QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

h
LEGE sema huo waya bei gani mkuu tujichange, haiwezekani tukose burudani kwasababu ya waya. Sio mbaya tukikuwezesha, maana kazi unayoifanya ya kutupatia hii burudani sio ndogo aisee.
ahahaha mkuu nishaununua now ndio nafika home hapa naweka mambo sawa then najitahidi kabla sijafumba jicho niweke kitu japo cha kuonyesha kuwa tupo pamoja wakuu
 
h

ahahaha mkuu nishaununua now ndio nafika home hapa naweka mambo sawa then najitahidi kabla sijafumba jicho niweke kitu japo cha kuonyesha kuwa tupo pamoja wakuu
Sawa mkuu, tunasubiri.

Pole na majukumu.
 
SEHEMU YA 61


lakini awali ya yote kuna kitu nataka
kuuliza”
“ Uliza Monica”
“ jana tulipofanya mapenzi
hukutumia kinga.Una hakika uko salama?
David Zumo akatabasamu na kusema
“ Nilitegemea ungeniuliza swali
kama hilo.Naomba nikuhakikishie
kwamba usiku wa jana ni usiku wa
kwanza kwangu kufanya mapenzi na
mwanamke ambaye si mke wangu.Toka
nimefunga ndoa na Pauline sijawahi
kujihusisha na mahusiano na mwanamke
mwingine yoyote zaidi ya mke
wangu.Mimi na Pauline tunapendana sana
na tunaaminiana mno” akasema David
wakatazamana kwa muda kisha David
akasema
“ Monica ni wakati wa kujiandaa
kuna mgeni atakuja kuungana nasi hapa
leo.Ukishaoga na kujiandaa pale ukutani
kuna vitufe vitano,utabonyeza kitufe
namba moja na watakuja watumishi
kukuhudumia kisha baada ya hapo
tutaungana kwa mlo wa asubuhi akasema
David na kutoka mle chumbani akampa
nafasi Monica kujiandaa
“ Tayari maisha yangu
yamebadilika.Monica wa jana si Monica
wa leo.Ama kweli maisha yana maajabu
makubwa.Sikuwahi kuota kama siku moja
nitaishi maisha makubwa kama haya”
akawaza Monica na kuingia bafuni
kuoga.Alipomaliza kuoga akafuata
maelekezo aliyopewa na David
akabonyeza kitufe namba moja na
haikumalizika dakika moja wakaingia
wanawake zaidi ya sita kwa ajili ya
kumuandaa Monica.Kila mmoja alikuwa
na kazi yake.
 
SEHEMU YA 62



DAR ES SALAAM – TANZANIA
Zaidi ya dakika nne sasa rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania Ernest
Mkasa alikuwa amesimama katika dirisha
la chumba chake akitazama nje.Agatha
mke wake akamfuata taratibu
“ Ernest darling” akasema na
kumshika kiunoni.
“ Kuna jambo gani linakusumbua?
Nimekuona kwa siku mbili tatu
umebadilika sana na ninakufahamu vizuri
lazima kuna kitu kinakisumbua akili
yako.Niambie tafadhali kama kuna kitu
kinakuumiza kichwa .”
Ernest akageuka na kumtazama
mkewe akamshika mabegani na kusema
“ hakuna tatizo lolote Agatha,niko
kawaida.Kwa leo nina kikao cha dharura
cha baraza la mawaziri,kuna jambo la
dharura la kujadili ndiyo maana unaniona
katika hali hii.Kikao hakitakuwa chepesi”
akasema Ernest na mke wake akaonekana
kustuka
“ Kuna mambo gani ya dharura
mnakwenda kujadili katika kikao hicho?
Akauliza Agatha
“ Siwezi kukueleza kwa sasa hadi
hapo baadae” akasema Ernest na mke
wake akamtazama kwa macho
makali.Hakuonyesha kufurahishwa na
jibu lile
“ Ernest toka lini umeanza kunificha
mambo? Kila kinachoendelea katika ofisi
yako umekuwa unanitaarifu na kuniomba
ushauri lakini nashangazwa leo umeamua
kunificha mambo hayo ya dharura
mnayokwenda kuyajadili.Au umepata
mshauri mwingine unayemuamini zaidi
yangu? Akauliza Agatha

Agatha
si
hivyo
unavyodhani.Nitaongea nawe baadae kwa
kirefu lakini kwa sasa ngoja niwahi
ofisini” akasema Ernest na kuchukua
mkoba wake akatoka na kumuacha mke
wake akishangaa
“ This is strange!!.Whats going on?
Haijawahi kutokea hata mara moja Ernest
akagoma kunieleza jambo.Kabla ya kikao
chochote anachokwenda lazima mimi na
yeye tukae tujadili lakini leo amegoma
kabisa .Kuna kitu kinaendelea ambacho
nahitaji kukifahamu” akawaza Agatha na
kuchukua simu yake akazitafuta namba za
makamu wa rais akampigia.
“ hallo Madam first lady” akasema
Muhsin
“ Muhsin ,hukunipa mrejesho
wowote kuhusu lile jambo nililokuomba
ulifuatilie jana” akasema Agatha
“ Agatha sikuona sababu ya kukupa
mrejesho kwa sababu vijana niliowatuma
hawakuweza
kugundua
jambo
lolote.Katika ule muda uliosema kuna
makabidhiano yatafanyika,kuna gari
 
SEHEMU YA 63


liliingia katika ubalozi wa Chia lakini
ililikuwa ni gari la mizigo na inaonekana
kuna mzigo uliwasilishwa pale
ubalozini.MUkasha naye aliwasili hapo
ubalozini lakini alikuwa peke yake na
baada ya muda akatoka akiwa peke yake ”
“ Are you sure Muhsin? Akauliza
Agatha
“ Ndiyo Agatha.Ninawamini vijana
niliowatuma katika kazi hiyo”
Agatha akafikiri kidogo kisha
akasema
“ Ok Muhsin una taarifa ya
kinachokwenda kujadiliwa katika kikao
cha dharura cha baraza la mawaziri
alichokiitisha rais leo?
“ hapana Agatha,sina taarifa zozote
kuhusu yanayokwedna kujadiliwa katika
kiako hicho.” Akasema Muhsin na ukimya
mfupi ukapita,Agatha akasema
“ Muhsin lakini jitahidi uwe
mchunguzi wa kila jambo Kwa sasa tuko
katika hatua muhimu sana ya kufanikisha
mambo makubwa kwa hiyo hatupaswi
kulala.Kila mtu acheze nafasi yake
vizuri.Utanieleza kitakachojadiliwa katika
hicho kikao kwani Ernest amegoma kabisa
kunieleza chochote”
“ sawa madam nitakujulisha usihofu
“ akasema muhsin,Agatha akakata simu.
“Ninamfahamu vizuri Ernest
kuliko mtu yeyote ,kuna jambo zito
linalomsumbua na analifanya siri.Nitajua
tu kinachoendelea “akasema Agatha.
Ernest mkasa aliingia ofisini kwake
lakini alihisi kichwa chake kizito kufanya
kazi yoyote.
“ What I’m going to do today,i
s
very dangerous but I have to do it because
it’s the right thing .Nimechoshwa na
kupelekwa pelekwa kama gari
bovu.Maneno aliyoyaongea Austin jana
yalinichoma sana na siwezi tena
kuendelea kuwa daraja la watu wachache
kufanikisha mipango yao haramu.Lazima
nisimame kama rais niwapiganie
wananchi
wangu
wanyonge
walionichagua.Kwa kuanzia muswada wa
haki za binadamu ninaufuta kuanzia
leo.Nafahamu kitendo cha kuufuta
muswada huo kutawastua sana hawa watu
na wataanzisha mapambano na mimi na
kwa namna walivyo na nguvu ninaweza
kuuawa kama alivyouawa rais
aliyenitangulia .Alikataa kushiriki katika
mipango yao na kilichofuata
wakamuua.I’m so scared.These people are
monsters”akawaza Ernest na kufungua
kompyuta yake akafungua sehemu
alikohifadhi picha za Monica alizozitoa
mtandaoni akaanza kuzitazama moja
baada ya nyingine akajikuta akitabasamu.
“Ninaomba majibu yatoke na
kunihakikishia kuwa Monica ni
mwanangu kwa sababu kile
ninachokifanya sasa hivi ni kwa ajili
yake.Kama atakuwa kweli ni mwanangu
nitamlinda kwa kila namna
nitakavyoweza kwani wabaya wangu
wakifahamu kuwa ni mwanangu basi
watamtumia kama fimbo ya
kunipigia.Lakini sina wasiwasi kwani
Austine yupo na atakubali kubaki
Tanzania kwani yale yote aliyoyataka
nimeyatekeleza.Nimetokea kumuamini
sana Austine ni kijana mwenye akili nyingi
na mwenye ujuzi wa hali ya juu.Alitaka
kuuliwa kwa sababu tayari alikwisha
kuwa kikwazo kwa watu na hasa
Alberto’s.Sifahamu aligundua nini hadi
wakataka kumuua lakini naamini ni jambo
zito.Austin amenikosha sana kwa namna
anavyojiamini”
 
SEHEMU YA 64


*******************
Austin aliwasili salama nyumbani
kwake akifungua mlango wa gari
akamshusha Dr Marcelo na kumsaidia
kutembea hadi sebuleni.
“Damn ! you are so heavy
!!”akasema Austin na kumsaidia Marcelo
kuketi sofani .Akaenda jikoni na kurejea
na chupa mbili za maji moja akampatia
Marcelo.
“Thank you”akasema Marcelo.
“You are welcome “akajibu Austin
huku akifungua chupa na kunywa
maji.Marcelo naye akanywa maji halafu
Austin akauliza ,
“How do you feel?unasikia maumivu
yoyote?”
“Ndiyo ninahisi maumivu katika zile
sehemu
zilizoshonwa”akasema
Marcelo.Austin akainuka akaenda
chumbani na kurejea na paketi ya dawa.
“Kunywa hizo zitakusaidia
kupunguza maumivu wakati utaratibu wa
kumpata daktari ukiendelea”akasema
Austin.
Marcelo akamtazama Austin kwa makini
na kuuliza ,
“Who are you?
“I’m Austin”
Marcelo akamtazama Austin kwa
makini na kusema,
“Nafurahi kukufahamu Austin
lakini nahitaji kufahamu kwanini niko
hapa?”
“Marcelo sina jibu la kukupa kwa
swali lako.Kazi yangu niliyopewa ilikuwa
kukutoa hospitali na kukuleta hapa kwa
hiyo sifahamu chochote kuhusu
wewe.Nitafurahi endapo hutaniuliza swali
lolote kama hilo bali usubiri mtu
aliyenituma kazi atakapofika naamini
utakuwa na muda mzuri wa kuzungumza
naye na kumuuliza maswali.Kwa sasa
naomba nikupeleke ukapumzike nina kazi
za kufanya”akasema Austin akamsaidia
Marcelo kunyanyuka akampeleka
kupumzika.
 
SEHEMU YA 65


“Kazi ya kwanza nimemaliza,sasa
nataka kutafuta namna nitavyo jenga
urafiki na Monica na kumfanya
aniamini”akawaza Austin.
“Kuna kitu kimoja ambacho
kinaweza kuniweka karibu na Monica
ambacho ni matindo.Nimesoma taarifa
zake jana usiku mtandaoni na kufahamu
Monica anamiliki kampuni ya kubuni
mitindo mavazi iliyojizolea umaarufu na
soko kubwa afrika mashariki.Kitu kingine
nilichokifahamu kuhusu Monica ukiacha
mitindo ni mtu anayependa sana kujitoa
kwa jamii.Ana taasisi yake ya kusaidia
watu wenye matatizo hususani watoto na
wazee wasiojiweza.Hizo ni sehemu mbili
pekee ambazo naweza kuzitumia
kutengeneza urafiki na Monica. Aidha
mitindo au kusaidia jamii” akachukua
chupa yake ya maji akamalizia maji yote
yaliyokuwamo na kuendelea kutafakari
“Sina utaalamu wowote na masuala
ya mitindo inaweza ikanichukua muda
kidogo kujifunza na kuifahamu vyema fani
hii.Sina muda huo wa kujifunza nadhani
niachane na mitindo na niingie katika
masuala ya kujitoa kwa jamii.Hata hivyo
nikiamua niingie kwa kutumia upande
huo wa kusaidia jamii itanilazimu niwe na
kiasi kikubwa cha pesa.Nitazungumza na
rais atakapokuja leo usiku aniwezeshe
kiasi cha kutosha cha pesa .Kazi hiyo ya
kujenga urafiki na Monica nitaianza rasmi
kesho ila kwa siku ya leo nataka kwenda
kufanya manunuzi ya vitu mbali mbali
muhimu nitakavyovihitaji kama vile
kompyuta zenye kasi na uwezo
mkubwa,nahitaji mavazi mazuri ya
gharama ili kujiweka nadhifu kila
mara,nahitaji simu kadhaa kwa
mawasiliano.Kwa ujumla kuna vitu vingi
vya lazima nitakavyovihitaji.” Akawaza
Austin na kulikumbuka tukio lililotokea
hospitali ya St Lucia.
“ Naamini umakini ulikuwa mkubwa
na sikuacha chochote kinachoweza
kunitambulisha kama mhusika wa tukio
lile.Naamini hata wakifanya uchunguzi
hawataweza kunipata” akawaza Austin
 
SEHEMU YA 66


KINSHASA – DRC
“ Monica samahani kama nitakufuru
lakini lazima nikiri kuwa Mungu ana
upendeleo .Kuna watu amewapendelea
uzuri wa kipeke kabisa.Mmoja wa watu
hao ni wewe .Una uzuri ambao hauelezeki
kwa maneno.Itoshe tu kusema kwamba
uzuri wako ni wa kipekee.Nitamshukuru
Mungu kwa siku zote kwa kunikutanisha
nawe.” Akasema David
“ Ahsante sana David lakini Mungu
hana upendeleo .Kwake sote ni sawa
hakuna mzuri wala mbaya.” Akasema
Monica .David akatabasamu akamshika
mkono wakaelekea katika chumba cha
chakula kwa ajili ya kupata kifungua
kinywa.Kabla hawajaanza kupata kifungua
kinywa mlango ukagongwa wakaingia
watu wanne walioonekana ni wana
usalama na nyuma yao akafuata Pauline
mke wa David Zumo.Monica alihisi aibu
lakini Pauline alionekana kuwa
mchangamfu na uso wenye
tabasamu.Akasalimiana kwanza na David
Zumo halafu akamfuata Monica
wakasalimiana na wote wakajumuika kwa
mlo ule wa asubuhi.Baada ya kupata
kifungua kinywa wakatoka wakaelekea
katika bustani nzuri iliyokuwa pembeni ya
ziwa dogo.Ulinzi ulikuwa mkali sana
kulizunguka jumba lile la kifahari la David
huku eneo lote likiwa na ukimya mkubwa
sana.Ni sauti za ndege ndizo
zilisikika.Waliketi katika viti vya kifahari
vyenye nakshi za dhahabu
“ Monica napenda kutumia fursa hii
kukukaribisha tena kwa mara nyingine
katika himaya hii ya kifalme.Ninasema ya
kifalme kwani muda si mrefu sana
nitatawazwa kuwa mfalme wa kwanza wa
Congo.Nadhani tayari nimekwisha kueleza
kuhusu jambo hii.” Akasema David huku
akitabasamu na kumgeukia mkewe
Pauline
“ Pauline leo ni siku ya furaha kubwa
kwetu kwani hatimaye maombi yetu
yamejibiwa .Monica amekubali ombi la
kuolewa nami.”akasema David na kwa
furaha Pauline akainuka na kumkumbatia
Monica kwa furaha
“ Ahsante Monica .Ahsante sana kwa
uamuzi
wako
huu
wa
busara.Nakuhakikishia hautajutia uamuzi
huu uloufanya.Binafsi nimetokea
kukupenda sana na nimeridhia kwa moyo
 
SEHEMU YA 67


mweupe uwe mke wa pili.Ninampenda
David sana na ninataka awe na furaha
katika maisha yake na mimi sina uwezo
wa kukamilisha furaha yake kama
nilivyokueleza jana.Kuja kwako kutaifufua
upya furaha yetu.Nakuahidi tutaishi kwa
amani na upendo kwani jambo hili ni mimi
ndiye niliyekuwa nalihitaji sana” akasema
Pauline huku machozi ya furaha
yakimtoka
“ Kwa niaba ya Pauline “ akasema
Daniel
“ Napenda nikushukuru sana Monica
kwa kukubali ombi letu.Kama alivyosema
Pauline maisha yetu yatakuwa mazuri na
yenye furaha zaidi na Mungu akijalia
kupitia kwako tunaweza kumpata mrithi
wangu .Kwa hiyo Monica wewe ni mtu
muhimu sana kwetu na kutokana na
umuhimu huo hatuna tena haja ya
kuendelea kuvuta muda zaidi.Taratibu za
ndoa hii zitaanza mara moja .Kesho
nitakuwa na maongezi na baraza la wazee
wa Congo na nitawafahamisha kuhusu
suala hili.Baada ya hapo nitatuma rasmi
ujumbe Tanzania kwa wazazi wako kuja
kuanza taratibu za uchumba na baada ya
hapo tutatangaza ndoa.Sitaki jambo hili
lichukue muda mrefu toka sasa.Nataka
nitakapotawazwa kuwa mfalme wa
kwanza wa Congo tayari tuwe tumefunga
ndoa.Kuhusiana na sherehe za ndoa hiyo
nitamuachia Pauline kwani yeye ni
mtaalamu sana katika mambo hayo”
akasema David.Uso wa Monica ulionyesha
wasi wasi kidogo.
“ Monica uso wako unaonyesha wasi
wasi ,usiogope mpenzi kila kitu kitakuwa
kizuri.Hakuna
kitakachoharibika”
akasema Pauline
“ Pauline kuna kitu kinanitatiza
kidogo.Ninajiuliza je raia wa Congo
watanipokea na kunikubali?
David akatabasamu na kusema
“ Usihofu Monica.Watu wangu
wananipenda na wanapenda ila
ninachokipenda mkuu wo kwa hiyo hata
wewe watakupenda na kukuheshimu
kama malkia wao” akasema David na wote
watatu wakatabasamu wakaendelea na
maongezi yaliyokuwa marefu yenye
furaha yaliyotawaliwa na vicheko
 
SEHEMU YA 68


DAR ES SALAAM – ANZANIA
Agatha mkasa mke wa rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania akiwa
ofisini kwake amejiegemeza kitini huku
mkono wake mmoja ukiwa shavuni,simu
yake ikaita akaichukua haraka na
kutazama mpigaji alikuwa ni makamu wa
rais Muhsin Abdulkareem.Haraka haraka
akabonyeza kitufe cha kupokelea
“ Hallow” akasema
“ Agatha nimekupigia kukujulisha
kuwa kikao kimemalizika muda si mrefu
na kilichotokea huwezi kuamini.Kila mtu
hapa bado yuko katika mshangao ”
“ Nini kimetokea Muhsin? Akauliza
Agatha kwa wasi wasi
“ Rais ameufuta ule muswada wa
haki za binadamu uliotarajiwa
kuwasilishwa bungeni katika kikao
kijacho”
“ No ! that’s not true!! He cant do that
!! Akasema Agatha
“ It’s true Agatha.Kulikuwa na
mvutano mkali sana na kama ujuavyo
karibu baraza lote la mawaziri tuliubariki
muswada ule kwa hiyo tulijitahidi kwa
kila namna tuwezavyo kupinga maamuzi
ya rais lakini yeye ndiye mwenye kauli ya
mwisho na tukajikuta tukishindwa
kumzuia asiufute.” akasema Muhsin
“ Bado siamini kama Ernest anaweza
akafanya kitu kama hicho.Tafadhali
Muhsin
nieleze
ukweli.Ernest
ninayemfahamu mimi hawezi kufanya
jambo hilo.”
“ Ni vigumu kuamini Agatha lakini
huo ndio ukweli wa kilichotokea.Mpaka
sasa hakuna anayeamini lakini hicho
ndicho kilichotokea.Ernest wa leo siye
Yule mwenzetu tunayemfahamu.Amekuwa
ni mtu mwingine tofauti kabisa.Tumepata
pigo Agatha.Tumerudishwa nyuma hatua
ishirini” akasema Muhsin.Uso wa Agatha
ulishindwa kuzuia kuonyesha mshangao
na hasira alizopata kutokana na taarifa ile
ya makamu wa rais.
“ This is unbelievable.Why he did
that? Nini kimemuingia Ernest na
kumfanya achukue maamuzi haya ? Nani
kamshawishi afanye hivi? He betrayed
us.!! Dah !! ni vigumu sana kuamini”
akasema Agatha
 
SEHEMU YA 69


Agatha nimekupigia kukupa taarifa
hizo ili uwataarifu wakuu kilichotokea.”
akasema Muhsin
“ What am I going to tell them?
Akauliza Agatha
“ The truth..tell them everything”
akajibu Muhsin na kumfanya Agatha avute
pumzi ndefu na kusema
“ I think you know what happens to
traitors”
“ Yes I know.Ernest must die” akajibu
Muhsin.
“ Na hii ina maana kwamba una
nafasi kubwa ya kushika nafasi ya urais
pindi Ernest akiondolewa”
“ Yes I know that” akajibu Muhsin
“ Ouh Ernest ,Ernest nani
amemshawishi akafanya jambo hili la
kipuuzi wakati anajua kabisa
kitakachotokea.? Akawaza Agatha na
katika macho yake ikaonekana michirizi
ya machozi
“ Muhsin ahsante kwa
taarifa.Tutawasiliana baadae” akasema
Agatha na kukata simu.Alihisi
kuchanganyikiwa
“ Whats going on? Kitu gani au nani
amembadilisha Ernest? Naamini lazima
ipo sababu kubwa na lazima niijue.Kwa
hiki alichokifanya Ernest kitaifanya nchi
itikisike kwani amevunja kiapo chake na
ametusaliti.Ninampenda Ernest ,nimetoka
naye mbali lakini kwa hili alilolifanya hata
mimi sintakuwa na huruma naye.Hatuna
huruma kwa wasaliti.Nguvu kubwa
imetumika katika kuhakikisha sheria ile
inafika bungeni na kupitishwa na Ernest
ameshiriki katika mchakato wake toka
mwanzo,lakini kitendo cha kutugeuka
katika hatua za mwishoni ni sawa na
uhaini na adhabu ya msaliti yeyote
anayepatikana miongoni mwetu ni
kifo.Ernest amekitafuta kifo chake
mwenyewe na hakuna namna ya
kumsaidia,he must die.Nchi hii tayari
tumewekeza nguvu kubwa na kufanikiwa
kushika zile sehemu zote za muhimu na
muswada huu ulikuwa na umuhimu
mkubwa sana kwetu lakini Ernest tayari
ameonekana kuwa kikwazo .Hatuhitaji
vikwazo vyovyote katika kutekeleza
malengo yetu kwa hiyo Ernest lazima
aondoke” akawaza Agatha akiwa na hasira
zisizoelezeka
 
SEHEMU YA 70


aada ya kumaliza kikao cha
dharura cha baraza la mawaziri,rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania Ernest
Mkasa akaendelea na ratiba yake ya siku
ambapo alikutana na mabalozi wa mataifa
mbaimbali pamoja na wageni wengine
waliomtembelea ikulu.Rais alimuagiza
mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu
asambaze taarifa katika vyombo vyote vya
habari ili viwatangazie watanzania kuwa
atalihutubia taifa ifikapo saa mbili kamili
za usiku.
Ilipofika saa moja za jioni rais
akarejea katika makazi yake kwa ajili ya
kufanya maandalizi ya hotuba atakayoitoa
kwa taifa usiku.Hakutaka mtu mwingine
yeyote amuandalie hotuba kama
ilivyozoelekea ,hakutaka jambo analotaka
kulieleza livuje.Tayari mke wake bi
Agatha alikwisha rejea nyumbani kitambo
na toka aliporudi alikuwa amejifungia
chumbani .Ernest alipoingia chumbani
alimkuta mkewe anaongea na simu na
mara tu alipomuona mumewe,akakatisha
maongezi na kumtazama mumewe kwa
hasira.Walitazamana kwa sekunde kadhaa
bila kusemeshana halafu Ernest
akauvunja ukimya
“ Natumai tayari umekwisha sikia
kilichotokea”
Agatha akainuka akamsogelea
Ernest
“ What have you done Ernest?
Akauliza huku amekunja sura kwa
hasira.Ernest hakujibu kitu akabaki
anamtazama
“ What have you done you fool!!
Akasema Agatha na ghafla sura ya Ernest
ikabadiika.Akapandwa na hasira
“ Na iwe mwanzo na mwisho
kunidharau kiasi hiki “ akasema Ernest
kwa hasira
“ yes you are a fool Ernest.Kwa nini
umefanya jambo la kijinga kama hili?
Sikuwahi hata mara moja kufikiri kuwa
unaweza kuwa mjinga kiasi hiki.Nini
kimekubadilisha
Ernest?
Nani
amekudanganya?
 
MKUU NATAKASIKU 2 HIZI HASA BAADAE NIIFUNGIE KAZI TUIMALIZE KABISA SEASON YA 2.TATIZO KUBWA NI MDA MKUU NOW SAA 8 HII NA MORNING MAJUKUMU KAMA KAWA
Imekuwa fupi fupi tupiamo vingine tuhangaike navyo siku nzima
 
MKUU NATAKASIKU 2 HIZI HASA BAADAE NIIFUNGIE KAZI TUIMALIZE KABISA SEASON YA 2.TATIZO KUBWA NI MDA MKUU NOW SAA 8 HII NA MORNING MAJUKUMU KAMA KAWA
Asante mkuu kwa hii kitu, tuliimiss sana. Tunakuomba kama inawezekana ongeza ukubwa wa hivi vipande, vimekuwa vifupi sana siku hizi, halafu havienei kwenye page, huu mtindo haufurahishi.

Nimeona nitoe ya moyoni.

Yote kwa yote, story ni tamu na inazidi kukolea.
 
Back
Top Bottom