QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

SEHEMU YA 36

Tayari inakaribia saa moja za jioni na
muda wa Monica kwenda kuonana na
David Zumo ukikaribia lakini bado Monica
alikuwa anatafuta nguo nzuri atakayovaa
usiku huo.Kitandani kulikuwa na magauni
manne ameyaweka .Kila moja ni zuri
lakini hakujua avae lipi.Akasimama
akayaangalia magauni yale na mwisho
akaamua kuchukua gauni jekundu akavaa
pamoja na koti refu jepesi la rangi
nyeusi.Ama kweli ungebahatika kuonana
naye usiku huu ungewapa hongera
waliosema kwamba Monica ni mrembo
kuliko wote Afrika.Alipendeza kuliko
kawaida.Akajitazama katika kioo
akatabasamu
“ Mtu ninayekwenda kuonana naye
ni mtu mzito kwa hiyo lazima nipendeze
.Ingekuwa ni mtu wa kawaida tu
nisingejiremba hivi ningeenda kawaida
tu.Huyu ni rais wa nchi kwa hiyo
ninalazimika kupendeza “ akawaza
Monica na mlango wa chumba chake
ukagongwa,akaenda
kuufungua
akakutana na mtumishi wake Maria
“ Madam nimepigiwa simu na walinzi
kuna wageni wako wanasema wanatoka
katika ubalozi wa Kongo hapa nchini”
akasema Maria
“ Ahsante Maria wakaribishe
sebuleni ninakuja sasa hivi” akasema
Monica na kuendelea kujipamba na baada
ya muda akachukua pochi yake na kutoka
chumbani kwake akaelekea sebuleni
ambako kulikuwa na watu watatu
wamekaa na wote wakashindwa kuzuia
mshangao wao baada ya kumuona Monica
.
“ Jean Pierre Muyeye” akasema
Monica huku akitabasamu.Muyeye
akainuka na kumpa mkono Monica
“Madam Monica” akasema Muyeye
na wale watu wengine alioongozana nao
wakasimama wakamsalimu Monica
“ Nadhani uko tayari tunaweza
kuondoka? Akauliza Muyeye
“ Ndiyo tunaweza kuondoka “
akasema Monica kisha wakaongozana
hadi nje wakaingia katika gari la ubalozi
wa Kongo wakaondoka .
“ Ama kweli msichana huyu ana
uzuri wa kipekee kabisa.Ninavyomfahamu
David Zumo anapenda sana watoto wazuri
kama huyu na nina hakika kabisa lengo
lake si kuchangia miradi ya Monica kama
anavyotaka bali anamtaka Monica
kimapenzi.” Akawaza Muyeye wakati
safari ikiendelea.
Hatimaye wakawasili hoteli ya
kifahari yenye hadhi ya nyota tano ya
Kobe Village hoteli ambayo maraisi wengi
wanapotembelea Tanzania hufikia.Ni
hoteli inayotajwa kuwa na huduma za hali
ya juu na bei ya juu zaidi kuliko zote afrika
mashariki.Gari likasimama na haraka
haraka Muyeye akashuka na kuufungua
mlango wa upande aliokaa Monica
,akashuka kisha akamuomba amfuate
wakapanda lifti kuelekea ghorofani kilipo
chumba cha rais David Zumo.Walinzi wa
rais David walikuwa tayari na taarifa za
ujio wa Monica hata hivyo
hawakumruhusu apite hivi hivi bila
kukaguliwa wakaukagua mkoba aliobeba
na kuhakikisha hakukuwa na silaha au
kitu chochote hatarishi alichobeba.David
Zumo ni mmoja wa maraisi wanaotajwa
kuwa na ulinzi mkali sana miongoni mwa
marais wa afrika.
Jean Pierre Muyeye akamuongoza
Monica kuingia katika sebule kubwa ya
 
SEHEM YA 37

chumba cha rais David Zumo ambaye
wakati wakiingia alikuwa akiongea na
simu lakini mara tu alipomuona Muyeye
akiwa ameongozana na Monica akasitisha
maongezi na mtu aliyekuwa akiongea naye
simuni
“ Mungu wangu..!! huyu Monica ni
binasamu wa kawaida kweli?? Uzuri wake
unanipa shaka sana yawezekana akawa ni
kiumbe mwingine huyu” akawaza David
Zumo.Pierre Muyeye akasimama kwa
adabu na kusema
“ Mheshimiwa rais mgeni wako huyu
hapa amefika salama” akasema Muyeye na
kumgeukia Monica
“ Madam Monica huyu ndiye
mwenyeji wako ,rais wa jamhuri ya
kidemokrasia
ya
Kongo,David
Zumo.Karibu sana Madam” akasema
Muyeye na kuinama kwa adabu kuonyesha
heshima kisha akatoka nje na kumuacha
David Zumo akiwa na Monica peke yao
mle ndani
“ Monica karibu sana.” Akasema
David huku akimpa mkono Monica
“ Ahsante sana mheshimiwa rais”
akajibu Monica kwa adabu na David Zumo
akamkaribisha sofani.
“ Monica ni furaha yangu kukutana
nawe usiku wa leo na kabla ya yote
ninapenda kwanza kusema ahsante sana
kwa kukubali mwaliko wangu wa kutaka
kuonana nawe usiku huu.” Akasema David
Zumo rais mwenye haiba ya aina yake
“ Hata mimi nimefurahi sana
kukutana nawe mheshimiwa rais kwani
nimekuwa nikikusoma na kukutazama
kupitia vyombo vya habari lakini leo hii
nimekutana nawe ana kwa ana.Ni heshima
kubwa sana kukutana nawe mheshimiwa
rais” akasema Monica huku akitabasamu
“ Nafurahi kusikia hivyo
Monica.Jambo la pili nataka nikupongeze
sana kwa mafanikio makubwa uliyoyapata
na hasa kwa kutangazwa na jarida kubwa
la the Face kuwa mwanamke mrembo
zaidi barani Afrika.Hongera sana
unastahili heshima hiyo kubwa.Heshima
hii uliyopewa na jarida la The Face
imekupaisha hadi nje ya mipaka ya
Tanzania na kutufanya hata sisi wengine
ambao hatukuwa tumekufahamu hapo
kabla kukufahamu.Hongera vile vile kwa
mambo ambayo umekuwa ukiyafanya kwa
jamii.Tanzania inapaswa kujivunia sana
kuwa na mtu kama wewe” akasema David
“ Ahsante sana David.Napenda na
mimi nitumie nafasi hii kukupongeza sana
kwa kazi kubwa uliyoifanya katika nchi
yako ya Kongo.Ni kazi kubwa na ya
kutiliwa mfano.Kongo ya sasa si ile ya
miaka ile.Hongera sana mheshimiwa rais”
akasema Monica na kuufanya uso wa
David Zumo ukachanua kwa tabasamu
kubwa kisha akainuka na kufungua chupa
ya mvinyo akammiminia Monica katika
glasi na kumpatia
“ Samahani Monica nilipaswa
kukukaribisha kinywaji toka ulipoingia
lakini tumejikita moja kwa moja katika
maongezi.” Akasema David
“ Ahsante sana mheshimiwa rais”
akajibu Monica na kunywa funda dogo la
mvinyo...
“ Monica usiku wa leo nina maongezi
kadhaa kuhusiana na miradi ya
kimaendeleo unayoifanya lakini kabla ya
yote ningependa kwanza kukukaribisha
kwa chakula cha jioni nilichokiandaa kwa
 
SEHEM YA 38

heshima yako.Karibu kwa chakula
Monica” akasema Monica kisha David
akamuongoza kuelekea katika chumba
cha chakula ambamo chakula maalum
kilikwisha andaliwa .David Zumo
akamkaribisha Monica mezani kwa ajili ya
chakula.Baada ya kula wakarejea tena
sebuleni kuendelea na maongezi yao.
“ Monica sitaki nichukue muda
mrefu sana wa kuongea nawe usiku huu
sitaki mwenzi wako awe na wasi
wasi.Unajua sisi wanaume hata kama
akiwa na uhakika kwamba umekuja
sehemu salama kuonana na rais lakini
bado hawezi kukosa kuwa na
wasiwasi.Kwa hiyo naomba nijielekeze
moja kwa moja katika ile ambacho
nimekuitia hapa usiku huu” akasema
David Zumo na kumfanya Monica atoe
kicheko kidogo.
“ Mbona unacheka Monica? Akauliza
David Zumo ambaye anatajwa kuwa ni rais
ambaye huongea kwa hisia kubwa
“ Hakuna wasi wasi wowote
mheshimiwa rais kwani sina mume bado
kwa hiyo tunayo nafasi ya kuongea
mambo mbalimbali kama utapenda”
akasema Monica na uso wa David
ukajenga tabasamu
“ Nilimuuliza swali la mtego ili nijue
kama ana mpenzi au hana lakini kumbe
hana mpenzi.” Akawaza David Zumo na
kusema
“ Monica nimefuatilia baadhi ya
shughuli unazozifanya na nimejikuta
nikiguswa sana.Hongera sana kwanza kwa
kujitoa kusaidia jamii yako.Ni wengi
wanajitahidi kufanya kama unavyofanya
lakini wengi hawafanyi kwa kujitolea
kama unavyofanya.Nimeguswa zaidi sana
na huu mradi wa kujenga shule ya watoto
wenye ulemavu wa kutoona na kutosikia
ambao unautafutia fedha.Naona tuanzie
hapo nataka kupata taarifa za kina
kuhusiana na mradi huo na wapi umefikia
hadi sasa na nini kinahitajika na kama
kuna miradi mingine pia ningependa
kuifahamu ni ipi na nini kinahitajika.Watu
kama ninyi mnatakiwa kuungwa sana
mkono kwa kila hali” akasema David na
kunywa funda la mvinyo.
“ Ahsante sana mheshimiwa rais kwa
kunikaribisha usiku huu .Ni heshima
kubwa umenipa ya kunikaribisha mahala
hapa .Ahsante kwa chakula kizuri.Vile vile
napenda nikushukuru sana kwa
kuonyesha kuguswa na baadhi ya kazi
ninazozifanya hususani mradi huu wa
ujenzi wa shule ya watoto wenye ulemavu
wa kutoona na kutokusikia.Msaidizi wako
Jean Pierre Muyeye aliniambia kwamba
kama usingekuwa na mkutano leo hii
nawe ungehudhuria mbio hizo” akasema
Monica na kuachia tabasamu
“ Ni kweli Monica laiti kama
nisingekuwa na kikao leo hii ningeungana
nawe katika mbio hizo lakini kwa vile
sikuwa na nafasi nikalazimika kumtuma
Muyeye aje aniwakilishe” akasema David
“ Ahsnate sana mheshimiwa David
kwa ushiriki wako.Kwa ufupi tu ni
kwamba mimi nina taasisi ambayo
hushughulika
kutatua
matatizo
mbalimbali ambayo imejielekeza zaidi
katika matatizo ya watoto na wazee
wasiojiweza ambao ni kundi
linaloonekana
kusahaulika
sana.Tumekuwa tukitoa misaada mbali
mbali mahospitalini kusaidia watoto
wadogo na hata wazee kwa kuwajengea
makazi bora,kuwasaidia huduma za afya
 
SEHEM YA 39

chakula na mambo mengine .”
akanyamaza akameza mate na kuendelea
“ Katika utafiti tulioufanya
tumegundua kuna kundi moja
limesahaulika sana ni la watoto wenye
ulemavu wa kutoona na kutosikia kwa
pamoja.Kundi hili linazidi kuongezeka na
kwa takwimu tulizonazo ni zaidi
ya watoto
mia nne na hamsini wenye ulemavu wa
aina hii.Tumegundua watoto wenye
ulemavu wa aina hii wanakumbana na
changamoto nyingi sana katika maisha yao
kwa hiyo kwa vile jukumu la taasisi yangu
ni kuwahudumia watoto tumeamua
kulibeba jukumu hili la kuwasaidia watoto
wenye aina hii ya ulemavu kwa
kuwajengea shule yenye miundo mbinu
rafiki na ambamo wataishi na kutapata
elimu na malezi.Ujenzi wa shule
unakadiria kugharimu zaidi ya shilingi
bilioni mia tatu za kitanzania.Itakuwa ni
shule ya aina yake na tunategemea
kuifanya iwe ya kimataifa kwani kwa
miaka ya mbele tutakuwa tukipokea
watoto kutoka hata katika nchi nyingine
jirani ” Monica akanyamaza akanywa
funda dogo la mvinyo akaendelea
“ Tumejaribu kutafuta wafadhili
kutoka nje ya nchi lakini tumejikuta
tukikumbana na vikwazo mbalimbali
hivyo nikaona ni bora kama tukijitajidi
kufanya jambo hili wenyewe kwa kuanzia
na nguvu zetu kidogo tulizonazo.Kwa hiyo
tumeazimia kufanya mambo kadhaa ili
kukusanya fedha za kuanza ujenzi wa
shule hiyo .Tumeazimia kufanya mambo
matatu.Kwanza ni kuandaa mbio za nusu
marathoni ambazo zimefanyika leo na
kushirikisha watu toka nchi mbalimbali
maalum kabisa kwa ajili ya kuchangia
ujenzi wa shule hii na ninashukuru
muitikio umekuwa mkubwa na tumevuka
lengo tulilokusudia kukusanya.Huu
umekuwa ni mwanzo mzuri sana .Baada ya
mbio tutaandaa onyesho la mavazi ambalo
nalo litakuwa maalum kwa ajili ya
kukusanya fedha .Litakuwa ni onyesho
kubwa kuwahi kufanyika afrika mashariki
kwani tumewaalika wabunifu na
wanamitindo wakubwa duniani na lengo
likiwa kutunisha mfuko wa ujenzi wa
shule hii.Baada ya onyesho hilo la mavazi
tutaandaa pia chakula maalum
tutakachowakaribisha watu mbali mbali
viongozi wa serikali,mashirika na watu
binafsi ambao watachangia fedha.Baada
ya matukio hayo matatu ninaamini
tutakuwa na kiasi cha kutosha
kutuwezesha kuanza ujenzi wa shule
hiyo.Kwa hiyo mheshimiwa rais hiyo
ndiyo mipango ambayo mimi na taasisi
yangu tumepanga kuifanya ili kuweza
kupata fedha za ujenzi wa shule hiyo ya
watoto wenye ulemavu wa kutoona na
kusikia” akasema Monica na kuinua glasi
ya mvinyo akanywa funda dogo kama
kawaida yake .David Zumo naye akanywa
funda kubwa la mvinyo na kusema
“ Hongera sana Monica .U
mwanamke jasiri sana ambaye juhudi
zako
zinastahili
kuungwa
mkono.Umeonyesha ujasiri mkubwa na
kwa hilo lazima nikupongeze.Kama
nilivyokueleza awali kwamba mimi
nimeguswa sana na jambo hili na niko
tayari kukusaidia.Fedha zinazohitajika
kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ni nyingi
na pengine baada kukusanya fedha katika
matukio hayo yote matatu fedha zinaweza
zisitoshe .Kabla sijasema kiasi ambacho
mimi nitachangia katika ujenzi huo
unategemea kupata kama shilingi ngapi
katika matukio hayo yote matatu?
“ Tunatarajia kukusanya kiasi cha
shilingi bilioni ishirini hadi hamsini.”
“ Ni kiasi kidogo sana ambacho
itachukua muda mrefu kuikamilisha shule
hiyo.Ninaiona kiu ya kutaka kuimamilisha
shule hiyo kwa wakati lakini kikwazo
kitakuwa ni fedha.Mimi kwa upande
wangu nitachangia kiasi cha shilingi
bilioni mia mbili na sabini .Nina hakika
kwa kiasi hicho hatua kubwa itakuwa
imepigwa “ akasema David.Monica
akapatwa na mstuko hakuwa ametegemea
kama David Zumo angeweza kuchangia
kiasi kikubwa kama kile cha fedha.Kwa
sekunde kadhaa akabaki ameduwaa
akimtazama
David
aliyekuwa
akitabasamu halafu akainuka na kwenda
kumpa mkono
 
SEHEMU YA 40


“ Mheshimiwa rais ahsante sana kwa
msaada huu mkubwa ambao sikuwa
nimeutarajia kabisa.Kiasi hiki kikubwa
ulichokitoa kinakwenda kuimaliza kabisa
shule hiyo.Ahsante sana mheshimiwa rais
na sijui hata nikushukuruje kwa msaada
huu mkubwa.Watu wa Kongo wana bahati
sana kukupata rais mwenye moyo wa
huruma kama wewe” akasema Monica na
kwa furaha aliyokuwa nayo akashindwa
kujizuia kutoa machozi.Akatoa kitambaa
na kufuta machozi.
“ Samahani mheshimiwa rais ni
kawaida yangu kila ninapokuwa na furaha
iliyopitiliza hushindwa kujizuia machozi
kunitoka “ akasema Monica
“ Usijali Monica.Toka moyoni
nimeguswa sana na jambo hili
unalolifanya na ndiyo maana niko tayari
kutoa kiasi chochote cha mchango kwa
ajili ya kuwasaidia watu wenye matatizo
mbalimbali.Mungu ametujaalia wachache
kuwa na utajiri ili tuutumie utajiri huo
kwa wale masikini wasiokuwa na uwezo
.Kwa hiyo ninatamini sana katika kusaidia
watu masikini na ninawapenda sana wale
wanaojitolea kuwasaidia watu masikini.
Kwa hiyo naomba ufahamu kuwa mchango
huu mdogo nilioutoa nimeutoa kwa moyo
mmoja na si kwa sababu ya utajiri nilio
nao.” Akasema David Zumo
“ David huu si mchango mdogo kama
unavyosema .Ni mchango mkubwa sana na
ninaiona namna ndoto yangu ya
kuwasaidia watoto hawa wenye mahitaji
makubwa.Ahsante sana mheshimiwa rais
kwa kuifanya ndoto yangu iwe
kweli.Nimeupokea mchango huu kwa
moyo mmoja na ninakuahidi kiasi hiki cha
fedha ulichokichangia kitatumika kama
kilivyokusudiwa” akasema Monica
“ Monica mimi niko pamoja nawe na
nitakuunga mkono katika kila jambo
ambalo umekusudia kulifanya kwa jamii
yako.Ukiacha shule hii unayotarajia
kujenga ,ni jambo lipi ambalo umekusudia
kulifanya iwapo ungepata fedha za
kutosha? Akauliza David Zumo
“ Kwa sasa akili yangu nimeielekeza
katika shule hii ya watoto hawa wenye
mahitaji maalum lakini kuna mambo
mengi ambayo kama ningekuwa na fedha
za kutosha ningeweza kuyafanya .Kuna
jambo ambalo nimekuwa nalifikiria pia
nalo ni kuhusu kujenga kambi za
wazee.Hii ni sehemu kubwa ya jamii
ambayo imeonekana kusahaulika
kabisa.Wazee wanapata wakati mgumu
sana na imefikia hatua uzee unaonekana
ni kama adhabu.Nataka kuwe na kambi
kwa ajili ya kuwatunza wazee katika kila
mkoa ambako watapatiwa huduma mbali
mbali na watakuwa na uzee mzuri.Hiyo ni
ndoto yangu nyingine baada ya kumaliza
kwanza suala hili la shule ya watoto wenye
uhitaji” akasema Monica
“ Monica naomba ufahamu kuwa
siku zote mimi nitakuwa pamoja nawe
katika mipango yako yote na nihesabu
kama mdau namba moja wa miradi yako
ya kusaidia jamii na nitawaleta pia wadau
wengine rafiki zangu ambao kwa pamoja
tutakupa ushirikiano mkubwa.Kitu cha
msingi unachotakiwa kufanya ni kuwa na
mawasiliano ya karibu na kila pale
unapohitaji msaada Fulani usisite
kuniambia.” Akasema David
“ Ahsante sana mheshimiwa rais
sintasita kukutaarifu jambo lolote au kila
pale nitakapokuwa nimekwama katika
kitu chochote.Ahsante sana kwa kuwa
msaada mkubwa kwangu.Ni Mungu pekee
ndiye atakayekulipa kwa namna
ulivyojitoa kusaidia watu wake wenye
matatizo mbali mbali” akasema
 
SEHEM YA 41

“ Dah !! siamini macho
yangu.Nilikuwa nazungumza na binadamu
au malaika? Akajiuliza David kisha
akajimiminia tena mvinyo na kuunywa
wote
“ Monica si binadamu wa kawaida
.Kwa muda huu mfupi niliokaa naye
nimegundua kwamba ni binadamu wa
kipekee kabisa.Nimekutana na wanawake
wengi lakini sijawahi kukutana na
mwanamke yeyote mwenye walau
kuukaribia uzuri wa Monica.Huyu ni
mwanamke ambaye sintakubali nimkose
katika maisha yangu.Nitafanya kila
niwezalo hadi nihakikishe nimempata
Monica.” Akasema David na kunywa tena
mvinyo.Alionekana ni kama mtu
aliyechanganyikiwa alikuwa anazunguka
zunguka mle sebuleni.
“ Nimeanzisha vita lazima
nihakikishe
ninaimaliza
na
ninashinda.Ninasema ni vita kwa sababu
naamini Monica anawachanganya
wanaume wengi kwa uzuri wake na wengi
lazima wameweka ahadi kama yangu ya
kuhakikisha wanampata kwa hiyo lazima
kuna ushindani mkubwa hapa na ndiyo
maana nikasema kwamba hii ni sawa na
vita ya kumgombania mwanamke.Najua
lazima atakuwa na mpenzi wake na ni
wazi huyo mpenzi wake lazima atakuwa ni
mtu mwenye fedha nyingi lakini lazima
atapambana na mimi tajiri namba moja
afrika kwa hiyo hakuna tajiri anayeweza
kuniumiza kichwa mimi na hakuna
mwanamke anayeweza kukataa kuogelea
katika bahari ya utajiri labda awe
malaika.Hata Monica nina hakika hana
ubavu wa kunikataa.Lakini hata hivyo
ninatakiwa kujenga mazoea ya karibu
sana na wazazi wake.Nikifanikiwa
kuwaweka karibu wazazi wake basi
nitakuwa nimeshinda vita hii bila kutumia
nguvu kubwa.” Akawaza David na kunywa
tena funda kubwa la mvinyo

Monica
lazima
awe
wangu...Nitakuwa mwanaume mwenye
furaha sana duniani kama nitakuwa na
Monica mwanamke ambaye hata mke
wangu ambaye niliamini ni mzuri kuliko
wote niliowahi kuwaona hamfikii hata
robo.Utajiri nilionao utakuwa na maana
kama nitampata Monica.” Akaendelea
kuwaza David Zumo.
 
SEHEMU YA 42

aada ya kutoka kuonana na rais
David Zumo,Monica alimuelekeza Jean
Pierre Muyeye ampeleke moja kwa moja
nyumban kwa wazazi wake.Usiku huu
hakutaka kwenda nyumbani kwake.
“ Huu ni kama muujiza
kwangu,sikuwa nimetegemea kabisa
kupata kiasi hiki kikubwa cha fedha kwa
haraka namna hii ili kukamilisha mradi
ule mkubwa.Nilikuwa na uhakika wa
kuzipata
lakini
sikujua
ningezipataje.Ahsante Mungu kwa
kuendelea kusimama nami na
kunifanikishia mambo yangu.” Akawaza
Monica wakati safari ya kurejea nyumbani
ikiendelea
“ David Zumo ..” akawaza na
kutabasamu baada ya picha ya David
kumjia kichwani
“ Nimepata bahati ya kipekee ya
kukutana uso wa uso na rais huyu mwenye
sifa lukuki na kikubwa zaidi ana roho
nzuri pengine kupita marais wote . Ni rais
ambaye amelifanya taifa la Kongo kuwa
taifa kubwa afrika.Uchumi wake umepaa
kwa kasi kubwa.Naweza kusema kwamba
raia wa Kongo wana bahati sana ya
kumpata rais mpenda watu kama huyu.Ni
rais anayeguswa na matatizo ya watu.”
Akawaza Monica na kukumbuka maongezi
yake na David.
“Toka moyoni nimeguswa sana na
jambo hili unalolifanya na ndiyo maana
niko tayari kutoa kiasi chochote cha
mchango kwa ajili ya kuwasaidia watu
wenye matatizo mbalimbali.Mungu
ametujaalia wachache kuwa na utajiri ili
tuutumie utajiri huo kwa wale masikini
wasiokuwa na uwezo .Kwa hiyo ninatamini
sana katika kusaidia watu masikini na
ninawapenda sana wale wanaojitolea
kuwasaidia watu masikini. Kwa hiyo
naomba ufahamu kuwa mchango huu
mdogo nilioutoa nimeutoa kwa moyo
mmoja na si kwa sababu ya utajiri nilio
nao.”.
Maneno haya ya David Zumo
yakaendelea kuzunguka katika kichwa cha
Monica.
“ Ni wazi alitoa mchango wake huu
kwa moyo na wala si kwa utajiri
alionao.Sijui nitamshukuruje mtu
huyu.Sioni namna bora ya kumshukuru
zaidi ya kumuombea ili awe na moyo huo
huo wa kusaidia watu wenye matatizo
mbali mbali “ akaendelea kuwaza Monica.
Alifika nyumbani kwa wazazi wake
akaagana na akina Muyeye akaelekea
ndani.Benedict na mkewe tayari walikuwa
wamelala
Monica
akawaamsha.Walishangazwa sana na ujio
ule wa Monica usiku ule.
“Monica is everything ok my dear?
Akauliza Bi Janet mama yake Monica kwa
wasi wasi
“ Msihofu jamani hakuna tatizo”
akajibu Monica kuwatuliza wazazi wake
walioanza kuwa na wasi wasi
“ Samahani kwanza kwa kuwaamsha
ila nisingeweza kulala bila kuja uonana
nanyi usiku huu” akasema Monica
“ Kwani kuna nini Monica? Akauliza
Bi Janet
“ Nimetoka kuonana na rais wa
jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo David
Zumo” akasema na kunyamaza
 
SEHEMU YA 43

Nini kimetokea huko? Akauliza bi
Janet aliyeonekana kuwa na shauku
kubwa ya kutaka kufahamu kilichojiri
“ Mambo yamekwenda vizuri
sana.Nimeonana na David tumeongea na
kikubwa alichohitaji kuonana nami ni kwa
ajili ya kuchangia katika mradi wangu wa
shule .Alitaka kufahamu nimefikia wapi
kuhusu mradi huo nikamueleza hatua
ninazochukua kukusanya kwanza fedha
kabla ya kuanza ujenzi.Baada ya kumpa
mchanganuo wote wa mradi ndipo akatoa
mchango wake.Gharama nzima ya mradi
ni kiasi cha shilingi bilioni mia tatu na
yeye ametoa mchango wa shilingi bilioni
mia mbili na sabini “ akasema Monica na
kumkumbatia mama yake
“ Wow !! this is wonderfull !!
akasema bi Janet akiwa na mshangao
“ Bilioni mia mbili na
sabini!!!..akasema mzee benedict naye
akiwa katika mshangao
“ Mwanangu una bahati kubwa
sana.Katika dunia ya leo hakuna
binadamu anayeweza akakupatia kiasi
kikubwa kama hicho cha pesa.Huyu rais ni
mtu mwenye moyo wa ajabu sana.”
Akasema mzee Benedict
“ Ni kweli baba.Hata mimi mpaka
sasa bado naona jambo hili ni kama ndoto
lakini ni kitu cha kweli kabisa” akasema
Monica na machozi yakaanza kumtoka
baba yake akamkumbatia na kumfuta
machozi
“ Ouh my queen you are crying
again” akasema mzee benedict
“ I cant help it dady.Nina furaha
iliyopitiliza.Ndoto yangu ya muda mrefu
inakwenda kutimia.Nilikuwa naumiza
kichwa sana namna nitakavyoweza kupata
fedha za kuniwezesha kuijenga shule
hiyo,nilikuwa namlilia Mungu sana na
amesikia kilio change na hatimaye fedha
zimepatikana” akasema Monica
“ Monica unapaswa kumshukuru
sana Mungu kwani amekupa upendeleo
wa ajabu.Kila uchao anazidi kukufungulia
milango ya mafanikio.Anazina juhudi zako
na moyo wako wa kusaidia watu wenye
matatizo mbali mbali na ndiyo maana
amekuwa anakubariki kila siku”
“ Usemayo ni ya kweli kabisa
baba.Ninapaswa kumshukuru sana Mungu
kwa Baraka zake hizi.Hiki kilichotokea leo
naona ni kama muujiza tu.Sikuwa
nimetegemea kama David Zumo angeweza
kutoa kiasi hiki kikubwa cha
fedha.Nimezoea kupewa msaada wa
milioni kadhaa lakini si mabilioni mengi
kama haya.”
“ Monica Yule ni rais na vile vile ni
tajiri namba moja kwa hiyo ulikuwa
unazungumza na mtu mkubwa sana na si
wale uliowazoea wa kutoa ahadi za milioni
moja moja.Huyu ni mtu mzito na ndiyo
maana ametoa mchango mkubwa
kulingana na uwezo wake”
“ Ukiacha mchango alioutoa kwa ajili
ya shule ,ameahidi pia kunipa ushirikiano
nitakapoanza ule mradi wangu wa kujenga
makambi ya wazee katika kila mkoa.David
ni mtu anayeonekana kuguswa sana na
matatizo ya watu wanyonge na ndiyo
maana hata watu wa nchi yake
wanampenda na wamekubali kubadili
vifungu vya katiba ili David atawale kwa
miaka mingi.Tukiachana na hayo kuna
jambo lingine” akasema Monica na
kunyamaza
 
SEHEMU YA 44


Jambo gani hilo Monica? Akauliza
Bi Janet
“ David anahitaji kuonana nanyi
kesho jioni”
Mzee Ben na mkewe wakatazamana
“ Anataka kuonana nasi? Kuna nini
kwani? Akauliza mzee Ben kwa furaha
iliyochanganyika na wasi wasi
“ Hakuna chochote kibaya ila
anahitaji tu kuwafahamu.Aliniuliza kama
wazazi wangu bado wako hai nikamjibu
ndiyo akasema kwamba anahitaji
kuwafahamu” akasema Monica
“ Wow ! tutakwenda kuonana
naye.Huu ni mwaliko mkubwa sana.Ni
heshima kubwa kualikwa na mtu mkubwa
kama huyu.Tutakwenda kuonana naye
hiyo kesho” akasema mzee Ben.
Baada ya maongezi yaliyochukua
takribani saa nzima Monica akaenda
kulala katika chumba chake kilichopo
hapo katika nyumba ya wazazi wake
Alijitupa kitandani lakini macho
hayakuonyesha dalili zozote za kupata
usingizi.Kuna kitu kimoja tu ambacho
kilikuwa kimejaa kichwani kwake ni
David Zumo.
“ Sijawahi kukutana na mtu mwenye
roho nzuri kama David.Ni tajiri namba
moja afrika lakini hana majivuno ni
mcheshi na kinachonivutia zaidi kwake ni
moyo wa huruma alio nao kuweza
kusaidia watu wenye matatizo mbali
mbali.” Akawaza Monica akiendelea
kujigeuza kitandani.
“ Kukutana na kujenga urafiki na
mtu kama David ni mwanzo wa kuelekea
katika mafanikio makubwa na kutimiza
ndoto zangu nyingi nilizonazo.Hii naweza
kusema kwamba ni bahati ya kipekee sana
kuwa na ukaribu na mtu kama huyu
ambaye anaweza kunifanikishia mipango
yangu mingi ya kusaidia jamii
masikini.Naamini nikipata nafasi ya
kutosha ya kuongea naye kuna mambo
mengi ambayo anaweza akanisaidia kama
vile kujenga zahanati kwa ajili ya akina
mama vijijini mahala ambako kuna
changamoto kubwa ya huduma za afya
nk.” Kichwa cha Monica kilikuwa na
mawazo mengi sana kuhusiana na David
Zumo na ilimchukua muda mrefu kupata
usingizi.
 
Ndio habari za asubuhi, na miaka mia moja ya upadri,

Asee nilikua naomba uzuru sintofika leo jumuia nimepata dharula .




LEGE,
Hapo utahusika kujibu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Ngoja kabisaa niende chumbani
 
Mkuu LEGE fanya umwage mzigo wa kutosha tushatoka ibada tayari. Okoa ndoa na pesa zetu make weekend kama hii mishale kama hii ndo mida ya kubembea kaunta!
Angusha mibuyu ya kutosha shemeji yako afurahi make hii ni zaidi ya alcohol!
 
Mkuu LEGE fanya umwage mzigo wa kutosha tushatoka ibada tayari. Okoa ndoa na pesa zetu make weekend kama hii mishale kama hii ndo mida ya kubembea kaunta!
Angusha mibuyu ya kutosha shemeji yako afurahi make hii ni zaidi ya alcohol!
haina shida mkuu inabidi speed ya week end iwe kubwa zaidi ya siku za kawaida dozi ya week end iwe inawalaza jf unaamka jf unashinda jf na kulala jf. harafu shemeji akikuuliza unachart na nani unampa tuu naye anogewe
 
Z
kaeni mkao wa kula story nyingine toka kwa mtunzi yule yule aliyetunga peniela now kaja na kitu kiitwacho queen monica. kutana na kijana AUSTIN JANUARY mtanashati na jasusi hatari anafanya mambo makubwa sana.

ALBERTOS kundi hatari linalotaka kuitawala dunia limeingia pia tanzania
F gfcfc
 
Back
Top Bottom