QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

mkuu LEGE hii ya leo inaitwa mwanaukome.....daaadekiii....!!!.....keep it on....
 
Mkuu Lege Tuwekee Japo Viwili vya kulalia Tusherehekee\Tuhuzunikie Ushindi Wa Mnyamaaaaa
Kubwa la Maadui Mfalme wa Nyika Baba La Baba.....
 
Mkuu Lege Tuwekee Japo Viwili vya kulalia Tusherehekee\Tuhuzunikie Ushindi Wa Mnyamaaaaa
Kubwa la Maadui Mfalme wa Nyika Baba La Baba.....
Mkuu Lege Tuwekee Japo Viwili vya kulalia Tusherehekee\Tuhuzunikie Ushindi Wa Mnyamaaaaa
Kubwa la Maadui Mfalme wa Nyika Baba La Baba.....
mkuu sio viwili vya kulalia bali leo nataka tukeshe wote jf wapenda story wotee msiniangushe.ili siku ninapo banwa na majukum msilalamike sanaa now nishaseti mambo nataka nianze kuachia mwendelezo mpaka season ya 1 iishe tuanze season ya pili
 
Ni makusudi na maringo tu
APA ukute anatuchora na acc nyingine na kujifanya mmoja wa wanataka story,
Ana
Unaah Huyu
Kila akiweka story matatizo , wakati ukitizama mahudhurio yake huko nyuma sii hivi
Acha unaa
Luge
mkuu vipi ushamalizaa kusoma ?? kizuri kula na nduguyo mkuu hapa ndio kijiweni kwetu kamwe siwezi kuwaangusha nipatapo nafasi kama hivi leo .na siku huwa hazifanani mkuu ukiona G usiwe unamind sana coz kunamaisha nje ya jf
 
mkuu vipi ushamalizaa kusoma ?? kizuri kula na nduguyo mkuu hapa ndio kijiweni kwetu kamwe siwezi kuwaangusha nipatapo nafasi kama hivi leo .na siku huwa hazifanani mkuu ukiona G usiwe unamind sana coz kunamaisha nje ya jf
Unataka tuyamalize weka kwanza mzigo
Hapa kasi tu! Nshamaliza kitambo
 
6726f4b32d81167414498e1eed17ac1c.jpg
 
mkuu sio viwili vya kulalia bali leo nataka tukeshe wote jf wapenda story wotee msiniangushe.ili siku ninapo banwa na majukum msilalamike sanaa now nishaseti mambo nataka nianze kuachia mwendelezo mpaka season ya 1 iishe tuanze season ya pili
Tunasubiri, tuko tayari kabisa... @TeamMasimulizi
 
SEHEMU YA 8T

“ Baba ulisema jana nisiondoke bila kuja
kukuona.Kuna jambo lolote ulitaka
kunieleza? Akauliza Monica wakiwa garini
wakielekea hospitali
“ Ndiyo Monica .Kuna jambo ambalo
tunataka kuzungumza nawe lakini
itakuwa ni baadae tukiwa pamoja na
mama yako.”
“ Ni jamb......” akasema Monica lakini
mara simu yake ikaita,akazitambua
namba zile
“ David Zumo” akasema na kumfanya
mzee Ben atabsamu
“ Pokea” akasema
“ Hallow mheshimiwa rais”
“ Hallow Monica habari za asubuhi?
Umeamka salama?
“ Nimeamka salama mheshimiwa
rais sijui wewe”
“ Nimeamka salama Monica.Vipi hali
ya rafiki yako?
“ Hivi sasa ninaelekea hospitali
kujua hali yake lakini hadi jana usiku hali
yake ilikuwa inaendelea vizuri.”
“ Sawa Monica nimekupigia
kukujulia hali na vile vile kukufahamisha
kuwa asubuhi ya leo nitaondoka kurejea
Kongo .Nimefurahi sana kukutana nawe
ana kwa ana na ningependa sana kama
ningeweza kuonana nawe kabla ya
kuondoka lakini kutokana na majukumu
uliyonayo haitawezekana ila tutazidi
kuwasiliana” akasema David
“ Ahsante sana mheshimiwa
rais.Ninashukuru sana kwa msaada
mkubwa ulionisaidia.Nakuombea usafiri
salama natumai tutazidi kuwasiliana”
“ Ahsante Monica.Karibu sana
Kongo.Nitakutumia mwaliko rasmi wa
kuja kutembea Kongo”
“ Sawa nitashukuru sana
mheshimiwa rais” akasema Monica
“ Kwa heri Monica” akasema David
na kukata simu
“ He’s a good person” akasema mzee
Ben baada ya Monica kumaliza
kuzungumza na David
“ Ndyo baba,David zumo ni mtu
mzuri ana roho nzuri.Anapenda sana
kusaidia” akajibu Monica na safari
ikaendelea hadi walipofika hospitali.
Tayari Daniel na watu wengine
walikwisha fika pale hospitali kumtazama
Dr Marcelo ambaye alikuwa anaendelea
vizuri.Tayari alikwisha fumbua macho
lakini hakuweza kuongea .Bado tukio
lililotokea la Dr Marcelo kurejea na uhai
baada ya kuwa amekwisha thibitishwa
kufariki liliendelea kuwa vinywani mwa
watu na wengi walitaka kuthibitisha kama
tukio lile ni kweli limetokea.
Monica na baba yake waliondoka
pale hospitali baada ya kuridhika kuwa
hali ya Dr Marcelo ilikuwa inaendelea
vizuri.Moja kwa moja walirejea nyumbani
Monica akaenda chumbani kwake
kujiandaa kwa ajili ya kuelekea kazini
kwake,mzee Ben naye akaelekea
chumbani kwake ambako alimkuta
mkewe Jane
“ Anaendeleaje Dr Marcelo? Akauliza
Jane
“ Anaendelea vizuri ,amekwisha
fumbua macho lakini bado hajaweza
kuzungumza chochote.”
“ Poor Marcelo.Mungu atamsaidia
atapona” akasema Jane.
“ Tayari umemueleza Monica
ulichotaka kumueleza? Akauliza Jane
“ Hapana sijamueleza.Tutamueleza
wote wawili jioni ya leo” akasema mzee
Ben
“ Sawa Ben” akasema Janet
 
SEHEMU YA 88

onica aliwasili ofisini kwake lakini
hakuweza kufanya chochote kwani kichwa
chake kilikuwa na mawazo mengi sana na
kubwa lililomuumiza kichwa ni kuhusiana
na tukio la kupigwa risasi Dr Marcelo.
“ Ni nani aliyempiga Dr Mareclo
risasi na kwa nini? Akajiuliza
“ Inawezekana tukio la kupigwa
risasi linahusiana na lile la kupotea kwa
vitu vyake na hasa kitabu alichopewa na
baba yake? Akaendelea kujiuliza Monica
bila kupata jibu ,na moja kati ya simu zake
tatu za mezani ikaita akaipokea.
“ Dada Monica,Daniel yuko hapa
mapokezi anahitaji kuonana nawe,”
akasema msichana wa mapokezi.Monica
akafikiri kidogo na kusema
“ Sawa mruhusu aingie ndani”
akasema Monica .Baada ya kama dakika
tatu hivi mlango wa ofisi ya Monica
ukafunguliwa na Daniel akaingia.
“ Daniel karibu sana.Umepata taarifa
zozote za kuhusiana na Dr Marcelo?
Akauliza Monica
“ Nimeongea na dada yake Julieth
muda mfupi uliopita amenihakikishia
kwamba Marcelo anaendelea vizuri .”
akasema Daniel huku akiketi kitini.
“ Oh thank God “ akasema Monica
“ Monica samahani sana kwa kufika
hapa kwani najua ulinieleza awali
kwamba nisifike tena ofisini kwako lakini
imenilazimu kuja.” Akasema Daniel
“ Oh Daniel forget about what
happened.Sote tulikuwa na hasira na
tuliongea mambo ambayo hayakutoka
moyoni.Unakaribishwa hapa muda
wowote Daniel”
“ Thank you” akasema Daniel halafu
ukapita ukimya mfupi
“ Monica sina amani toka jana, hili
suala zima la Macelo limenichanganya
sana na nimekuwa najiuliza maswali
mengi bila majibu.Kwanza mtu kaingia
chumbani kwake akavunja kasiki na
kuchukua baadhi ya vitu muhimu na moja
ya vitu alivyovichukua ni faili lenye
kuonyesha Dr Marcelo ni mgonjwa wa
saratani ya damu uliloletewa hapa.Baada
ya tukio hilo Marcelo anapigwa risasi na
watu wasio julikana na halafu cha
kushangaza zaidi Marcelo akafariki na
kurejea tena.Hili ni suala ambalo binafsi
limenifanya nikose usingizi.Nimeona nije
kwako kwa pamoja tulijadili suala hili
pengine tunaweza kupata mwanga Fulani”
akasema Daniel
“ Hata mimi jambo hili
limenichanganya sana.Kwanza sifahamu
lengo la mtu aliyelileta lile faili kwangu na
vile vile sifahamu kwa nini amepigwa
risasi.Simfahamu Dr Marcelo kwa undani
sana kwani tumefahamiana si muda
mrefu lakini wewe ni rafiki yako wa siku
nyingi na unamfahamu kiundani unadhani
anaweza kuwa na ugomvi na mtu yeyote?
“ Dr Marcelo ni mtu ambaye hana
ugomvi na mtu yeyote.Ni mtu mpole sana
na hapendi magomvi.Kila mtu anashangaa
kwa nini amepigwa risasi” akasema Danie
“ Jana mchana alinipigia simu
akanitaka nionane naye na tulipokutana
akaniambia kitu Fulani .Alisema kwamba
wakati akitafakari aligundua kwamba
katika vitu vilivyochukuliwa na mtu
aliyefungua kasiki lake ni kitabu ambacho
aliwahi kupewa na baba yake kabla
hajafariki.”
“ Kitabu? Akauliza Daniel
 
SEHEMU YA 90

Kitabu? Akauliza Daniel
“ Ndiyo alisema kwamba kuna kitabu
alipewa na baba yake ambacho ni
mwongozo katika kazi zake za kitabibu na
kabla hajakisoma kitabu hicho alipewa
namba ambazo alitakiwa apige ili apewe
maelekezo ya namna ya kukitumia kitabu
hicho.Kwa mujibu wa Dr Marcelo ni
kwamba hajawahi kukifungua kitabu
hicho kujua kiliandikwa nini lakini jana
baada ya kukumbuka kwamba nacho
kimepotea ikamlazimu azitafute zile
namba alizopewa apige kwa ajili ya
kupewa maelekezo akapiga lakini simu
ikapokelewa na kukatwa na jioni ya siku
hiyo akapigwa risasi.Cha kushangaza zaidi
mtu huyo alichukua kitabu hicho pamoja
na lile faili akaacha mamilioni ya fedha
yaliyokuwamo katika kasiki” Akasema
Monica.Daniel akatafakari na kusema
“ Monica jambo hili ulilonieleza
limezidi kunichanganya zaidi na kulifanya
suala hili kuzidi kuwa gumu.Kitabu hicho
kina nini hadi huyu mvamizi akichukue na
kuacha mamilioni ya fedha yaliyokuwamo
katika kasiki? Akauliza Daniel na wote
wakabaki kimya baada ya sekunde kadhaa
Daniel akakumbuka kitu.
“ Monica kuna kitu
nimekumbuka.Siku moja nilikuwa na
Marcelo sehemu Fulani usiku tukipata
kinywaji .Hii ilikuwa ni baada ya kumaliza
masomo yake nchini China.Alinieleza
kwamba anatakiwa akafanye upasuaji
wake wa kwanza kwa binti mmoja ambaye
anasumbuliwa na tatizo la mishipa ya
fahamu ya kichwa.Usiku huo alikuwa na
wasiwasi mwingi na hakusita kunieleza
kuhusu wasi wasi alionao kwani kwa hali
ya mgonjwa huyo ilivyo ni wazi kama
angefanyiwa upasuaji lazima angepoteza
maisha.Uliponieleza kuhusu hicho kitabu
nimekumbuka kitu,usiku huo alinieleza
kwamba ili kuifanya operesheni hiyo
analazimika kwenda kupitia mwongozo
wake.Hakunieleza ni mwongozo upi
anakwenda kuusoma lakini baada ya
kunieleza kuwa alipewa kitabu cha
mwongozo na baba yake sasa nimepata
picha kwamba Marcelo alikuwa
anamaanisha kwenda kuusoma
mwongozo ambao ni hicho kitabu
alichopewa na baba yake.” Akasema
Daniel
“ Nini kilitokea kwa mgonjwa?
Akauliza Monica
“ Alifanikiwa kumfanyia upasuaji.He
saved her.”
“ Wow !..akasema Monica
“Kama ni hivyo ni wazi Marcelo
alikisoma kitabu hicho na akafanikiwa
kuokoa maisha ya mgonjwa, kwa nini basi
Marcelo anidanganye kuwa hajawahi
kukisoma hicho kitabu?
“ Hata mimi nashangaa” Akajibu
Daniel na ukimya ukapita
“ Nakumbuka msichana ambaye
alimfanyia upasuaji ule alipona akawa
rafiki yake sana na walikuwa
wakionekana pamoja sehemu mbali mbali
na sote tukajua labda wamekuwa wapenzi
.”
“ Unamfahamu? Akauliza Monica
“ Ndiyo ninamfahamu anaitwa
Lilian.”
“ Marcelo hakuwahi kunieleza
kuhusu jambo hilo “ akasema Monica
“ Marcelo ni msiri sana wa mambo
yake mengi.Hata hili suala la saratani ya
damu ya damu sikuwa nikilifahamu
pamoja na ukaribu wetu wa muda mrefu.”
Sasa unashauri nini Daniel
,tuwasiliane na familia yake tuwape
taarifa hizi? Akauliza Monica
“ Hapana let us stay out of this.Suala
hili si jepesi kama tunavyodhani.Kuna
vyombo vya usalama ambavyo vinafanya
uchunguzi na hakuna ulazima wa sisi
kuingilia uchunguzi wao.” Akasema
“ Lakini Daniel,hatuwezi kuwa na
taarifa kama hizi ambazo zinaweza
kusaidia uchunguzi halafu tukakaa
kimya.Lazima na sisi tutoe mchango wetu”
akasema Monica
“ Monica,Marcelo ni rafiki yetu lakini
kwa suala hili nakuomba tusijihusishe
kabisa labda hadi hapo tutakapoombwa
.Tuviachie vyombo vya usalama vifanye
kazi yake .Tunachotakiwa kufanya ni
kumuombea Marcelo apone haraka”
akasema Daniel.Monica akainamisha
kichwa akazama katika mawazo kisah
akasema
“ Daniel nadhani nahitaji
kupumzisha kichwa.Haya mambo
yamenifanya nishindwe hata kufanya kazi
yoyote leo japokuwa nina kazi nyingi za
kufanya.Take me somewhere Daniel
where I can clear my mind.” Akasema
Monica.Huku akitabasamu Daniel
akamshika mkono wakatoka mle ofisini
wakaondoka.
 
SEHEMU YA 91

Ernest Mkasa rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania akitokea kukagua
maendeleo ya upanuzi wa bandari ya Dar
es salaam alielekeza msafara wake uingie
White Rhino hotel.Hii ni moja ya hoteli
inayomilikiwa na rais huyu .White Rhino
hotel imesambaa katika nchi mbali mbali
za afrika na katika baadhi ya nchi za
Ulaya.Mara nyingi Ernest hupenda kuja
hapa kupata chakula,kupumzika katika
bustani nzuri zenye wanyama mbali mbali
na wakati mwingine hukutana na wageni
wake kwa ajili ya maongezi ya faragha.
Alipokewa na watumishi wa hoteli
akasalimiana nao halafu akaongozana na
meneja wa hoteli hadi katika lifti
wakapanda ghorofani
“ Tayari Jane amekwisha fika?
Akauliza Ernest kwa sauti ndogo
“ Amekwisha fika mheshimiwa
rais,yupo chumbani anakusubiri” akajibu
meneja wa hoteli
Walipanda hadi ghorofa ya ishirini
na mbili wakashuka na kuelekea katika
mlango ulioandikwa Presidential suit
5.Ernest akawafanyia ishara walinzi wake
wabaki nje ,meneja wa hoteli
akamfungulia mlango rais akaingia
ndani.Katika sofa zuri jeupe alikuwa
amekaa mwanamama mmoja ambaye
licha ya umri wake kuonekana kuwa
mkubwa lakini sura yake bado ilionyesha
uzuri wa aina yake.Uso wa Ernest
ukachanua kwa tabasamu pana sana
baada ya kuiona sura ile nzuri ya Yule
manamama ambaye alisimama na
kumfuata Ernest wakakumbatiana kwa
furaha
“ I missed you Janet.I missed you so
much” akasema Erbnest na kumbusu Janet
“ I missed you too Ernest” akasema
Janet na kumkumbatia Ernest kwa nguvu
zaidi wakanyonyana ndimi na huku wote
wakihema kwa kasi na kutoa miguno
wakavua nguo na kuingia katika mtanange
.Dakika kumi na tano zilitosha sana
kumaliza mtanange ule ambao uliwaacha
wote wawili wakihema kama wakimbiaji
wa mbio ndefu.
“ Jane sijui nikwambie nini “
akasema Ernest huku akimtazama Janet
“ Kwa nini Ernest?
“ Pamoja na kwamba umri wetu
umesonga sana lakini kila ninapokutana
nawe ninazikumbuka zile enzi zetu za
ujana.Unanifanya nijione bado ni kijana
sana” akasema Ernest na wote wakacheka
“ Ernest you don’t have an idea how
much I missed you.Wewe ni tofauti sana
na wanaume wengine wote ambao
nimewahi kukutana nao.Ninapofanya
nawe mapenzi hata kwa muda mfupi
ninaipata raha ambayo siwezi kuipata
toka kwa wanaume wengine.Wewe
utabaki kuwa shujaa wangu daima”
akasema Janet na kumbusu Ernest.Ukapita
ukimya mfupi Ernest akasema
“ Jane ulimssitiza Mukasha kwamba
unahitaji kuonana nami leo na kwa
msisitizo uliompa nikajua kuna jambo la
msingi sana na ndiyo maana nikasitisha
ratiba zangu za mchana wa leo ili nipate
nafasi ya kukutana nawe.So tell me
sweetheart Kuna jambo unataka
kunieleza?
Jane akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Ndiyo Ernest kuna jambo la
muhimu nataka kukueleza
“ Nieleze Jane” akasema Ernest
“ Nimekuja kukueleza kwamba Ben
tayari amehisi kuna kitu kinaendelea kati
yetu .”
“ What ? How? Akauliza Ernest akiwa
katika mstuko mkubwa

Sifahamu
amejuaje
lakini
amenihakikishia
kwamba
atafanya
 
SEHEMU YA 92


uchunguzi wake na endapo atagundua
kwamba ni kweli sisi tuna mahusiano basi
ama zetu ama zake.Kwa hiyo Ernest we
have to put an end to what we’re doing”
akasema Janet .Ernest akamtazama kwa
macho ya uoga na kusema
“ Jambo hili limenishangaza
sana.Tumekuwa tunakutana kwa siri kwa
zaidi ya miaka ishirini sasa lakini
ninachojiuliza why now? Kwa nini ahisi
sasa? Akauliza Ernest ,Janet hakujibu kitu
akabaki kimya
“ Jane tafadhali naomba unieleze nini
kimetokea hadi Ben akahisi mimi na wewe
tuna mahusiano kwa sababu hainiingii
akilini kabisa kwa miaka hii yote Ben aje
ahisi leo mimi na wewe tuna mahusiano.”

Hakuna
tatizo
lolote
Ernest,nadhani kuna tetesi atakuwa
amepewa” akajibu Jane
“ Kapewa na nani? Jane naomba
tafadhali unieleze ukweli.Ninakufaamu
vizuri kuliko mtu mwingine yeyote kuliko
hata mumeo.I know that you are hiding
something from me.Tafadhali Jane mmi na
wewe tumekuwa tunaelezana siri zetu
hata zile kubwa.Nieleze kuna tatizo gani ?
Ben amehisi vipi kuwa mimi na wewe tuna
mahusiano?
Ninakusisitiza
unieleze
ukweli kwa sababu ninamfahamu vizuri
Ben .Kama amesema atafanya uchunguzi
basi lazima atafanya na endapo atagundua
kwamba mimi na wewe ni kweli tuna
mahusiano basi suala hilo litachukua sura
mpya.Ben anakupenda sana na kwa ajili
yako anaweza akafanya jambo lolote baya
kwetu na hasa hasa kwangu.Najua hawezi
kuniua kwa silaha lakini kama unavyojua
Ben ananifahamu kiundani,anaifahamu
historia yangu chafu ya nyuma kwa hiyo ni
rahisi sana kwa mtu kama huyu
kuniharibia taswira yangu kwa jamii.Ni
kweli nimepitia mambo mengi machafu
katika kutafuta utajiri na hadi nimefika
hapa katika nafasi hii kubwa ya uongozi
wa nchi.Endapo wananchi watafahamu
historia ya rais wao wanayempenda nina
hakika nitakuwa rais wa kwanza duniani
kupigwa
mawe
na
wananchi
hadharani.Kabla hatujafika huko natakiwa
kujua nini kimetokea ,nini kinaendelea ili
niweze kuchukua hatua za haraka kama
zitahitajika
ili
kuzuia
madhara
yanayoweza kutokea endapo jambo hili
litagundulika,lakini endapo utaendelea
kunificha na mambo yakaharibika basi
nitakua na kitu kimoja tu cha kufanya “
akasema
Ernest
na
kunyamaza
akamtazama Janet
“ Whats that Ernest? Akauliza jane
“ To kill Ben” akasema Ernest kwa
sauti ndogo.Jane akastuka akamtazama
Ernest kwa macho makali
“ Mbona umestuka Jane? Akauliza
Ernest

Ernest
tafadhali
naomba
usithubutu
kuwaza
kitu
kama
hicho.Ukimuua Ben it’ll be the end of us
all.Ben is all I have na kwa ajili yake niko
tayari kufanya lolote hata kama ni baya
kwa hiyo nakuomba mawazo machafu
kama hayo uyaweke pembeni kwani
endapo utafanya kitu kama hicho utaingia
katika vita na mimi na unajua mimi ni
mbaya kuliko hata Ben.” Akasema Janet
“ Janet najua unampenda sana Ben
na uko tayari kwa lolote kwa ajili yake na
ninafahamu pia kwamba wewe ni mbaya
zaidi lakini usisahau kuwa mimi ndiye
niliyewabadili mkawa hivi mlivyo
leo,mambo yote niliwafundisha mimi kwa
 
SEHEMU YA 93


hiyo msisahau kuwa mimi ndiye mwalimu
wenu na nina roho mbaya kama ya shetani
kwa mtu anayenikorofisha na kutaka
kuchezea maslahi yangu.So my dear Jane
don’t wait for the situation to get ugly,tell
me everything now!! Akasema Ernest
“ Hakuna ujanja I have to tell him the
truth.Bila hivyo mambo yanaweza kuwa
mabaya sana.Ben na Ernest wote ni watu
wenye hasira na wasiokubali kushindwa
kirahisi kwa hiyo endapo hawa wawili
wataingia katika uadui basi haitakuwa
vita ndogo.Itatuhusisha wengi.Sitakiwi
kuacha jambo hili likafika huk....” Janet
akastuliwa na sauti ya Ernest
“ Janet muda unakwenda na nina
mambo mengi ya kufanya.Kama kuna
jambo unataka kunieleza basi wakati
wake ni sasa” akasema Ernest akainuka na
kuanza kuvaa
“ Naomba ukae chini Ernest”
akasema Janet .Ernest akakaa kitandani
“ Ernest kuna tatizo kubwa”
“ Nieleze Jane ni tatizo gani hilo?
Akauliza Ernest.Janet akavuta pumzi
ndefu na kusema
“ Ni jambo ambalo limetokea miaka
mingi iliyopita wakati ule Ben
alipokamatwa
nchini
China
na
nikakufuata kukuomba umsaidie ,ukatoa
sharti kwamba ili umsaidie ni lazima
nikubali kufanya mapenzi nawe.Sikuwa na
namna nyingine ninakubali kuanzisha
mahusiano nawe lakini tulipofanya mara
moja tukanogewa na kuchonga mzinga
tukaendelea kulamba asali hadi hii
leo.Kuna
jambo
lilitokea
ambalo
sikukueleza na sikutaka kukueleza wewe
au mtu yeyote Yule lakini kutokana na hali
ya mambo inavyokwenda nimejikuta sina
ujanja zaidi ya kumueleza Ben na ndiyo
chanzo cha haya yote ambayo yanataka
kutokea” akasema Janet
“Nini kimetokea Jane? Akauliza
Ernest kwa wasi wasi.Jane akakohoa
kidogo kurekebisha koo halafu akasema
“ Ernest wakati wa mahusano yetu ya
mwanzo kipindi Ben akiwa nchini China
kuna jambo lilitokea.”
“ Nieleze Jane mbona hutaki
kuniambia ni jambo gani hilo lilitokea?
“ We had a daughter” akasema
Jane.Uso wa Ernest akaonyesha mstuko
mkubwa sana.Akasimama na kumtazama
Jane kwa uoga.
“ Hebu rudia tena kile ambacho
umekitamka Janet” akasema Ernest
“ Nimekwambia kwamba we had a
daughter”
“ Oh my God !! akasema Ernest na
kwenda dirishani akachungulia nje na
kurudi kwa kasi akapiga magoti pembeni
ya Janet
“ Janet please tell me it’s not a lie”
akasema Ernest ambaye alionekana kama
mtu aliyechanganyikiwa
“ Its true Ernest “ akajibu Jane.
Ernest machozi yalianza kumlenga
“ Oh my God !! akasema na
kusimama akachukua kitambaa na
kujifuta machozi
“ Kwa nini hukuwahi kunieleza
jambo hili mapema? Kwa nini unanieleza
leo ? akauliza Ernest huku bado machozi
ya furaha yakiendelea kumtoka
“ Ernest hii ilikuwa ni siri yangu
ambayo niliapa kufa nayo na sikutaka mtu
yeyote alifahamu jambo hili.Nisingeweza
kukueleza kuhusu suala hili kwani
nakufahamu you are a monster.Watoto
 
SEHEMU YA 94

wako watatu umewatoa kafara katika
kufanikisha
mambo
yako
ya
utajiri.Sikutaka mwanangu naye afanywe
kama
ulivyowafanya
wanao
wengine.Endapo ningekueleza mapema
kuhusu suala hili ni wazi lazima
ungemchukua mtoto jambo ambalo
sikutaka litokee.” Akanyamaza na kumeza
mate.Ernest alikuwa ni kama mtu
aliyechanganyikiwa
“ Oh my God..Oh my God !!! akasema
Ernest na halafu akaenda tena kupiga
magoti mbele ya Janet
“ Tell me Janet where is my
daughter..ouh sorry where is our
daughter? Akauliza
“ Mwananetu yupo .Ni Monica”
akasema Janet na kuzidi kumchanganya
Ernest
“ Monica? Akauliza kwa mshangao
“ Ndiyo ni Monica”
“ Monica malkia wa Afrika?
“ Ndiye huyo.” Akajibu Janet.Ernest
akainua mikono juu ishara ya
kumshukuru Mungu halafu akamtazama
tena Janet

Janet
tafadhali
naomba
unihakikishie kwamba hiki unachonieleza
ni kitu cha kweli na si masihara” akasema
Ernest
“ kwa nini nifanye masihara katika
jambo kubwa kama hili? Siwezi kukutania
Ernest ni kweli mimi na wewe tuna mtoto
ambaye ni Monica.”
“ Ben analifahamu jambo hili?
Umemueleza?
“ Ndiyo anafahamu nimelazimika
kumueleza ukweli”
“ Amesemaje? Akauliza Ernest
“ Kama ilivyo kwa mwanaume yeyote
haikuwa habari nzuri kwake ambayo
hakuwa ametegemea kuisikia.Alistuka
sana .Ben anampenda sana Monica na
haikuwa rahisi kuamini kuwa si mwanae
lakini amekubaliana nami na hatuna
mgogoro mkubwa ila hatuwezi kuwa sawa
tena kama zamani tayari kuna doa kubwa
limeingia katika ndoa yetu .Ben ameumia
sana na kilichomuumiza zaidi si mimi
kuzaa nje ya ndoa kwani hata yeye anao
watoto aliowazaa nje ya ndoa ingawa
amenificha lakini ninawafahamu na sina
ugomvi
naye
katika
hilo
,ila
kilichomuumiza zaidi ni mtu niliyezaa
naye yaani wewe.Hakutegemea kabisa
mtu kama wewe ungeweza kumfanyia
kitendo kama hiki hasa kwa namna
mnavyoheshimiana.Amekasirishwa sana
na hilo na ndiyo maana ameahidi kufanya
uchunguzi kubaini kama mimi na wewe
bado tunaendelea na mahusiano yetu na
ameahidi kufanya kitu kibaya sana kama
akigundua kuhusu hilo ndiyo maana
nimekuja kukuomba kwamba kwa sasa
tusimame kwanza kukutana hadi hapo
baadae mambo yatakapotulia ndipo
tuendelee” akasema Janet.Ernest akaketi
pembeni yake akamshika mikono
 
SEHEMU YA 95


Janet nimekosa neno la kusema kwa
surprise hii kubwa uliyonifanyia.Ninauona
ni kama muujiza umenitokea.Watoto
wangu wote tayari nimewapoteza na
niliamini kuwa nitakufa bila ya kuwa na
mrithi wa mali zangu .Kuniambia kwamba
una mtoto wangu kumenipa furaha
ambayo siwezi kuielezea na ndiyo maana
unaniona
niko
kama
mtu
aliyechanganyikiwa .Hizi ni taarifa nzito
sana kuwahi kuzisikia .Ouh Janet Janet ...”
akasema Ernest na kumkumbatia Janet
akamwagia mabusu
“ Kuna swali moja ambao nataka
unijibu.Ilikuaje hadi ukamueleza Ben
suala hili? Najua lazima iko sababu so tell
me”
“ Ernest naomba nikueleze ukweli
kwamba Monica nimemlea katika maadili
makubwa sana ni mwanamke
anayejitambua na anayejithamini
sana.Mpaka leo pamoja na umaarufu wake
bado hatujamfahamu mpenzi wake.Ni
binti anayejitunza sana. Amekuwa karibu
na wanaume kadhaa ambao baada ya
kuwafanyia uchunguzi nimekuwa
nikibaini kasoro kadhaa kwao lakini
Monica ana imani kwamba si muda mrefu
atampata mwanaume Yule ambaye
amekuwa akimuhitaji kwa maisha yake
yote” akanyamaza akameza mate na
kuendelea
“ Juzi alikuja rais wa jamhuri ya
kidemokrasia ya Kongo David Zumo
ambaye baada ya kusikia kuhusiana na
shule ambayo Monica anataka kuijenga
kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa
kutokuona na kusikia ,akaguswa na
akataka
kuchangia
mchango
wake.Alimualika Monica katika hoteli
alikofikia na kweli akampatia mchango
mkubwa wa mabilioni ya fedha.Siku
iliyofuata akatualika mimi na Ben
kukutana naye tukaenda na wakati
tukiendelea na chakula tukapata habari
kuwa mmoja wa marafiki wa Monica
amepigwa risasi ikanilazimu mimi na
Monica kuondoka na kwenda hospitali
nikamuacha
Ben
na
David
wakiongea.Katika maongezi yao David
Zumo aliweka wazi nia yake ya kutaka
kumuoa Monica.”
“ What ?? !! Ernest akastuka sana
“ David Zumo ameweka wazi nia
yake ya kutaka kumuoa Monica.Amedai
kwamba anampenda sana na kwamba
atatupa msaada mkubwa kiuchumi na
kutupaisha kimataifa.Ben alikubali lakini
mimi sikukubaliana hata kidogo na suala
hilo na ndiyo hapo ugomvi wetu
ulipoanzia ikanilazimu kumueleza Ben
ukweli kuwa hana kauli yoyote juu ya
Monica kwani si mwanae wa damu.Ben
alitaka kwenda kumueleza Monica kuhusu
jambo hili ,nikamzuia asifanye hivyo lakini
kwa makubaliano maalum.”
“ Makubaliano gani hayo? Akauliza
Ernest
“ Tumekubaliana kwamba suala hili
litabaki siri yetu lakini Monica aolewe tu
na David.Sikuweza kulikataa hilo kwani
siko tayari kuyaharibu maisha ya Monica
au kuivuruga familia yangu Monica
atakapofahamu kuwa Ben si baba yake
mzazi.”
“ No that’s not going to
happen.Mwanangu aolewe na David
Zumo? Hapana hiyo haiwezekani kabisa.I
swear I wont let that happen !! akasema
Ernest
“ Ernest nisikilize kwa makini
.Hakuna chochote unachoweza kufanya
kuhusu suala hili kwa sasa na hautafanya
chochote
kuzuia
jambo
hili
lisifanyike.Tayari tumekwisha fanya
maamuzi na lazima uyaheshimu.Monica
ataolewa na David Zumo that’s final !!
akasema Janet kwa sauti ya ukali
“ Janet kama Monica ni mwanangu
kweli kama unavyodai siko tayari aolewe
 
SEHEMU YA 96

na David Zumo.Japokuwa ni tajiri namba
moja afrika lakini siko tayari amuoe
mwanangu. !! akasema Ernest
“ Ernest nimekwisha kwambia
kwamba huwezi na usijaribu kulivuruga
hilo.”
Ernest akamtazama Janet kwa
macho makali na kusema
“ Kwa maana hiyo hutamtambulisha
Monica kwangu kuwa mimi ni baba yake
mzazi?
“ Hapana.Hiyo itabaki ni siri yetu sisi
watu watatu na Ben ataendelea kuwa baba
yake.I want to save my family from falling
apart.Pindi Monica akitambua kuwa Ben si
baba yake mzazi familia yangu itameguka
na nitabaki mwenywe.Familia yangu ni
kitu kikubwa sana kwangu kuliko hata
mali nilizonazo kwa hiyo nitailinda kwa
gharama zozote zile.” Akasema Janet
“ Monica nakubaliana nawe kwamba
suala hili kama Monica akilifahamu
litamuumiza na kweli familia yako
itavurugika sana lakini na mimi nina haki
kama baba na yeye Monica ana haki ya
kumfahamu baba yake mzazi.Kama
hukunipa haki ya kumlea mwanangu
huwezi kumnyima Monica haki ya
kumfahamu baba yake mzazi.”
“ Ernest ninafahamu unazo haki
kama baba mzazi lakini ninakuomba sana
kwa sasa tuliache suala hili kama
lilivyo.Hii ni hatua kubwa imefanyika
umefahamu kuwa una mtoto na hata kama
ukifa leo basi mrithi unaye.Muache aolewe
na David Zumo na aendelee na maisha
yake na suala hilo niachie mimi nitajua
kitu cha kufanya.Nakuahidi ntamleta
kwako Monica akufahamu.Haitakuwa
rahisi lakini nakuahidi kwamba lazima
nitamleta Monica akufahamu ila kwa sasa
naomba tuyaache mambo yatulie kwanza
.Suala hili twende nalo taratibu hatua kwa
hatua lakini tukienda nalo kwa kasi
tutaharibu kila kitu” akasema Janet.Ernest
akainama akafikiri kwa muda na kusema
“ Sawa Janet nimekuelewa japo
kidogo lakini nataka nikushukuru kwa
kuamua kunieleza ukweli wa jambo
hili.Nashukuru kwa kuniletea habari
njema sana ambazo zimeirudisha furaha
ya maisha yangu ambayo nilikwisha
ipoteza.Nipe muda na mimi nikatafakari
kwa siku ya leo suala hili halafu
nitakwambia nimefikiria tufanye nini
kuhusu namna bora ya kulimaliza hili
suala .”
“ Ernest kwa sasa hatutaweza
kuonana kama utanihitaji basi utanipigia
simu na kama kuna suala la kujadili basi
tutajadili lakini hatutaweza kuonana tena
kwa hivi karibuni.”
“ Sawa nimekuelewa Jane.Nitatafuta
kila namna hadi nionane nawe tena kwani
bado kuna mengi ambayo mimi na wewe
tunapaswa tuongee.Ahsante kwa taarifa
hizi njema na kuyang’arisha tena maisha
yangu.I love you so much” Akasema Ernest
na kumbusu Janet kisha akatoka mle
chumbani.
“ Sikutegemea kabisa kama siku
moja jambo hili litakuja kufika
hapa.Sikutaka kumueleza Ernest lakini
kwa hali ilivyo sikuwa na ujanja ilikuwa
lazima nimueleze ukweli kabla mambo
hayajawa magumu kwani sina hakika
kama suala hili litakuwa na mwisho
mzuri.I’m so scared” akawaza Janet baada
ya Ernest kutoka mle chumbani.
“ Ngoja niondoke hapa niwahi
nyumbani leo jioni kuna kikao kati yetu na
 
Back
Top Bottom