SEHEM YA 29
Ni saa tano za usiku sasa Mzee benedict
Mwamsole na mke wake Janet wako
chumbani kwao wakijipumzisha baada ya
shughuli za kutwa nzima.
“ Ben kuna jambo lilitokea jana na
sikutaka kukwambia mapema nilitaka
kwanza nifanye uchunguzi wangu”
akasema Janet
“ Ni jambo gani hilo kwa sababu
nawe huishiwagi mambo” akasema mzee
Ben huku akitoa kicheko kidogo
“ Katika sherehe ya Monica jana
Daniel Yule kijana wa mzee Swai
hakuwepo
inaonekana
hakualikwa.Nadhani Monica aliyafanyia
kazi maneno yangu”
“ Uliongea na Monica kuhusu suala
hilo? Akauliza mzee Ben
“ Ndiyo niliongea naye na
kumtahadharisha kuhusu ukaribu na
Daniel “ akasema bi Janet
“ Hukupaswa kufanya hivyo.Monica
ataona kama vile tunaingilia masuala yake
binafsi” akasema Ben
“ Hapana siwezi kukaa kimya wakati
ninamuona kabisa mwanangu yuko karibu
na chui mwenye ngozi ya
kondoo.Nilimtahadharisha
awe
muangalifu asije akaingia katika mitego ya
Yule kijana.Kutomuona Daniel jana katika
sherehe ni dalili za wazi kwamba tayari
amekwisha anza kumkwepa kijana yule
mchafu wa tabia.” Akasema bi Janet na
baada ya sekunde kadhaa akaendelea
“ Jana wakati sherehe ikiendelea
Monica alikuwa anazunguka zunguka
kusalimia watu mbali mbali walioalikwa
na baadae akapotea ghafla .Nilikuwa
nikimfuatilia na nikamuona akiondoka na
kijana mmoja hivi mtanashati sana
ambaye ni mara ya kwanza kumuona naye
wakaeleka kule kwenye bwawa la
kuogelea ambako kuliandaliwa meza
.Nadhani Monica alipanga kukutana na
kijana Yule kule ili waongee mambo
yao.Niliwafuatilia na kuwakuta wakiwa
wamezama katika maongezi na kwa
namna nilivyowakuta kuna kila dalili
kwamba kuna kitu kinaendelea kati yao.”
Akanyamaza tena na baada ya muda
akaendelea.
“ Kijana huyo anaitwa Dr Marcelo
Richard.Kwa mujibu wa Monica ni
kwamba kijana huyo ni mmoja wa
wafadhili wa mradi wake wa kujenga
shule ya watoto walemavu.Lakini kwa
mtazamo wangu kuna kitu zaidi ya
ufadhili nilichokiona kati yao.Kama
kawaida yangu nilifanya utafiti wangu
nilitaka kumfahamu Dr Marcelo ni kijana
wa namna gani”
“ Umepata majibu gani ? akauliza
mzee Ben
“ Dr Marcelo ni kijana msafi wa
tabia,ni msomi mzuri,anatoka katika
familia tajiri ,hajawahi kuwa na mke na
hana tabia chafu za kubadilisha wanawake
kama alizonazo Daniel.Anaongoza
hospitali inayofadhiliwa na familia yake
inayohudumia wagonjwa wa saratani ya
damu.Kwa ujumla ni kijana mwenye sifa
nzuri na ni kijana anayeweza kumfaa sana
Monica ila kuna tatizo moja.” Akasema Bi
Janet na kunyamaza
“ Tatizo gani hilo? Akauliza Ben.Bi
Janet akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Dr Marcelo ana tatizo la saratani ya
damu”..
Zilipita kama dakika mbili za ukimya
mzee Ben akasema
“ Kwa namna ulivyowaona kuna
dalili zozote za Monica na huyo Dr Marcelo