QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

Uko vizuri ndugu lege.. Sikutarajia kusoma vipande hivyi Kwa mda huu.. Umejitahidi Sana kurusha vipande ingawa umetingwa.. Mungu awe nawe
 
Hadithi nzuri lakini isije kuwa mambo ya Shigongo mgonjwa kuugua muda mrefu!
 
Nina hisia na watu wawili kupanga shambulizi hili namba moja mama Monika baada ya kutuma fail ameona hakuna dalili ya kuachana sasa bora aue kabisa, wa pili Rais David wa Congo huenda kaweka wachunguzi ili kumfuatilia Monica sasa wamebaini Dr Marcelo ni mmoja kati ya watu watamfanya Monica kuwa mgumu kumkubali kimapenz Rais David sasa dawa ni kuua tu! Huo ni mtazamo Wangu wa huko tuendapo kumtambua mtu alofanya shambulizi kwa Dr Marcelo
 
story imeanzaa kunoga sasa...!!.. maana maswali tata yameanza,ndipo naona utamu unakolea...
kitabu kiko wapi..??.kwani aliyepigiwa simu na dr marcelo kwa maelekezo ya baba ake amekata simu..??..je monica akijua mama ake ndie anahusika na wizi wa file la taarifa za ugonjwa wa marcelo atafanyeje.??..mzee benedict nae kalishwa na mr prezdaa ambacho ni tamu kutema na chungu kumeza.....
nani anauhusika na shambulio la dr.marcelo..??...

thanx Lege..keep on..!!
 
SEHEMU YA 67


need to come back because I want to say
how sorry I am for those awfull things I
said to you.I love you brother..” akawaza
Daniel huku machozi yakimtoka .Kila
aliyekuwamo mle chumbani alikuwa
anawaza lake lakini ghafla kikatokea kitu
kilichowastua
wote,mashine
yenye
kuonyesha mwenendo wa mapigo ya moyo
ikaanza
kutoa
mlio.Haraka
hakara
madakatri wakaitwa na kutoka kila kona
wakaanza kukimbia kuelekea katika
chumba alimolazwa Dr Marcelo na
kuwataka ndugu wote watoke.Mashine ile
ilionyesha kwamba moyo wa Dr Marcelo
ulisimama kufanya kazi yake .Juhudi za
kuustua moyo ili uendelee na kazi
zikaanza lakini juhudi zote zikaonekana
kushindwa kufanikiwa.
“ I’m so sorry.He’s gone” Dr Mchemo
akawaambia madaktari wenzake baada ya
kumpima
na
kuhakikisha
kweli
amefariki.Kwa
huzuni
Madaktari
wakaanza kutoka mle chumbani na
kuwaachia wauguzi kazi ya kuundoa mwili
ule wa Dr Marcelo kuupeleka katika
chumba cha kuhifadhia maiti
Wakiwa nje ndugu na jamaa wa Dr
Marcelo walishuhudia wadaktari wakitoka
ndani ya chumba kile wakiwa vichwa
chini.Dr Mchemo akawataka ndugu tu wa
karibu waende ofisini kwake.Kwa namna
madaktari walivyotoka ndani ya kile
chumba haikuhitaji tena maelezo mengi
juu ya kilichotokea.Watu wengine tayari
wakaanza kuangua vilio.Daniel aliyekuwa
amesimama na Monica alistushwa mno na
jambo lile akamshika mkono Monica na
kwa haraka wakaelekea katika chumba
ulimo mwili wa Dr Marcelo .Wauguzi
walikuwa bado wanajiandaa ili waanze
kuzifungua baadhi ya mashine zilizokuwa
zimeunganishwa
mwilini
mwa
Dr
Marcelo.Monica
akashindwa
kujizuia
kuangua
kilio
kikubwa
,Daniel
akamkumbatia
na
kumsihi
anyamaze.Ghafla kikatokea kitu ambacho
hakuna aliyekuwa amekitarajia.
Mashine
yenye
kuonyesha
mwenendo wa mapigo ya moyo wa Dr
Marcelo
ambayo
bado
haikuwa
imeondolewa ikaanza kufanya kazi
kuashiria kwamba moyo wa Dr Marcelo
ulianza kufanya kazi tena
“ What ???!! Daniel akastuka na
kuwastua wale wauguzi ambao waliacha
kufanya kazi zao na kubakiwa na
mshangao wasiamini macho yao.Ni kweli
mashine ile ilionyesha moyo wa Dr
Marcelo
ulikuwa
unafanya
kazi
tena.Haraka haraka mmoja wao akatoka
mbio huku akipiga ukelele kuwaita
madaktari ambao walijaa mle chumbani
.Lilikuwa ni tukio la ajabu ambalo hakuna
aliyewahi kulishuhudia.Kila mmoja mle
chumbani ilikuwa ni mara yake ya
kwanza kushuhudia kitu kama kile.Watu
wote waliokuwa wakilia wakanyamaza
baada ya kupata taarifa za kilichotokea.
Ulikuwa ni mshangao kwa kila
mtu.Ni jambo ambalo halikuzoeleka mtu
ambaye tayari alikwisha thibitishwa na
madaktari
bingwa
kuwa
amefariki
kuzinduka.Madaktari hawakutaka kutoka
mle chumbani wakiendelea kufuatilia hali
ya Dr Marcelo ili waone kama kuna
chochote kitakachotokea lakini vipimo
vyote vilionyesha kila kitu kilikuwa
kinaendelea vizuri.
 
SEHEMU YA 68

Saa tisa za usiku Monica na mama yake
wakiwa wameongozana na walinzi wa
David Zumo wakarejea nyumbani.Mzee
Benedict tayari alikwisha rejea nyumbani
kitambo na hakuwa amelala alikuwa
amekaa sebuleni akiwasubiri warejee.
“ Vipi hali ya huko ikoje? Mgonjwa
anaendeleaje? Akauliza mzee
“ Mhh !! kilichotokea huko si kitu
kidogo.” Akasema bi Janet.
“ Nini kimetokea He’s dead? Akauliza
mzee Benedict
“ Hapana hajafariki” akasema bi
Janet na kuvuta pumzi ndefu.Monica
alikuwa ameinama hakuweza kuongea
chochote
“ Hebu niambieni nini kimetokea
huko? Akauliza.Monica akasimama
“ Dady I’m so tired .I have to go sleep
now,mother will tell you everything”
akasema Monica
“ Sawa Monica nenda kapumzike
tutaonana asubuhi.Usiondoke bila ya
kuona nami kwanza nina mambo ya
muhimu sana ya kuzungumza nawe”
akasema mzee Benedict naye akainuka
akamshika mkono mke wake
wakaongozana kuelekea chumbani kwao.
“ Jane nini kimetokea huko
hospitali? Akauliza Ben
“ Ni mambo makubwa Ben.Kwanza
mmemaliza salama na mheshimiwa rais?
“ Ndiyo tumekuwa na mazungumzo
mazuri sana yenye mafanikio
makubwa.Nitakueleza kila kitu naomba
kwanza unieleze kilichotokea hospitali”
akasema Ben
“ Kilichotokea hospitali leo imebaki
ni gumzo.Kila mtu ameshikwa na
mshangao.Nilikuwa nasoma mambo haya
katika vitabu lakini leo hii nimeshuhudia
kwa macho yangu.”
“ Nini kimetokea Jane?
“ Dr Marcelo Yule rafiki wa Monica
aliyepigwa risasi alifanyiwa upasuaji na
baada ya upasuaji akapelekwa katika
chumba cha uangalizi maalum.Akiwa mle
,wakaruhusiwa baadhi ya watu wake wa
karibu akiwamo Monica kuingia na
kumuangalia japokuwa hakuwa na
fahamu.Wakati wakiwa mle ndani
mashine ya kuonyesha mwenendo wa
mapigo ya moyo ikaonyesha kwamba
moyo haukuwa ukifanya kazi,madaktari
wakafanya kila jitihada kuustua moyo ili
uendelee na kazi lakini zikashindikana na
Marcelo akafariki dunia.Wakati madaktari
wametoka na kuwaacha wauguzi
washughulikie kuiondoa maiti ndipo
kilipotokea kitu cha ajabu sana.Moyo wa
Marcelo ghafla ukaanza kufanya kazi
tena.He came back to life again.Jambo hili
limemshangaza kila mtu na hakuna
aliyetaka kuamini.Hadi sasa bado
madaktari wanaendelea kuulizana nini
kimetokea kwa sababu ni wazi Dr Marcelo
alikuwa amefariki dunia kabisa.Ben haya
ni maajabu makubwa sana na katika
maisha yangu sijawahi kuyashuhudia ni
mara ya kwanza leo kushuhudia mtu
aliyefariki akirejewa na uhai.” Akasema Bi
Janet
“ Dah ! kweli huu ni muujiza
mkubwa.Mambo haya huwa yanatokea
mara chache sana duniani.” Akasema mzee
Ben
“ Kweli ni muujiza.Hakuna aliyekuwa
ametegemea.Wote tulijua Marcelo tayari
amekufa and its over lakini baada ya muda
moyo wake ukaanza kufanya kazi tena
kweli ni muujiza.Madaktari hawatalala leo
wakijaribu kuchunguza nini kimetokea”
akasema Bi Janet
 
SEHEMU YA 69

Kwa hiyo hali yake ikoje kwa
ujumla? Akauliza Ben
“ Mpaka sisi tunaondoka hali yake
ilikuwa inaendelea vizuri.Mashine zote
zilionyesha maendeleo yake ni mazuri”
“ Monica ameumizwa sana na jambo
hili.” Akasema Ben
“ Ni kweli Ben.Jambo hili la kupigwa
risasi kwa rafiki yake Marcelo
limemuumiza
sana.Kuna
kitu
nimekigundua leo.Inaoneana wazi kabisa
Monica anampenda sana huyo Marcelo na
kama hisia zangu zilivyokuwa sahihi siku
ile nilipowakuta kule bwawani usiku
wakiongea nilijua kabisa lazima kulikuwa
na kitu kinachoendelea.Tatizo ni kwamba
jambo hilo halitawezekana kwani Marcelo
ni mgonjwa na sina hakika kama Monica
analifahamu hilo.Kuna ulazima wa
kumueleza mapema kuhusu jambo hili
kabla hawajaenda mbali zaidi.” Akasema
bi Janet
“ Tuachane na hayo ya hospitali.Nini
kiliendelea tulipoondoka? Akauliza Janet
“ Mlipoondoka kumekuwa na
mazungumzo mazito lakini yenye manufaa
makubwa kwetu.”
“ Haya nishirikishe na mimi
kilichojiri” akasema Janet
“ Kuna mambo kama mawili
makubwa tuliyoongea.Kwanza David
Zumo alinieleza kwamba amenifuatilia na
kugundua kuwa mimi ni mfanyabiashara
bilionea hapa nchini lakini akasema
kwamba anataka kunifanya niwe
mfanyabiashara mkubwa zaidi nijulikane
afrika na duniani kwa ujumla.Kuna kikao
ambacho hukutanisha mabilionea mia
moja wa dunia anataka siku moja na mimi
niwepo katika kikao hicho” akasema Ben
“ Wow ! hizo ni habari njema.Mtu
huyu ni mwema sana.Ana moyo wa
kusaidia na ndiyo maana hata Mungu
anambariki” akasema bi Janet kwa furaha
“ Ni kweli Jane.Huyu mtu ana moyo
wa kusaidia na toka moyoni ameahidi
kunipaisha kimataifa.Lakini kuna jambo
moja analihitaji toka kwangu,toka kwetu”
Ben akanyamaza kidogo na kusema
“ David Zumo anampenda
Monica.Anataka kumuoa” akanyamaza
baada ya mke wake aliyekuwa amekaa
kitandani kuinuka na kumtazama kwa
macho makali sana.
“ Tell me it’s a joke Benedict”
akasema bi Janet
“ Hapana si utani Janet.Ametamka
David Zumo kwa mdomo wake kuwa
anampenda na anataka kumuoa Monica.”
Akasema Ben .Mke wake akasimama
akamtazama benedict
“ oh my God why it have to be her??
Akauliza Janet.Ben akatabasamu na
kusema
“ Mwanetu ana bahati ya kipeke
sana.Kila siku milango yake ya mafanikio
inazidi kufunguliwa.Yote hii ni kwa
sababu ya upendo wake mkubwa kwa
watu.Juzi tu ametangazwa kuwa mrembo
kuliko wote afrika na leo hii tajiri namba
moja afrika anajitokeza na kutaka
kumuoa.Huoni hizo ni Baraka ? Hii ni
bahati ya kipekee sana .” Akasema mzee
Ben.Mkewe akaendelea kumtazama kwa
hasira
“ Umemjibu nini? Akauliza Janet
“ Ningemjibu nini zaidi ya jibu moja
tu la ndiyo” akasema Ben
“ Benedict are you crazy? Akauliza bi
Janet
 
SEHEMU YA 70


Kwani vipi Janet.Jambo hili lina
ubaya gani? Mtu kama David ndiye
ambaye
Monica
amekuwa
akimuhitaji.Tumesubiri kwa muda mrefu
Monica ampate mwanaume mzuri wa
kumfaa na Mungu amejibu maombi yake
amemletea mwanaume wa maisha
yake,ambaye anampenda kwa moyo wake
wote.Wanasema mvumilivu hula
mbivu,Monica amevumilia kwa muda
mrefu na sasa ni wakati wake wa kuzila
mbivu kwani anakwenda kuwa malkia
halisi wa afrika .Anakuwa mke wa tajiri
namba moja wa af..”
“ Oh my God !! Benedict are you
crazy??!!!! Akauliza bi Janet kwa hasira
“ Janet kuna tatizo gani katika hilo?
That what we’ve been dreaming for
her,right?.Monica kumpata mwanaume
atakayempenda ilikuwa ni ndoto yako
kubwa na sasa kuna tatizo gani wakati
ndoto hiyo imetimia tayari? Amejitokeza
mwanaume
mwenye
sifa
unazozitaka.David bado kijana ,ni raisi wa
nchi,ni tajiri namba moja afrika kwa
ujumla ni mtu mwenye sifa zote za
kumuoa Monica.Zaidi ya yote anakwenda
kutusaidia sana kiuchumi.Anakwenda
kutupaisha imataifa zaidi na sisi tutaingia
katika orodha ya matajiri wa dunia kwani
uwezo huo anao.” Akasema Benedict
Mke wake akamtazama kwa hasira
huku akihema mfululizo na kusema
“ Toka moyoni mwako unakubali
kweli Monica aolewe na David Zumo?
Akauliza.Bila kupepesa macho mzee Ben
akajibu
“ Kwa moyo mweupe kabisa
ndiyo,nataka Monica aolewe na David
Zumo.Sina kipingamizi chochote katika
jambo hilo kwani naamini Yule ndiye hasa
mwanaume anayemfaa...”
Bi Janet akamtazama mumewe na
kutikisa kichwa
“ Sikutegemea kama siku moja
unaweza ukawa na akili za kijinga namna
hiyo.How could you be so stupid Benedict?
Kauli ile ikampandisha hasira mzee
Benedict akainuka kwa hasira
“ Am I stupid?? Akauliza kwa hasira
“ yes you are stupid.Unamuangamiza
mwanao huku ukiona.Huoni kuwa huo ni
ujinga uliopitiliza?”
“ Mjinga ni wewe hapa ambaye
hutaki kuona mwanao akiwa na
furaha.Kila mwanaume ambaye mwanao
anampata wewe unamkataa.Unataka
aolewe na nani na shetani? Sasa mimi
natoa kauli yangu ya mwisho kuwa Monica
ataolewa na Daviz Zumo.Hiyo ni kauli
yangu ya mwisho na hakuna wa
kuipinga.Kesho asubuhi nitaongea na
Monica na kumfahamisha kuhusu jambo
hili na ninaamini hata yeye mwenyewe
atakubali”
“ Why are you doing this Benedict?
“ Hii ni kwa faida ya Monica.Nataka
Monica aishi maisha mazuri na yenye
furaha.Hii si nafasi ya kuiacha..” akasema
Benedict
“ Unafanya kwa ajili ya Monica au
kwa ajili yako mwenyewe?
“ Both..Kwa ajili ya Monica na kwetu
pia”
“ Please let me out of this.Katu siwezi
kushiriki katika mambo ya kipumbavu
kama hayo.” Akasema bi Janet kwa hasira
“ Tafadhali Jane naomba usinidharau
.Mimi nimekwisha amua na hakuna wa
kupingana na mimi.Mimi ndiye mwenye
 
SEHEMU YA 71

kauli ya mwisho humu ndani.” Akasema
mzee Benedict kwa hasira akionekana
kukasirishwa sana na kauli ile ya mke
wake.Bi Janet naye akapandwa na hasira
akasema
“ Benedict umenilazimisha nifanye
kile ambacho sikuwa nimekikusudia
kukifanya kwa hiyo naomba unisikilize
kwa makini sana” Akasema bi Janet na
kuvuta pumzi ndefu
“ Kwanza kabisa napenda
nikukanushe kuwa wewe si mwenye kauli
ya mwisho humu ndani bali mimi ndiye
mwamuzi wa mwisho wa jambo lolote
humu ndani.Kwa muda mrefu
nimekuachia ufanye maamuzi kwa sababu
ya kukuheshimu lakini humu ndani
mwenye madaraka ya kusema kitu kiwe ni
mimi.I’m the head of this house and not
you.You are just a man but you are
nothing. “ akanyamaza na kumtazama
mzee Benedict aliyekunja sura yake kwa
hasira
“ Nani aliyekwambia kwamba wewe
ndiye mkubwa wa nyumba hii? Akauliza
Benedict kwa hasira
“ Benedict ninapoongea nataka
utulie nani kakupa ruhusa ya kuzungumza
wakati sijamaliza? Ngoja nimalize
kuzungumza na wewe ndipo
utazungumza.Umenilazimisha mwenyewe
nifanye hivi kwa hiyo usinione mbaya.”
Akasema Janet na kumtazama Benedict
kwa hasira
“ Kwa kuwa nilikwisha kueleza awali
kuwa mimi ndiye mwenye kauli ya
mwisho humu na ndiye kiongozi basi kauli
yangu ya mwisho ni kwamba Monica
haolewi na David Zumo.Thats final.Ni
afadhali akaolewa na Yule mtu aliyekufa
akarudi kuliko kuolewa na David..”
akasema Janet
“ Janet you must be insane..!!! Yaani
Monica aolewe na Yule mfu? That will
never happen.Ninasema hivi Monica
ataolewa na David Zumo na hakuna wa
kulipinga hilo si wewe wala nani.Najua
unasema kwamba wewe ndiye mwenye
kauli ya mwsho kutokana na sehemu
kubwa ya mali tulizonazo kuwa
zimetokana nawe lakini hiyo hainifanyi
nishindwe kusimama kama mwanaume
katika masuala makubwa ya watoto
wangu.Sina shida na mali zako kwani
muda si mrefu nitakuwa na mali nyingi
kushinda hizi dunia yote watanifahamu
lakini linapokuja suala la watoto huna
kauli yoyote na ninaomba usijaribu
kufanya chochote kulifaya suala hili
lishindikane.I swear Janet nitafanya kitu
ambacho hukuwa umekitazamia..!!!
akasema mzee Benedict kwa hasira
“ Benedict utanifanya nini? Utanua?
Chunga maneno unayoyangea Ben wakati
unafahamu kabisa unaongea na
nani.Nakushangaa umetowa wapi kiburi
cha kuongea nami namna hiyo wakati
unanifahamu fika kwamba mimi ni mtu wa
namna gani.Nakuonya Ben achana kabisa
na suala hili.Sitaki kabisa uingilie masuala
ya watoto wangu ”
“ They are my children !! Huwezi
kunipangia chochote juu ya watoto wangu
.Nimesema Monica ataolewa na David
Zumo and that’s final.Ninakuomba
usiongee chochote tena nisije nikakufanya
kitu kibaya usiku huu nikabaki najuta”
Bi Janet akamtazama kwa hasira na
huku midomo ikimtetemeka akasema

Nilikwambia
kwamba
unanilazimisha nifanye kila ambacho
sikuwa nimekusudia kukifanya.Unanivuta
mikono kufanya jambo gumu sana kwangu
lakini sina namna nyingine ya kufanya
zaidi ya kukueleza ukweli ili tulimalize
suala hili ambalo ni wewe mwenyewe
umelianzisha.I’m not ready to see you
send my daughter to the hell so I’m going
to fight with all my strength I have.Kwa
kuanzia nataka nikuweke wazi kuhusu
jambo moja.Monica is not your daughter”
 
SEHEMU YA 72

Mzee Benedict akamtazama mkewe kwa
hasira halafu akajikuta akitabasamu na
kuachia kicheko
“ Sijawahi kuona mwanamke mjinga
kama wewe katika hii dunia.Huyu mtoto
ulimzaa vipi bila mimi? Akauliza na
kuachia kicheko kidogo
“ Narudia tena Monica si
mwanao.Lifahamu hilo na utambue kuwa
huna mamlaka ya kuamua chochote juu
yake.” Akasema Janet.
“ Unasema nini Jane? Monica si
mwanangu ? akauliza mzee Benedict
“ Nadhani umenisikia vizuri
nimerudia mara mbili kukueleza kuwa
Monica si mwanao.” Akasema Jane.
“ Kama si mwanangu ni nani?
Mjomba wangu? Akauliza mzee Benedict

Nisikilize
vizuri
na
unielewe,Monica si mwanao.Si damu
yako.Monica ana baba yake.Wewe ni mlezi
wake tu.”
“ That’s not true.!! That,s a lie..!!!
akasema mzee Benedict kwa hasira.
“ Its not a lie my dear Benedict.Its the
truth.Monica is not your daughter.I’m
sorry I lied to you about this” akasema
Janet
“ Hapana si kweli.Hii ni janja yako ya
kutaka jambo hili lisifanikiwe.” Akasema
Benedict
“ Benedict uko tayari kufanya kipimo
cha DNA kuthibitisha hiki ninachokisema?
Akauliza Janet.Mzee Benedict akabaki
kimya amesimama akimtazama mke wake
“ Nijibu Banedict uko tayari
tukapime ili uthibitishe Monica si
mwanao? Akauliza bi Janet .Uso wa mzee
Benedict ukaloa jasho akakaa kitandani
akaweka mikono kichwani.
“ Anachokisema huyu mwanamke
kinaweza kuwa kweli au ni sehemu ya
ulaghai wake ili kuufanya mpango wangu
na David Zumo ushindwe kufanikiwa?Why
she’s doing this? Akawaza mzee Benedict
huku jasho likimtiririka.
“ Siwezi kukubali huyu mwanamke
akanishinda na kuyakosa yale yote
niliyokubaliana na David Zumo” akawaza
Benedict na kuvuta droo yake iliyoko
kitandani akatoa bastora na kumfuata
mkewe aliyekuwa amekaa upande wa pili
wa kitanda machozi yakimtoka.mzee
Benedict akamuwekea bastora kichwani
“ tell me the truth Janet,or I’ll kill you
!!.. akasema mzee Benedict
“ Ben that’s the truth” akasema
Janet.Mzee Ben akamtazama kwa hasira
na huku mkono wake uliokuwa na bastora
ukimtetemeka kwa hasira
“ Kama unadai mimi si baba yake
nani basi ni baba yake? Akauliza mzee
Benedict.
“ Put the gun down Benedict you are
not going to shoot me.” Akasema Janet na
kuushika mkono wa mzee Benedict
uliokuwa na bastora taratibu akaushusha
chini.
“Sit !! akasema Janet kwa sauti kali
na mzee Benedict akaketi kitandani
pembeni yake.
“ I’m sorry Ben..Real sorry.This is the
sercret I’ve kept for years but I cant keep it
any longer.Ni wakati sasa wa kuufahamu
ukweli wote.” Akasema Janet
“ Just tell me who is the father of
Monica ” akasema mzee Benedict
Janet akafikiri kidogo na kusema
“ Ernest Mkasa” akasema Janet na
kumfanya mzee Benedict amrukie kama
Simba na kumkaba koo.
“ How could you do something like
that Janet??!! Akauliza Benedict kwa
hasira .Janet akajitutumua kwa nguvu na
kumsukuma Ben akaanguka chini.

Huyu
mjinga
alitaka
kuniua.”akawaza Janet huku akikohoa
mfululizo.
Mzee Benedict akaegemea kitanda
akilia
machozi.Janet
akageuka
akamtazama na kumsogelea akamshika
bega.
 
SEHEMU YA 73

“ Benedict I’m very sorry” akasema
bi Janet
“ Janet tumekuwa pamoja kwa miaka
mingi
hadi
sasa
tumekuwa
wazee.Tumepitia mambo mengi sana
makubwa,mazuri na mabaya,mimi na
wewe tuna historia kubwa lakini katika
safari yetu hii ya maisha hadi hapa
tulipofika hakuna siku ambayo nimewahi
kuumia na kujuta kukutana nawe kama
siku hii ya leo.Naomba nikuweke wazi
kuwa umeuchana chana moyo wangu .Ni
kweli wewe ndiye chanzo cha hizi maIi
zote ingawa tunaolifahamu hilo ni mimi na
wewe tu lakini kwa hili ulilolifanya naapa
sintakusamehe kamwe.I’ll never forgive
you Janet.Ulidai kwamba Ernest ni rafiki
yako na anatusaidia kuondokana na
umasikini lakini kumbe unatembea naye
!!” Akasema mzee Benedict huku mwili
ukimtetemeka kwa hasira.
“ Hata usiponisamehe Ben I don’t
care.Nilifanya nililopaswa kulifanya kwa
ajili ya kutusaidia kuondoka katika
maisha yake magumu tuliyokuwa
nayo.Bila kufanya vile katu tusingekuwa
na maisha haya.” Akasema bi Janet kwa
sauti kali.
“ Sasa nimegundua kwamba kwa
miaka hii yote ambayo tumeishi wote
tumeishi
katika
ulaghai
mkubwa.Hukuwahi
kunipenda
hata
kidogo.” Akasema Benedict
“ Kama nisingekuwa nakupenda Ben
nisingekuwa nawe hadi muda huu”
akasema Janet
“ Lier !!Huna hata chembe ya upendo
ndani mwako .Mwanamke una roho ya
kishetani.Sikujua kama una roho mbaya
namna hii.Kwa nini usingenieleza jambo
hili toka mapema nijue?
“ Samahani kwa hilo Ben.Nakiri
nilifanya kosa kutokukueleza.Niliogopa
kukueleza kwa sababu niliogopa
ungeumia sana kwani nafahamu namna
unavyonipenda.Nimeishi na siri hii
moyoni kwa muda mrefu na nimekuwa
nikijaribu kutafuta ujasiri wa kukueleza
lakini nimeshindwa. Hili ni jambo la aibu
na
ndiyo
maana
sikutaka
lijulikane.Nisamehe
Ben
.Nisamehe
sana.Najua nimekuumiza mno.Hata mimi
ninaumia vile vile kwani sijui uso wangu
nitauweka wapi pindi Monica akilifahamu
jambo hili.Tafadhali naomba tusilifanye
jambo hili kuwa gumu Ben.Tushauriane
nini cha kufanya.” Akasema Janet kwa
sauti ya chini.
Mzee
Benedict
aliendelea
kuinamisha kichwa alikuwa na mawazo
mengi.Akainua kichwa na kuuliza
“ Ernest anafahamu kuwa Monica ni
mwanae? Akauliza mzee Ben
“ Hapana hafahamu kama Monica ni
mwanae” akasema Janet
“ Kwa nini hukumueleza ukweli?
Akauliza Ben na Janet akashindwa kujibu
kitu akabaki kimya
“ Answer me Jane kwa nini
hukumueleza ukweli Ernest kuhusiana na
Monica?

Because
I
don’t
love
him.Ninamfahamu Ernest si mtu mzuri na
ndiyo maana sikutaka afahamu Monica ni
mwanae kwani kama angefahamu basi
angeweza kumchukua kitu ambacho
sikuwa tayari.Sikutaka Monica akaishi na
Ernest” akasema Janet na kuinamisha
kichwa.
 
SEHEMU YA 74


“ How could you ..!.” akasema Ben
lakini akajikuta akishindwa kumalizia
alichotaka kukisema akainamisha kichwa
.Baada ya muda akauliza
“Niambie nani ni baba wa Nathan?
Akauliza mzee Ben
“ Ni wewe” akajibu Jane
“ Are you sure?
“ Yes..!!
“ Niambie Jane nani ni baba wa
Nathan kwa sababu sikuamini tena kwa
lolote lile.”
“ Nathani ni mtoto wako,uamini
usiamini lakini huo ndio ukweli.Nathani ni
mwanao na hilo halina ubishi.”
“ Vyovyote utakavyosema Jane kaa
ujue kuwa sintokuamini tena ,una roho ya
kishetani”
“ Usianze kunitusi Ben..” akasema
Janet
“ Sikutusi Jane huo ni ukweli.You are
a devil !!
“ Don’t call me a devil Ben ..Kama
mimi ni shetani na wewe utakuwa nani?
Usijifanye malaika hapa Ben.We’re both
devils.Tumefanya mambo mengi mabaya
kwa hiyo huu si muda wa kuanza
kushutumiana nani
shetani
nani
malaika.Jambo
limetokea
na
tunachopaswa kukifanya kwa sasa ni
kujadili tunatokaje katika dimbwi hili la
matope kwani sote tumepakaa matope na
tunatakiwa tuyafute matope haya kabla
watu hawajauona uchafu huu tulioufanya ”
Akasema Jane
“ Usiseme tumepakaa matope wewe
ndiye uliyepakaa matope na si mimi.Kama
ni aibu basi itakuwa juu yako na si mimi.”
Akasema Ben
“ Ben usidhani sifahamu uchafu
wako.Watoto wangapi umezaa na
wanawake wako huko nje unadhani
siwajui? Ninakufahamu vizuri sana Ben na
ninafahamu
kila
unachokifanya
.Ninafahamu makahaba wako wote
unaotembea nao na ndiyo maana
nikasema kwamba tunatakiwa tujisafishe
matope haya tuliyopakaa kabla siri zetu
hazijaanza kutoka nje ya nyumba hii.”
Akasema Janet.UKapita ukimya wa dakika
tano mzee Ben akasema
“ Ukitaka kujisafisha matope hayo
unayoyasema anza kwa kumueleza ukweli
Monica.”akasema mzee Ben na Janet
akabaki kimya.
“ Ni jambo gumu sana lakini lazima
ulifanye.Lazima Monica ajue ukweli wote”
“ Ben I cant do that.She’s going to
hate me forever”
“ Kwa hiki ulichokifanya unastahili
kuchukiwa.Ni jambo baya mno umelifanya
Jane.Anastahili akuchukie sana kwa
sababu
utamsababishia
maumivu
makubwa.Utazivuruga ndoto zake nyingi
alizonazo” akasema Mzee Ben.
“ Ben I don’t want to hurt my
daughter.Please let’s keep this secret
between us. Hakuna yeyote anayefahamu
kuwa Monica si mwanao zaidi yangu.Lets
us take this secret to our graves.Monica
ataendelea kuwa mwanao na familia yetu
itaendelea kuwa moja na yenye
amani.Tukimueleza ukweli atatuchukia
mno na ataumia sana jambo ambalo sitaki
litokee
kwani
ninampenda
sana
Monica.Wewe utabaki kuwa baba yake
kwani umemlea kwa upendo mkubwa
toka akiwa mdogo hadi leo hii.Nakuomba
Ben tusikubali jambo hili likaivuruga
familia yetu.Tumetoka mbali sana na huu
 
SEHEMU YA 75


ni wakati wa kufurahia matunda ya kazi
ngumu tuliyokwisha ifanya huko nyuma
na si kuibua mifarakano.Sote tumefanya
makosa mengi .Wewe pia Ben una watoto
wa nje ambao ninawafahamu lakini
sijawahi kukuuliza chochote kuhusu
jambo hilo kwa hiyo hakuna msafi kati
yetu.”
Akasema
Janet.Mzee
Ben
akainamisha kichwa akafikiri kwa muda
kisha akasema
“ Kama unataka iwe hivyo lazima
tukubaliane jambo moja” akasema Ben
“ Jambo gani Ben?
“ Monica aolewe na David Zumo”
“ What ???.. Janet akastuka
“ Umenisikia vizuri Jane,kama
unataka jambo hili liendele kuwa siri na
mwanao asilifahamu basi ridhia Monica
aolewe na David Zumo na kila kitu
kitakuwa kimekwisha.”
“ Hilo haliwezekani Ben.Ninasema
hilo sikubaliani nalo”
“ kama hukubaliani nalo basi lazima
Monica aufahamu ukweli wote and she’ll
hate you forever.Do you want her to hate
you??Si yeye peke yake atakayekuchukia
bali Nathan pia .Wote watakuacha peke
yako.Unataka hilo litokee? Akauliza mzee
Ben.Janet akabaki kimya
“ Ukimya huo unaonyesha kwamba
hauko tayari kwa hiyo basi tunakubaliana
kuwa Monica aolewe na David Zumo”
akasema mzee Ben.Janet akafikiri kwa
muda kisha akasema
“ Ben please don’t do that.We are
sending our daughter to hell !!..Utajiri wa
David Zumo hauna uhalali.Ameuchuma
utajiri wake kutoka kwa raia masikini wa
Kongo,amekuwa akifuja rasilimali za nchi
yake kwa hiyo utajiri wake una
laana.Kukubali Monica aolewe na David ni
kumuingiza mwananetu katika laana
hiyo.Tafadhali Ben tusifanye hivyo.”
Akasema Janet huku akitoa machozi
“ Janet huo ndio msimamo wangu
ambao siwezi kuubadili.Monica lazima
aolewe na David Zumo.Kuna faida nyingi
sana kwa jambo hilo kwa hiyo kama
ukitaka tuendelee kuishi kwa amani na
furaha Monica lazima akubali kuolewa na
David Zumo.” Akasema Ben na kuinuka
akatoka mle chumbani akaelekea sebuleni
katika ukuta kulikuwa na picha kubwa
waliyopiga wote kama familia.Akaitazama
na kulengwa na machozi
 
SEHEMU YA 76

“ Sikujua kama siku moja Jane angekuja
kuniumiza kiasi hiki. Ninafahamu ni
mwanamke mwenye roho ya ukatili lakini
sikutegemea kama angefikia kufanya
jambo hili.Nilimpenda sana Jane toka
tukiwa bado vijana wadogo na nilikuwa
tayari kufanya jambo lolote kwa ajili ya
kuwa naye.Nilikubali kufanya mambo
mengi tu ya hatari kwa lengo moja tu la
kuishi naye maisha mazuri lakini leo
ameniumiza sana na sijui Monica ataumia
vipi akilifahamu jambo hili.” Akawaza na
kwenda kuketi sofani
“ Ernest Mkasa.!! Akasema kwa sauti
ndogo na kukunja sura
“ Kumbe Jane alikuwa na mahusiano
ya siri na Ernest.Dah !! ama kweli hakuna
rafiki wa kweli katika hii dunia.Ernest ni
rafiki yetu mkubwa na ambaye alijitolea
sana kutusaidia kwa hali na mali hadi
tukafika hapa tulipofika lakini kumbe
alikuwa na lengo lake nyuma ya
pazia.Simuamini tena Jane na nina hakika
hadi sasa bado yeye na Ernest
wanaendeleza mahusiano yao.What am I
going to do ?? akajiuliza mzee Ben .Alihisi
kichwa kimekuwa kizito sana akajilaza
sofani
“ Ernest Mkasa wa sasa si Yule wa
kipindi kile tuliyekuwa tukimfahamu.Kwa
sasa ni mtu mkubwa ,and he’s very
powerfull.Ni rais wa Tanzania.Ni mtu
ambaye nilimuamini sana na sikutegemea
kama angeweza kunifanyia usaliti
mkubwa kama huu.Japokuwa kwa sasa
ana nguvu kubwa lakini siwezi kumuacha
hivi hivi lazima nitafute namna ya
kupambana naye.I must fight him.”
Akawaza mzee Benedict
“ Nimepitia mambo mengi sana
magmu na ya kusikitisha lakini sijawahi
kuumia kama nilivyoumizwa na jambo hili
la
kuambiwa
Monica
si
mwanangu.Ninawapenda Monica na
Nathan kuliko kitu chochote katika hii
dunia na kwa sababu hiyo nitapambana
kwa ajili yao.Monica ataendelea kuwa
mwanangu hadi siku ninaondoka katika
dunia hii na hakuna wa kulibadili
hilo.Hata hivyo I must do something ..”
akawaza na kuinuka akaenda tena
kuitazama ile picha waliyopiga wote kama
familia wakiwa na nyuso zenye tabasamu
“ I must destroy Ernest Mkasa.”
Akawaza na kufungua mlango akatoka na
kukaa kibarazani akitazama angani
“ Ernest is my best
friend,amenisaidia sana hadi kufika hapa
nilipofika lakini kwa hili alilolifanya katu
siwezi kuvumilia,I must destroy him.”
Akawaza huku sura yake ikionyesha wazi
kuwa alikuwa amedhamiria kukifanya kile
alichokuwa anakiwaza
“ Yes I must destroy him...Siwezi
kuvumilia kufanyiwa kitendo kama
hiki.Ernest Mkasa must be destroyed.”
Akawaza na kupiga ngumi ukutani kwa
hasira halafu akaelekea sebuleni na kukaa
sofani kichwa chake kikiwa kizito kwa
mawazo.
Janet Mwamsole alikaa kitandani na
alishindwa kuyazuia machozi yasimtoke.
“ My family is falling apart..!!
akasema kwa sauti ndogo na kuchukua
kitambaa akafuta machozi.
“ I took years to build this family
lakini kwa kosa moja nililolifanya miaka
zaidi ya ishirini iliyopita kazi yote kubwa
niliyoifanya kwa miaka mingi imekuwa
bure.Familia
yangu
inakwenda
kugawanyika.Monica akigundua kwamba
Ben si baba yake mzazi hakutakuwa na
familia tena.Atanichukia sana na hatataka
kuniona tena.Si yeye peke yake bali
familia nzima watanichukia.Nitabaki peke
yangu.Hapana sitaki hilo litokee.Familia
hii niliyonayo ni kila kitu kwangu kuliko
hata hizi mali nilizonazo kwa hiyo
nitafanya kila niwezalo kuhakikisha
familia hii haigawanyiki.Ngoja nikubaliane
 
SEHEMU YA 77

na hiki anachokitaka Ben yaani Monica
aolewe na David Zumo.Japokuwa moyo
wangu hautaki jambo hili lakini hakuna
namna lazima nikubali ili mimi na Ben
tuweze kwenda sawa.” Akawaza na kufuta
tena machozi
“ Sikutaka mtu yeyote aifahamu siri
hii lakini sijui kitu gani leo kimenifanya
niitoe.Ni siri ambayo niliapa kwenda nayo
kaburini lakini kwa kuamua kuiweka wazi
kwa Ben nimevuruga kila kitu.Ben will
never trust me again.Ninampenda Ben
sana na hata yeye ananipenda sana na
sikufanya jambo hili kwa makusudi bali
ilinilazimu kufanya mapenzi na Ernest
Mkasa.Sikuwa na namna nyingine ya
kufanya zaidi ya kufanya vile .” akawaza
Jane na kuanza kukumbuka historia ya
nyuma alikotoka na Benedict
DAR ES SALAAM
“ Janet tafadhali naomba ufanye kila
linalowezekana uweze kunitoa humu
ndani.Wewe
ndiye
pekee
ninayekutegemea ukishindwa wewe basi
maisha yangu yote yatamalizikia
gerezani.” Akasema kijana mmoja
aliyekuwa
amesawajika.Mwanamke
aliyekuwa akionge anaye mwenye uzuri
wa kipekee akafuta machozi na kusema
“ Ben nimejitahidi sana kufanya kila
linalowezekana lakini mpaka sasa
sijafanikiwa .Kesi hii mawakili wengi
wanaiogopa kwani kijana uliyemgonga na
kufa ni mjukuu wa mmoja wa waziri
mstaafu ambaye ana heshima kubwa hapa
nchini.Kila mwanasheria ambaye
ninamtafuta atusimamie katika kesi hii
anakuwa na mashaka kama anaweza
akashinda.”
“ Janet you have to do
something.Mimi sikuwa na makosa bali
wao ndio walionigonga na gari lao na
inaonekana walikuwa wamelewa.Kwa nini
hawataki kulizingatia hili na wanataka
waniangamize wakati sina hatia?
Tafadhali Jane ninakutegemea sana.Wewe
ndiye unayeweza kuniokoa katika
hili.Tafadhali
naomba
unisaidie
Jane.Nikiendelea kukaa humu ndani
mipango yetu yote itashindwa
kufanikiwa.Dont you believe me Jane?”
Akauliza Ben.Janet akafuta machozi na
kusema
“ I believe you Ben.Nitakwenda
kutafuta namna nyingine ya
kufanya.Usivunjike moyo mpenzi
wangu.Mungu atatusaidia na tutashinda
hii kesi.” Akasema Janet na kuagana na
mpenzi wake akatoka mle gerezani huku
machozi yakimtoka.Hakutaka kupoteza
muda akaingia katika teksi iliyompeleka
pale gerezani akamuamuru dereva
aondoke.
“ Huu ni mkosi gani unanikuta mimi?
Kwa nini maisha yangu yamebadilika na
kuwa magumu namna hii? Sikuwahi hata
mara moja kuhisi kuwa maisha yangu siku
moja yatakuwa namna hii .Wazazi wangu
ni matajiri lakini hawako tayari kunisaidia
kwa namna nilivyowakorofisha. Akawaza
Janet na kufuta machozi
“ Laiti kama nisingejiigiza katika
mahusiano na Ben na kupata mimba yote
haya yasingetokea.Hivi sasa ningekuwa
mbali sana na ningekuwa na maisha
mazuri lakini nilishawishika na kuingi
akatika mahusiano na Ben na sasa haya
ndiyo
yanayonikuta.Hakuna
wa
 
Back
Top Bottom