SEHEMU YA 116
Mukasha you have two daughters
,right?
“ Yes Mr president.Wote wako chuo
kikuu”
“ ‘Good.Hebu pata taswira
unatazama picha mtandaoni ya wanawake
wakishiriki mapenzi ya jinsia moja au
wanafunga ndoa na unagundua mmoja wa
wanaoonekana pichani ni mwano
,utajisikiaje?
Sura ya Mukasha ikabadilika
“ Mungu atanisamehe kwa hicho
nitakachokifanya .Naapa nitaondoa shingo
ya mtu !!
“ It hurt ,right? Akaulizi Ernest
“ So badly.Mtoto ambaye
unamtegemea akuzalie wajukuu halafu
anaolewa na mwanamke mwenzake!!!!
Inaumiza sana.Ni laana kubwa hiyo”
“ Unavyohisi kuumizwa na jambo
hilo ndivyo wengi wa wazazi
watakavyoumia
pindi
Alberto’s
wakifanikiwa mipango yao kwani lengo
lao kubwa ni hilo la kuruhusu mapenzi ya
jinsia moja.Tunatakiwa kuungana pamoja
kuzuia jambo hili lisitokee hapa nchini
kwetu na kuwaathiri watoto
wetu.Nakubali nimefanya kosa kuwapa
mwanya mashetani hawa wa kupenya
lakini naamini pia bado ninayo nafasi ya
kuwazuia wasiendelee na mipango yao
miovu na ndiyo maana nakuomba uwe
waziri mkuu ili tutengeneza baraza la
mawaziri la watu watiifu na wazalendo na
kwa pamoja tuisaifisha nchi hii” akasema
Ernest.Mukasha akafikiri kwa muda na
kusema
“ Mheshimiwa rais,ninakubali nafasi
hiyo ya uwaziri mkuu .Nataka tuisafishe
nchi.Nataka wanangu na wajukuu zangu
waishi katika nchi yenye neema na si nchi
yenye laana” akasema Mukasha .Ernest
akainuka na kumpa mkono wa pongezi
“ Ahsante sana Mukasha kwa uamuzi
huo. Usihofu Mungu anaiona nia yetu
njema na atatutangulia katika vita hii na
tutashinda.”
“ Nashukuru Mheshimwa rais kwa
kuniamini lakini kuna jambo moja nataka
nikuombe”
“ Jambo gani? Omba chochote
Mukasha”
“ Promise me that my family will be
safe.My wife and my two daughters will all
be safe”
“ I promise you Mukasha.I’ll do
whatever I can to protect you and your
family.I give you my word”
“ Thank you mr Prsident” akasema
Mukasha
“ Nitakuteua kwanza kuwa mbunge
halafu nitalipeleka jina lako katika kikao
kitakachofuata cha bunge kwa ajili ya
kuidhinishwa na wabunge. Na baada ya
hapo tutaunda serikali”
“ Mheshimwia rais uliniambia
kwamba Alberto’s wana wafuasi wengi pia
bungeni ,unadhani ukipeleka bungeni jina
la mtu ambaye si mfuasi wao
wataliidhinisha ? Nina hofu tunaweza
kushindwa”
Ernest akafikiri kidogo na kusema
“Uko sahihi Mukasha .Alberto’s wana
wafuasi wengi bungeni lakini nitawatumia
wabunge wa vyama pinzani ambao
wakiungana na wale wachache ambao si
wafuasi wa Alberto’s basi tutakuwa na
uhakika wa kufikisha idadi ya kura
zinazohitajika.Nitajitahdi
sana
kuzungumza na wabunge mmoja mmoja
kutafuta uungwaji mkono katika
hili.Usihofu Mukasha,utapita tu na
utakuwa waziri mkuu mpya wa
Tanzania.Nitateua pia wabunge wapya
kumi kwa mujibu wa mamlaka niliyonayo
na
hawa
wote
watakuwa
mawaziri.Tunatakiwa kuwa makini sana
katika kufanya uteuzi wa watu hawa “
Ernest akanyamaza kidogo na kusema
“ Mukasha nadhani tumelimaliza
suala hili kwa hiyo ni wakati wa kwenda
kuonana na Austin.Kuna mzigo
ninampelekea.Vipi kuhusu zile laini za
simu umefanikiwa kuzipata? Yanahitajika
mawasiliano ya karibu kwani sitaki
kwenda kwa Austin kila siku ili watu
wasigundue na kuanza kumfuatilia
Austin.”
“ Ndiyo mheshimiwa rais ,ninazo
hapa”
“ Good.Lakini kabla hatujakwenda
huko kuna jambo nataka kulifanya “
akasema Ernest akainuka akaelekea
katika chumba kidogo kunamohifadhiwa
vyombo vya chakula akachukua kisu
halafu akachukua kisanduku cha huduma
ya kwanza akamtaka Mukasha waelekee
bafuni.Walipoingia bafuni Ernest akavua
shati na kupasua sehemu Fulani katika
mkono wake wa kushoto akaingiza vidole
viwili na kutoa kitu Fulani kidogo
“ Mukasha zuia damu tafadhali
isiendele kutoka” akasema Ernest akiwa
na maumivu makali.Haraka haraka
Mukasha akachukua dawa na kumtibu
Ernest jeraha lake.Baada ya hapo Ernest
akajisafisha damu na kukisafisha kile
kifaa alichokitoa mkononi na
kumuonyesha Mukasha
“ Hiki ni kifaa ambacho rais
huwekewa mkononi na ambacho
huwawezesha walinzi wa rais kufahamu
kila mahala aliko .Kuanzia sasa nitakuwa
nakiweka kifaa hiki mfukoni na
nitakapokuwa nakwenda sehemu muhimu
kama kwa Austin nitakuwa nakiacha hapa
kifaa hiki ili wasinifuatilie” akasema
Ernest