QUEEN MONICA SEASON 3
SEHEMU YA 1
ILIPOISHIA SEASON ILIYOPITA
“He’s
here.Austin
tayari
amekuja.Ngoja nikamchukue yupo
mapokezi “ akasema Linah na kutoka
.Baada ya dakika tano akarejea akiwa
ameongozana na kijana mmoja mtanashati
sana mwenye sura iliyojaa tabasamu
“Wow! What a handsome guy”
akawaza Monica baada ya kumuona
Austin.Alikuwa ni kama mtu aliyepigwa na
butwaa kwa kitu alichokuwa anakitazama
mbele yake.
“Monica “ akaita Linah na kumstua
Monica
“Huyu anaitwa Austin January.Ndiye
mgeni Yule niliyekueleza alikuwa
anakutafuta”
“Austin huyu ndiye Monica Benedict
mwamsole,mkuu wa kampuni hii” LInah
akafanya utambulisho.Monica akasimama
na kumpa Austin mkono.
“Karibu sana Austin.Nimefurahi
kukutana nawe”
“Hata mimi nimefurahi sana kuonana
nawe Monica” akasema Austin na kuketi
katika sofa.Linah akatoka na kuwaacha
Monica na Austin pale ofisini.
ENDELEA..................................
“ Uzuri wa Monica si uzuri wa
kawaida, naweza kumfananisha na viumbe
toka sayari nyingine.Ni uzuri usioweza
kuelezeka kwa maneno.” Akawaza Austin
huku akimtazama Monica kwa jicho la
wizi.
“ Austin karibu sana “ Monica
akaanzisha maongezi
“ Ahsante sana Monica.Pole kwa
safari.Nilifika hapa jana nikataarifiwa
kwamba ulikuwa safarini nje ya nchi.”
“ Ni kweli Austin nilikuwa nje ya nchi
nimerejea jana jioni na nilipofika
nilitaarifiwa kwamba ulifika hapa
kunitafuta”
“Natumai msaidizi wako Linah
amekwisha kueleza kwa ufupi kuhusu
mimi na nini kilichonileta hapa kwako.”
“ Ndiyo alinieleza” akajibu Monica
“ Vizuri.Kwa ufupi naitwa Austin
January,ni mtanzania lakini kwa sasa nina
uraia wa Afrika ya kusini.Kikazi mimi ni
mkurugenzi wa utawala na fedha katika
kampuni ya kitalii ya A.A safari yenye
makao yake makuu nchini Afrika ya
kusini.Tunawapokea watalii toka nchi
mbali mbali duniani na kuwapeleka
sehemu mbali mbali za bara la Afrika.Vile
vile tunazo hoteli zinaitwa AA 5 stars hotel
ambazo zimesambaa katika sehemu mbali
mbali za bara la Afrika.Kwa kifupi naweza
kusema kwamba kampuni yetu ni moja
kati ya kampuni kubwa na bora kabisa za
utalii hapa Afrika” akasema Austin
“Nimefurahi sana kukufahamu
Austin.Mimi ni Monica Benedict ni
mkurugenzi wa kampuni hii
inayojishughulisha na masuala ya ubunifu
na utengenezaji wa mavazi.Tunabuni
mavazi hapa na kupeleka bunifu zetu
katika viwanda vya ndani na nje ya
nchi.Sidhani kama nitakuwa najisifu
nikisema kwamba kampuni yetu ni moja
kati ya kampuni bora kabisa ya mavazi
katika ukanda huu wa Afrika
mashariki.Mbali na mavazi ninayo pia
taasisi yangu inayojisghughulisha na
kusaidia jamii yenye uhitaji na hapa
tumejikita zaidi kusaidia watoto na wazee
wasiojiweza”
“ Hicho ndicho haswa kilichonileta
hapa kwako Monica “ akasema Austin kwa
furaha
“ Kampuni yetu ina kitengo kidogo
cha kusaidia miradi mbali mbali ya kijamii
katika sehemu zile ambazo tuna ofisi zetu.
Tumekuwa tukichangia ujenzi wa
mashule,hospitali n.k.Kwa sasa tuko katika
maandalizi ya kufungua ofisi zetu hapa Dar
es salaam kwa hiyo tunataka kuanza
kushiriki pia katika miradi mbalimbali ya
kijamii lakini kabla ya kufanya hivyo
tumeona tujifunze kwanza toka kwa
wenzetu ili tufahamu ni sehemu gani
tunaweza na sisi kuwekeza nguvu zetu
hapa Tanzania.Kwa hiyo Monica nimekuja
hapa kwako kujifunza kwani wewe na
taasisi yako tayari mnao uzoefu wa
kutosha na mazingira ya huku Tanzania na
kama itawezekana tunaweza kushirikiana
katika baadhi ya miradi ya kijamii” Austin
akanyamaza na kurekebisha tai yake na
kumtazama Monica
“ Austin nimefurahi kusikia kwamba
na ninyi pia mnajishughulisha katika
kusaidia jamii masikini zenye uhitaji
.Hakuna shaka sisi na ninyi tutashirikiana
katika miradi mbali mbali .Jamii masikni
hapa Tanzania zina changamoto nyingi
sana mfano elimu,afya,maji safi na salama
n.k.Haya ni maeneo ambayo sisi tumeyapa
kipaumbele kikubwa kwa kushjirikiana na
wafadhili mbali mbali tumeweza kujenga
vituo zaidi ya kumi na sita vya
afya,madarasa zaidi ya hamshini,visima
vya m,ai zaidi ya sitini katika sehemu
mbalimbali nchini wanakopishi watu
masikini .Tumekuwa tukifadhili matibabu
ya wazee wasiojiweza,kuwasaidia misaada
mingine muhimu kama vile chakula
n.k.Tumekuwa pia tukifadhili pia elimu
kwa watoto toka jamii masikini mfano kwa
sasa tuko katika hatua za mwisho za ujenzi
wa shule kubwa ya watoto wenye ulemavu
wa kutokuona na kusikia.Haya ni baadhi tu
ya mambo ambayo mimi na taasisi yangu
tumekuwa tukiyafanya”akasema Monica
“ Hongereni sana Monica” akasema
Austin.Monica akainuka akaliendea kabati
na kutoa karatasi tatu kubwa akampatia
Austin
“ Hiyo ni shule ambayo tunaanza
kuijenga hivi karibuni.Pesa tayari
tumeipata na kilichobaki ni kumpata
mkandarasi ili ujenzi uanze mara moja”
Uso wa Austin ukapambwa na
tabasamu kubwa
“ Monica unastahili pongezi kubwa
sana kwa hili ulilolifanya.Jamii hii ya
walemavu wana uhitaji mkubwa na
wamesahaulika sana katika jamii
zetu.Shule hii itakuwa ni mkombozi
mkubwa kwao” akasema Austin
“ Ahsante Austin” akasema Monica
na mara mlango ukafunguliwa akingia
Linah.Akamnong’oneza kitu Monica na
kutoka
“Austin nimetaarifiwa kuwa
ninahitajika eneo la ujenzi kuna watu toka
wizarani wamefika na wananisubiri”
akasema Monica
“ Oh ! sawa Monica.Ninashukuru
sana kwa kunipokea vizuri na nina imani
tutapata wasaa mzuri zaidi wa
kulizungumzia suala hili kwa upana
.Nikutakie kila la heri katika kazi zako”
akasema Austin huku akiinuka
“Nashukuru pia kukufahamu
Austin.Nitatafuta nafasi nyingine tukae
tuzungumze kwa kirefu juu ya suala hili”
akasema Monica wakaagana lakini kabla
Austin hajatoka mle ofisini Monica
akasema
“ Austin kama hutojali tunaweza
kuongozana kwenda eneo la ujenzi?
Austin ambaye tayari alikuwa
ameukaribia mlango akageuka haraka
haraka na kusema
“ Hakuna tatizo Monica tunaweza
kwenda