LEGE
JF-Expert Member
- Oct 14, 2011
- 5,122
- 9,209
- Thread starter
- #401
SEHEMU YA 78
kumlaumu kwa maisha haya kwani
nimeyataka mwenyewe ninachopaswa ni
kusimama na kupambana kumtoa Ben
gerezani kwani nikishindwa kufanya
hivyo atafungwa.Kesi hii inamuendea
vibaya sana.Si yeye aliyesababisha ajali ile
lakini kwa kuwa mtu aliyefariki katika
ajali hiyo ni mjukuu wa mwanasiasa basi
kesi yote inamuangukia yeye.I must save
him” akawaza Janet kisha akamuelekeza
dereva ampeleke Papaya supermarket.
“ Baba anaweza kabisa kunisaidia
katika jambo hili.Natamani nikampigie
magoti nimuombe msamaha ili anisaidie
lakini
hatakuwa
tayari.Msaada
anaonisaidia wa kumlea mwanangu
Nathani unatosha .Lazima nipambane
mwenyewe.Namshukuru mama ambaye
amekuwa akinipa msaada mkubwa sana
kama si yeye sijui ningeishi vipi hapa
mjini.” Akawaza Janet .
Dereva taksi akamfikisha Janet,
Papaya supermarket akashuka na kuanza
kupiga hatua kuelekea ndani kununua
mahitaji aliyoyataka lakini mara akastuka
baada ya kumuona mtu Fulani akiwa
amekaa nje ya gari la kifahari akiongea na
mwenzake
“ Ernest !! akasema kwa mshangao
na kisha akaanza kupiga hatua
kumuendea.Yule kijana naye alipomuona
Janet akastuka sana
“ Janet !! akasema na kisha wote
wakakumbatiana.
“ Jane is that you?? Akauliza Ernest
“ Ni mimi Ernest.” Akajibu
Jane.Ernest akamuomba samahani Yule
mtu aliyekuwa anaongea naye
wakakubaliana kukutana siku nyingine
“ Jane sikutegema kabisa kuuoana
nawe.I’ve been searching for you
everywhere lakini sijafanikiwa kukuona”
akasema Ernest
“ Mbona nipo Ernest nimejaa tele
hapa mjini.Ninapambana tu na
maisha.Vipi wewe maisha yako
yanakwendaje? Akauliza Jane
“ Mambo yangu siwezi kusema ni
mabaya.Ni kama unavyoniona” akasema
Ernest huku akitabasamu
“ Vipi wewe mambo yako
yanakwendaje? Akauliza Ernest lakini
Janet akasita kidogo
“ Jane una haraka sana? Kama huna
haraka sana tunaweza kupata nafasi
tukakaa mahali tukaongea?
“ Bila tatizo” akasema Jane na
kwenda kumlipa dereva taksi pesa yake
kisha akaongozana na Ernest hadi katika
gari lake la kifahari wakaondoka
“ Jane nilihitaji sana kukuona lakini
kila ninayemuuliza hana habari zako na
hakuna anayejua unapoishi” akasema
Ernest wakiwa garini.Jane akatabasamu
na kusema
“ Maisha yangu sitaki yajulikane
ndiyo maana sitaki kumuelekeza rafiki
yangu yeyote mahali ninakoishi.” Akasema
Jane
Hawakuwa na maongezi mengi
garini kwani muda mwingi Ernest alikuwa
akiongea na simu.Waliwasili La 403
Casino wakashuka garini na kuingia ndani
ya kasino lile ambalo Ernest alionekana
kujulikana sana kwani alisalimiana na
watu mbalimbali aliowakuta mle ndani
.Ernest akamuongoza Jane hadi katika
chumba kimoja kizuri kikubwa
“ Jane karibu sana La 403 Casino.Hii
ni moja ya biashara ninazozimiliki kwa
sasa” akasema Ernest na kumfanya Jane
astuke .
“ That’s not true” akasema Jane
“ Its true Jane.Kitu gani
kinachokufanya usiamini? Akauliza Ernest
huku akicheka
“ Ernest nimestuka tu sikutegemea
kabisa kama ungeweza kumiliki kitu
kikubwa kama hiki” akasema Janet
“ Si hii moja tu bali ninazo biashara
nyingine nyingi tu sehemu mbalimbali
.You are talking to a man.” Akasema Ernest
kwa majigambo
“ Hongera sana Ernest.Umejitahidi
sana .Nakumbuka hata tukiwa shule ndoto
yako siku zote ilikuwa ni kuwa mtu
mkubwa.Sasa nimeyaamini maneno yako”
akasema Janet.Ernest akafungua friji
akatoa kinywaji na kumkaribisha
Janet.Halafu akasema
“ Haya Janet nieleze maisha yako
yakoje? Akasema Ernest na uso wa Janet
ukachanua kwa tabasamu pana.
“ Ouh Jane uzuri wao bado ule ule na
sasa umezidi maradufu.Lile tabasamu lako
ambalo lilikuwa linanipa uchizi bado
lipo.You are so beautifull Jane” akasema
Ernest
“ Ernest bado hujaacha yale maneno
yako tu” akasema Anna na kunywa funda
dogo la kinywaji
“ Niambie Jane.Maisha yako
yanakwendaje? Tell me everything about
your life” akasema Ernest.Janet akavuta
pumzi ndefu na kusema
“ Ernest sijui nianzie wapi kukueleza
kuhusu maisha yangu.Lakini kwa ujumla
naweza kusema kwamba maisha yangu si
mazuri sana.Si maisha yale ambayo
nilikuwa ninaota kuyaishi.Naweza kusema
kwamba ndoto zangu sijaweza
kuzitimiza.” Akasema Jane.Ernest
akamtazama halafu akanywa kinywaji
kidogo akapokea simu iliyokuwa ikiita
kisha akamgeukia Jane
kumlaumu kwa maisha haya kwani
nimeyataka mwenyewe ninachopaswa ni
kusimama na kupambana kumtoa Ben
gerezani kwani nikishindwa kufanya
hivyo atafungwa.Kesi hii inamuendea
vibaya sana.Si yeye aliyesababisha ajali ile
lakini kwa kuwa mtu aliyefariki katika
ajali hiyo ni mjukuu wa mwanasiasa basi
kesi yote inamuangukia yeye.I must save
him” akawaza Janet kisha akamuelekeza
dereva ampeleke Papaya supermarket.
“ Baba anaweza kabisa kunisaidia
katika jambo hili.Natamani nikampigie
magoti nimuombe msamaha ili anisaidie
lakini
hatakuwa
tayari.Msaada
anaonisaidia wa kumlea mwanangu
Nathani unatosha .Lazima nipambane
mwenyewe.Namshukuru mama ambaye
amekuwa akinipa msaada mkubwa sana
kama si yeye sijui ningeishi vipi hapa
mjini.” Akawaza Janet .
Dereva taksi akamfikisha Janet,
Papaya supermarket akashuka na kuanza
kupiga hatua kuelekea ndani kununua
mahitaji aliyoyataka lakini mara akastuka
baada ya kumuona mtu Fulani akiwa
amekaa nje ya gari la kifahari akiongea na
mwenzake
“ Ernest !! akasema kwa mshangao
na kisha akaanza kupiga hatua
kumuendea.Yule kijana naye alipomuona
Janet akastuka sana
“ Janet !! akasema na kisha wote
wakakumbatiana.
“ Jane is that you?? Akauliza Ernest
“ Ni mimi Ernest.” Akajibu
Jane.Ernest akamuomba samahani Yule
mtu aliyekuwa anaongea naye
wakakubaliana kukutana siku nyingine
“ Jane sikutegema kabisa kuuoana
nawe.I’ve been searching for you
everywhere lakini sijafanikiwa kukuona”
akasema Ernest
“ Mbona nipo Ernest nimejaa tele
hapa mjini.Ninapambana tu na
maisha.Vipi wewe maisha yako
yanakwendaje? Akauliza Jane
“ Mambo yangu siwezi kusema ni
mabaya.Ni kama unavyoniona” akasema
Ernest huku akitabasamu
“ Vipi wewe mambo yako
yanakwendaje? Akauliza Ernest lakini
Janet akasita kidogo
“ Jane una haraka sana? Kama huna
haraka sana tunaweza kupata nafasi
tukakaa mahali tukaongea?
“ Bila tatizo” akasema Jane na
kwenda kumlipa dereva taksi pesa yake
kisha akaongozana na Ernest hadi katika
gari lake la kifahari wakaondoka
“ Jane nilihitaji sana kukuona lakini
kila ninayemuuliza hana habari zako na
hakuna anayejua unapoishi” akasema
Ernest wakiwa garini.Jane akatabasamu
na kusema
“ Maisha yangu sitaki yajulikane
ndiyo maana sitaki kumuelekeza rafiki
yangu yeyote mahali ninakoishi.” Akasema
Jane
Hawakuwa na maongezi mengi
garini kwani muda mwingi Ernest alikuwa
akiongea na simu.Waliwasili La 403
Casino wakashuka garini na kuingia ndani
ya kasino lile ambalo Ernest alionekana
kujulikana sana kwani alisalimiana na
watu mbalimbali aliowakuta mle ndani
.Ernest akamuongoza Jane hadi katika
chumba kimoja kizuri kikubwa
“ Jane karibu sana La 403 Casino.Hii
ni moja ya biashara ninazozimiliki kwa
sasa” akasema Ernest na kumfanya Jane
astuke .
“ That’s not true” akasema Jane
“ Its true Jane.Kitu gani
kinachokufanya usiamini? Akauliza Ernest
huku akicheka
“ Ernest nimestuka tu sikutegemea
kabisa kama ungeweza kumiliki kitu
kikubwa kama hiki” akasema Janet
“ Si hii moja tu bali ninazo biashara
nyingine nyingi tu sehemu mbalimbali
.You are talking to a man.” Akasema Ernest
kwa majigambo
“ Hongera sana Ernest.Umejitahidi
sana .Nakumbuka hata tukiwa shule ndoto
yako siku zote ilikuwa ni kuwa mtu
mkubwa.Sasa nimeyaamini maneno yako”
akasema Janet.Ernest akafungua friji
akatoa kinywaji na kumkaribisha
Janet.Halafu akasema
“ Haya Janet nieleze maisha yako
yakoje? Akasema Ernest na uso wa Janet
ukachanua kwa tabasamu pana.
“ Ouh Jane uzuri wao bado ule ule na
sasa umezidi maradufu.Lile tabasamu lako
ambalo lilikuwa linanipa uchizi bado
lipo.You are so beautifull Jane” akasema
Ernest
“ Ernest bado hujaacha yale maneno
yako tu” akasema Anna na kunywa funda
dogo la kinywaji
“ Niambie Jane.Maisha yako
yanakwendaje? Tell me everything about
your life” akasema Ernest.Janet akavuta
pumzi ndefu na kusema
“ Ernest sijui nianzie wapi kukueleza
kuhusu maisha yangu.Lakini kwa ujumla
naweza kusema kwamba maisha yangu si
mazuri sana.Si maisha yale ambayo
nilikuwa ninaota kuyaishi.Naweza kusema
kwamba ndoto zangu sijaweza
kuzitimiza.” Akasema Jane.Ernest
akamtazama halafu akanywa kinywaji
kidogo akapokea simu iliyokuwa ikiita
kisha akamgeukia Jane