QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

Hebu tulieni kwanza, kuna wengine walijiita Jaji Elibariki kwenye Peniela, kilichotokea wote walijuta.
Mkuu umesababisha nicheke kwa sauti hadi jiran yangu kanishangaaa[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
SEHEMU YA 115




ni wangu .Baada ya kukutana na Austin
ndipo nilipopata ujasiri wa kuachana na
kupambana
na
Alberto’s.Nataka
mwanangu na watoto wake waishi katika
nchi yenye neema iliyobarikiwa na si
katika nchi yenye laana.Kwa hiyo mimi na
Austin tumeungana na tunapigana vita hii
kwa pamoja.Tunataka kuwaondoa
Alberto’s hapa nchini na kuiondoa kabisa
mizizi yake yote.Nilipopokea uongozi ,taifa
hili lilikuwa imara kama lilivyoachwa na
waasisi wetu kwa hiyo sitaki kulibomoa
kwa mikono yangu kwa hiyo nitapambana
kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa ile
ile iliyoachwa na wazee wetu.Mukasha hili
si jambo jepesi.Ni jambo la hatari kubwa
kwani hawa jamaa ni watu hatari kama
nilivyokueleza na wanaweza wakanitoa
uhai sekunde yoyote lakini pamoja na
hatari hiyo iliyopo nimeamua kupambana
nao.” Akanyamaza.Mukasha akahisi joto
akavua koti.Ernest akaendelea
“ Mukasha nimekueleza haya yote wa
sababu wewe ni mmoja wa watu
wachache ninaowamini .Pili ninataa uwe
mshirika wangu katika mapambano kwani
ninafikiria kukuteua kuwa waziri mkuu
mpya wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania”
Kauli ile ya Ernest ikamstua sana
Mukasha akasimama na kumtazama rais
kwa macho ya woga
“ hapana mheshimiwa rais !!
akasema Mukasha
“ Mheshimiwa rais mimi sistahili
nafasi hiyo.Ahsante kwa kuniamini na
kunipa heshima hii kubwa lakini
nakuomba utafute mtu mwingine anayefaa
.Mimi naomba uniache katika nafasi hii
niliyo nayo sasa “ akasema Mukasha
.Ernest akavuta sehemu ya mwisho ya
sigara akapuliza moshi hewani na
kumtazama Mukasha
“ Mukasha hakuna mtu mwingine
ambaye ninamuamini kwa sasa kumpa
nafasi hiyo ya uwaziri mkuu zaidi
yako.Nahitaji mtu wa kufanya naye kazi
,nahitaji mtu wa kusaidiana naye
kuisafisha nchi hii,na mtu huyo ni
wewe.Endapo utakataa nafasi hii
utanifanya niwe na mashaka labda
pengine nawe unashirikiana nao kwa siri”
“ mheshimiwa rais naomba
usinifikirie hivyo tafadhali.Watu hao
siwafahamu na leo ni mara ya kwanza
kuwasikia toka kwako.Kinachonifanya
nikatae ni kwamba nafasi hii ni kubwa
mno kwangu.Sitaki kukuangusha
mheshimiwa rais.Niko tayari kukuunga
mkono katika mapambano haya hata
kuyaweka rehani maisha yangu lakini si
kwa nafasi ya uwaziri mkuu.Naomba
unielewe kwa hilo mheshimiwa rais”
akasema Mukasha
“ Ninakuelewa Mukasha na
ninaelewa kinachokupa wasiwasi
kuikubali nafasi hii.Unawaogopa Alberto’s
,unaogopa kufa”
“ Hapana mheshimiwa rais japokuwa
ni watu hatari lakini nakuhakikishia
siwaogopi hata kidogo.” Akasema
Mukasha.
“ If you ‘re not scared of them then
join me in this war.Nikiwa nawe kama
waziri mkuu itakuwa rahisi sana
kuendehsa mapambano haya na
tutatengeneza baraza dogo la mawaziri la
watu tunaowaamini na tutahakikisha
tunawang’oa kabisa Alberto’s hapa
nchini.Mzizi wao mkuu ulikuwa ni ofisi ya
rais lakini kwa sasa tayari mzizi huo
umetetereka na ninaamini hivi
tuongeavyo lazima watakuwa katika
mikakati mizito ya kuhakikisha haraka
wawezavyo wananiondoa mimi ambaye
tayari nimekuwa kikwazo kwao ili
mipango yao ifanikiwe.Uwezo huo wanao
kwani wamenizunguka kila kona.Kwa hiyo
nataka muda huu mfupi nilio nao niutumie
vizuri kuhakikisha kama si kuingoa kabisa
mizizi yote ya Alberto’s nchini basi
ninawadhoofisha kabisa.Siwezi kufanya
jambo hili peke yangu bali nahitaji nguvu
za ziada toka kwa watu wachache
ninaowaamini na wewe ukiwa mmoja
wao.Kwa hiyo Mukasha nakuomba
uikubali nafasi hii kwa manufaa ya nchi.”
Akasema Ernest.Mukasha akainamisha
kichwa akatafakari halafu akasema
“ Mheshimwia rais ,kama
nilivyokueleza awali kuwa mimi
nitapambana pamoja nawe bega kwa bega
lakini si kwa nafasi hii ya uwaziri
mkuu.Niko tayari kushirikiana nawe
kumtafuta mtu ambaye anafaa kwa nafasi
hiyo”
Ernest akainamisha kichwa akafikiri
kwa muda akainua kichwa na kusema
 
SEHEMU YA 116




Mukasha you have two daughters
,right?
“ Yes Mr president.Wote wako chuo
kikuu”
“ ‘Good.Hebu pata taswira
unatazama picha mtandaoni ya wanawake
wakishiriki mapenzi ya jinsia moja au
wanafunga ndoa na unagundua mmoja wa
wanaoonekana pichani ni mwano
,utajisikiaje?
Sura ya Mukasha ikabadilika
“ Mungu atanisamehe kwa hicho
nitakachokifanya .Naapa nitaondoa shingo
ya mtu !!
“ It hurt ,right? Akaulizi Ernest
“ So badly.Mtoto ambaye
unamtegemea akuzalie wajukuu halafu
anaolewa na mwanamke mwenzake!!!!
Inaumiza sana.Ni laana kubwa hiyo”
“ Unavyohisi kuumizwa na jambo
hilo ndivyo wengi wa wazazi
watakavyoumia
pindi
Alberto’s
wakifanikiwa mipango yao kwani lengo
lao kubwa ni hilo la kuruhusu mapenzi ya
jinsia moja.Tunatakiwa kuungana pamoja
kuzuia jambo hili lisitokee hapa nchini
kwetu na kuwaathiri watoto
wetu.Nakubali nimefanya kosa kuwapa
mwanya mashetani hawa wa kupenya
lakini naamini pia bado ninayo nafasi ya
kuwazuia wasiendelee na mipango yao
miovu na ndiyo maana nakuomba uwe
waziri mkuu ili tutengeneza baraza la
mawaziri la watu watiifu na wazalendo na
kwa pamoja tuisaifisha nchi hii” akasema
Ernest.Mukasha akafikiri kwa muda na
kusema
“ Mheshimiwa rais,ninakubali nafasi
hiyo ya uwaziri mkuu .Nataka tuisafishe
nchi.Nataka wanangu na wajukuu zangu
waishi katika nchi yenye neema na si nchi
yenye laana” akasema Mukasha .Ernest
akainuka na kumpa mkono wa pongezi
“ Ahsante sana Mukasha kwa uamuzi
huo. Usihofu Mungu anaiona nia yetu
njema na atatutangulia katika vita hii na
tutashinda.”
“ Nashukuru Mheshimwa rais kwa
kuniamini lakini kuna jambo moja nataka
nikuombe”
“ Jambo gani? Omba chochote
Mukasha”
“ Promise me that my family will be
safe.My wife and my two daughters will all
be safe”
“ I promise you Mukasha.I’ll do
whatever I can to protect you and your
family.I give you my word”
“ Thank you mr Prsident” akasema
Mukasha
“ Nitakuteua kwanza kuwa mbunge
halafu nitalipeleka jina lako katika kikao
kitakachofuata cha bunge kwa ajili ya
kuidhinishwa na wabunge. Na baada ya
hapo tutaunda serikali”
“ Mheshimwia rais uliniambia
kwamba Alberto’s wana wafuasi wengi pia
bungeni ,unadhani ukipeleka bungeni jina
la mtu ambaye si mfuasi wao
wataliidhinisha ? Nina hofu tunaweza
kushindwa”
Ernest akafikiri kidogo na kusema
“Uko sahihi Mukasha .Alberto’s wana
wafuasi wengi bungeni lakini nitawatumia
wabunge wa vyama pinzani ambao
wakiungana na wale wachache ambao si
wafuasi wa Alberto’s basi tutakuwa na
uhakika wa kufikisha idadi ya kura
zinazohitajika.Nitajitahdi
sana
kuzungumza na wabunge mmoja mmoja
kutafuta uungwaji mkono katika
hili.Usihofu Mukasha,utapita tu na
utakuwa waziri mkuu mpya wa
Tanzania.Nitateua pia wabunge wapya
kumi kwa mujibu wa mamlaka niliyonayo
na
hawa
wote
watakuwa
mawaziri.Tunatakiwa kuwa makini sana
katika kufanya uteuzi wa watu hawa “
Ernest akanyamaza kidogo na kusema
“ Mukasha nadhani tumelimaliza
suala hili kwa hiyo ni wakati wa kwenda
kuonana na Austin.Kuna mzigo
ninampelekea.Vipi kuhusu zile laini za
simu umefanikiwa kuzipata? Yanahitajika
mawasiliano ya karibu kwani sitaki
kwenda kwa Austin kila siku ili watu
wasigundue na kuanza kumfuatilia
Austin.”
“ Ndiyo mheshimiwa rais ,ninazo
hapa”
“ Good.Lakini kabla hatujakwenda
huko kuna jambo nataka kulifanya “
akasema Ernest akainuka akaelekea
katika chumba kidogo kunamohifadhiwa
vyombo vya chakula akachukua kisu
halafu akachukua kisanduku cha huduma
ya kwanza akamtaka Mukasha waelekee
bafuni.Walipoingia bafuni Ernest akavua
shati na kupasua sehemu Fulani katika
mkono wake wa kushoto akaingiza vidole
viwili na kutoa kitu Fulani kidogo
“ Mukasha zuia damu tafadhali
isiendele kutoka” akasema Ernest akiwa
na maumivu makali.Haraka haraka
Mukasha akachukua dawa na kumtibu
Ernest jeraha lake.Baada ya hapo Ernest
akajisafisha damu na kukisafisha kile
kifaa alichokitoa mkononi na
kumuonyesha Mukasha
“ Hiki ni kifaa ambacho rais
huwekewa mkononi na ambacho
huwawezesha walinzi wa rais kufahamu
kila mahala aliko .Kuanzia sasa nitakuwa
nakiweka kifaa hiki mfukoni na
nitakapokuwa nakwenda sehemu muhimu
kama kwa Austin nitakuwa nakiacha hapa
kifaa hiki ili wasinifuatilie” akasema
Ernest
 
SEHEMU YA 117


kiwa
chumbani
kwake
amejipumzisha baada ya mizunguko
aliyofanya,saa yake ya mkononi ikatoa
mlio akainuka haraka na kuibonyeza
ikamuonysha sababu ya mlio ule.Kulikuwa
na mtu getini.Akafutika bastora yake
kiunoni akatoka kuelekea getini.
Akafungua mlango mdogo wa geti kwa
tahadhati kubwa na kukutana na Evans
akiwa ameongozana na mheshimwa rais
kama kawaida yao.Akawakaribisha ndani
na kabla hawajangia sebuleni Ernest
akasema
“ Austin leo nataka Mukasha na
Evans nao pia washiriki maongezi kwani
tutakayoyazungumza yanawahusu pia
wao”
“ Hakuna tatizo mheshimiwa rais.”
Akasema Austin wakaingia sebuleni.Kabla
ya maongezi kuanza Ernest akampatia
Austin begi lililojaa fedha.Austin
akalifungua na kutabasamu
“ Wow ! It’s cash” akasema na
kulichomoa bunda moja akalitazama na
kufunga begi.
“Ahsante mheshimiwa rais kwa
mzigo huu ,utanisaidia sana” akasema
Austin.
“ Usijali Austin.Muda wowote
utakapohitaji kitu chochote usisite
kunitaarifu na utakipata .By the way
Mukasha amefanikisha kupata laini za
simu ambazo utazitumia kwa mawasiliano
baina yetu.”
“ Ahsante mheshimiwa rais”
akasema Ernest na baada ya muda
akaendelea.
“ Austin nadhani tayari umekwisha
sikia kuhusu mabadiliko mengine
niliyoyafanya leo.Nimemteua mkuu mpya
wa majeshi .Kwa kufanya hivyo nimezidi
kuikata mizizi ya Alberto’s.Nitaendelea
kukata mzizi moja mmoja hadi nihaikishe
wamekosa nguvu na kufa.Nimempandisha
cheo Luten jenerali Lameck Msuba kuwa
jenerali na kumteua kuwa mkuu mpya wa
majeshi Tanzania.Hili lilikuwa pendekezo
lako na nina hakika Jenereali msuba ni
mtu mzalendo na ambaye tutashirikiana
naye katika vita hii” akasema Ernest
.Mukasha na Evans wakatazamana Austin
akasema
“ Ahsante mheshimiwa rais kwa
kulikubali pendekezo langu.Lameck
Msuba ni mtu muadilifu na
mtiifu.Ninamfahamu vyema na hautajutia
uteuzi huo”
“ Tukiachana na hilo la mkuu wa
majeshi ,nimefanya pia uteuzi wa waziri
mkuu japokuwa bado sijautangaza lakini
nimeona niwajulishe kwa kuwa ninyi ni
wenzangu
katika
mapambano
haya.Nahitaji kuunda baraza la mawaziri
lenye watu ambao hawatakuwa na
mafungamano na Alberto’s.Wengi wa
wabunge waliomo katika bunge letu tayari
ni wafuasi wa Alberto’s kwa hiyo
nimeamua kuteua wabunge kumi kwa
mujibu wa mamlaka ya kikatiba
niliyonayo na hao wote kumi watakuwa
mawaziri.Miongoni mwa hao kumi atatoka
waziri mkuu mpya ambaye atakuwa ni Mr
Mukasha”
“ Mukasha !!! Evans akasema kwa
mshangao.Ni yeye pekee aliyeonekana
kustushwa sana na kauli ile ya rais
kwamba amemteua Mukasha kuwa waziri
mkuu.Ernest akamtazama Evans na
alionyesha wazi kutofurahishwa na
mshangao ule wa Evans
“ Evans ninaamini sikukosea
kukukaribisha katika kikao hiki cha
kujadili mambo mazito ya nchi.Kwa ufupi
tu ni kwamba kuna mambo makubwa
yanaendelea hapa chini kwa sasa na watu
hawa unaowaona humu ndani ni pekee
wanaopambana kuiokoa nchi hii
isitumbukie katika laana.Nimeamua na
wewe pia ushiriki katiaka kikao hiki kwa
kuwa nawe ni mmoja wa watu wachache
ninaowamini wanaweza kuwa na mchango
mkubwa katika mapambano haya kwa
hiyo nakuomba utulie na usubiri wakati
wako ukifika utafahamishwa kila kitu juu
ya mambo yanayoendelea.Kwa sasa
naomba usichangie jambo lolote uwe
msikilizaji tu” akasema Ernest na
kumgeukia Austin
“Kwa hiyo Austin nimemteua
Mukasha awe waziri mkuu mpya.Ni mtu
ambaye ninamuamini sana,ni mzalendo
wa kweli.Nimeongea naye na amekubali
kwa hiyo nitatangaza uteuzi wake kama
mbunge yeye pamoja na wenzake kumi na
baada ya hapo nitaliwasilisha bungeni jina
lake ili likapigiwe kura na wabunge na
hatimaye
kuidhinishwa.Ninafahamu
haitakuwa kazi nyepesi lakini nitajitahidi
 
sehemu ya 118




kwa kadiri niwezavyo ili Mukasha apite na
kuwa waziri mkuu”
“ Ni uteuzi mzuri mheshimiwa rais
na sina mashaka naye ila Mukasha
anapaswa afahamu kinachoendelea hivi
sasa na awe tayari kwa lolote hata ikibidi
kuifia nchi yake.Hatuhitaji msaliti katika
mapambano haya kwani yeyote ambaye
atathubutu kwenda kinyume na sisi basi
atakumbana na mkono wangu na
ninakuhakishia mheshimiwa rais na wote
mlioko humu kwamba ninapokwua
kazinihuwa sina urafiki kwa hiyo
atakayediriki kutusaliti ataufahamu
unyama wangu” akasema Austin
“ Usihofu Austin.Tayari nimekwisha
mueleza kila kitu na amekubali kwa moyo
mmoja kushirikiana nasi katika
mapambano haya.Kuhusu usaliti ,sahau
kabisa hilo jambo kwani watu hawa
wawili ninawamini mno”akasema Ernest
“ Good!! Akasema Austin
“ Baada ya kumpata waziri
mkuu,kinachofuata ni kufanya mabadiliko
katika kikosi cha kumlinda rais kama
ulivyopendekeza.Nimekuachia wewe suala
hili ulishughulikie nataka hadi kesho uwe
tayari na majina ya watu
unaowapendekeza watakaounda kikosi
cha kumlinda rais.Pamoja na kufanya
mabadiliko hayo lakini kikosi hicho
kitakuwa chini ya Evans.Naomba uchague
watu mahiri sana ambao wataimudu kazi
hii na zaidi ya yote wawe tayari kuyaweka
maisha yao hatarini kunilinda” akasema
Ernest .Austin akamtazama rais na
kusema
“ Ahsante mheshimiwa rais kwa
kuona umuhimu wa pendekezo langu na
kulikubali.Mimi ni mzoefu katika mambo
haya kwa hiyo nitaunda kikosi kidogo
lakini chenye watu mahiri sana na
ninakuhakikishia mheshimiwa rais
utapata ulinzi wenye uhakika toka kwa
watu hao.”
“ Nafurahi kusikia hilo.Naomba sasa
Mukasha na Evans mnisubiri hapo nje nina
maongezi binafsi na Austin” akasema
Ernest na Evans wakatoka kama
walivyotakiwa na rais
“ Austin nipe taarifa za maendeleo ya
kazi yetu.Umefanikiwa kuonana na
Monica? Akauliza Ernest
“ Sijafanikiwa bado kuonana naye
,nilitaarifiwa yuko nje ya nchi lakini
atarejea hivi karibuni .Nitakwenda tena
kesho ofisini kwake kupata uhakika zaidi
ni lini atarejea”
“ Naomba ujitahidi sana
Austin,ufanye kila uwezalo kupata
sampuli kwa ajili ya kipimo cha
vinasaba.Ninataka jambo hili lifanyike
haraka ili nifahamu kama Monica ni
mwanangu au siyo nijue namna ya
kumlinda.Japokuwa
nafsi
yangu
inaniambia kweli Monica ni mwanangu
lakini lazima niwe na uhakika na uhakika
utapatikana pale tu nitakapofanya kipimo
cha vinasaba”

Usihofu
mheshimiwa
rais,nakuhakikishia jambo hili lazima
litafanikiwa tu.Naomba unipe siku
kadhaa”
“ Nakuamini Austin ila nilitaka tu
kukupa msisitizo kwani haya yote
ninayafanya kwa sababu ya
Monica.Tuachane na hayo,vipi kuhusu
Marcelo anaendeleaje?
“ Anaendelea vizuri.Yuko chumbani
amejipumzisha .Kuna taarifa yoyote toka
kwa David Zumo?
“ Ndiyo.Nimeongea naye mchana wa
leo na akaniambia kwamba niendelee
kumuhifadhi Marcelo mahala pa siri na
asiruhusiwe kuonana na mtu yoyote hadi
hapo atakapotoa maelekezo mengine.Kwa
hiyo Marcelo ataendelea kukaa hapa hadi
hapo tutakapopata maelekezo mengine
toka kwake”
“ Suala hili la Marcelo linaonekana ni
suala pana ” akasema Austin
“ Kuna mambo ambayo yananipa
ugumu kuyaelewa lakini sitaki kujihusisha
na suala hili wakati huu ambao kuna
mambo mazito yanatukabili”
“Uko sahihi Austin.Suala hili la
Marcelo
linaonekana
ni
gumu.Tusishughulike
nalo
kwa
sasa.Tukiachana na hayo kuna jambo
lingine ambalo sikuwanimekueleza hapo
awali ambalo ni la muhimu sana
ukilifahamu”
“ Nakusikiliza mheshimiwa rais”
akasema Austin.Ernest akafikiri kidogo na
kusema
 
Back
Top Bottom