabaab.”
Tariq akacheka na kusema
“ Nafahamu unao uwezo wa kuniachia huru lakini si kirahisi rahisi namna hiyo.Niambie unahitaji kitu gani toka kwangu? Akauliza Tariq
“ Ni kweli kuna kitu nakihitaji toka kwako.
“ Unahitaji nini?
“ nahitaji kuzungumza na kiongozi mkuu wa Alshabaab.Sina mawasiliano yake na sijui namna ya kumpata hivyo nimekuja kwako ili uniunganishe naye.”
“ Unataka kuzungumza na kiongozi wa Alshabaab? Kuna watanzania wametekwa nyara?
“Nipe mawasiliano na kiongozi
wako .Kuhusu nini nataka kuzungumza naye ni mambo yasiyo kuhusu”
Ilimchukua Tariq zaidi ya dakika
tatu kufumbua mdomo wake na kusema
“ Nimechoka kukaa humu ndani.Nitakusaidia uzungumze na kiongozi wetu anaitwa Habib Alzaraq.Huwezi kumfikia yeye mwenyewe .Unapaswa uzungumze
kwanza na msaidizi wake anaitwa Aziz.” akasema Tariq na kumtajia rais namba Fulani akapiga kisha akaiweka simu katika sauti kubwa na kuiweka mezani.
“ hallow” ikasema sauti ya upande wa pili.Tariq akaanza kuzungumza na mtu Yule wa upande wa pili kwa lugha
ya kisomali ambayo Ernest hakuielewa.Baada ya dakika nne za maongezi Tariq akamtazama rais
“ Subiri baada ya muda kidogo
utazungumza na Habib.” Akasema Tariq na baada ya dakika mbili kupita
ikasikika sauti nzito
“ Tariq !!
Tariq akazungumza na mtu Yule kwa zaidi ya dakika kumi kwa lugha ya kisomali halafu akamtazama rais
“ haya zungumza na habib”
Ernest akaichukua simu na kuita
“ hallow Habib”
“ mheshimiwa rais.Nimeambiwa kwamba unahitaji kuzungumza nami.Imenishangaza kidogo kwani mimi ni adui wa marais wengi wa dunia hii
.Wewe ni rais wa kwanza kutaka
kuzungumza nami moja kwa moja.Niambie unahitaji nini? Akasema Habib
“Habib kuna jambo nataka
kuzungumza nawe lakini naomba
kwanza nitoke hapa ndani niende nje
sehemu tulivu ili tuzungumze vizuri.Usikate simu tafadhali” akasema Ernest na kutoka mle ndani.Akaongozana na walinzi wake hadi nje akawataka wasogee mbali anataka kuzungumza na simu
“Hallow habib” akaita
“ Hallow mheshimiwa rais
,nakusikia “ akasema habib
“ Habib kuna jambo nataka unisaidie”
“ Unahitaji msaada wa Alshabaab?
“ Ndiyo habib”
“Msaada upi unahitaji?
“ Kesho kutwa kuna majengo
mawili nataka kuyalipua .Moja ni hoteli iko hapa Dar es salaam na lingine ni jengo la bunge mjini Dodoma.”
“ Mhh !!.Habib akaguna
“ Kuna nini hadi ukafikia maamuzi
hayo? Nimestuka kusikia kwamba unataka kulipua ukumbi wa bunge.”
“ usitake kujua kwa nini
Habib.Naomba nisikilize vizuri.Haya ni matukio makubwa ambayo hayajawahi kutokea hapa nchini kwetu na damu nyingi itamwagika hasa za viongozi kwa hiyo basi nataka baada tu ya
mashambulio hayo kutokea Alshabaab wajitokeze na kudai kuwa wao ndio wahusika wakuu wa mashambulio hayo yote mawili .Sababu kuu ya kufanya mashambulio hayo ni kuitaka serikali ya Tanzania iwaondoe wanajeshi wake wanaolifundisha jeshi la Somalia.”
Ukapita ukimya mfupi Habib akasema
“Mheshimiwa rais hilo ni tukio kubwa sana na kwa namna yoyote ile Alshabaab tukidai kuhusika na
shambulio hilo hatutakuwa na dirisha la
kutokea kwani tutapigwa toka kila upande .Hata hivyo bado tunaweza kuzungumza na tukakubaliana .Nini
utatupatia kama malipo yetu kwa jambo
hilo?
“ Nitawapatia Tariq.Nafahamu ni mtu wenu wa muhimu sana na
mmekuwa mkimtafuta kwa muda mrefu bila kujua mahala aliko.” Akasema
Ernest na Habib akaangua kicheko
“Kuubeba mzigo mzito namna hiyo kwa ajili ya Tariq? Hiki ni kichekesho
.Tariq hatuko naye kwa zaidi ya miaka mitano na bado shughuli zetu zinaendelea kama kawaida na Alshabaab imeendelea kuwa
tishio.Tariq si mtu muhimu sana kwetu” “kwa hiyo mnahitaji nini? Akauliza
Ernest
“ Tunahitaji kitu chenye thamani
kinachoweza kuendana na mzigo huo mzito tutakaobeba “
“Nini basi mnahitaji? Pesa?
“Hatuhitaji pesa .Tunazo za kutosha kujiendesha na ziada.Nipe muda nikae na makamanda wangu
tujadili jambo hili.Nitakupigia simu leo
saa tano usiku nitakwambia tunachokihitaji” akasema Habib na kukata simu.Ernest akarejea katika helkopta na kurejea ikulu

*******************
 
Sehemu ya 37

Wakiwa na nyuso zenye furaha,
Job na Dr Marcelo walilizunguka gari la
Amarachi ambalo ndani yake alikuwemo Amarachi na Austin waliowasili wakitokea hospitali.Job
akaufungua mlango wa upande aliokaa
Austin.
“ karibu nyumbani Austin”
“ Ahsante Job” akajibu Austin
“ Hallow Austin” akasema Dr
Marcelo
“ Hallo Marcelo” akasema Austin
“ Pole sana Austin”akasema
Marcelo akionekana kuwa na hofu
“ Ahsante” akajibu Austin.Job akamshusha Austin akamtegemeza na kumpeleka sebuleni.
“ Pole sana Austin.Vipi maendeleo yako,unajisikiaje? Akauliza Job
“ Ahsnate sana Job.Naendelea vizuri.maumivu ni ya kawaida sehemu zile zilizofanyiwa upasuaji .habari za hapa? Akawaza Austin
“ habari nzuri.hakuna tatizo.Usalama umedhibitiwa hapa na ndiyo maana hujaniona
hospitali.Nilimuachia Amarachi
majukumu yote ya hospitali”
“ Good.Ahsante sana nyote kwa juhudi mlizofanya kuokoa maisha yangu.Nipe ripoti ya operesheni yetu tumefikia wapi? Nini tayari kumefanyika hadi hivi sasa? Akauliza Austin .Kabla Job hajajibu Marcelo akasimama
“ Samahani jamani.Kuna jambo nataka niseme kabla maongezi hayajaendelea” akanyamaza na kumuelekezea macho Austin
“ Austin napenda nichukue nafasi hii kukuomba msamaha sana kwa
jambo la kijinga nililolifanya
lililopelekea haya yote yakatokea.Umenusurika kifo kwa sababu ya ujinga wangu.Maria aliniambia nimfungue akajisaidie na
mimi nikashikwa na huruma nikadhani
ninatenda wema.Nisamehe sana Austin”
akasema Marcelo na kupiga magoti
“ Inuka Marcelo” akasema Austin
“ Siwezi kukulaumu kwa ulichokifanya kwani hukutegemea kama jambo lile lingetokea.Hakuna kati yetu aliyetegemea kama Maria angeweza
kuwa mtu hatari.Naamini kwa
kilichotokea kuna funzo umelipata .Sina tatizo nawe Dr Marcelo tuungane sote katika mapambano haya.Wewe ndiye uliyenifumbua macho kuhusu Maria
kwa hiyo napaswa mimi kusema ahsante sana” akasema Austin .Dr
Marcelo akainuka na kumfuata Marcelo akampa mkono
“Ahsante Marcelo.Ahsante sana
.Mapema leo nilizungumza na Job nikamueleza kwamba mimi pia ni mwenzenu japokuwa sina utaalamu wowote wa mambo ya upelelezi lakini
bado naweza kuwa na msaada hata
mdogo.Mimi ni daktari nitawahudumia pale mtakapohitaji matibabu kwa mfano kwa sasa Austin yuko hapa nyumbani ni jukumu langu kumuhudumia.Naombeni msinibague .Nioneni ni mwenzenu mnitumie kila pale mtakapohitaji
msaada wangu” akasema Dr Marcelo
“ Marcelo wewe ni mwenzetu na usihisi kutengwa.Tunahitaji sana msaada wako japokuwa kuna wakati unaweza kuona kama hatukushirikishi
ni kutokana na mambo yetu haya kuwa ya hatari ,lakini fahamu kuwa una msaada mkubwa kwetu” akasema
Austin na kuwatazama akina Job
“ Job na Amarachi naomba mtambue rasmi kuwa huyu anaitwa Dr Marcelo Yuko chini ya ulinzi wangu .Ni mtu ambaye tunapaswa kumlinda kwa
kila namna .Suala lake ni kubwa na
mtalifahamu hapo baadae”
“ Karibu sana Marcelo”akasema
Amarachi
“Ahsanteni sana nyote.Naomba sasa nielekee jikoni kuandaa chakula” akasema Marcelo na kuelekea jikoni
“ Job nilikuuliza awali kuhusu ni
wapi tumefikia katika operesheni yetu? Akauliza Austin
“Tulipofikia mpaka sasa ni kwamba Maria tunaye hapa ndani na leo hii tumempata pia baba yake Boaz.Pongezi kubwa kwa Amarachi
kwani ndiye aliyefanikisha kumdhibiti Maria na leo hii ndiye aliyemleta Boaz” “Ahsante Amarachi kwa yote
uliyoyafanya.Mungu alikuleta kwa wakati muafaka.Umefanya kazi kubwa ambayo sikuwa nimeitegemea kabisa”
“Ahsante Austin kwa kuniamini”
akasema Amarachi
“ Now let’s get back to work.Tunatakiwa kwanza kufahamu huyu Maria ni nani.Sote tumeshuhudia kitu alichokifanya ambacho hakuna aliyekitegemea kwa hiyo ni mtu hatari zaidi ya tunavyodhani .Lengo la
kumpata Boaz lilikuwa ni kupata taarifa za kumuhusu Mukasha ambaye rais alikuwa amefikiria kumteua kuwa
waziri mkuu.Jana usiku Job ulimueleza
rais kuhusiana na uchunguzi tunaoufanya juu ya Mukasha.Kwa bahati nzuri hatuna tena haja ya kuendelea na uchunguzi huo kwani
tayari rais ametuamini kwa hiyo ombi letu limejibiwa na amebadili mawazo ya kumteua Mukasha kuwa waziri mkuu.”akasema Austin
“ Oh thank you Lord” akasema Job
“ Boaz tutamuhoji kuhusu suala la
Marcelo kwani ndiye anayemtafuta kwa gharama kubwa na alinipa mimi kazi ya kumtafuta.Tunapaswa kufahamu kwa
nini anamtafuta Marcelo? Pamoja na rais kutuamini kuhusu Mukasha lakini bado tutaendelea kumfuatilia hadi tufahamu mtandao wake wote.Tutamfikia hadi huyu bilionea anayejita dogo Bill na tutahakikisha tunampata mtoto Millen ”
Sura ya Job ikabadilika baada ya
Austin kumtaja mwanae Millen.Austin akamtazama kwa muda na kusema
“ Jambo lingine ni kwamba rais alinipa kazi ya kutafuta sampuli toka kwa Monica kwa ajili ya kipimo cha vinasaba .Kazi hiyo tayari imekamilika na tunayo sampuli ya nywele toka kwa Monica na rais.Kinachofuata ni
kuziwasilisha sampuli hizo maabara nje
ya nchi kwa ajiliya kipimo hicho na
Amarachi utasimamia zoezi hilo.Rais ameahidi kutupa ushirikiano mkubwa.Nitazungumza naye baadae ikiwezekana iwepo ndege maalum kwa ajili ya kupeleka sampuli hizo nje ya
nchi kwa vipimo.Kwa umuhimu wa suala hili rais hataweza kukataa” akasema Austin
“Austin samahani kidogo.Umesema kwamba tayari
tumepata sampuli ya nywele ya Monica
na rais kwa ajili ya kipimo cha vinasaba.Monica ana husiana na rais? Akauliza Amarachi
“Amarachi kuna mambo kadhaa
unahitaji kuyafahamu kuhusiana na operesheni hii inayoendelea na moja wapo ya mambo unayopaswa kufahamu ni hili la kuhusiana na hiki kipimo cha vinasaba tunachotaka kukifanya.Kwa
ufupi ni kwamba rais Ernest
amefahamishwa hivi karibuni na mwanamke ambaye aliwahi kuwa na mahusiano naye enzi za ujana wake kwamba wakati wa mahusiano yao waliwahi kupata mtoto ambaye ndiye Monica.Rais anataka kufanya kipimo cha vinasaba ili kupata uhakika kama kweli Monica ni mwanae”
“ Mpaka hapo nimekuelewa Austin lakini Monica anafahamu chochote
kuwa rais ni baba yake mzazi?
“ hapana bado hafahamu chochote.Rais anataka kwanza afanye kipimo kwa siri na akihakikisha kuwa kweli ni mwanae basi atamueleza ukweli wote.” Akasema Austin
“ Nashukuru Austin kwa kunielewesha lakini kuna kitu na mimi nataka kuchangia katika suala hili.Uliponiambia nichukue nywele ya
Monica sikuelewa kama ulihitaji kwa
ajili ya kipimo hiki cha vinasaba.Kwa kawaida unapohitaji sampuli ya nywele kwa ajili ya kufanya kipimo cha
vinasaba unatakiwa kuipata nywele ambayo imeanzia katika mzizi wake.Hii tuliyonayo haifai kutumika kama
sampuli kwa sababu niliikata tu bila
kuchukua na mzizi wake.Kwa mujibu wa wataalamu usahihi wa kipimo cha vinasaba kwa kutumia sampuli ya
nywele ni asilimia 80.Sampuli nyingine
ambayo inaweza kuwa nzuri zaidi ni kucha halisi,usahihi wake ni asilimia
95.Tunaweza pia kutumia sampuli nyingine kama vile mswaki lakini unahitajika mswahi uliotumika kwa muda huo huo kwani hewa hukausha mswaki ndani ya dakika thelathini.” Akasema Amarachi na kuwatazama Austin na Job
“Ahsante sana Amarachi kwa
darasa hilo zuri.Mimi sikuwa na
ufahamu wowote kuhusiana na mambo haya ya kipimo cha vinasaba.Kwa maelezo hayo uliyoyatoa ni wazi kwamba hatuna sampuli hapa.”
Akasema Austin
“ Ndiyo hatuna sampuli
.Tunatakiwa kutafuta sampuli zinazofaa na si hizi tulizo nazo” akasema Amarachi.Austin akafumba macho akazama mawazoni halafu akasema
“ This is what we’re going to do” akasema na kunyamaza kidogo halafu akaendelea
“ Monica aliniambia nimsaidie
kuonana na rais ana maongezi naye binafsi.Nitaongea na rais na lazima atakubali kuonana naye .Nataka iwe ni usiku wa leo.Tutakutana pale katika nyumba ya rais aliyonipa niishi kwa
chakula cha usiku.Tutamuwekea
Monica dawa ya usingizi katika kinywaji na halafu tutachukua sampuli tunazozitaka” akasema Austin
Job na Amarachi wakabaki kimya wakimtazama
“Nafahamu mmeshangaa lakini hatuna namna nyingine ya kufanya ili kuzipata sampuli hizo labda kwa kumueleza ukweli Monica kitu ambacho hatuwezi kukifanya.Kazi yetu ni kupata sampuli na kushughulikia kipimo na matokeo kumpa rais.Kwa hiyo usiku wa leo tutafanya zoezi hilo na tutachukua sampuli.Nitakwenda na Amarachi
katika zoezi hilo .Job wewe utabaki hapa
nyumbani ukiimarisha usalama hadi hapo tutakaporejea” akasema Austin
“Hakuna neno Austin tunakusikiliza wewe na neno lako ni
mwongozo kwetu.Tutafanya kama
ulivyoelekeza”
“Kuna jambo nataka nilishauri ndugu zangu” akasema Amarachi
“Kama mtakubaliana nami hakuna haja ya kupeleka sampuli nje ya nchi
kwa ajili ya kufanya kipimo cha vinasaba.Hapa hapa nchini kuna maabara nzuri za kisasa zenye uwezo mkubwa wa kufanya kipimo hicho na
kutoa majibu ndani ya muda mfupi.Pale Bernadetha hospital kuna maabara kubwa na nzuri sana .Kati ya siku moja
au mbili tutakuwa tumepata majibu.Kama hakuna sababu za msingi za kupeleka sampuli nje ya nchi
nashauri tufanyie kipimo hapa hapa nchini .Ninafahamiana na daktari mkuu wa maabara ile kwa hiyo nitawasiliana naye na baada tu ya kuzipata sampuli
nitaziwasilisha kwake kwa ajili ya
vipimo.”
“Wazo lako ni zuri sana na hata mimi nakubaliana nalo.Kuna ulazima gani wa kupeleka sampuli nje ya nchi? Akauliza Job
“Lengo la rais kutaka kipimo hicho kikafanyike nje ya nchi ni ili kuepuka uchakachuaji lakini ushauri wa
Amarachi ni mzuri na hata mimi nakubaliana nao kwa hiyo kipimo hicho tutakifanyia hapa hapa nchini katika maabara aliyoipendekeza Amarachi.Ahsante sana Amarachi kwa mara nyingine tena umekuwa ni
msaada mkubwa kwetu” akasema
Austin na wote wakatabasamu
“ Hilo la sampuli nadhani tumelimaliza .Kuna jambo lingine ambalo sikuwa nimewajulisha” akasema Job
“ Boaz na Maria wamefikia katika
hoteli moja.Nililifahamu hilo baada ya kuwapekua na kuwakuta wote na kadi za kufungulia milango ya hoteli
.Nilikwenda katika hoteli hiyo
nikachukua chumba nikalipia siku mbili halafu nikaingia katika chumba cha Monica .Nilichukua kompyuta yake iliyokuwa kitandani,pia nikachukua
pochi yake iliyokuwa na pesa na kadi
tatu za benki.Sikuweza kuingia kupekua katika chumba cha Boaz kwani tayari wahudumu walikuwa wameingia wakifanya usafi.Nilichofanikiwa
kukipata kwa Boaz ni simu yake tu.Nina uhakika tukiipekua kwa makini
tunaweza kupata kitu chochote cha kutusaidia katika uchunguzi wetu” akasema Job
“kazi nzuri Job.Vipi hali zao
zinaendeleaje? Akauliza Austin
“Wote wanaendelea vizuri
.Marcelo anawaandalia chakula.”akajibu
Austin
“Good” akasema Austin
“Nenda kavilete hivyo vifaa vyao tuanze kuvifanyia uchunguzi mara moja” akasema Austin
“Austin kwa nini usipumzike
kwanza halafu baada e ndipo tuifanye kazi hiyo ? Amarachi pia anahitaji kupumzika hajapumzika toka jana”akasema Job\
“Job hatuna muda wa kupumzika.Tuna kazi nyingi zinazotukabili kwa hiyo hatupaswi kupumzika.Kila dakika tunayoipata tunapaswa kuitumia vyema.Watu tunaowawinda nao pia wanatuwinda
.Tutapumzika tutakapokamilisha kazi” akasema Austin na Job akapanda ghorofani.Marcelo akaingia sebuleni
akiwa na sinia lenye mchanganyiko wa
vyakula Austin akatabasamu
“ Ahsante marcelo” akasema Amarachi akachukua bakuli la supu na kumnywesha Austin.Job akarejea akatabasamu,akaweka pembeni vifaa alivyokuja navyo naye akajipakulia chakula .Wakati wakiendelea kula akaja tena Dr Marcelo na sinia lingine lenye chakula
“ Chakula cha wageni wetu kiko tayari” akasema na Job akaacha kula wakaongozana na Marcelo hadi katika chumba alimofungwa Maria
,akaufungua mlango.Marcelo akamlisha chakula.Job hakutaka kumfungua .Maria alionekana kulemewa na njaa alimaliza chakula chote .Alipomaliza kula Job akamfungua akapelekwa chooni huku bastora ikiwa nyuma yake.Alionekana kudhoofika sana.Alijisaidia huku Job
akimtazama,hakutaka kumpa hata
sekunde moja akiwa peke yake.Alipomaliza akarejeshwa katika kile chumba akafungiwa katika kiti.Job akageuka na kupiga hatua kuondoka Maria akamuita
“ hey !! Job akageuka
“ How’s Austin? Is he dead? Akauliza Maria.Job akamsogelea.Marcelo aliyekuwa amesimama mlangoni akamuita
“ Job !!
Job akamtazama Maria kwa hasira na bila kusema chochote akageuka na kuondoka
“ Jaribu kupunguza hasira
Job.Nimekuona kila unapomuona Maria unakuwa na hasira kali.” Akasema Marcelo
“ Kila nikimtazama yule
mwanamke napatwa na hasira
kali.Alitaka kumuua Austin ambaye ni
mtu muhimu sana kwangu”
“ Austin ni mtu muhimu kwetu sote.Ameniokoa toka kwa watu
waliokuwa wananitafuta waniue na kwa bahati nzuri mtu ambaye ananitafuta
yuko humu humu ndani leo.” Akasema Marcelo Job akachukua chakula kilichobaki akamtaka Marcelo arejee sebuleni ,akaufungua mlango wa chumba alimo Boaz na bila
kumsemesha akamfungua mikono
akampa chakula ale.Boaz akamtazama
Job aliyekuwa amemsimamia na bastora akauliza
“ Whats the meaning of this? Nani
kawatuma mnifanyie hivi? Ni rais? Akauliza Boaz.Job hakujibu kitu
“Kijana unanifahamu mimi ni nani? Waliokutuma unifanyie hivi wamekudanghanya kijana wangu na
wamekuingiza katika moto.Mimi si mtu
wa kufanyiwa hivi.Mimi ni mtu mbaya sana lakini ninaweza kukusaidia.Ninzao pesa nyingi na ninaweza nikakupa kiasi kikubwa cha pesa ukaniachia huru na ninaweza kukusaidia hata ukaenda
mbali nje ya nchi ukayaanza maisha yako mapya.Ninakupa ofa hii kijana wangu uchague mwenyewe.” Akasema
Boaz
“ Eat !! akasema kwa ukali Austin na kumzuia Boaz asiendelee.Boaz akaonekana kukasirika na kulisukuma lile sinia la chakula chote kikamwagika.Job hakumsemesha akamfunga tena mikono
“Umemwaga chakula changu?Unajua ni pesa na muda gani vimetumika kuandaa chakula hiki? Ahsante tutaonana baadae” akasema
Job na kutoka mle chumbani akarejea
chini
“Wanaendeleaje Maria na Boaz? Akauliza Austin
“Wanaendelea vizuri.Maria alitaka kufahamu maendeleo yako lakini sikumjibu kitu” akasema Job
“ Good.Atafahamu baadae
ninaendeleaje” akasema Austin
“ I loved her with all my heart.Sikuwahi kufikiri kama Maria anaweza kuwa namna hii.Tuachane na hayo na tuendelee na zoezi letu” akasema Austin
“ Simu ya Boaz haikuzimwa na amepigiwa na watu kadhaa,wa kwanza ni Mukasha”
Wote wakatazamana .Job akaendelea
“Pili amepigiwa na mtu anaitwa
Peter chui.Ninamfahamu mtu mwenye
jina hili ambaye ni muuzaji mkubwa wa
magari hapa Dar es salaam.Sijui kama ni huyu aliyempigia Boaz au kuna Peter
chui mwingine.Tutafuatilia.Simu ya tatu
imetoka kwa Julieth”
Dr Marcelo aliyekuwepo pale sebuleni akastuka jina lile lilipotajwa.
“ Samahani Job unaweza kunitajia
namba za huyo Julieth? Akauliza Marcelo na Job akamtajia namba hizo.Mstuko mkubwa ukaonekana katika sura ya Marcelo.
“ Vipi Marcelo mbona umestuka? Unamfahamu Julieth?
“ namba hizo ni za Julieth dada yangu” akasema Marcelo na wote wakabaki na mshangao.Austin aliyekuwa amelala sofani akataka
kuinuka ili aketi lakini akagugumia kwa maumivu.
“Easy Austin…easy..” akasema Job
na kumsaidia Austin kuketi
“Nimestuka sana .Sikujua kama Julieth na Boaz wana mawasiliano” akasema Marcelo
“ Nilishangazwa awali imewezekanaje Boaz akawa na taarifa zote za Marcelo.Tayari jibu limepatikana kumbe Julieth ndiye
anayempa taarifa zako zote.We need to get her as quick as possible.Tukimpata huyu kuna mambo mengi tutayafahamu kuhusu Boaz.Marcelo unaweza
kutusaidia kumpata Julieth? Akauliza
Austin
“ Bado siamini jambo hili lakini nitawasaidia kumpata.” Akasema Marcelo
“ Kitu kingine tayari tunao uthibitisho kuwa Boaz na Mukasha wanawasiliana kwa hiyo lazima kuna
mambo Boaz anayafahamu kuhusu
Mukasha na mtandao wake,atatusaidia sana kuyajua” akasema Austin.
“ Kweli Austin,ulikuwa sahihi
kuhusu Boaz na Mukasha.Hawa ni watu wa karibu na tunatakiwa kuwachimba hadi mzizi wao” akasema Job
“Washa hiyo kompyuta ya
Maria.Tunatakiwa kuichunguza kwa makini na kuona kama kuna chochote tunaweza kukipata kinachoweza kutusaidia katika kumchunguza Maria.Hakutegemea kama angeweza kugundulika kwa hiyo naamini
hakupata muda wa kufuta mambo yake aliyohifadhi katika kompyuta yake.” Akasema Austin.Amarachi akaiwasha kompyuta ile lakini ilihitaji namba za
siri kufunguka.
“ Kunahitajika namba za siri kuifungua” akasema Amarachi
“ sawa tutashughulika naye baadae
kwa sasa tushughulikie kwanza kumpata Julieth.Marcelo chukua simu ya Amarachi mpigie simu Julieth mueleze kuwa unahitaji kumuona.Mwambie uko sehemu umejificha na utamtuma mtu aende
kumchukua.” Akasema Austin.Amarachi
akaziandika zile namba za Julieth katika simu yake akapiga na kumpa Marcelo simu
“hallow” Ikasema sauti ya mwanamke upande wa pili
“ hallow Julieth” akasema Marcelo
“ Marcelo ??!! akasema Julieth kwa mshangao baada ya kuitambua sauti ya mtu aliyempigia simu
“ Julieth tafadhali naomba usilitaje jina langu wala usiongee kwa nguvu kama uko karibu na watu wengi sogea pembeni tafadhali” akasema Marcelo
“ Marcelo unaendeleaje? Uko
wapi? Akauliza Julieth
“ Ninaendelea vizuri .Kwa sasa nimejificha sehemu Fulani kwa rafiki yangu.Vipi wewe unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri.Hofu kubwa ni kwako.Hatulali tunakuombea Mungu huko uliko uwe salama.Una hakika uko salama? Tafadhali nieleze mahali ulipo nahitaji sana kuonana nawe” akasema
Julieth
“Hata mimi nina hamu sana ya kuonana nawe lakini kwa sasa hali ya usalama si nzuri.Kuna watu wananitafuta waniue kwa hiyo
ninaweza kukuweka hata wewe katika
hatari”
“Hapana Marcelo nahitaji sana kukuona.Mimi ni ndugu yako na siogopi hata kama kuna hatari.Kuna jambo la
muhimu sana nataka kuzungumza
nawe” akasema Julieth
“Sawa Julieth.Namtuma rafiki yangu anakuja kukuchukua .Nielekeze mahala ulipo.Lakini naomba tafadhali usimueleze mtu yeyote kama
nimekupigia simu na hakikisha hakuna mtu anayejua unakwenda wapi”
“ Nimekulewa Marcelo nitakuwa makini sana.Muelekeze huyo rafiki yako hapa katika saluni yangu .Akifika
aegeshe gari na anipigie simu
anielekeze aina ya gari alimo na mimi nitatoka na kuingia moja kwa moja
katika gari hilo na kuondoka.” Akasema
Julieth
“ Ahsante Julieth.Ninamtuma rafiki yangu sasa hivi” akasema Marcelo na kukata simu .Jasho lilikuwa linamtoka usoni.
“ You did great” akasema Austin
“Job jiandae uende kumchukua
Julieth.Tahadhari kubwa inatakiwa katika zoezi hili” Akasema Austin na kabla Job hajajibu kitu simu ya Boaz ikaita.Mpigaji alikuwa Julieth
“ Julieth anampigia Boaz” akasema

Job
“ lazima lengo lake ni kumtaarifu
kuwa ameongea na Marcelo.Amarachi utaongozana na Job kwa nyuma ili kuimarisha ulinzi.Ninahisi kunaweza kuwa na hatari akienda Job peke yake.Huu ni matandao mkubwa” akasema Austin na mara ukaingia ujumbe katika simu ya Boaz
“Darling uko wapi leo? Mbona
nakupigia hupokei simu? Kuna jambo nataka kukueleza la muhimu mno naomba unipigie mara uupatapo ujumbe huu”
“Mhh !! Job akaguna
“ Ina maana Boaz na Julieth ni
wapenzi? !! akauliza Marcelo kwa mshangao
“ Mjibu huo ujumbe mwambie
kwamba uko katika kikao na huwezi kumpigia mwambie akwambae ana jambo gani anataka kukueleza?
Akasema Austin.Job akaandika ujumbe
na kumjibu Julieth na baada ya muda mfupi ukaingia ujumbe katika simu ya Boaz ulitoka kwa Julieth
“Pole sana darling.Nimepigiwa
simu na Marcelo sasa hivi yuko sehemu amejificha.Ninaelekea huko kwenda kuonana naye.Nitakupa taarifa zote nitakaporejea.”
Dr Marcelo alihisi kuchanganyikiwa.Uso wake ulionyesha hasira za wazi na machozi yakamlenga
“ Ndugu yangu wa damu kumbe
ndiye anayeniuza!!! Akasema kwa hasira
“ Pole sana Marcelo.Sasa
tumekwisha pata jibu la uhakika kwamba Julieth na Boaz ni washirika.Job na Amarachi tusipoteze muda nendeni mkamchukue Julieth mara moja.Umakini unatakiwa sana katika zoezi hili” akasema
Austin.Jobakapanda ghorofani akarejea na bastora mbili akampa moja Amarachi
“ Huko tuendako yanaweza yakatokea mapambano ,lazima tujiandae vya kutosha” akasema Job
“ Job please make sure you bring
Julieth here” akasisitiza Austin
“ usihofu Austin.Julieth atafika hapa ndani ya muda mfupi ujao” akasema Job na kuingia katika gari
lake.Amarachi naye akaingia katika gari
lake wakaondoka.
“ Nimeumia sana Austin.Kwa nini ndugu yangu wa damu anifanyie hivi? Kwa nini? Akauliza Marcelo
“ Marcelo maisha ya sasa yamebadilika sana .Ubinadamu hakuna
na watu wamekuwa wanajijali mno wao
wenyewe kuliko wenzao.Waliobobea katika maandiko wanasema kwamba haya yote yalitabiriwa yatatokea na tunashuhudia yanatokea kwa hiyo yasikuumize sana.Jipe moyo tuendelee na mapambano.Julieth analetwa hapa
na atatueleza kwa nini amefanya haya aliyoyafanya? Akasema Austin
“Austin inaniumiza mno dada yangu kunifanyia hivi.Analipwa kiasi gani na Boaz? Ngoja tumsubiri aje atueleze kila kitu” akasema
Marcelo.Austin akamtazama na kusema
“ Nilimuamini Maria kwa asilimia
mia moja kuwa ndiye mwanamke wa maisha yangu.Nilikuwa tayari kuachana na kila kitu kwa ajili yake.Sikuwahi kupenda kama nilivyompeda
.Alinionyesha upendo wa hali ya juu kiasi kwamba nilijiona mwanaume mwenye bahati kuliko wanaume wote duniani.Lakini kumbe nilikuwa najidanganya na Yule Yule ambaye
nilikuwa tayari kufanya lolote kwa ajili yake ndiye aliyetaka kunitoa uhai wangu.Kwa hiyo usiumie sana Marcelo.Si wewe peke yako
uliyeumizwa na mtu uliyemuamini.Matukio haya ya
kusalitiwa na wapendwa wetu yanatupa somo kuwa tusiwaamini sana watu
.Muda wowote wanaweza badilika na kutujeruhi.Muamini Mungu pekee yeye hawezi kubadilika .Yeye ni muaminifu
daima ,Mweleze siri zako atakutunzia”
akasema Austin na kwa mbali Marcelo akatabasamu
“ Umeongea maneno mazito hapa
mwisho Austin.Sikutegemea kama nawe kuna nyakati huwa unatafakari kuhusu Mungu” akasema Marcelo huku akitabasasmu
“ Who do you think I am? A devil? Akauliza Austin huku akicheka kidogo
“ Hapana simaanishi hivyo ila kwa namna ulivyo ukiwa kazini hakuna atakayeamini kuwa kuna wakati huwa unamkumbuka Mungu.Ukiwa kazini unakuwa mtu mwingine tofauti kabisa”
“Nakubaliana nawe Marcelo,kazi
hizi wakati mwingine hutufanya tutoke katika ubinadamu .Hata hivyo mimi ni msomaji mzuri wa maandiko na ninaamini katika Mungu.Nilipokuwa
Afrika ya kusini nilitaka kubadili maisha
yangu na kuanza maisha
mapya.Sikufikiria tena kufanya kazi hizi” akasema Austin na kunyamaza akafikiri kidogo kisha akamuomba Marcelo ampatie simu yake iliyokuwa mezani.Akazitafuta namba za rais akampigia
“ hallow Austin” akasema rais
“ Mheshimiwa rais,nimekupigia kukutaarifu kuwa tayari nimetoka hospitali na sasa niko nyumbani “
“ Nafurahi kusikia hivyo
Austin.JItahidi upate mapumziko ya kutosha.Kama kutatokea mabadiliko yoyote unitaarifu mara moja” akasema
rais
“ Ahsante mzee.Kuna jambo lingine nataka nikujulishe”
“ Sema Austin”
“ Ni kuhusu zile sampuli za nywele”
“ Ndiyo nakusikia”akasema rais
“ Baada ya kupata ufafanuzi toka kwa mtaalamu wa masuala haya ya vinasaba tumegundua kwamba zile sampuli hazitaweza kufaa kwani
inatakiwa nywele iliyong’olewa na mzizi wake.”
“Oh my God ! so what are we going
to do?
“Tutafanya hivi.Monica aliniomba nimuombee nafasi ya kuonana nawe kuna mambo ya msingi anataka
kuzungumza nawe.Hii ni nafasi nzuri ya kuweza kulifanya zoezi la kuchukua sampuli zinazotakiwa kwa
usahihi.Usiku wa leo nitaandaa chakula
kule katika ile nyumba uliyonipa
.Nitakuomba uhudhuria na Monica pia atahudhuria.Tutamuwekea dawa za usingizi katika kinywaji na akisha lala tutachukua sampuli tunazozihitaji
mbele yako na kisha tutamchoma
sindano ya kumzindua .Sampuli tunazozihitaji ni nywele ,damu kidogo,na kucha kama hatakuwa
ameweka kucha za bandia.Jambo lingine tumeona hakuna ulazima wowote wa kupeleka sampuli nje ya nchi kwa
kipimo wakati hata hapa Dar es salaam
kuna maabara kubwa zenye uwezo wa kufanya kipimo hicho na kutoa majibu ndani ya muda mfupi.Kwa hiyo mheshimiwa rais baada ya kuchukua sampuli hizo kipimo kitafanyika hapa hapa nchini.Hatutapeleka tena nje ya nchi” akasema Austin na kukaa kimya
“ Mheshimiwa rais !!..akaita Austin
“ Samahani Austin,nilikuwa natafakari kidogo haya uliyonieleza.Hata hivyo siwezi
kukukatalia jambo lolote ambalo wewe
unaona lina manufaa kwetu.Jioni ya leo
nitafika kwa ajili ya chakula kama
ulivyopanga.Hata mimi nina hamu sana ya kuonana na Monica” akasema rais
“ Ahsante sana mheshimiwa
rais.Nakushukuru kwa kukubali ombi langu.Tutaonana hiyo usiku”
“ Ahsante Austin” akasema rais na kukata simu
“ Rais amenielewa sasa ni zamu ya Monica.Naamini naye atanielewa pia” akawaza Austin na kuzitafuta namba za Monica akampigia
“ hallow my ghost” akasema Monica huku akicheka baada ya kupokea simu
“ Am I a ghost? Akauliza Austin
huku naye akicheka kidogo
“ Ofcourse you are.Only ghost can survive four bullets” akasema Monica kwa utani
“ Vipi maendeleo yako
Austin?Nimefurahi kusikia tena sauti yako”
“Ninaendelea vizuri .Tayari
nimetoka hospitali .Niko nyumbani napumzika”
“ King’ang’anizi sana wewe.Umeshinikiza hadi umeruhusiwa kutoka.Jitahidi upate mapumziko ya kutosha” akasema Monica
“ Nitajitahidi Monica” akasema Austin na kimya cha sekunde kadhaa kikapita.
“Monica nimekupigia simu kukujulisha kwamba nimezungumza na rais na ameomba kuonana nawe kama ulivyoomba.”
“ Austin tafadhali acha utani”
“ Sikutanii Monica.Kweli rais amekubali”
“ Oh my gosh.!.Thank you so much
Austin.Lini nitaonana naye?
“ leo usiku”
“ Tonight?!! Monica akashangaa
“ yes tonight” akasema Austin
“ Oh my gosh !! I can’t believe it.Nitaonana naye wapi?
“ At my place”
“Your place ?Monica akaonyesha mshangao kidogo
“ Yes at my place”
Monica akafikiri kidogo na kusema
“Sipafahamu nyumbani kwako”
“ Nitamtuma Amarachi atakuja kukuchukua.Anza kujiandaa kwa ajili ya chakula cha usiku na rais”
“ Ahsante Austin.Tutaonana hiyo jioni” akasema Monica na kukata simu na kuruka ruka kwa furaha
“ Sijui nitamlipa nini Austin kwa
hili alilonifanya kunikutanisha na rais.Ni
jambo kubwa ambalo sikuwa
nimelitegemea kabisa.Hatimaye baada ya kuonana na rais nitaonana pia na Marcelo.Nahitaji sana kufahamu maendeleo yake.Vile vile nataka afahamu kuwa mimi ndiye
niliyemsaidia na kwa pamoja tuone namna ya kuweza kumtoa hapa alipo ili aendelee na maisha yake.” Akawaza Monica
Dr Marcelo alipatwa na mshangao mkubwa aliposikia Austin akizungumza na Monica simuni
“Austin nimesikia unazungumza na Monica.Ni Monica yupi huyo? Akauliza.Austin akamtazama kwa sekunde kadhaa na kusema
“ Your friend.Monica Benedict mwamsole”
Uso wa Marcelo ukaonyesha
mshangao mkubwa
“ Do you know her? Akauliza
“ Yes I know her”
“ Oh ! Austin kwa nini hukunieleza awali kama unamfahamu Monica? I’ve been dying to see her.She’s the only friend I asked her to help me escape
from hospital.Toka hapo sijawahi kuonana naye tena .Austin tafadhali naomba unisaidie nionanae naye.Nakuomba sana Austin” akasema Marcelo.Austin akamtazama kwa muda na kusema
“UsijaliMarcelo utaonana naye lakini si sasa hivi”
“Tafadhali Austin nisaidie sana.” Akaendelea kuomba Marcelo
“ Marcelo kwa kuwa wewe ni mtu wetu wa karibu kuna jambo nataka nikuweke wazi.Monica ni mtoto wa
rais”
“ Mtoto wa rais? Marcelo
akashangaa
“ ndiyo.Ni mtoto wa rais.Hata rais mwenyewe amelijua hilo siku chache zilizopita na amenipa mimi kazi ya kutafuta sampuli toka kwa Monica kwa ajili ya kipimo cha vinasaba ili kuthibitisha kama kweli ni
mwanae.Kwa hiyo Marcelo zoezi hilo litakapokamilika nitakukutanisha na Monica”
“ Ahsante Austin kwa taarifa
hizo.Sampuli tayari mmezipata?
“ Bado hatujazipata ila tuko mbioni kuzipata”
“Austin naomba pale utakapopata
majibu ya kipimo unijulishe na mimi tafadhali.Monica ni mtu wangu wa muhimu sana”
“Nitakujulisha usijali” akasema
Austin na kumuomba Marcelo amuache apumzike”
********************
 
Mkuu Nemesis kama vipi iweke yote kabisa tujue hii imemalizika watu tuweze kufokasi kwenye mambo mengine badala ya Monica!!
Miezi minne Sasa tangu tuanze kusumbuana Na LEGE!!
 
ha ha ha! LEGE ndiyo kamanda wetu bila yeye tungebaki arosto, hapa nafanya kwa hisani yake tu. Mzigo upo msihofu, utashuka. Weekend hii lazima tumalize Season 4 yote, then tutamsubiri LEGE kwa season 5 ambayo ndiyo coras ya riwaya hii.
Twende kazi mkuu
 
Back
Top Bottom