SEHEMU YA 33
Mr President lets go straight to the
point.Why you are here? Umefanikiwa
nilichokuomba?
Ernest hakujibu kitu akachukua
simu yake akazitafuta namba za balozi wa
Tanzania nchini China akapiga na simu
ikapokelewa
“ Habari za usiku huu mheshimiwa
balozi.Samahani sana kwa kukuamsha
mida hii ambayo huko kwenu ni usiku
mwingi” akasema Ernest
“ Bado sijalala mheshimiwa rais
kwani uliniahidi kunipigia usiku hivyo
niko macho nikisubiri simu yako.”
Akasema balozi
“ Nashukuru sana balozi.Sitaki
nichukue muda wako mwingi.Naomba
nizungumze na Linda kama yuko hapo
karibu” akasema rais
“ Ninaye hapa mheshmiwa rais”
akasema balozi na kumpa Linda simu ili
azungumze na rais.Ernest akaweka sauti
kubwa ili Austin aweze kusikia kila kitu
“ Mheshimiwa rais shikamoo baba”
akasema Linda.Mara moja Austin
akaitambua sauti ile na kutabsamu huku
machozi yakimlenga.
“ Marahaba hujambo Linda?
“ Sijambo “ akajibu Linda
“ Samahani Linda hebu nieleze
historia yako kwa ufupi” akasema rais
“ Naitwa Linda January,ninatokea
Tanzania.Nilikamatwa hapa China na
kufungwa miaka kumi na tano kwa kosa la
kujaribu kuingiza madawa ya
kulevya.Ninashukuru mheshimiwa rais
umenisaidia
nimeweza
kutoka
gerezani.Ninaomba mheshimiwa rais
nitakaporejea nyumbani nisiendelee na
kifungo.Nakuahidi sintajihusisha tena na
biashara hii ya dawa za kulevya,nakuomba
sana baba” akasema Linda na kwa mbali
akasikika akilia kwa kwikwi.Austin naye
akashindwa kuyazuia machozi kumtoka.
“ Linda nimekusikia na
ninakuhakikishia kwamba hautakwenda
gerezani tena.Nitakuandalia mpango
mzuri sana wa maisha yako mapya na kwa
sasa utaendelea kukaa hapo hapo kwa
balozi wetu China.Utapata kila
unachokihitaji.Naomba umpe simu balozi
tafadhali” akasema Ernest na kuagana na
balozi akamgeukia Austin
“ Ahsante sana mheshimiwa rais.Sina
neno zuri la kukushukuru kwa hili
ulilonifanyia ila nakuahidi kukufanyia
kazi yako kwa ufanisi mkubwa.Now we
can talk” akasema Austin
“ Nilikwambia Austin kwamba nina
nguvu ya kuweza kumtoa dada yako
gerezani.Baada ya kulitimiza ombi lako ni
nafasi yako sasa kunisikiliza nikueleze
kile ambacho nimekuitia hapa Tanzania”
akasema Ernest
“ Mheshimiwa rais kabla
hujaendelea naomba nikuulize swali moja
tu na ninaomba unipe jibula kweli”
“ Uliza Austin nitakujibu bila wasi
wasi”
Austin akamtazama Rais kisha kwa
sauti ya taratibu akauliza
“ Mr president are you one of them?
“ One of them? Unazungumzia akina
nani? Rais naye akauliza
“ The Alberto’s ́” akajbu Austin.
Mstuko aliuopata Ernest Mkasa rais
wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
ulikuwa mkubwa na wa wazi.Haraka
haraka akajifanya kama vile hajastuka na
kuuliza