SEHEMU YA 70
Kwani vipi Janet.Jambo hili lina
ubaya gani? Mtu kama David ndiye
ambaye
Monica
amekuwa
akimuhitaji.Tumesubiri kwa muda mrefu
Monica ampate mwanaume mzuri wa
kumfaa na Mungu amejibu maombi yake
amemletea mwanaume wa maisha
yake,ambaye anampenda kwa moyo wake
wote.Wanasema mvumilivu hula
mbivu,Monica amevumilia kwa muda
mrefu na sasa ni wakati wake wa kuzila
mbivu kwani anakwenda kuwa malkia
halisi wa afrika .Anakuwa mke wa tajiri
namba moja wa af..”
“ Oh my God !! Benedict are you
crazy??!!!! Akauliza bi Janet kwa hasira
“ Janet kuna tatizo gani katika hilo?
That what we’ve been dreaming for
her,right?.Monica kumpata mwanaume
atakayempenda ilikuwa ni ndoto yako
kubwa na sasa kuna tatizo gani wakati
ndoto hiyo imetimia tayari? Amejitokeza
mwanaume
mwenye
sifa
unazozitaka.David bado kijana ,ni raisi wa
nchi,ni tajiri namba moja afrika kwa
ujumla ni mtu mwenye sifa zote za
kumuoa Monica.Zaidi ya yote anakwenda
kutusaidia sana kiuchumi.Anakwenda
kutupaisha imataifa zaidi na sisi tutaingia
katika orodha ya matajiri wa dunia kwani
uwezo huo anao.” Akasema Benedict
Mke wake akamtazama kwa hasira
huku akihema mfululizo na kusema
“ Toka moyoni mwako unakubali
kweli Monica aolewe na David Zumo?
Akauliza.Bila kupepesa macho mzee Ben
akajibu
“ Kwa moyo mweupe kabisa
ndiyo,nataka Monica aolewe na David
Zumo.Sina kipingamizi chochote katika
jambo hilo kwani naamini Yule ndiye hasa
mwanaume anayemfaa...”
Bi Janet akamtazama mumewe na
kutikisa kichwa
“ Sikutegemea kama siku moja
unaweza ukawa na akili za kijinga namna
hiyo.How could you be so stupid Benedict?
Kauli ile ikampandisha hasira mzee
Benedict akainuka kwa hasira
“ Am I stupid?? Akauliza kwa hasira
“ yes you are stupid.Unamuangamiza
mwanao huku ukiona.Huoni kuwa huo ni
ujinga uliopitiliza?”
“ Mjinga ni wewe hapa ambaye
hutaki kuona mwanao akiwa na
furaha.Kila mwanaume ambaye mwanao
anampata wewe unamkataa.Unataka
aolewe na nani na shetani? Sasa mimi
natoa kauli yangu ya mwisho kuwa Monica
ataolewa na Daviz Zumo.Hiyo ni kauli
yangu ya mwisho na hakuna wa
kuipinga.Kesho asubuhi nitaongea na
Monica na kumfahamisha kuhusu jambo
hili na ninaamini hata yeye mwenyewe
atakubali”
“ Why are you doing this Benedict?
“ Hii ni kwa faida ya Monica.Nataka
Monica aishi maisha mazuri na yenye
furaha.Hii si nafasi ya kuiacha..” akasema
Benedict
“ Unafanya kwa ajili ya Monica au
kwa ajili yako mwenyewe?
“ Both..Kwa ajili ya Monica na kwetu
pia”
“ Please let me out of this.Katu siwezi
kushiriki katika mambo ya kipumbavu
kama hayo.” Akasema bi Janet kwa hasira
“ Tafadhali Jane naomba usinidharau
.Mimi nimekwisha amua na hakuna wa
kupingana na mimi.Mimi ndiye mwenye