SEHEMU YA 48
kumpata mwanaume ambaye ataufanya
moyo wangu usimame.Kidogo Dr Marcelo
alikuwa anakaribia kufikia vigezo vyangu
na niliamini ni mwanaume pekee
anayeweza kunifaa lakini suala hili la
ugonjwa tayari limeweka doa mipango
yangu.It’s obvious siwezi kuwa na
mahusiano ya kimapenzi na Dr Marcelo
tena badala yake ataendelea kuwa rafiki
yangu wa karibu sana.Inaniuma lakini
sina
namna
nyingine
ya
kufanya.Yawezekana labda Marcelo
hakuwa fungu langu ,sintokata tamaa
nitaendelea kumlilia Mungu ili siku moja
aniletee mwanaume ambaye amemuandaa
kwa ajili yangu.” Akaendelea kuwaza
Monica
Aliwasili katika makazi ya
Daniel,akafunguliwa geti akaingia ndani
,akashuka garini na moja kwa moja
akaelekea sebuleni.Daniel akataarifiwa
kuwa Monica tayari amekwisha wasili
akashuka haraka kwenda kuonana naye.
“ Monica ..’ akasema Daniel kwa
furaha huku uso wake ukiwa katika
tabasamu ,akamsogelea Monica na kutaka
kumkumbatia ,akamzuia
“ Monica kuna tatizo gani? Mbona
unaonekana hauko sawa? Akauliza
Daniel.Monica akamtazama kwa macho
makali na kulitupa lile faili mezani
“ Daniel mimi na wewe tumekuwa
watu wa karibu sana na sikutegemea
kabisa kama ungeweza ukafanya kitu cha
kijinga kama hiki ulichokifanya.” Akasema
Monica kwa ukali Daniel akabaki na
mshangao
“ Monica kuna nini? Akauliza Daniel
“Unajifanya hujui ulichokifanya?
Ninashukuru ulichotaka nikifahamu
nimekifahamu lakini nakuhakikishia
kwamba
hautakipata
kamwe
ulichokikusudia.” Akasema Monica.Daniel
akalichukua lile faili na kulifungua,sura
yake ikaonyesha mstuko mkubwa
“ Monica what is this? Akauliza
Daniel
“ Unajifanya hujui kilichomo humo?
Akauliza Monica
“ Monica hili ni faili linalomuhusu Dr
Marcelo !!
“ Ulitaka nifahamu kuhusu ugonjwa
wa Dr Marcelo ? Nashukuru umenisaidia
nimeufahamu lakini nakuhakikishia
kwamba jambo unaloliota katu
halitakuwa.Ulitaka niufahamu ugonjwa
wake ili nisiwe karibu naye kwani lengo
lako ni kuwa na mimi lakini
nakuhakikishia kwamba kwa hilo
umekosea sana.Mimi nitaendelea kuwa na
Dr Marcelo kwani ni mtu ambaye
nimemchagua kuwa rafiki yangu wa
karibu na hata kama nikiamua kuingia
katika mahusiano naye ya kimapenzi
hakuna wa kunizuia kwa hilo na sintojali
ugonjwa wake kwani ndiye mwanaume
anayenifaa . “ akasema Monica kwa hasira
“ Monica naomba unisikilize kwa
makini.Mimi sijafanya jambo kama hili na
katu siwezi kufanya kitu kama hiki za
zaidi ya yote nimekuwa karibu na Dr
Marcelo na sikuwahi kulifahamu jambo
hili.Hajawahi
kunieleza
kama
anasumbuliwa na maradhi ya saratani ya
damu.Kingine ni kwamba ni kweli mimi na
Dr Marcelo tulipishana kauli lakini sina
sababu yoyote ya kufanya hivi hata kama
ningekuwa nafahamu kuhusu ugonjwa
wake.Nimekuwa nawe karibu kwa muda
mrefu unanifahamu vizuri sina tabia kama
hivi.