QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

SEHEMU YA 33


Mr President lets go straight to the
point.Why you are here? Umefanikiwa
nilichokuomba?
Ernest hakujibu kitu akachukua
simu yake akazitafuta namba za balozi wa
Tanzania nchini China akapiga na simu
ikapokelewa
“ Habari za usiku huu mheshimiwa
balozi.Samahani sana kwa kukuamsha
mida hii ambayo huko kwenu ni usiku
mwingi” akasema Ernest
“ Bado sijalala mheshimiwa rais
kwani uliniahidi kunipigia usiku hivyo
niko macho nikisubiri simu yako.”
Akasema balozi
“ Nashukuru sana balozi.Sitaki
nichukue muda wako mwingi.Naomba
nizungumze na Linda kama yuko hapo
karibu” akasema rais
“ Ninaye hapa mheshmiwa rais”
akasema balozi na kumpa Linda simu ili
azungumze na rais.Ernest akaweka sauti
kubwa ili Austin aweze kusikia kila kitu
“ Mheshimiwa rais shikamoo baba”
akasema Linda.Mara moja Austin
akaitambua sauti ile na kutabsamu huku
machozi yakimlenga.
“ Marahaba hujambo Linda?
“ Sijambo “ akajibu Linda
“ Samahani Linda hebu nieleze
historia yako kwa ufupi” akasema rais
“ Naitwa Linda January,ninatokea
Tanzania.Nilikamatwa hapa China na
kufungwa miaka kumi na tano kwa kosa la
kujaribu kuingiza madawa ya
kulevya.Ninashukuru mheshimiwa rais
umenisaidia
nimeweza
kutoka
gerezani.Ninaomba mheshimiwa rais
nitakaporejea nyumbani nisiendelee na
kifungo.Nakuahidi sintajihusisha tena na
biashara hii ya dawa za kulevya,nakuomba
sana baba” akasema Linda na kwa mbali
akasikika akilia kwa kwikwi.Austin naye
akashindwa kuyazuia machozi kumtoka.
“ Linda nimekusikia na
ninakuhakikishia kwamba hautakwenda
gerezani tena.Nitakuandalia mpango
mzuri sana wa maisha yako mapya na kwa
sasa utaendelea kukaa hapo hapo kwa
balozi wetu China.Utapata kila
unachokihitaji.Naomba umpe simu balozi
tafadhali” akasema Ernest na kuagana na
balozi akamgeukia Austin
“ Ahsante sana mheshimiwa rais.Sina
neno zuri la kukushukuru kwa hili
ulilonifanyia ila nakuahidi kukufanyia
kazi yako kwa ufanisi mkubwa.Now we
can talk” akasema Austin
“ Nilikwambia Austin kwamba nina
nguvu ya kuweza kumtoa dada yako
gerezani.Baada ya kulitimiza ombi lako ni
nafasi yako sasa kunisikiliza nikueleze
kile ambacho nimekuitia hapa Tanzania”
akasema Ernest
“ Mheshimiwa rais kabla
hujaendelea naomba nikuulize swali moja
tu na ninaomba unipe jibula kweli”
“ Uliza Austin nitakujibu bila wasi
wasi”
Austin akamtazama Rais kisha kwa
sauti ya taratibu akauliza
“ Mr president are you one of them?
“ One of them? Unazungumzia akina
nani? Rais naye akauliza
“ The Alberto’s ́” akajbu Austin.
Mstuko aliuopata Ernest Mkasa rais
wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
ulikuwa mkubwa na wa wazi.Haraka
haraka akajifanya kama vile hajastuka na
kuuliza
 
SEHEMU YA 34


lberto’s ? Who are they? Akauliza
rais huku sauti yake ikionyesha
kitetemeshi kwa mbali
“ Nijibu kama nawe ni mmoja wao au
vipi? Akauliza Austin
“ Sifahamu unazungumzia watu gani
Austin .I don’t know those people and I’m
not one of them” akasema Ernest
“ Show me your hands” akasema
Austin na kumfanya rais ahamaki
“ What are you trying to do Austin?
Mimi ndiye niliyekuita hapa na unapaswa
kunisikiliza na si kuanza kuniuliza
maswali hayo ya hovyo!!
“ Mheshimiwa rais nimekuuliza swali
rahisi sana na ninataka unijibu ndiyo au
hapana.Nina sababu zangu kukuuliza
hivyo.Ukamilifu wa kazi yako unayotaka
kunipa utategemea sana jibu la swali
nililokuuliza” akasema Austin .Ernest
akamtazama Austin kwa makini
“ Austin unanishangaza sana.I real
don’t know what you are talking
about.Naomba tusipoteze muda Austin
kujadili mambo yasiyokuwa na msingi
wowote.Tayari nimekwisha fanya
ulichotaka nikufanyie kwa hiyo ni zamu
yangu kufanya kile ninachotaka uifanye !!
“ Mheshimiwa rais sijakataa
kuifanya kazi yako .Nitaifanya tena kwa
ufanisi mkubwa lakini ufanisi wake
utategemea jibu la swali nililokuliza.Kama
unakiri kuwa wewe si mmoja wao basi
nionyeshe mkono wako wa kulia”
akasema Austin
“ Austin kwani hao Alberto’s ni akina
nani? Umewafahamu vipi? Wanahusiana
nini na wewe? Akauliza Ernest
“ Tuokoe muda mheshimiwa rais
.Nonyeshe kiganja cha mkono wako wa
kulia” akasema Austin.Ernest akamtazama
kwa makini akagundua kuwa Austin
hakuwa akiongea kwa masihara hata
kidogo bali alimaanisha alichokiongea.
“ Mr President..” akasema Austin
“ Kama hutaki kunionyesha kiganja
chako cha mkono wa kulia utanifanya
niamini kuwa nawe pia ni mmoja wao na
kama ni kweli basi kutakuwa na ugumu
wa mimi kufanya kazi yako” akasema
Austin
“ Austin what do you real want?
Akauliza Ernest .
“ Mheshimiwa rais nipe jibu moja ili
twende sawa.Are you one of them? Austin
akauliza tena.Taratibu Ernest Mkasa
akainua mkono wake wa kulia na
kumuonyesha Austin kiganja chake.Austin
akamsogelea na kukikagua kiganja kile
kwa umakini mkubwa kisha akasema
“ Ok good.You are not one of them,
but you know them right? Akauliza na rais
akabaki kimya
“ Mr President do you know them?
“ Austin let’s not talk about this.Hili
si suala dogo kama unavyofikiria”
akasema rais.
“Sentensi hiyo mheshimiwa rais
inanipa uhakika kuwa unawafahamu watu
hao ni akina nani.Naomba sasa unieleze
kazi unayotaka nikufanyie” akasema
Austin .kabla Ernest hajasema chochote
simu yake ikaita.Akatazama mpigaji
alikuwa David Zumo rais wa jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo.
 
SEHEMU YA 35


KINSHASA – JAMHURI YA KIDEMOKRASIA
YA CONGO
Msafara uliombeba Monica uliwasili
katika jumba la mapumziko la rais David
Zumo lililokuwa nje kidogo ya jiji la
Kinshasa.Lilikuwa ni jumba kubwa la
kupendeza na ulinzi ulikuwa mkali
.Mlango wa gari alilopanda ukafunguliwa
Monica akashuka
“ Monica karibu sana katika kasri la
mapumziko la mtukufu rais David Zumo”
akasema Jean Piere Muyeye kisha
akamuongoza Monica kupita katika zuria
jekundu kuelekea ndani.Walipanda hadi
ghorofa ya nne ambako kulikuwa na
utulivu wa aina yake.Pierre Muyeye
akamuongoza hadi katika mlango wenye
nakshi za dhahabu akabonyeza kengele na
mlango ukafunguka.
“ Kutokea hapa ni watu wachache tu
wanaoruhusiwa kufika.Mimi nitabaki
hapa na wewe utaelekea ndani kuonana
na rais.Tafadhali usiogope Monica”
akasema Muyeye.
“ Ninaogopa Muyeye” akasema
Monica
“ Usiogope Monica.Hakuna tatizo
lolote sehemu hii ni salama mno.Nenda
tafadhali rais anakusubiri” akasema
Muyeye. Monica akalivuka lango lile zuri
ambalo lilijifunga mara tu alipopita
.Alipita katika milango kadhaa na kila
alipokaribia mlango ulijifungua na
kujifunga alipopita .Mlango wa mwisho
ulipofunguka alijikuta akiingia katika
sebule kubwa na nzuri.
“ Usiogope Monica niko hapa”
Ikasikika sauti ya David Zumo
“ David !! akasema Monica kwa
mstuko kidogo baada ya kumuona David
Zumo akiwa amesimama katikati ya
sebule ile akitabasamu.Usiku huu hakuwa
amevaa mavazi ya kawaida ambayo
amezoeleka kuonekana nayo alivaa ngozi
ya chui na kichwani alivaa kofia yenye
manyoya ya Simba
“ Karibu sana Monica.Karibu katika
kasri la kifalme la David Zumo.Hapa ndipo
ninapokuja kupumzika kila ninapohitajika
kupumzisha kichwa changu.Najua
umestuka kidogo kwa mavazi haya
niliyovaa.Haya
ndiyo
mavazi
nitakayokuwa nikivaa kama mfalme wa
Congo pale nitakapotawazwa rasmi kuwa
mfalme wa kwanza wa Congo.Monica
nadhani kuna jambo ambalo itakuwa
vyema ukalifahamu toka kwangu
mwenyewe ambalo nahisi umeshawahi
kulisikia kwani linapigiwa kelele nyingi na
baadhi ya mataifa makubwa.Ninataka
kuigeuza Congo kuwa nchi ya kifalme na
utafiti umefanyika na unaonyesha asilimia
themanini ya raia wa Congo wanataka nchi
yao iwe ya kifalme.Muswada unaandaliwa
ili upelekwe bungeni na bunge likiridhia
basi itafanyika kura ya maoni na wananchi
wataamua kama wanataka nchi ya kifalme
au vipi.Endapo wataamua kuwa wanataka
Congo iwe nchi ya kifalme basi
nitatawazwa kuwa mfalme David wa
kwanza na kama ilivyo kawaida kwa nchi
zenye utawala wa kifame uko mmoja ndio
hutawala kwa hiyo basi familia yangu
itatawala Congo kwa vizazi na vizazi.”
Akasema David Zumo huku akitabasamu
“ Tuachane na hayo ,napenda
nikushuru sana Monica kwa kukubali
mwaliko wangu.Umeacha shughuli zako
nyingi za muhimu na kuja Congo.Ahsante
sana” akasema David
Hata mimi nashukuru sana David
kwa
makaribisho
mazuri
niliyoyapata.Sijawahi pewa heshima
 
we jamaa kiboko.....
monica hatoki...uwezekano wa kuachia papuchi ni mkubwa mnoo...sana..!!...
 
Kuna time nahisi Rais Zumo ana akili sana yawezekana huyo mwanamama Paulina akawa sio mkewe ila katengenezwa tu kumpanga Monica manake mke halali awe hivo kweli mhhhhh
 
Back
Top Bottom