Queen Sendiga, pendeza basi mama, tunaokutazama tufurahi!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga ni mwanamke yuko kitofauti kidogo.
Siwezi kusema ni mwanamke ambaye hajipendi lakini haiba yake hadharani inabidi iboreke.
Kama mwanamke lazima apendeze, avutie, na hiyo ndio raha ya kumtazama hata kwenye runinga.

Mama Samia tukimtazama kwenye runinga, anavutia, ni mwanamke anapendeza.

Sasa Queen,suka yako ya mabutu au twende kilioni, heri hata ungevaa kilemba, haipendezi ulivyo.
Hata leo sherehe kuuubwa mkoani Manyara, mabutu!
Aaah!

Tupe raha Queen, pendeza kidogo.

UPDATE
Personally nimejifunza mengi kutokana na uzi huu.
Nawapongeza wachangiaji hata wale walionipinga kwa sababu za kimsingi kabisa.
However, kuna suala linajitokeza, DRESS CODE ya Public officials nchini ikoje?
Mwenye hiyo DRESS CODE atubandikie tafadhali.
 
Mke wa mtu apendeze umtazame hili ufanye nini?
 
Mtoto wa Majengo Mbeya. Mpwa wa Nyirenda aliyepandisha bendera Kilimanjaro
 
Hiyo style yake ndo wengine anatuvutia kumuangalia...nilipanda nae flight Dar Dom mwezi March alikaa siti ya mbele yangu nilitamani nimsemeshe nilikua naangalia kichwa chake hadi tunafika. Kama unataka kuona wenye mawigi na misuko kila aina kasimame Makumbusho stendi pale utachoka mwenyewe
 
Hapo mbona yeye anajiona katoka ile mbaya. Au Wewe unataka apendezeje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…