QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

SEHEMU YA 78

kumlaumu kwa maisha haya kwani
nimeyataka mwenyewe ninachopaswa ni
kusimama na kupambana kumtoa Ben
gerezani kwani nikishindwa kufanya
hivyo atafungwa.Kesi hii inamuendea
vibaya sana.Si yeye aliyesababisha ajali ile
lakini kwa kuwa mtu aliyefariki katika
ajali hiyo ni mjukuu wa mwanasiasa basi
kesi yote inamuangukia yeye.I must save
him” akawaza Janet kisha akamuelekeza
dereva ampeleke Papaya supermarket.
“ Baba anaweza kabisa kunisaidia
katika jambo hili.Natamani nikampigie
magoti nimuombe msamaha ili anisaidie
lakini
hatakuwa
tayari.Msaada
anaonisaidia wa kumlea mwanangu
Nathani unatosha .Lazima nipambane
mwenyewe.Namshukuru mama ambaye
amekuwa akinipa msaada mkubwa sana
kama si yeye sijui ningeishi vipi hapa
mjini.” Akawaza Janet .
Dereva taksi akamfikisha Janet,
Papaya supermarket akashuka na kuanza
kupiga hatua kuelekea ndani kununua
mahitaji aliyoyataka lakini mara akastuka
baada ya kumuona mtu Fulani akiwa
amekaa nje ya gari la kifahari akiongea na
mwenzake
“ Ernest !! akasema kwa mshangao
na kisha akaanza kupiga hatua
kumuendea.Yule kijana naye alipomuona
Janet akastuka sana
“ Janet !! akasema na kisha wote
wakakumbatiana.
“ Jane is that you?? Akauliza Ernest
“ Ni mimi Ernest.” Akajibu
Jane.Ernest akamuomba samahani Yule
mtu aliyekuwa anaongea naye
wakakubaliana kukutana siku nyingine
“ Jane sikutegema kabisa kuuoana
nawe.I’ve been searching for you
everywhere lakini sijafanikiwa kukuona”
akasema Ernest
“ Mbona nipo Ernest nimejaa tele
hapa mjini.Ninapambana tu na
maisha.Vipi wewe maisha yako
yanakwendaje? Akauliza Jane
“ Mambo yangu siwezi kusema ni
mabaya.Ni kama unavyoniona” akasema
Ernest huku akitabasamu
“ Vipi wewe mambo yako
yanakwendaje? Akauliza Ernest lakini
Janet akasita kidogo
“ Jane una haraka sana? Kama huna
haraka sana tunaweza kupata nafasi
tukakaa mahali tukaongea?
“ Bila tatizo” akasema Jane na
kwenda kumlipa dereva taksi pesa yake
kisha akaongozana na Ernest hadi katika
gari lake la kifahari wakaondoka
“ Jane nilihitaji sana kukuona lakini
kila ninayemuuliza hana habari zako na
hakuna anayejua unapoishi” akasema
Ernest wakiwa garini.Jane akatabasamu
na kusema
“ Maisha yangu sitaki yajulikane
ndiyo maana sitaki kumuelekeza rafiki
yangu yeyote mahali ninakoishi.” Akasema
Jane
Hawakuwa na maongezi mengi
garini kwani muda mwingi Ernest alikuwa
akiongea na simu.Waliwasili La 403
Casino wakashuka garini na kuingia ndani
ya kasino lile ambalo Ernest alionekana
kujulikana sana kwani alisalimiana na
watu mbalimbali aliowakuta mle ndani
.Ernest akamuongoza Jane hadi katika
chumba kimoja kizuri kikubwa
“ Jane karibu sana La 403 Casino.Hii
ni moja ya biashara ninazozimiliki kwa
sasa” akasema Ernest na kumfanya Jane
astuke .
“ That’s not true” akasema Jane
“ Its true Jane.Kitu gani
kinachokufanya usiamini? Akauliza Ernest
huku akicheka
“ Ernest nimestuka tu sikutegemea
kabisa kama ungeweza kumiliki kitu
kikubwa kama hiki” akasema Janet
“ Si hii moja tu bali ninazo biashara
nyingine nyingi tu sehemu mbalimbali
.You are talking to a man.” Akasema Ernest
kwa majigambo
“ Hongera sana Ernest.Umejitahidi
sana .Nakumbuka hata tukiwa shule ndoto
yako siku zote ilikuwa ni kuwa mtu
mkubwa.Sasa nimeyaamini maneno yako”
akasema Janet.Ernest akafungua friji
akatoa kinywaji na kumkaribisha
Janet.Halafu akasema
“ Haya Janet nieleze maisha yako
yakoje? Akasema Ernest na uso wa Janet
ukachanua kwa tabasamu pana.
“ Ouh Jane uzuri wao bado ule ule na
sasa umezidi maradufu.Lile tabasamu lako
ambalo lilikuwa linanipa uchizi bado
lipo.You are so beautifull Jane” akasema
Ernest
“ Ernest bado hujaacha yale maneno
yako tu” akasema Anna na kunywa funda
dogo la kinywaji
“ Niambie Jane.Maisha yako
yanakwendaje? Tell me everything about
your life” akasema Ernest.Janet akavuta
pumzi ndefu na kusema
“ Ernest sijui nianzie wapi kukueleza
kuhusu maisha yangu.Lakini kwa ujumla
naweza kusema kwamba maisha yangu si
mazuri sana.Si maisha yale ambayo
nilikuwa ninaota kuyaishi.Naweza kusema
kwamba ndoto zangu sijaweza
kuzitimiza.” Akasema Jane.Ernest
akamtazama halafu akanywa kinywaji
kidogo akapokea simu iliyokuwa ikiita
kisha akamgeukia Jane
 
SEHEMU YA 79

“ Jane kwa nini lakini uliyaharibu maisha
yako namna hii? Haukupaswa kuishi
maisha ya namna hii.Baba yako ni mtu
tajiri alikusomesha katika shule nzuri
sana ambayo wanasoma watoto wa watu
wazito lakini sijui nini kikatokea ukaingia
katika mapenzi na Yule kijana ambaye
hakuwa wa kiwango chako ukapata
mimba na kuacha shule.Kwa nini ulifanya
hivyo Jane?
“ Ernest naweza kukubali kwamba
nilifanya makosa sana kupata mimba ile
wakati nikiwa shule lakini siwezi
kumlaumu mtu yeyote kwani nilifanya
maamuzi mimi mwenyewe.”
“ Unadhani ulifanya maamuzi ya
busara? Akauliza Ernest
“ Kwa macho ya wengi hapana lakini
kwangu mimi ndiyo.Nilifanya maamuzi
sahihi.” Akasema Janet na ukimya
ukatanda.Janet hakuonyesha kupendezwa
na swali lile la Ernest
“ Baada ya kupata mimba ile baba
alinitaka nikaitoe ili niendelee na masomo
lakini sikuwa tayari ,akaniambia nichague
mawili kati ya mapenzi na shule
nikachagua mapenzi.Nlifanya hivyo kwa
kuwa ninampenda sana Ben na ndiyo
maana nikawa tayari kuacha kila kitu kwa
ajili yake kwa hiyo maisha haya ninayoishi
sasa niliyachagua mwenyewe.This is
love,true love.” akasema Janet.Ernest
akanywa kinywaji na kusema
“ I see.Lakini nimekuwa najiuliza
swali hili kila siku bila kupata jibu”
“ Swali gani Ernest? Akauliza jane
“ Jane ulikuwa ni msichana mzuri
kuliko wote shuleni na kila mwanaume
alikuwa anataka kukupata .Shule yetu
ilijaa vijana watoto wa mabilionea lakini
katika hao wote hukumuona hata mmoja
hadi ukaenda kuzama mapenzini na Yule
kijana asiye na mbele wala nyuma
.Alikupa nini Yule kijana? Ana kitu gani
ambacho wengine hawana?
Janet akatabsamu na kusema

Alichonacho
Ben
hakuna
mwanaume mwingine chini ya jua ambaye
anaweza kuwa nacho that’s why I gave up
everythuig for him” akasema Jane.Ernest
akainua glasi akanywa funda lingine na
kusema
“ Anyway tuachane na hayo Jane
nafahamu msimamo wako kwani
nimekuhangaikia kwa miaka mingi lakini
sikufanikiwa kupata hata busu” akasema
Ernest na wote wakacheka
“ Niambie hivi sasa unaishi wapi?
Unafanya kazi gani? Maisha yako yakoje?
“ Ernest kama nilivyokueleza ni
kwamba maisha yangu ninayajua
mwenyewe.Si mazuri sana kama yale
niliyokuwa natazamia kuishi.Mimi na
mume wangu tunaishi maisha ya kawaida
sana kama watu wengine.Sina kazi yoyote
mpaka sasa ila Ben ydeye amekuwa
anajishughulisha na biashara ya boda
boda.”
“ Boda boda?!! Akauliza Ernest kwa
mshangao
“ Ndiyo mbona umeshangaa?
Akauliza Jane
“ Lazimka nishangae Jane.Baba yako
analalia fedha lakini wewe unaishi kwa
kutegemea kipato cha boda boda?
“Ndiyo Ernest.Fedha alizonazo baba
ni
zake
na
wala
hazinihusu
mimi.Nimejifunza kuishi kutokana na
kipato chetu kidogo and we’re happy with
our life.Kuna nyakati mama amekuwa
ananisaidia hapa na pale namshukuru
sana kwa kuendelea kunilea” akasema
Jane
“ Jane utanisamehe kwa hili lakini si
kwamba ninadharau kipato hicho cha
mumeo lakini kwa mwanamke kama
wewe unapaswa uwe na maisha mazuri
sana katika jumba kubwa la kifahari uwe
na magari yako ya kifahari kwa ufupi
 
SEHEMU YA 80

unatakiwa uishi kama malkia.” Akasema
Ernest na ukimya ukapita
“ Jane tuachane na hayo mambo
yamekwisha pita tuangalie ya sasa na
mbele.Baada ya kupotezana kwa miaka
mingi tumekutana tena na japokuwa kila
mmoja kwa sasa tayari ana maisha yake
lakini hii haituzuii kuendeleza urafiki
wetu.Kwa ufupi ni kwamba mimi kwa sasa
nina mchumba anaitwa Miriam na kama
ikimpendeza Mungu ndiye ambaye
nitafunga naye ndoa kwa hiyo sote tuko
katika mahusiano.” Akasema Ernest na
kunywa funda la mvinyo akaendelea
“ Jane nimeguswa sana na maisha
yako japokuwa hujanieleza kwa undani ila
nafahamu kuwa hukupaswa kuishi katika
aina hii ya maisha kwa hiyo mimi kama
rafiki yako ambaye kwa sasa nina uwezo
mkubwa nataka nikusaidie nikutoe katika
maisha haya na ufikie yale maisha
uliyokuwa unayahitaji and please don’t
say no.This is just a help for a friend and
nothing else.” Akasema Ernest na Janet
akatabasamu
“ You know how to tie my hands
Ernest lakini hata hivyo umekuja kwa
wakati muafaka kabisa.I real need your
help right now” akasema Janet
“ Thank you Jane for accepting my
help.Tell me what do you want me to help?
Janet akavuta pumzi ndefu na
kusema
“ Ben alikuwa anaendesha gari
ambalo aliazima kwa mmoja wa rafiki
zake akiwa barabarani alipata ajali na
katika ajali hiyo mtu mmoja alifariki
dunia.Inasemekana mtu huyo aliyefariki
dunia ni mjukuu wa mmoja wapo wa
wanasiasa wakubwa hapa nchini kwa hiyo
kuna shinikizo kubwa la kutaka Ben
afungwe ingawa hakuwa na hatia kwani
yeye ndiye aliyegongwa lakini kibao
kimegeuka na anatajwa kuwa ndiye
aliyegonga.Nimejitahidi sana kutafuta
msaada wa kisheria sehemu mbali mbali
lakini wengi wa mawakili wanaigopa kesi
hii
kwani
wanafahamu
kuwa
hawatashinda na kuharibu sifa yao.Ernest
nahitaji wakili wa kuweza kumsimamia
Ben katika kesi hii kwani bila kumpata
wakili mzuri atafungwa.Sitaki Ben
afungwe kwani yeye ndiye kila kitu
kwangu.Tafadhali Ernest kama una uwezo
wa kunisaidia katika hilo naomba
unisaidie ” akasema janet machozi
yakamtoka.Ernest akainuka akamsogelea
akamfuta machozi na kusema
“ Usilie Janet.Niachie mimi suala hilo
na ninakuhakikishia litakwisha na
hutaamini macho yako.”
“ Real ??!
“ Niamini Jane.Kwanza hesabu kama
suala hilo tayari limekwisha kwani liko
ndani ya uwezo wangu.”
“ Ahsante sana Ernest” akasema
Janet kwa furaha na kumkumbatia Ernest
kwa nguvu
“ Hilo ni moja,lakini baada ya kesi
kumalizika nataka nimfundishe Ben
kazi.Nataka aanze kufanya biashara
kubwa kubwa na kupata fedha nyingi
kuliko biashara hiyo anayoifanya ya boda
boda.Nakuhakikishia Jane nitafanya kila
lililo ndani ya uwezo wangu hadi mtakuwa
watu matajiri.”
“ Ahsante sana Ernest .Naamini ni
mpango wa Mungu kutukutanisha kwani
nilikwisha kata tamaa na sikujua
ningefanya nini” akasema Janet.
 
SEHEMU YA 81

Kumbu kumbu hii ikamtoa machozi
Janet.
“ Ernest alifanikiwa kumtoa Ben
gerezani na kesi ikamalizika.Mpaka leo
sifahamu alifanya nini kulimaliza suala lile
lakini nilichokuwa nakitaka mimi ni
Benedict atoke gerezani. Baada ya Ben
kutoka gerezani ndipo maisha yetu
yalipobadilika.Ernest
changed
our
life.Sidhani kama ninapaswa kumshukuru
au kumlaani kwa hapa alipotufikisha
lakini moyoni ninajuta kumfahamu ”
akawaza Janet.
Mzee Benedict bado alikuwa amekaa
sofani
akiwa
na
mawazo
mengi.Alikumbuka
mambo
mengi
kuhusiana na safari ya maisha yake toka
alipokutana na Janet lakini kubwa ni siku
aliyokutana na Ernest kwa mara ya
kwanza na maisha yake yakabadilika
DAR ES SALAAM - LA 403 CASINO
Kiza tayari kimetanda angani gari la
kifahari lilipofunga breki katika maegesho
maalum kwa ajili ya watu muhimu tu
wanaokuja katika kasino hili.Mlinzi
mwenye sare maalum za ulinzi aliyekuwa
akilinda eneo lile la maegesho akasogea
na kuufungua mlango na toka ndani ya
gari lile akashuka Benedict Mwamsole na
mke wake Janet.
“ Wow ! Sijawahi kufika hapa katika
kipindi chote cha maisha yangu.” Akasema
Benedict kwa mshangao mkubwa
kutokana na uzuri wa mahali pale.Dereva
akashuka garini na kuwataka wamfuate.
Hii ilikuwa ni jioni ya siku ambayo
mahakama ilimuachia huru Ben kwa
kutokuwa na ushahidi wa kutosha
kuhusiana
na
shitaka
lililokuwa
linamkabili.Ilikuwa ni siku ya furaha
kubwa kwa Ben na kipenzi chake
Janet.Usiku huu walifika hapa La 403
Casino
kuja
kuonana
na
mtu
aliyefanikisha kuachiwa huru kwa Ben
ambaye ni Ernest Mkasa aliyewataka
wafike hapa kuonana naye na
kuzungumza mambo ya muhimu sana kwa
ajili yao
Dereva aliwaongoza hadi katika
ghorofa ya juu kabisa ya kasino hili kubwa
ambako
walimkuta
Ernest
akiwasubiri.Aliwakaribisha kwa furaha
kubwa.Kuliandaliwa chakula kizuri na
vinywaji na bila kupoteza muda wakala
kwanza chakula halafu maongezi
yakaanza
“ Sasa tunaweza kuanza maongezi
yetu” akasema Ernest
“ Ernest awali ya yote mimi na mume
wangu tunapenda sana kutoa shukrani
zetu za dhati kwako kwa kuweza
kulianikisha suala hili la kuimaliza kesi ile
iliyokuwa inamkabili.Sitaki kufahamu
umefanyaje lakini shida yetu sisi ni kesi ile
imalizike.Ahsante sana Ernest.Tuna deni
kubwa kwako” akasema Janet na kwa
mbali machozi yakamlenga
“ Janet ninyi ni marafiki zangu na
niko tayari kufanya jambo lolote lile kwa
ajili ya kuwasaidia marafiki zangu kwa
hiyo nilifanya nililoweza kufanya ili
kuimaliza ile kesi.Kwangu mimi haya ni
mambo madogo sana” akasema Ernest na
kutabasamu akaelekeza macho kwa Ben
“ Benedict pole sana kwa matatizo
lakini kwa mwanaume matatizo ni sehemu
ya maisha yetu .Kukaa jela si dhambi
kwani tukiwa kule tunaamini kuwa
tunaimarika zaidi na kuitazama dunia kwa
 
SEHEMU YA 82

jicho la tatu.Ninaamini kwa muda uliokaa
uko tayari umekwisha imarika vya
kutosha.You are now a man” akasema
Ernest
“ Usemayo ni ya kweli Ernest.Nikiwa
kule nimekutana na mambo mengi
ambayo sikuwa nimeyafahamu hapo
kabla,japokuwa sikuwa nimefungwa bado
lakini nikiwa mahabusu nimekutana na
watu wengi wenye makosa na tabia mbali
mbali.Kama
unavyosema
nimeimarika.Nimejifunza
mengi.Nashukuru sana kwa jitihada zako
za kunitoa gerezani” akasema Ben
“ Usijali Ben.Nilikutana na Jane siku
moja akiwa anakwenda supermarket na
akanieleza tatizo lako.Mimi na Monica ni
marafiki wa muda mrefu,tumesoma wote
sule moja hadi alipopata yale matatizo na
kuacha shule tukapotezana mimi
nikaendelea na masomo na harakati
nyingine za maisha .Tulipokutana tena
amekutana na mtu mwingne tofauti na
Yule aliyemfahamu tukiwa shule.Now I’m
a man. “ akasema na kuwasha sigara
akavuta halafu akaendelea
“ Sijifu lakini ninaweza kusema kwa
sasa niko katika orodha ya watu matajiri
hapa nchini.Ninamiliki biashara kadhaa
kubwa kubwa na hata hili kasino ni la
kwangu pia ninalimiliki kwa asilimia mia
moja.Watu
wengi
wanashangaa
nimewezaje kuwa na utajiri huu mkubwa
ndani ya kipindi hiki kifupi na katika mri
huu
mdogo.Wengine
wanasema
yawezekana mali hizi nilizonazo ni mali za
baba kwani wanamfahamu baba yangu ni
mtu tajiri lakini baba ana mchango mdogo
sana sehemu kubwa ya mali nimeitafuta
mwenyewe mwenyewe kwa jasho
langu.Kila kitu kinawezekana .Ukiwa na
nia na kuweka bidii utafanikiwa katika
kila jambo unalolifanya.Kwa hiyo hata
ninyi pia mnaweza mkayabadili maisha
yenu na mkafika hapa nilipo mimi na
kuishangaza dunia.” Akanyamaza akainua
glasi yake yenye pombe kali akanywa na
kuvuta mikupuko kadhaa ya sigara kisha
akasema
“ Usiku wa leo nimewaiteni hapa ili
kuongea mambo ya msingi sana kuhusiana
na mustakabali mzima wa maisha yenu.”
Akanyamaza tena akavuta sigara
akapuliza moshi mwingi na kuendelea
“ Janet alinieleza japosi kwa undani
sana kuhusiana na maisha yenu kwamba
hayakuwa mazuri na mimi kama rafiki
nimejitolea kwa hali na mali kuwasaidia
na kuwaondoa katika hali mliyonayo
sasa.Nitawaelekeza njia lakini mnatakiwa
mfanye kazi kwa bidii sana na kwa
kujituma ili kujikwamua kwa hiyo kabla
sijasema lolote nataka nipate uhakika
toka kwenu kama kweli mnaumizwa na
aina ya maisha mnayoishi na mnataka
kuachana nayo na kuwa matajiri kama
mimi” akasema Ernest na kuvuta tena
sigara
yake.Benedict
na
Janet
wakatazamana na kisha Jane akasema
`
“ Ernest hakuna mtu anayeufurahia
umasikini kwa hiyo kama kuna njia
ambayo una jua inaweza kutusaidia
kutukwamua kutoka katika hali hii ngumu
tafadhali tuonyeshe njia hiyo na sisi tupite
tuweze kujikwamua” akasema Jane

Nafurahi
kusikia
hivyo.Nitawasaidia” akasema na kuinua
tena glasi yenye pombe akanywa na
kuwatazama akina Jane kwa makini usoni
 
SEHEMU YA 83

“ Kwa kuwa mmekiri kuwa mko
tayari kufanya kazi ili kuachana na
umasikini mlionao basi nitawaonyesha
njia lakini nataka niwahakikishie kwamba
si kazi rahisi na inahitaji moyo mgumu na
kikubwa
ni
kwamba
pindi
nitakapowaeleza nini mnatakiwa mfanye
there is no turning back.Tunaelewana
ndugu zangu? Akauliza
“Tunakuelewa Ernest.” Wakajibu
Janet na Ben
“ Vizuri.Usiku huu nitawatambulisha
kwa washirika wangu ambao ninafanya
nao kazi .Tuna biashara mbali mbali
tunazifanya gizani.Ninaposema gizani sina
maana ya usiku bali ni biashara zile
ambazo serikali imekuwa inazipiga
vita.Siwafichi ndugu zangu ni vigumu sana
kuendelea na kuwa tajiri kwa biashara za
kufanya mchana.Utaendelea na kuwa tajiri
kama mimi kutokana na biashara za
gizani.Kuna biashara mbali mbali ambazo
tunazifanya mimi na washirika wangu
lakini kubwa ambayo kwa sasa ina pesa
nyingi mno ni biashara ya pembe za ndovu
.” akanyamaza na kuvuta sigara yake.Janet
na Ben wakatazamana.Ernest akaendelea
“ Biashara ya pembe za ndovu ni
biashara ambayo inaweza ikawatoa katika
umaskini kwa haraka sana kwani soko
lake ni kubwa mno duniani kwa sasa.
Kutokana na kupanuka kwa soko hilo la
pembe za ndovu duniani na kasi ya
kutoweka kwa tembo katika hifadhi zetu
serikali imeongeza ulinzi katika hifadhi na
hivyo kufanya upatikanaji wa meno ya
tembo uwe mgumu .Kwa sasa ni kama vita
kati ya wawindaji na askari wa
wanyamapori.Lakini naomba nisiwatishe
kwa sababu katika mtandao wetu kuna
watu wazito wakiwemo pia watu wakubwa
serikalini kwa hiyo kwetu sisi ni kazi
rahisi tu na hakuna ugumu mkubwa
tunaokutana nao.” Akanyamaza akanywa
pombe yake kali na kusema
“ Mimi sikuwa na ufahamu wowote
kuhusu mambo haya ni baba yangu ndiye
aliyeniingiza katika mtandao huu na mimi
nitawaingiza ninyi kwa kuwa kwa sasa
mimi ndiye kiongozi wao.I swear to you
endapo mtazingatia masharti na kujituma
umasikini utabaki historia kwenu”
akasema Ernest.
Mzee Benard akajifuta jasho
lililokuwa linamtiririka kwa wingi baada
ya kumbu kumbu ile kumjia.
 
SEHEMU YA 84

Usiku ule ndipo maisha yetu
yalibadilika.Ernest alitokea kuwa mtu
wetu wa karibu na alitusaidia sana
japokuwa haikuwa kazi rahisi lakini mimi
na Janet tulishirikiana bega kwa bega na
kama alivyosema Ernest maisha yetu
yalibadilika.Ilikuwa ni biashara ya hatari
kubwa na mara kadhaa tulinusurika kifo
lakini hatukukata tamaa na mwishowe
tukafanikisha malengo yetu tukawa
matajiri wakubwa.Mara kadhaa niliwahi
kukamatwa na kuweka gerezani lakini
kwa msaada wa Ernest na mtandao wetu
nilitoka gerezani.Ernest ni mmoja wa watu
ambao ninawaheshimu sana na kila leo
ninajiona kama nina deni kubwa kwake
kwani hata baada ya kuwa rais bado
ameendelea kutusaidia katika masuala
mbali mbali ya kibiashara lakini sikuwahi
kujua kama alikuwa na mahusiano na mke
wangu na hadi wakafikia hatua ya kuzaa
mtoto.Kwa hili alilolifanya la kukosa
uaminifu linanifanya niyafute yale yote
mazuri aliyoyafanya kwetu.I must destroy
Ernest.” Akawaza Ben.Akiwa bado
amesongwa na mawazo mengi mke wake
Bi Janet akatoka chumbani na kwenda
kuketi karibu na mumewe.
“ Ben..” akasema Bi janet kwa sauti
ya upole.Ben akainua kichwa akamtazama
“ Ben I’m real sorry for the awfull
things I said to you tonight.Sikupaswa
kutamka maneno kama yale kwa mtu
muhimu kama wewe.Ni hasira tu
zilizonifanya nikatamka maneno
yale.Nisamehe
sana
Ben.Nimetakafakarinimeliona
kosa
langu.Sikupaswa kabisa kukutamkia
maneno yale.” Akasema Bi Janet.Ben
akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Jane mimi na wewe tumetoka mbali
mno na tuna historia kubwa lakini kwa
mara ya kwanza katika maisha yangu
nathubutu kutamka kwamba umeniumiza
sana.Sijawahi kukutamkia neno hili hata
siku moja lakini leo nataka ufahamu hilo
kuwa umeniumiza sana si kwa maneno
uliyoyatamka bali kwa usaliti
ulionifanyia.Sikutegemea kabisa na wala
sikuwahi kuota kama siku moja ungeweza
kunisaliti hadi kufikia hatua ya kuzaa
mtoto halafu ukanificha jambo hili kwa
miaka hii yote hadi leo .I’m hurt ,deeply
hurt” akasema Ben.Mkewe bi Janet akafuta
machozi na kusema
“ Ben nadhani unafahamu namna
ninavyokupenda.Nilikupenda toka angali
ukiwa kijana usiye na kitu chochote usiye
na mbele wala nyuma.Niliwakataa vijana
wengi waliotoka katika familia tajiri kwa
ajili ya kuwa nawe.Hata nilipopata
ujauzito wa Nathan na ukanisistiza
kwamba nikatoe kwani hukuwa na uwezo
wa kunihudumia wakati huo ukiwa
mwanafunzi nilikataa na hata familia
yangu iliponitaka nikatoe ili niendelee na
masomo nikakataa pia na baba
akaniambia nichague kati ya wewe au
shule nikakuchagua wewe.I gave up
everything for you Ben.Baba alikwisha
niandalia maisha makubwa mazuri lakini
niliviacha hivyo vyote kwa sababu ya
upendo mkubwa nilio kuwa nao
kwako.Nimeishi nawe maisha ya
umasikini mkubwa na hata siku moja
sikuwahi kujilaumu wala kujutia maamuzi
yangu niliyoyafanya.Sikuwahi kumlaumu
mtu yeyote kwa maisha niliyokuwa naishi
kwani ni maisha niliyochagua kuishi na
nilikuwa na furaha sana.Kama kukusaliti
ningeweza kukusaliti wakati ule tukiwa
katika maisha ya dhiki kubwa laini
nilikuwa mvumilivu na sikuthubutu
kufanya hivyo” akasema Janet
 
SEHEMU YA 85

Yote uliyoyasema nakubaliana
nayo aslimia mia moja na ninamshukuru
sana Mungu kwa kumpata mwanamke
kama wewe ambae ni kwa jitihada zako
kubwa leo hii tuko hapa tulipo lakini hayo
yote uliyoyafanya pamoja na upendo
mkubwa ulio nao kwangu yanatiwa doa na
kitu kimoja tu kwamba umezaa nje ya
ndoa tena na mtu ambaye ni rafiki yetu
mkubwa.Nakubali hata mimi nimefanya
usaliti na nina watoto kadhaa nje ya ndoa
yetu na sikuwahi kukueleza na
utanisamehe kwa hilo lakini ni kwa watu
ambao si wa karibu yetu au
unaowafahamu.Wewe umetembea na
kuzaa na mtu wetu wa karibu sana.Ni aibu
kubwa hii.Tutaziweka wapi sura zetu Jane
jambo hili siku moja likivuja kwa watu?
Akauliza Ben.Janet ambaye machozi
hayakukauka machoni pake akasema
“ Ernest ni mtu ambaye alikuwa
ananitaka sana kimapenzi toka tukiwa
shule lakini hakufanikiwa.Na hata
tulipokutana tena baada ya miaka mingi
na akajitolea kutusaidia bado alikuwa
anaendelea na zile jitihada zake za
kunitaka kimapenzi lakini nilijitahidi sana
kumkwepa na kumueleza ukweli kwamba
jambo hilo haliwezekani kwani penzi
langu mimi nimelitoa kwa mtu mmoja tu
ambaye ni wewe.” Akanyamaza akafuta
machozi na kusema
“ Kuna ule wakati ulikamatwa nchini
China nikamfuata kwa ajili ya
msaada.Akaahidi kukusaidia lakini kwa
sharti moja tu kwamba lazima nifanye
naye mapenzi.Kwa wakati ule sikuwa na
mtu mwingine ambaye ningeweza
kumkimbilia na kumuomba msaada zaidi
ya Ernest hivyo nikalazimika kufanya naye
mapenzi lakini kwa lengo la kutaka
msaada wake.Baada ya kufanya naye
mapenzi akakusaidia ukaachiwa na
baadae ndipo nilipogundua kwamba nina
ujauzito wa Ernest.Niliogopa sana
kukueleza jambo kama lile la aibu na wala
sikumueleza Ernest na mpaka leo hii hajui
kama Monica ni mtoto wake.Hii ilikuwa ni
siri yangu ambayo nilipanga kwenda nayo
kaburini lakini ni jambo lililokuwa
linaniumiza sana .” akasema Janet.Ben
akawaza na kuuliza
“ Ilitokea mara moja tu au bado
mnaendelea na mahusiano kwa siri?
“ It happened just once..” Akasema
Janet
“ Nitafanya uchunguzi wangu na
endapo nitagundua kwamba wewe na
Ernest bado mna mahusiano na kwamba
mnakutana kwa siri I swear I will destroy
you both.God will forgive me for that but I
swear I will destroy you.Uwezo wa
kufanya hivyo ninao!!! Akasema Benedict
na kuinuka akaelekea chumbani na
kumuacha mke wake pale sebuleni
*****************
Sauti ya mlango kugongwa ilimstua mzee
Ben toka usingizini,akamtazama mkewe
aliyekuwa pembeni yake ambaye bado
alikuwa katika usingizi ,taratibu mzee Ben
akainuka na kwenda kuufungua mlango
akakutana na Monica
“ Monica “ akasema Mzee Ben
“ Shikamoo baba”
“Marahaba you are so early today”
“ Ndiyo baba nimeamka mapema
nataka nikamtazame rafiki yangu Dr
Marcelo aliyepigwa risasi jana lakini kabla
sijaelekea hospitali nimeona nije nikuone
 
SEHEMU YA 86

kama ulivyokuwa umeniagiza jana
kwamba nisiondoke bila kuja kukuona”
akasema Monica
“ Sawa Monica.Nisubiri ninawe uso
nikupeleke hospitali” akasema mzee Ben
na kuingia bafuni akajimwagia maji
haraka haraka .Wakati anatoka bafuni
akamkuta mke wake tayari ameamka.
Hawakusalimiana akavaa haraka haraka.
“Unaenda wapi Ben? Akauliza Jane
“ Nakwenda hospitali na Monica”
akajibu Ben na kutoka akaongoza na
Monica hadi katika gari wakaondoka
kuelekea hospitali.Mara tu Benedict na
Monica walipoondoka Janet akachukua
simu na kuzitafuta namba Fulani akapiga
baada ya muda ikapokelewa
“ Hallow Madam Jane” ikasema sauti
ya upande wa pili ya mtu aliyepokea simu
“ Mukasha samahani kwa
kukusumbua asubuhi hii lakini nina jambo
la muhimu nataka unisaidie”
“ Bila samahani Madam
Jane.Nikusaidie nini?
“ Nataka kuonana na Ernest leo”
“ Leo ??
“ Ndiyo Mukasha.Nataka kuonana
naye leo.Tafadhali fanya kila
linalowezekana hadi nionane na Ernest
leo” akasema Janet
“ Sawa madam Jane ngoja nijitahidi
nione nitakavyofanya ,nitakujulisha
baadae”

Ahsante
sana
Mukasha.Nakutegemea sana tafadhali
usiniangushe” akasema Jane na kukata
simu
“ Lazima nionane na Ernest leo
nimueleze kwamba tunatakiwa tuwe
makini sana kwa sasa kwani Ben
anatuchunguza.Ninamfahamu Ben huwa
anamaanisha
anachokisema
na
amedhamiria kweli kufanya uchunguzi
kuhusu mimi na Ernest.Kwa miaka mingi
nimekuwa katika mahusiano ya siri na
Ernest bila ya Ben kujua.Najuta kwa nini
niliamua kumueleza ukweli Ben kwani
nimetibua na mambo mengine ambayo
sikutaka yajulikane.Nina mambo mengi
ambayo Ben hayajui kuhusu mimi na
akifanya
uchunguzi
anaweza
akayagundua.Natakiwa kuwa makini sana
kuanzia sasa.Kosa dogo tu linaweza
kusababisha
matatizo
makubwa.Ninampenda sana Ben lakini
hata Ernest ninampenda pia ni mtu
ambaye nimuhimu pia kwangu,sitaki
litokee jambo ambalo litanifanya nimkose
mmoja wapo wa watu hawa ” Akawaza
Jane
 
Nina hisia na watu wawili kupanga shambulizi hili namba moja mama Monika baada ya kutuma fail ameona hakuna dalili ya kuachana sasa bora aue kabisa, wa pili Rais David wa Congo huenda kaweka wachunguzi ili kumfuatilia Monica sasa wamebaini Dr Marcelo ni mmoja kati ya watu watamfanya Monica kuwa mgumu kumkubali kimapenz Rais David sasa dawa ni kuua tu! Huo ni mtazamo Wangu wa huko tuendapo kumtambua mtu alofanya shambulizi kwa Dr Marcelo
ulichoongea n kweli
 
Aliyechukua kitabu ndio aliyempiga risasi Dr. Marcelo, nina wasiwasi na yule aliyepigiwa simu na Dr. kwa zile namba alizopewaga na baba yake. Ni kama ameamua kumgeuka kwa kujua umuhimu wa kile kitabu.

Ni mawazo yangu tu jamani.
 
Asante sana LEGE, asubuhi imekuwa njema, nimeianza weekend vizuri, naamini nitaimaliza vizuri pia.

Keep it up bro!!
 
Ubarikiwe mtunzi ni kwamara ya kwanza nimeacha kwenda kazini kwa kusoma Uzi jamii forum najuta kwanini niliingia humu asubuhi! Maana nimeingia nikakutana na huu Uzi kila nikitaka kuacha utamu kolea aise kunawatu mmebarikiwa kwa kipaji hongera zako nafikiri sasa ninawatu wawili sasa MUHIMU the Bold na mwingine ni we we, Thank you much.
 
Back
Top Bottom