Sehemu ya 38
Amarachi na Job waliwasili katika jengo iliko saluni kubwa ya Julieth.Job akampigia simu Julieth akamfahamisha kuwa tayari amekwisha fika pale na kumuelekeza aina ya gari alimo
.Alipomaliza kuongea na Julieth
akampigia simu Amarachi
“ Tayari nimempigia simu na muda wowote atashuka.Kuwa makini”
akasema Job
“Niko makini Job.Mpaka sasa sijaona hatari yoyote” akasema
Amarachi aliyekuwa makini katika gari lake akitazama kama kuna hatari yoyote.Job hakukata simu akachomeka
spika za masikioni na kuiweka simu
mfukoni ili mawasiliano kati yake na
Amarachi yaendelee
Mlango wa gari la Job ukafunguliwa na mwanamke mmoja mwembamba mrefu mwenye umbo la uanamitindo akaingia
“ Are you Julieth? Akauliza Job
“ yes” akajibu Yule mwanamke
“Njoo ukae huku mbele.Sitaki mtu akae nyuma yangu” akasema Job na Julieth akahamia kiti cha mbele
“ Switch off you phone” akaamuru Job
“ Why ?? akauliza Julieth
“ Unataka kuonana na Marcelo ? “Ndiyo nataka”
“kama unataka kumuona tena
Marcelo basi utafuata maelekezo yangu.Zima simu yako” akaamuru Job na huku sura yake ameikunja Julioeth
akaizima simu yake
“Good.Now we can go” akasema
Job na kugeuza gari wakaondoka
“Job mpaka hapa sijaona hatari yoyote.Niko nyuma yenu” Amarachi akamwambia Job aliyekuwa anamsikia kupitia spika za masikioni alizokuwa amevaa
Safari ilikuwa ya kimya kimya hadi walipofika nyumbani kwa Job
“Marcelo amekuja kujificha mbali
namna hii !!akasema Julieth
“ Yah” akajibu Job na kufungua mlango akashuka ,Julieth naye akashuka wakaelekea sebuleni
Mara tu walipoingia sebuleni Julieth akakutanisha macho na Marcelo.Wote wawili wakabaki wanatazamana.Julieth akamkimbilia Marcelo na kumkumbatia
“ Oh Marcelo !!! akasema kwa
furaha
“ mambo vipi Julieth? Akauliza
Marcelo
“ mambo poa Marcelo unaendeleaje? Oh gosh hatulali tunakuwaza wewe kama uko mzima.Nashukuru sana uko salama Marcelo” akasema Julieth
“ Julieth tafadhali nenda uketi pale”Job akamuelekeza Julieth sehemu ya kuketi na muda huo huo Amarachi akaingia
“ It’s clear.Hakuna anayetufuatilia” akasema Amarachi ,Julieth akaonekana kushangaa
“Bila kupoteza muda naomba nikutambulishe Julieth kwa watu waliomo humu ndani” akasema Job
“ Yule aliyelala pale sofani anaitwa
Austin ndiye mkubwa wetu hapa. Mimi naitwa Job na huyu mwanamama
anaitwa Amarachi.Sisi ndio tunaomlinda kaka yako Marcelo dhidi ya wale wanaomtafuta wamuue na
wewe ukiwa mmoja wao” akasema Job na kumstua Julieth
“Julieth kuanzia sasa utakuwa mikononi mwetu na pengine hutaondoka salama katika jengo hili kama hutatueleza kile tunachotaka kukisikia” akasema Job
“ Samahani kaka Job.Sijakuelewa
unamanisha nini? Mimi ni ndugu yake Marcelo na siwezi katu kumfanyia kitu kama hicho.Unafahamu ni uchungu kiasi gani tulio nao kwa hayo yaliyompata ndugu yetu? Marcelo tafadhali waeleweshe wenzako” akaongea Julieth kwa ukali
“ Taratibu Julieth” akasema Marcelo
“ Julieth tunataka kufahamu
mahusiano yako na Boaz” akauliza Austin
“ Boaz??!! Julieth akauliza kwa mshangao
“ ndiyo”
“ Simfahamu mtu yeyote anaitwa
Boaz” akajibu Julieth
“ Are you sure? Akauliza tena Austin
“ yes I’m sure” akasema Julieth
“ Marcelo nini kinaendelea hapa? Mbona siwaelewi wewe na wenzako? Akauliza Julieth
“ Job” akaita Austin
“ Make her talk” akasema Austin aliyekuwa amelala sofani
“ Julieth welcome to the hell.You are going to answer all my questions.If you cant give me the right answers
you’ll never see the sun again!! Akasema Job huku akimtazama Julieth kwa macho makali
“ Tueleze wewe na Boaz mna mahusiano gani? Akauliza Job
“Jamani nimekwisha waeleza kwamba simfahamu mtu yeyote anayeitwa Boaz.Kama mna lengo la kuniua basi niueni lakini simfahamu Boaz” akasema Julieth .Job akachukua simu ya Boaz
“ Hii ni simu ya Boaz.Mawasiliano yako naye tunayo na hata ujumbe wa mwisho uliomtumia uko hapa” akasema Job na kumuonyesha Julieth ule ujumbe aliomtumia Boaz.Midomo ya Julieth ikamtetemeka akashindwa kuongea.
“ Nataka unijibu sasa.Unamfahamu
Boaz” akauliza Job
“ Hapana simfaham……..” Kabla hajamaliza Amarachi akaichomoa bastora
“ Huyu mwanamke anatuchezea
akili zetu!! Akasema na kumlenga
Julieth miguuni
“ Basi… basi!! Nitawaeleza kila kitu
!! akapiga ukelele Julieth .Bado Amarachi aliendelea kumtazama kwa hasira
“ It’s ok Amarachi .Let her talk”
akasema Job
Julieth akavuta pumzi ndefu akafuta machozi na huku akitetemeka akasema
“Ni kweli mimi na Boaz tuna mahusiano ya kimapenzi kwa muda mrefu toka angali baba hajafariki.” Akasema Julieth
“ tell us more !!! akafoka Job
“ Boaz ni mfanyabiashara wa dawa za kulevya na alikuwa rafiki wa baba ambaye naye alikuwa anajihusisha na biashara hiyo ya dawa za kulevya.”
“ What ?!! Marcelo akashangaa
“ Marcelo kuna mambo ambayo huyafahamu kuhusu baba .Kuna mambo mengi aliyokuwa anayafanya kwa siri
.Nilipoanza mahusiano na Boaz ndipo nilipofahamu kwa baba alikuwa anajihusisha na biashara hiyo na utajiri wake mkubwa ulitokana na hiyo biashara.” Akanyamaza akafuta machozi na kuendelea
“ Baada ya baba kufariki ,Boaz alinifuata akanieleza kuwa anakihitaji kitabu muhimu ambacho baba alikuachia.Alinipa namba za siri za kasiki lako nikaingia chumbani kwako na kukichuka kitabu hicho pamoja na
nyaraka zako mbali mbali likiwemo faili lenye historia ya ugonjwa wako ambalo lilipelekwa kwa mwanamke anaitwa Monica lengo likiwa ni kukuchanganya
ili usikumbuke kuhusu kitabu kwani ilisemekana kuwa wewe na Monica ni
wapenzi.Baada ya kukipata kitabu hicho nikasikia umepigwa risasi na yote hii ilikuwa ni mipango ya
Boaz.Ulipotoweka hospitali nilimtaarifu
Boaz akaja mara moja.Nilimpa kitabu kile nilichokichukua toka katika kasiki lako akakifungua na kudai kuwa si kile anachokihitaji.Ndani ya kitabu hicho kuna barua ambayo baba alikuandikia.Baada ya kugundua kitabu alichokihitaji si chenyewe Boaz amewekeza nguvu kubwa katika kukutafuta ili aweze kukipata kitabu hicho kwa gharama zozote.Uliponipigia nilimtaarifu Boaz kuwa umenipigia ili tukutafute na tukipate kitabu hicho.” Akasema Julieth na kunyamaza akatazama chini
“ Why are you doing this to me
Julieth? Akauliza Marcelo
“ I’m sorry Marcelo” akasema
Julieth na kuanza kulia.Amarachi akaufungua mkoba wa Julieth akatoa kitabu cheusi akampatia Marcelo
“ Kabla ya kifo chake baba alinipa kitabu hiki na sikuwahi kukifungua kujua nini kiliandikwamo ndani yake.” Akasema Marcelo
“ Hukuwahi kukifungua? Hujui kilichomo ndani? Akauliza Julieth
“ Ndiyo sijawahi kukifungua kitabu hiki na wala sifahamu kina nini ndani yake” akasema Marcelo na kuanza kukifungua kitabu kile kwa umakini mkubwa .Ndani ya kitabu kile akaikuta barua akaisoma kwa umakini na alipomaliza akampatia Austin
“ Dah ! akasema Austin alipomaliza kuisoma halafu akawapa Job na
Amarachi nao pia waipitie barua ile.Wote wakabaki kimya wakitazamana
baada ya kuisoma barua ile
“Job mfungie Julieth chumbani tutaendelea naye baadae” akaamuru Austin.Job akamshika mkono
“ Marcelo tafadhali naomba unisaidie!! Akasema Julieth lakini Marcelo hakujibu kitu.Job akampeleka katika mojawapo ya vyumba akamfungia na kurejea sebuleni
“ nadhani nyote mmeisoma barua na kuilewa vyema”akasema Austin
“ Mimi bado kuna mambo nahitaji kufafanuliwa.Dr Richard aliyeandika barua hii anaeleza kwamba alikuwa mfuasi wa Alberto’s na kwamba alikuwa anasimamia kukusanya mapato toka
kwa wafanya biashara wa dawa za kulevya walio chini ya Alberto’s.Hawa Alberto’s ni akina nani? Akauliza Amarachi
“Hata mimi ninataka kulifahamu
hilo kundi linalojiita Alberto’s” akasema Marcelo
Austin akawafahamisha Amarachi na Marcelo kila kitu kuhusiana na Alberto’s na kuwaacha na mshangao mkubwa
“ kwa hiyo “ akaendelea Austin
“ Dr Richard alikuwa akiwasimamia akina Boaz ambao ndio wafanya biashara ya dawa za kulevya walio chini ya mtandao wa Alberto’s.Nimeishi na Boaz kwa miaka kadhaa na amenitunza kama mwanae
na hata siku moja sikuwahi kuhisi kuwa ni mfuasi wa Alberto’s au anafanya biashara ya dawa za kulevya.Ni mtu
anayejua sana kuficha nyendo zake.Hata hivyo arobaini yake imewadia.hawezi kuchomoa kabhali yangu” akasema
Austin
“ This is a big war” akasema
Amarachi
“ Ni vita kubwa kwani watu tunaopambana nao ni watu wakubwa na wenye nguvu si hapa Tanzania tu bali duniani kwa ujumla.Pamoja na
ukubwa wao tusikate tamaa tupambane tuhakikishe tunaisafisha nchi” akasema Austin
“ kwa hiyo nini kinafuata ?
akauliza Amarachi
“ Tunatakiwa tukipate kitabu hicho anachokitafuta Boaz ambacho
kina orodha nzima ya wafanya biashara wa dawa za kulevya walio chini ya Alberto’s.Katika barua hii Dr Richard ameandika kwamba kitabu hicho amekihifadhi nyumbani kwa Vera.Huyu Vera ni nani? Austin akauliza
“ Vera ni mdogo wetu.Baba
alimzaa nje ya ndoa na hajawahi kumuonyesha mtu mwingine zaidi
yangu.Ninafahamu nyumbani kwake naweza kuwapeleka” akasema Marcelo
“ Good.Utaongozana na Job
kwenda huko sasa hivi .Hakikisheni mnakipata kitabu hicho” akasema Austin.Job akapanda ghorofani akarejea akiwa na begi dogo akamchukua
Marcelo wakaondoka
“ Amarachi niliambiwa na Job kwamba unamiliki hoteli? Akauliza Austin
“ Ndiyo ninamiliki hoteli kubwa hapa dar es salaam” akajibu Amarachi “Good.Nataka kiandaliwe chakula
katika hoteli yako kwa ajili ya usiku wa
leo.Kumbuka ni chakula maalum kwa ajili ya rais” akasema Austin
“ Sawa Austin ngoja nitoe maelekezo sasa hivi maandalizi yaanze mara moja” akasema Amarachi.
********************
Ni saa kumi na mbili za jioni Job na
Marcelo waliporejea nyumbani
wakitokea katika jukumu walilopewa na Austin kwenda kuchukua kitabu nyumbani kwa Vera.
“ Karibuni” akasema Amarachi
“ Austin yuko wapi? Akauliza Job
“ Nimemuacha chumbani anapumzika.Huko mtokako kuna mafanikio? Akauliza Amarachi
“ Ndiyo tumefanikiwa kukipata kitabu.Kuna lolote jipya hapa?
“ Hakuna jipya.Tunajiandaa kwa
ajili ya zoezi la usiku wa leo” akasema Amarachi.Job hakutaka maongezi zaidi akamfuata Austin ghorofani
“ Vipi Marcelo unajisikiaje?
Amarachi akamuuliza marcelo
“ Naendelea vizuri.Tumefanikiwa
kukipata kitabu japokuwa haikuwa rahisi lakini Job ametumia mbinu zake tukafanikiwa kuingia na kukichukua kitabu hicho”
“ Good.Mimi na Austin tutaondoka muda si mrefu kwenda kuonana na Monica usiku huu.Utabaki hapa na Job,jambo moja ninalotaka kukufahamisha kuhusu Job ni kwamba
ni mtu mwenye hasira za haraka ila fuata maelekezo yake na usibishane naye” akasema Amarachi
“ Ahsnate Amarachi kwa tahadhari hiyo.” Akajibu Marcelo
Austin akiwa katika chumba cha
kulala ,mlango ukagongwa na akumruhusu mgongaji aingie ndani,alikuwa ni Job.
“ Karibu Job” akasema Austin
aliyekuwa amekaa kitandani
“ Ahsante sana Austin” akajibu Job
na kuufungua mkoba akatoa kitabu cha kuhifadhia kumbu kumbu akamkabidhi Austin
“ Tumefanikiwa kukipata .Haikuwa rahisi hata hivyo Vera hatujamkuta ikanilazimu kutumia mbinu zetu na kuingia ndani tukakichukua kitabu”
“ Kazi nzuri.Mimi na Amarachi tunajiandaa kwenda kuonana na Monica usiku wa leo kwa hiyo nitakuachia kazi,nataka ukisome kitabu hiki chote ukielewe vyema kurasa kwa kurasa na nitakaporejea usiku wa leo utanipa
ripoti ya nini umekipata katika kitabu hicho.Baada ya hapo tutaanza mahojiano na watu wetu.Mgeni wa
kwanza atakuwa Boaz.” Akasema Austin
“ Sawa Austin.Kila kitu kitafanyika kama ulivyoelekeza.Utakaporejea
utakuta maandalizi ya mahojiano na watu wetu yamekamilika” akasema Job
akamsaidia Austin kushuka chini hadi katika gari la Amarachi wakaondoka Toka nyumbani kwa Job
walielekea moja kwa moja nyumbani kwa Amarachi.Aliingia ndani mwake akatoka na begi dogo akaingia garini wakaondoka
“ Mbona hujabadili mavazi? Austin akauliza
“ Nimeogopa
kuchelewa.Nimepakia kila kitu kwenye begi nitakwenda kuvalia hotelini tunakopita kuchukua chakula na wahudumu wa kutuhudmia” akasema Amarachi
“ Samahani sana kwa kuupoteza muda wako mwingi.Toka jana hujapata hata wasaa wa kupumzika.Hata hivyo umekuwa ni mtu wa muhimu sana kwetu zaidi ya nilivyotegemea”
akasema Austin
“ Oh Austin,usiwaze kuhusu mapumziko.Kuna kazi kubwa iko mbele yetu na tutapumzika baada ya kuikamilisha .Kwa sasa tuelekeze akili zetu kwanza katika afya na usalama
wako na pili majukumu mazito
tuliyoyabeba” akasema Amarachi
Waliendela na safari yao huku wakizungumza mambo mbali mbali hadi walipofika katika hoteli ya Amarachi.Austin hakushuka garini
.Amarachi akaichukua begi lake na kuingia hotelini akajiandaa wakati wakati wahukudmu wakipakia chakula na vitu vingine katika gari maalum.Austin akaitumia nafasi hiyo kumtumia ujumbe Monica kumuuliza kama tayari amekwishajiandaa na kumtaka amuelekeze alipo ili amtume
Amarachi akamchukue.Monica
akamuelekeza nyumbani kwake
Baada ya dakika kumi na tano,Amarachi akatokea akiwa amependeza vilivyo.
“Wow !Sijawahi kufanya operesheni iliyonikutanisha na wanawake wazuri kama hii.” Akawaza Austin akimshuhudia Amarachi akishuka ngazi
Kila kitu kinachohitajika kikapakiwa katika gari maalum wakaondoka..
“ Amarachi” akaita Austin
“ Nitakuwa sijatenda haki kama sintakupa hongera kwa namna ulivyopendeza usiku wa leo.” Akasema Austin na uso wa Amarachi ukajenga tabasamu kubwa
“ Ahsante sana Austin .Ni heshima
kubwa umenipa kuwa karibu yako na kufanya nawe kazi.Kupitia kwako
nimeweza kukutana na watu wakubwa kama rais wa nchi.Kwa kukutana nawe nimejiamini zaidi na ninaweza kufanya jambo lolote kwa muda wowote” akasema Amarachi na safari ikaendelea
“Austin kuna kitu nataka kukuuliza naomba uwe muwazi kwangu tafadhali”
“Uliza Amarachi”
“Leo asubuhi pale hospitali niliwashuhudia kwa mara ya kwanza wewe na Monica nikagundua kuna kitu kipo kati yenu ambacho aidha mnakijua au bado hamjakijua “
“ Kitu gani?
“Mnavutia sana mkiwa pamoja.Niliona namna Monica alivyokuwa akikulisha matunda.Kuna kitu kinawazunguka.”
Austin akatabasamu na kusema
“ Amarachi usiende huko tafadhali
.Mimi na Monica ni marafiki tu tena tumefahamiana muda si mrefu.Nilijenga urafiki naye baada ya kupewa kazi na
rais ya kutafuta sampuli kwa ajili ya kipimo cha vinasaba.Moyo wangu niliufungua kwa mwanamke mmoja tu ambaye ni Maria na mpaka sasa bado siamini kama Maria ambaye niliufungua moyo wangu kwake peke yake ndiye aliyetaka kunitoa uhai” akasema Austin
“ Pole sana Austin” akasema
Amarachi wakaendela na safari yao.
Walifika katika makazi ya Austin aliyopewa na rais.Jumba lilikuwa kimya sana japo taa za nje zilikuwa zikiwaka.Austin akafungua geti
wakaingia ndani akamkaribisha Amarachi na wale wahudumu na maandalizi yakaanza.Wakati wahudumu wakiendelea kuandaa
Austin akamtaka Amarachi akamchukue
Monica
*****************
Saa mbili na dakika kumi na nane Ernest Mkasa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akawasili
katika nyumba aliyompa Austin aishi.Ujio wake ulimstua Austin kwani haukuwa ule ujio wake wa kawaida aliouzoea.Hakuwa ameongozana na walinzi wake wa kawaida.Alikuwa ameongozana na makomando zaidi ya
kumi
Rais akawataka makomando wale wabaki nje akaingia ndani peke yake akiongozana na Austin.
“ Austin sikuwa nimekutaarifu mapema kuna maamuzi niliyafanya”
akasema rais na kunyamaza kidogo
halafu akasema
“ Nimebadilisha walinzi wa rais na kwa sasa ninalindwa na makomando wa jeshi.Kwa hiyo usisumbuke tena kuunda kile kikosi tulichokuwa tumekubaliana ukiunde.Ulinzi huu nilionao sasa ni wa uhakika mkubwa .Kwa sasa kilichopo mbele yetu ni kuendeleza mapambano” akasema rais
“ Oh !hilo ni jambo zuri umefanya mheshimiwa rais.Hata hivyo bado sikuwa nimekiandaa kikosi kile tulichokuwa tumeafikiana nikiunde.Limekuwa ni jambo zuri umenipunguzia kazi.” Akasema Austin
“ Vipi maendeleo yako ? akauliza rais
“ Ninaendelea vizuri .Ni maumivu
tu makali ndiyo yanayonisumbua lakini hilo ni jambo la kawaida tumekwishalizoea.Ninatumia dawa za kunisiadia
kuondoa maumivu ndiyo maana unaona ninaweza hata kutembea namna hii bila shida” akasema Austin.Ernest akamtazama na kusema
“ Austin you are amazing.Nikikutazama nashindwa niseme nini.Ni jana tu usiku risasi nne zimetolewa mwilini mwako lakini leo hii unaweza hata kutembea.You are so strong.Taifa linawahitaji wapambanaji kama wewe” akasema rais.
Austin akatabasamu na bila kusema chohote akamkaribisha rais sofani
“Maandalizi yanakwendaje?
Monica amekwisha fika” akauliza rais
“ Hapana bado hajafika.Amarachi amekwenda kumchukua”
“ Good.Vipi kuhusu Yule binti
aliyekujeruhi tayari mmemuhoji na kumfahamu ni nani? Boazi je kuna
lolote mmelipata toka kwake?
“ Hapana mheshimiwa rais,bado hatujawahoji ila usiku wa leo tutakapotoka hapa tutalifanya hilo zoezi.Tulichofanikiwa kukipata ni kitabu ambacho Boaz amekuwa anakitafuta kwa gharama kubwa na ndiye sababu ya kutaka kumuua Marcelo kwani pekee ndiye aliyekuwa anafahamu mahala kilipo kitabu
hicho.Dr Marcelo aliachiwa kitabu hicho
na baba yake ambaye naye alikuwa katika mtandao wa dawa za kulevya.Kitabu hicho kina orodha ya wafanya biashara wote wa dawa za kulevya walio chini ya Alberto.Tutakipitia kitabu hicho kwa
makini na tutakupatia orodha hiyo kwa ajili ya kuifanyia kazi.”
“ Hiyo ni hatua kubwa sana
mmeipiga Austin.kama tayari mmekipata kitabu chenye orodha hiyo kazi yetu itakuwa rahisi sana.Hakuna kati yao atakayesalimika.Wote watakutana na mkono wa sheria.Hii ni vita Austin kwa hiyo sintakuwa na mchezo na hawa jamaa hata kidogo.Nakuhakikishia nitawafyeka
wote na nchi hii itakuwa safi.” Akasema rais Ernest
“ Huo ndio hasa ujasiri unaotakiwa
kwa rais.Watu hawa wameiharibu mno nchi hii na vijana wetu.Vipi kuhusu Mukasha?.Tutahitaji pia kuufahamu mtandao wake .Mmoja wa watu walio katika mtandao wa Mukasha anaitwa dogo Bill ndiye sababu ya Job kuishikama kichaa kwa muda wa zaidi
ya miaka mitatu.Huyu dogo Bill
alimchukua mke wa Job na mwanae na mpaka leo hii hawajulikani walipo.Muda
ukiwadia tutaomba utusaidia kumpata Mukasha ili aweze kutusaidia kufahamu alipo mtoto wa Job” akasema Austin
“ Kuhusu Mukasha kama nilivyokueleza nitashughulika naye na muda utakapofika mkihitaji kumuhoji nitawasaidia kumpata” akasema rais na kunyamaza baada ya kengele ya getini kulia .Rais akamtaka Austin apumzike akafungua mlango na kumtaka mmoja
wa walinzi wake akafungue
geti.Alikuwa ni Amarachi.Akahojiwa na kujieleza akaingiza gari ndani .Austin akatoka kwenda kuwalaki.Amarachi ndiye aliyekuwa wa kwanza kushuka akafuatiwa na Monica
“ Hallo handsome Zombie!! Akatania Monica huku akicheka .Austin naye akacheka na Monica akamfuata
“ Karibu sana Monica.Hapa ndipo
ninapoishi”akasema Austin
“ Ahsante sana Austin.Vipi maendeleo yako”
“ Naendelea vizuri kama unavyoniona”
“ Austin take me inside .I’m scared of how these soldiers are looking at me” Monica akamnong’oneza Austin ambaye
alitabasamu wakaelekea sebuleni
“ Hawa wanajeshi wote unaowaona hapa ni walinzi wa rais.Tayari amekwisha fika” Austin
akamwambia Monica na kuwakaribisha sebuleni yeye na Amarachi
“ Hello ladies.Welcome” akasema
rais akiwa katika tabasamu
.Monica na Amarachi wakamsalimu kwa adabu.Amarachi akawaacha na
kwenda kusimamia maandalizi ya
chakula
“ karibu sana Monica .Nimefurahi kuonana nawe tena” akasema rais
“ Hata mimi nimefurahi sana mheshimiwa rais kupata fursa hii ya kuonana nawe” akajibu Monica kwa sauti yenye woga ndani yake
Waliendelea na maongezi mbali mbali hadi pale Amarachi alipowataarifu kuwa chakula kiko tayari.Wote wakaenda kujumuika mezani .Baada ya kula wahudumu
wakafanya usafi na kuondoka .Ndani ya nyumba wakabaki rais,Austin ,Amarachi na Monica
“Monica uluomba nafasi ya kuonana na rais .Uwanja ni wako sasa unaweza ukamueleza rais shida yako” akasema Austin huku akiinuka
“ Ahsnate sana Austin.Mungu
akubariki ” akajibu Monica na Austin akatoka pale sebuleni akaelekea katika chumba kingine na kuwaacha Monica na rais peke yao
“ karibu Monica .Austin alinieleza kuhusu ombi lako la kutaka kuonana nami na kwa kuwa alinisisitiza sana ikanilazimu kusitisha baadhi ya
shughuli zangu nyingine na kuja kukusikiliza.Kuwa huru kunieleza chochote unachotaka kunieleza” akasema rais
“ Ahsante sana mheshimwia rais
kwa kunipa heshima hii kubwa na sipati neno zuri la kukushukuru toka ndani ya moyo wangu nasema ahsante sana” akasema Monica
Ernest akatabasamu .Monica akaendelea
“ Mheshimiwa rais nina shinda
ambayo nataka unisadie kwani iko ndani ya uwezo wako.Ninaye rafiki yangu anaitwa Marcelo ambaye alipigwa risasi na watu wasiojulikana lakini kwa maajabu ya Mungu alipona na anaendelea vizuri.Akiwa hospitali aligundua kwamba kuna watu bado wanaendelea kumfuatilia wamuue na
akaniomba msaada wa kumtorosha pale hospitali bila ya mtu yeyote kufahamu.Sikujua ningemsaidia vipi
.Wakati nikitafuta namna ya kumsaidia nilipata safari ya ghafla ya kwenda Congo na nikiwa huko nikalazimka kumuomba msaada rais wa Congo
David Zumo ambaye alikupigia simu akakuomba umsaidie Marcelo.Nashukuru ulimsikia na kumsaidia Marcelo.Baada ya kurejea toka Congo nilihitaji sana kuonana na
Marcelo lakini kila nikimuomba David
awasiliane nawe akuulize mahala alipo Marcelo nimekuwa Napata majibu ya kusubiri.Leo asubuhi nilipofahamu
kuwa una ukaribu na Austin na vile vile wazazi wangu nilifurahi na ndiyo maana nikamuomba Austin anikutanishe nawe
ili niweze kukuomba mimi mwenyewe
unionyeshe mahali alipo Marcelo nikamtazame.Ni mtu wangu wa
muhimu sana” akasema Monica.Ernest akatabasamu na kusema
“ Nilijiuliza maswali mengi David aliponipigia simu kuniomba nimsaidie kumtoa Marcelo hospitali.Sikujua kama lilikuwa ni ombi lako”akasema Ernest huku akitabasamu
“ Ni mimi ndiye niliyemuomba anisaidie” akasema Monica.
“ Samahani kwa Swali hili Monica
wewe na David Zumo mmefahamiana vipi?
“ Mimi na David Zumo ni wachumba na tuko katika maandalizi
ya kufunga ndoa.”akajibu Monica huku akitabasamu.Jibu lile la Monica lilimstua sana Ernest lakini akajitahidi
kutabasamu
“ Hongera sana .Kumbe maandalizi yamekwisha anza.Mbona mimi sijapewa taarifa wakati ni mtu wa karibu na
familia yenu? Nitazungumza na wazazi wako wanieleze kwa nini wananitenga katika jambo kubwa kama hili ”
akasema Ernest huku akitabasamu
“ Bado tuko katika taratibu za awali za uchumba na utakapofika
wakati wa kujulishwa nyote mtafahamu
“ akasema Monica
“ Naweza kusema una bahati sana
Monica kwa kumpata Dav………….” Kabla hajamaliza sentensi yake
Amarachi akaingia akiwa na sinia lenye
glasi mbili za mvinyo .Akampatia moja
Amarachi na nyingine akampa rais.
“ Karibuni vinywaji”akasema huku akitabasamu na kutoka
“ Monica naomba tugonganishe glasi na tunywe kwa ajili ya kukutakia maisha mema na mafanikio katika mambo yako yote.” Akasema Ernest wakagonganisha glasi na kila mmoja akanywa funda kubwa
“ Monica nimelipokea ombi lako na nitakusaidia .Dr Marcelo amehifadhiwa sehemu salama.Utapelekwa kwenda kuonana naye na endapo kuna chochote ambacho ungependa nikusaidie usisite kunitaarifu.” Akasema Ernest
“ Ahs…..aahsante… ….ahsante sana
mheshimiwa rais” akajibu Monica ambaye tayari alianza kulemewa na usingizi mzito baada tu ya kunywa mvinyo ule
Baada ya dakika mbili akalala usingizi pale sofani.Amarachi na Austin wakaingia pale sebuleni wakiwa wamejianda tayari kabisa kwa zoezi la kuchukua sampuli
“ Mheshimiwa rais kila kitu kiko tayari sasa tunaweza kufanya zoezi letu
la kuchukua sampuli mbele yako”
akasema Austin
“ Austin una hakika hamjazidisha dawa za usingizi mlizomuwekea Monica
? Nimeshangaa muda umekuwa mfupi sana toka alipokunywa kinywaji na kupata usingizi wa ghafla”
“ Usihofu mheshimiwa rais kila
kitu kinakwenda sawa na hakuna tatizo.Baada ya kumaliza zoezi letu
tutamzindua” akasema Austin.Amarachi akaanza zoezi la kuchukua sampuli walizozihitaji
Walifanikiwa kuchukua sampuli kadhaa toka kwa Monica halafu wakachukua pia sampuli kama hizo toka kwa rais Ernest na zoezi likakamilika.Monica akachomwa sindano ya kumzindua
“ Mheshimiwa rais ahsante sana kwa ushirikiano wako katika zoezi hili
.Kinachofuata sasa ni kupeleka sampuli hizi maabara kwa ajili ya vipimo .Kama nilivyokufahamisha awali kwamba vipimo vitafanyika hapa hapa dar es salaam.kesho au kesho kutwa tutapata majibu” akasema Austin wakati wakimsubiri Monica azinduke
“ nashukuru sana Austin kwa
nnamna ulivyojitoa kuhakikisha jambo hili linafanikiwa.Licha ya misuko suko
yote lakini bado umesimama imara kuhakikisha hakuna kinachoharibika na kila kitu kinakwenda kama tulivyopanga.By the way kuna jambo ambalo sikuwa nimekujulisha bado” akasema rais akanyamaza na
kumtazama Austin kisha akaendelea
“Mdogo wako Linda kesho anaondoka kuelekea Canada.Tayari
kuna nyumba imepatikana kule kubwa na nzuri ,ataishi humo na atafunguliwa duka kubwa la kuuza bidhaa za kiutamaduni kutoka Afrika.Tayari
maelekezo yote nimekwisha mpa balozi wetu Canada ambaye ndiye atakayempokea na kuhakikisha kila kitu kinakwenda vizuri.Sikutaka kukueleza kuhusu suala hili sasa hivi lakini kwa namna unavyojituma katika kufanikisha kazi zangu nimeona nikueleze ili ufahamu kuwa hata mimi ninakujali pia
na ninayaheshimu makubaliano yetu.Kwa hiyo Austin kaa ukifanya kazi zako kwa amani ukifahamu kuwa
mdogo wako yuko katika mikono salama” akasema rais na tabasamu
kubwa likajengeka katika sura ya Austin
“ Ahsante mheshimiwa rais kwa hili ulilolifanya” akasema na wote wakageuka baada ya kusikia mguno toka kwa Monica aliyezinduka.Rais akamfuata
“ Monica ..Monica..” akaita rais Monica akajaribu kufumbua macho lakini yalikuwa mazito sana
“ Bado anahitaji muda kidogo wa
kupumzika” akasema Austin
“ Austin mimi nitamuacha Monica mikononi mwako hakikisha anafika nyumbani kwake salama.kama kuna lolote litatokea unijulishe mara moja”
akasema rais Ernest na kuagana na
Austin akaondoka
“ Good Job Amarachi.Wewe ni mtu mwenye vipaji vingi sana.Umenishanganza kwa namna ulivyoweza kuchukua zile sampuli toka kwa Monica kama wafanyavyo madaktari” akasema Austin na
Amarachi akatabasamu .Austin akaelekea sebuleni ambako tayari Monica alikwisha zinduka usingizini
“ Monica” akaita Austin
“ Austin sijui nini kimenitokea lakini nimejikuta nikipata usingizi wa ghafla sana baada ya kunywa kile kinywaji alichotuletea Amarachi.” Akasema Monica kwa uchovu
“ Pole sana Monica.Mvinyo ule aliowaletea Amarachi ni moja kati ya mvinyo mkali mno na anapenda
kutumia rais.Amarachi alikosea kukupa mvinyo bila kukuuliza
kwanza.Unajisikaje?
“ Nahisi mwili mzito na kila kiungo kinauma.Kuna chumba cha wageni hapa kwako nipumzike? Akauliza Monica
“ sawa Monica ngoja Amarachi akuandalie chumba ukapumzike” akasema Austin na kutoka akamuelekeza Amarachi akaandae chumba kwa ajili ya Monica.Chumba kilipokuwa tayari Monica akaenda kupumzika.
“ Sampuli zote zimekamiliika kwa hiyo kinachofuata ni kuziwasilisha maabara.Mimi nitabaki hapa na Monica kwani kwa hali hii hataweza kurejea nyumbani kwake.Wewe peleka sampuli hizi maabara na ukitoka huko uende nyumbani ukapumzike tutaonana asubuhi.” Akasema Austin
“ Hapana Austin siwezi kwenda
kupumzika nyumbani kwangu nikakuacha peke yako.Nikitoka
maabara nitarejea hapa.Unahitaji kuwa
na mtu karibu kwa hiyo nitarejea hapa na kama ni kupumzika nitapumzika hapa” akasema Amarachi wakaagana akaondoka kuelekea katika hospitali aliyokuwa ameipendekeza .
“ Imekuwa ni siku nzuri yenye mafanikio makubwa.Kila kitu tulichokipanga leo kimekwenda vyema.Ni wakati wa kupumzika sasa” akawaza Austin na kuelekea chumbani kujipumzisha.
********************