QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

SEHEMU YA 5


yako
yanakwenda
vizuri.Jiulize
imewezekanaje kwa David Zumo
kuwaacha wanawake hawa wote duniani
na kukuona wewe pekee ? Haya ni
maongozi ya Mungu.Please promise me
that when you come back you’ll give us a
good answer”
“Mama siwezi kukuahidi chochote
kwa sasa kwa sababu bado moyo wangu
hauna hisia zozote kwa David “
“Nimekuelewa Monica.Vipi masuala
ya usafiri? Tayari umekwisha fanya
utaratibu wa kupata tiketi ya ndege? Kama
bado nina rafiki yangu anaweza
akakusaidia kupata nafasi katika ndege
inayoondoka kila siku jioni kwenda
Congo.Ngoja nimpigie sim...”
“hakuna haja mama” Monica
akamkatisha mama yake ambaye tayari
alikuwa ameanza kutafuta namba za simu
za huyo rafiki yake.
“David anatuma ndege yake binafsi
kuja kunichukua “akasema
“Mungu akutangulie mwanangu na
mambo
yako
yote
yakafanikiwe.Nitamtaarifu baba yako
kuhusu jambo hili na nina hakika
atafurahi sana.Basi mimi ngoja nikuache
ukajiandae tutakutana uwanja wa ndege
mimi na baba yako tutakuja kukuaga”
akasema Bi Janet akaagana na mwanae
akaondoka
“Hata mimi sina haja ya kuendelea
kukaa hapa ngoja niondoke nikajiandae
kwa safari ya jioni.Hii itakuwa ni safari ya
kimya kimya sitaki mtu yeyote zaidi ya
wazazi wangu ajue kama ninasafiri.”
Akawaza Monica
******************
Ni saa sita na dakika kumi na nane za
mchana ,rais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania Ernest Mkasa akiwa ofisini
kwake ,mara akaingia msaidizi wake wa
karibu mzee Mukasha akiwa na faili
mkononi.
“ Karibu Mukasha.Umefanikiwa
kupata chochote ?
“Ndiyo mheshimiwa rais.NImeipata
faili lake lakini kuna mambo mengine
nimeyagundua kuhusu Austin January na
kubwa zaidi ni kuhusiana na mdogo wake
ambaye amefungwa nchini China baada ya
kukamatwa na dawa za kulevya.” Akasema
Mukasha
“Thank you Mukasha.Thank you so
much.Hii ni taarifa nzuri sana.Saa ngapi
atapiga simu?
Mukasha akaitazama saa yake ya
mkononi na kusema
“Kwa mujibu wa Mr Boaz alisema
Austin atapiga baada ya saa moja na kwa
mujibu wa saa yangu zimebaki dakika
kumi tu muda huo utimie”
“Good.Twende chumba cha faragha
tukaisubiri simu yake kule.Sitaki mtu
yeyote ajue tunaongea nini” akasema
Ernest wakatoka wakaelekea katika
chumba cha maongezi ya faragha.Ernest
akaanza kulipitia faili lile lenye nyaraka
mbali mbali zinazomuhusu Austin
January.
“Mukasha una uhakika Austin
atapiga simu? Akauliza Ernest baada ya
kumaliza kuzipitia nyaraka zile
“Atapiga mheshimiwa.Tuendelee
kusubiri kidogo” akasema Mukasha
“Nina wasi wasi sana kama atapiga “
“Usiwe na wasi wasi mheshimiwa
rais atap..” Kabla Mukasha hajamalizia
 
SEHEMU YA 6


sentensi yake ikapigwa simu katika
kompyuta iliyokuwa mbele ya rais ,bila
kuchelewa akabonyeza kitufe cha
kupokelea na katika kompyuta alionekana
kijana mmoja mtanashati sana akiwa
katika ofisi nzuri .Alikuwa ametulia na
hakuonekana kuwa na chembe ya wasi
wasi
“Shikamoo mheshimiwa rais,naitwa
Austin january” akasema Austin
“Marahaba Austin,habari za huko?
Maisha yanakwendaje?
“Habari nzuri na maisha mazuri
mheshimiwa rais,sijui nyie hapo
Tanzania”
“Sisi pia tunaendelea vizuri
,Tanzania iko salama” akasema Ernest.
“Nafurahi kusikia hivyo mheshimiwa
rais.Nimeelekezwa na mkuu wangu kuwa
una maongezi na mimi.Naomba twende
moja kwa moja katika kile unachohitaji
kuongea nami.”akasema Austin.Ernest
akakohoa kidogo na kusema
“Kwanza nashukuru sana Austin kwa
kukubali kuzungumza nami.Bila kupoteza
muda utaniwia radhi kama nitazungumza
mambo ambayo pengine hukupanga
kuyasikia.”
“ Endelea tu mheshimiwa rais”
akasema Austin
“ Austin ni mara ya kwanza mimi na
wewe
tunazungumza.Sikuwa
nimekufahamu hapo kabla hadi hivi
karibuni nilipoelezwa kuhusiana na
historia
yako
na
nini
kilikutokea.Nilipoingia
madarakani
nilielezwa kuhusiana na tukio lililokupata
wewe na wenzako ambalo lilitokea mwaka
mmoja kabla sijaingia madarakani.Taarifa
niliyopewa haikuwa kamili na
haikuzungumza chochote kuhusu wewe
kushiriki katika operesheni ile ya kwenda
kuwakomboa madereva wa kitanzania
waliotekwa nchini Somalia.Namshukuru
sana mmoja wa wasaidizi wangu wa
karibu ambaye amenifumbua macho na
kunieleza ukweli halisi wa tukio
hilo.Baada ya kuufahamu ukweli ndipo
nilipoanza
mchakato
wa
kukutafuta.Haikuwa kazi rahisi kwa mr
Boaz kukubali ombi langu la kutaka
kuonana nawe lakini baada ya majadiliano
marefu nashukuru akanielewa .”
akanyamaza na Austin akasema
“ Mheshimiwa rais,pamoja na
kuombwa na Boaz ambaye mimi namuita
baba lakini haikuwa rahisi kwangu
kukubali kuzungumza nawe hata hivyo
baada ya kunieleza kwamba una jambo la
muhimu la kuzungumza nami nikakubali
kukusikiliza kwa hiyo mzee wangu
naomba tuokoe muda na tujielekeze
katika suala la msingi unalotaka
kunieleza” akasema Austin
“Nitakueleza Austin usijali.Nilianza
kwanza na utangulizi.Kwa ufupi tu ni
kwamba nimekutafuta kwa jambo moja
kubwa.Ninataka urejee Tanzania”
akasema Ernest na wote wakabaki
kimya.Baada ya muda Austin akatoa
kicheko kidogo na kusema
“Me
??..Tanzania??Hahahahaha...That’s
impossible Mr President.Jambo hilo
haliwezekani kabisa”
“Kwa nini isiwezekane Austin?
“Do you real want to know? Kuna
watu wachache walionifanya nikaichukia
nchi yangu.I sacrificed my life for the
 
SEHEMU YA 7

country I real love.Mara kadhaa
nimenusurika kifo nikifanya kazi za nchi
yangu. Haikuwa rahisi kupenya katika
maeneno yanayomilikiwa na Alshabaab
lakini nilipenya na kufanikiwa kugundua
mahala walikofichwa watu wetu na
nikakiongoza kikosi maalum kwenda
kuwakomboa lakini pamoja na hayo yote
niliyoyafanya bado malipo yake ni kutaka
kuuawa.Mheshimiwa rais umenitonesha
kidonda ambacho tayari kimekwisha pona
“ akasema Austin na tayari sura yake
ilibadilika
“Samahani sana Austin kwa
kuirudisha tena kumbu kumbu hii katika
kichwa chako lakini pamoja na hayo
narejea tena kukuomba Austin kwama
nakuhitaji urejee Tanzania .Kunak......”
“Stop mr President!! Akasema Austin
“Naomba
ufahamu
kabla
hujaendelea mimi si raia wa Tanzania kwa
sasa.Tayari nimechukua uraia wa nchi
nyingine.Huku nina maisha mazuri na
nimekwisha achana na kazi zangu za
zamani.Tafadhali mheshimiwa rais
ninaomba mniache niishi maisha
yangu.Sihitaji bughudha kwa sasa.Kama
hakuna lingine mzee naomba tumalize
niendelee na shughuli zangu.”akasema
Austin
“Austin naomba tafadhali usiondoke
kwanza.Kuna
jambo
nataka
tuongee.Pamoja na mambo yote
yaliyotokea na kupelekea ubadili uraia
lakini wewe bado ni mtanzania.Uraia huo
ni karatasi tu lakini mwili wako una damu
ya Tanzania.Umezaliwa hapa,wazazi wako
waliishi hapa,ndugu zako wako hapa so
you belong here.This is your home.I beg
you my son please come back home.”
Akasema Ernest
“mheshimiwa rais naomba usipoteze
muda wako kwa kujaribu kunishawishi
nirejee .Nimekwisha sema Tanzania sirudi
tena so save your time” akasema
Austin.Ernest akashusha pumzi na kusema
“ Austin hapa mbele yangu ninalo
faili lenye mambo yote yanayokuhusu
wewe.Taarifa zako nyingi ziko
humu.Usiniulize nimezipataje kwani mimi
ni rais wa nchi na ninaweza kupata taarifa
za mtu yeyote Yule ninayemtaka.”
Akasema Ernest na Austin akaonekana
kustuka kidogo.
“Austin pole sana kwa kuwapoteza
wazazi wako wote wawili .Baada ya
wazazi wako kufariki kwa ajali ya ndege
wewe ulibaki na jukumu la kumlea mdogo
wako Linda.Baada ya tukio lile la Somalia
ulitoweka na kumuacha Linda katika
wakati mgumu sana.Alianza kushirikiana
na magenge ya vijana wahuni na baadae
alianza kujishughulisha na biashara ya
dawa za kulevya.”
“Oh my God !!..akasema Austin na
sura yake ikabadilika
“Austin you abandoned you
sister.Kwa hiyo usistuke kwa mabadiliko
ya tabia ya mdogo wako”

Hapana
sikumtelekeza
Linda.Sikutaka kumueleza mahala nilipo
kwa ajili ya usalama wake.Kama
angefahamu mahala nilipo asingekuwa hai
hadi leo hii.Hata hivyo nilimuachia mali
nyingi,utajiri wote wa wazazi waliotuachia
alibaki nao.Mali zangu zote alibaki
nazo.Hakupaswa kujiingiza katika mambo
hayo machafu” akasema Austin na
kuinamisha
kichwa.Alionekana
kuchomwa sana na suala lile.
 
SEHEMU YA 8

Austin !! akaita rais na Austin
akainua kichwa.
“ taarifa hii najua imekuumiza lakini
naomba upige moyo konde kwa hili
nitakalokwambia ambalo naamini
litakuumiza zaidi”
“ Don’t tell me she’s dead” akasema
Austin”
“ Hapana Austin mdogo wako
hajafariki yuko hai bado lakini kwa taarifa
tulizonazo ni kwamba Linda kwa sasa
anatumikia kifungo cha miaka kumi na
tano nchini China baada ya kukamatwa
akijaribu kuingiza dawa za kulevya nchini
humo.”
“ Ouh my God!! Akasema Austin na
kuinamisha kichwa
“ I know it hurt Austin but you have
to be strong.Sasa nisikilize kwa makini
Austin.Ninao uwezo wa kumuondoa ndugu
yako toka katika kifungo hicho
anachokitumikia” akasema Austin
“ Please help her Mr President”
akasema Austin na macho yake
yalionekana kulengwa na machozi
“ Kama nilivyokueleza kuwa uwezo
wa kumsaidia ninao lakini nitafanya hivyo
pale tu nawe utakapokubali kunisaidia”
Austin akafikiri kidogo na kusema
“ Unahitaji nikusaidie nini ?
“ Come back home.Kuna kazi ambayo
nataka kukupa.Ni kazi binafsi na ambayo
nina uhakika ni wewe pekee unayeweza
kuifanya kikamilifu.Nakuahidi kukupatia
ulinzi na chochote kile utakachohitaji.Ni
juu yako sasa kuamua ni kitu gani hasa
unakihitaji”
Austin akafikiri kwa muda na
kusema
“ Mheshimiwa rais sina cha kuamua
kwani tayari umekwiswha nifunga mikono
.Nitakuja Dar es salaam kuifanya kazi yako
kwa ajili ya kumsaidia mdogo wangu
lakini naomba uniahidi kuwa baada ya
kazi yako kukamilika utaniacha niondoke
zangu nikaendelee na maisha yangu”
“ Nakuahidi hivyo Austin.Mara tu
kazi yangu itakapokamilika utakwenda
kuendelea na maisha yako”
“ Ahsante mheshmiwa rais.Lini
unanihitaji Tanzania ? Lini mchakato wa
kumtoa dada yangu gerezani
utaanza?Ningependa nitakapoanza kazi
yako tayari dada yangu awe ametoka
gerezani
au
anakaribia
kutoka.Kitukingine ambacho nataka
nikubaliane nawe ni kwamba baada ya
kutoka gerezani sitaki Linda arejee
Tanzania nataka umtafutie makazi katika
nchi nyingine akaishi maisha mazuri.Huko
afunguliwe biashara au atafutiwe kazi
nzuri aifanye.Tunakubaliana katika hilo?
Akauliza Austin
“ Hilo ni suala dogo sana kwangu
Austin.Ninakuahidi kufanya kama
unavyotaka.Kuhusu lini ninakuhitaji
Tanzania,ninakuhitaji
haraka
sana.Nitatuma ndege sasa hivi ije
ikuchuke ili hadi usiku wa leo uwe
umefika hapa Dar es salam.”
“ Sawa mheshimiwa rais.Nitakuja
Tanzania”
“ Austin nashukuru sana kwa
kunikubalia ombi langu .Nakuahidi kila
nilichokuahidi nitakitekeleza.”
“ Mr President I’m doing this for my
sister so you don’t have to thank me .Kama
si yeye katu nisingekuja Tanzania”
 
SEHEMU YA 9

Pamoja na hayo bado nakushukuru
pia Austin”
“Mheshimiwa
rais
naomba
nikukumbushe kuwa ujio wangu Tanzania
ni siri kati yangu nawe.Watu waliotaka
kuniua wakati ule bado wapo na wana
nguvu kwa hiyo wakifahamu kuwa niko
nchini lazima maisha yangu yatakuwa
hatarini .Nadhani umenielewa.”
“ Nimekuelewa Austin na niko
makini sana kwa hilo.Usihofu utakuwa
salama”
“ Ahsante mheshimiwa rais”
“ Ahsante Austin utataarifiwa na
msaidizi wangu mara tu ndege
itakapowasili hapo afrika kusini.”
Akasema Ernest na kuagana na Austin.
“ Thank you Mukasha .Wewe ndiye
uliyefanya hili jambo likafanikiwa”
“ Ahsante mheshimiwa rais” akajibu
Mukasha huku naye akitabasamu
“ By the way Mr President nimesikia
ukimuahidi Austin kumsaidia kumtoa
mdogo wake gerezani.Are you going to do
that? Akauliza Mukasha
“ Im a man of my words so Yes I’m
going to do that.NItamsaidia mdogo wake
Austin kutoka gerezani, kwa sasa jambo
ninalolihitaji ni kuonana na balozi wa
China hapa nchini jioni ya leo kwa hiyo
andaa kikao .Halafu jioni ya leo pia nataka
kuonana na mkuu wa magereza.Vikao
vyote hivi ni vya siri na vitafanyikia pale
hotelini kwangu.Jambo lingine ambalo
nataka ulifanye ni kuandaa makazi ya
Austin kwa muda wote atakaokuwa hapa
nchini.Ninayo nyumba yangu kule Mikinda
ambayo ilikuwa imekodishwa na ubalozi
wa Denmark lakini kwa sasa haikaliwi na
mtu baada ya balozi kuondoka .Ni nyumba
nzuri ya kisasa ambayo naamini
itamfaa.Ina ghorofa mbili,ina nafasi ya
kutosha ,ina kila kitu ndani,bwawa la
kuogelea ,chumba cha mazoezi na hata
mfumo wake wa usalama ni mkubwa na
wa kisasa.Nitahitaji vile vile gari tatu za
kifahari zikae mle ndani ambazo Austin
atazitumia.Nitampigia simu Hussein
magari, tutachukua magari hayo
kwake.Yeye huuza magari mazuri mapya
na ya kisasa.Vitu vingine anavyovihitaji
atakuja kutueleza pindi akifika huku”
akasema rais na kuongozana na Mukasha
wakatoka ndani ya kile chumba.
*****************
Hali ya Dr Marcelo iliwaridhisha
madaktari kuwa hakuhitajika tena kuwa
katika kile chumba cha wagonjwa walio
katika hatari.Maendeleo yake yalitia moyo
sana na hivyo akatolewa na kupelekwa
katika chumba kingine.
Mchana huu ndani ya chumba
walikuwemo baadhi ya ndugu jamaa na
marafiki waliokuja kumjulia hali.Miongoni
mwa watu waliokuwemi mle chumbani
alikuwamo Daniel.Pamoja na Dr Marcelo
kuonyesha maendeleo mazuri lakini bado
hakuwa anaweza kuzungumza chochote
.Madkatari waliendelea na uchunguzi wa
kubaini kitu gani kilichosababisha Dr
Marcelo akashindwa kuzungumza licha ya
hali yake kuendelea vizuri.Aliweza kusikia
kila pale alipoitwa na hata kutabasamu
lakini hakuweza kuongea.
Muda uliowekwa kwa ajili ya
kuwatazama wagonjwa ulikaribia
kumalizika hivyo wengi wa waliokuja
kuwatembelea wagonjwa walianza
kuondoka.Watu walipopungua mle
 
SEHEMU YA 10


chumbani Dr Marcelo akamfanyia ishara
Daniel asogee karibu.Katika meza
iliyokuwa karibu na kitanda kulikuwa na
kijitabu kidogo na kalamu akaomba
apatiwe akachana karatasi na kuandika
“ Monica yuko wapi?
Daniel naye akaandika
“Amechelewa mchana huu atakuja
jioni”
Dr Marcelo akaichukua karatasi na
kuandika
“ Wasiliana naye mwambie
namuhitaji sasa hivi afike hapa hospitali”
Baada ya Daniel kuusoma ujumbe
ule wa Marcelo akatoka akachukua simu
yake kwa lengo la kumpigia Monica lakini
kabla hajapiga Julieth dada wa Marcelo
akatokea.
“ Marcelo anahitaji nini? Akauliza
Julieth na Daniel akampatia ile karatasi
aisome ,akasogea pemeni na kumpigia
simu Monica
“ Hallow Daniel habari yako?
Akasema Monica
“Nzuri Monica.Uko wapi mida hii?
Mbona hujafika hospitali kumtazama
Marcelo?
“ Nimeshindwa kufika mchana huu
nimepata safari ya dharura hivyo niko
katika maandalizi.Anaendeleaje?
“ Maendeleo yake si mabaya ila bado
hajaweza
kuzungumza.Madaktari
wanahisi labda ni tatizo la kisaikolojia na
wanashauri kwamba awe karibu na watu
wake wa karibu muda mwingi hii inaweza
kumsaidia akaweza kuzungumza
tena.Nimewasiliana naye muda mfupi
uliopita kwa njia ya maandishi na
amenisisitiza kwamba anahitaji sana
kukuona sasa hivi.” Akasema
Daniel.Monica akatafakari kidogo halafu
akasema
“ Daniel bado uko hapo hospitali?
“ Ndiyo bado niko hapa”
“ Sawa ninakuja hapo muda si mrefu”
akasema Monica
Mara tu alipomaliza kuzungumza na
Daniel ,akavaa haraka haraka akaingia
garini na kuondoka kuelekea
hospitali.Aliwasili hospitali na kukuta
tayari muda wa kutazama wagonjwa
umekwisha,akashuka garini na kuelekea
moja kwa moja katika chumba
alimohamishiwa Marcelo.Nje ya chumba
hicho akamkuta Daniel akimsubiri.
“ Ahsante kwa kuja Monica.Marcelo
anakuhitaji sana”akasema Daniel.
“ Vipi maendeleo yake?
“ Ni kama vile nilivyokueleza simuni
“ akasema Daniel na kuufungua mlango
wakaingia ndani .Uso wa Dr Marcelo
ukajenga tabasamu baada ya kumuona
Monica.Julieth na Daniel wakatazamana
wakatabasamu
“ How are you Marcelo? Akauliza
Monica huku akisogea karibu na kitanda
cha Dr Marcelo ambaye alimtazama bila
kutamka chochote.
“ Usijali Marcelo utapona tu.”
Akasema Monica huku akionekana
kulengwa na machozi.Dr Marcelo
akamfanyia ishara Daniel ampatie kalamu
na karatasi akaandika ujumbe Fulani na
kumpatia Monica.
“ Soma kwa siri”
ndivyo kichwa cha
ujumbe ule kilivyosomeka.Baada ya
kichwa kile ujumbe ukaendelea.
“ Monica fanya lolote uwezalo unitoe
hapa hospitali kwani ninataka kuuawa.One
of them visited me last night.Please do it
 
Ndio maana story ikianza huwa ikimbilii kusoma, hadi ifike mbele halaf ndio nianza sasa [emoji56] saivi ntililika nayo tu,

Asante mkuu LEGE, pia pongezi nyingi kwa mwandishi wa story!
 
Hee paouch yake anaiheshim
Na kuitunza kama ukoma
Hahahaaaa Peniela kugawa ilikuwa ni kazi aliyosomea, alitengenezwa, na alikuwa mtamu balaa, ukigusa hutoki. Japo ni story lakini nilikuwa nawaonea wivu waliokuwa wanamkula, hahahahaa. Penny ni noma sana.
 
  • Thanks
Reactions: Oxx
Back
Top Bottom