SEHEMU YA 92
uchunguzi wake na endapo atagundua
kwamba ni kweli sisi tuna mahusiano basi
ama zetu ama zake.Kwa hiyo Ernest we
have to put an end to what we’re doing”
akasema Janet .Ernest akamtazama kwa
macho ya uoga na kusema
“ Jambo hili limenishangaza
sana.Tumekuwa tunakutana kwa siri kwa
zaidi ya miaka ishirini sasa lakini
ninachojiuliza why now? Kwa nini ahisi
sasa? Akauliza Ernest ,Janet hakujibu kitu
akabaki kimya
“ Jane tafadhali naomba unieleze nini
kimetokea hadi Ben akahisi mimi na wewe
tuna mahusiano kwa sababu hainiingii
akilini kabisa kwa miaka hii yote Ben aje
ahisi leo mimi na wewe tuna mahusiano.”
“
Hakuna
tatizo
lolote
Ernest,nadhani kuna tetesi atakuwa
amepewa” akajibu Jane
“ Kapewa na nani? Jane naomba
tafadhali unieleze ukweli.Ninakufaamu
vizuri kuliko mtu mwingine yeyote kuliko
hata mumeo.I know that you are hiding
something from me.Tafadhali Jane mmi na
wewe tumekuwa tunaelezana siri zetu
hata zile kubwa.Nieleze kuna tatizo gani ?
Ben amehisi vipi kuwa mimi na wewe tuna
mahusiano?
Ninakusisitiza
unieleze
ukweli kwa sababu ninamfahamu vizuri
Ben .Kama amesema atafanya uchunguzi
basi lazima atafanya na endapo atagundua
kwamba mimi na wewe ni kweli tuna
mahusiano basi suala hilo litachukua sura
mpya.Ben anakupenda sana na kwa ajili
yako anaweza akafanya jambo lolote baya
kwetu na hasa hasa kwangu.Najua hawezi
kuniua kwa silaha lakini kama unavyojua
Ben ananifahamu kiundani,anaifahamu
historia yangu chafu ya nyuma kwa hiyo ni
rahisi sana kwa mtu kama huyu
kuniharibia taswira yangu kwa jamii.Ni
kweli nimepitia mambo mengi machafu
katika kutafuta utajiri na hadi nimefika
hapa katika nafasi hii kubwa ya uongozi
wa nchi.Endapo wananchi watafahamu
historia ya rais wao wanayempenda nina
hakika nitakuwa rais wa kwanza duniani
kupigwa
mawe
na
wananchi
hadharani.Kabla hatujafika huko natakiwa
kujua nini kimetokea ,nini kinaendelea ili
niweze kuchukua hatua za haraka kama
zitahitajika
ili
kuzuia
madhara
yanayoweza kutokea endapo jambo hili
litagundulika,lakini endapo utaendelea
kunificha na mambo yakaharibika basi
nitakua na kitu kimoja tu cha kufanya “
akasema
Ernest
na
kunyamaza
akamtazama Janet
“ Whats that Ernest? Akauliza jane
“ To kill Ben” akasema Ernest kwa
sauti ndogo.Jane akastuka akamtazama
Ernest kwa macho makali
“ Mbona umestuka Jane? Akauliza
Ernest
“
Ernest
tafadhali
naomba
usithubutu
kuwaza
kitu
kama
hicho.Ukimuua Ben it’ll be the end of us
all.Ben is all I have na kwa ajili yake niko
tayari kufanya lolote hata kama ni baya
kwa hiyo nakuomba mawazo machafu
kama hayo uyaweke pembeni kwani
endapo utafanya kitu kama hicho utaingia
katika vita na mimi na unajua mimi ni
mbaya kuliko hata Ben.” Akasema Janet
“ Janet najua unampenda sana Ben
na uko tayari kwa lolote kwa ajili yake na
ninafahamu pia kwamba wewe ni mbaya
zaidi lakini usisahau kuwa mimi ndiye
niliyewabadili mkawa hivi mlivyo
leo,mambo yote niliwafundisha mimi kwa