Quick Reminder: Ewe Shabiki wa Simba na Yanga punguza matarajio

Quick Reminder: Ewe Shabiki wa Simba na Yanga punguza matarajio

Kuna watu eti baada ya Vipers kufungwa 5 na Raja casablanca jana basi eti wameshajihesabia wana points zao sita toka kwa vipers. Lol.
Hiki ni moja ya kichekesho katika Soka. Naona mnyama amesahau wakati anakula tano away, Nyumbani alikua anafanya nini. Vipers atatoa mechi moja ngumu sana kwa Mnyama.
 
Kwani wao wamesahau walivyokuwa wanapiga hamsa jamaa?

Kilichowakuta Vipers ni karibu Mgeni, Sasa wamekaribishwa rasmi ligi ya makundi, na ile timu ni ukanda mwingine, lakini mechi yao na Simba ni ya kawaida sana kwao kwani ni ukanda mmoja timu zote mbili kila timu INA uwezo wa kupata matokeo iwe Kampala au Dar es salaam.
Nakubaliana na wewe kabisa. Naamini Vipers wana-mindset ya kuamini wanamuweza simba, wanapaweza kwa Mkapa. Ogopa sana timu ya namna hiyo. Hii confidence effect yake ni kufa nyingi au kushinda.
 
kwahio imani yako uto yupo njia salama kama mleta uzi alivotahadhalisha kwamba vinyesi mnajiamini sana na kwamba hakuna mtu wa kuwazuia kwenye kundi lenu? Na unaamini makolo hawana kabisa kikosi cha kupambana na kuvuka kundi lao kisa hawakusajili vizuri si ndio uto? Ila kumbuka mbumbumbuni kumeongezeka
Chama
Phili
Ntibanzokinza
Baleke na wengine wazuri ambao hawakuwepo last czon, na unakumbuka wazi simba ile ya kina sako na kibu denga ilivowatoa kamasi bingwa mtetezi berkane na orlando pirates kwa kikosi kile tu, je uto huoni kama ngada fc wana advantage kuliko hata wewe? Ukiangalia hata bettings wamewapa makolo odds zinazokaribiana na za timu mwenyeji leo hii! Ila uto sioni hili, by the way tupunguze matarajio sana.

Hizi forum zetu kupata mtu mpya ni kazi sana.

Hebu fikiria hapa mtu kutoka malawi huko amejua kiswahili hapa ataelewa nini?

Ataona tunaongolea vitu ambavyo hawezi kupata rejea.

Sio TZ tuna dunia yetu hakika.
 
Unashushaje matarajio kwa timu kama yanga labda uwe umerogwa

nyau sio ya kushusha matarajio, hutakiwi kuwa na matarajio kabisa

timu kama kombaini ya timu za shule kucheza umitashumita/umiseta
 
Msimu wa Nabi atuachie timu yetu umefika
 
Wakati Yanga inafanya usajili nyinyi mlikuwa mnazurura tu na kupiga Picha na Manzoki, Sasa kila mtu atavuna alichopanda.
Wewe Ni mgumu Sana kuelewa somo..umepewa shule ya bure kwamba punguza mihemuko..
Nakuona ukilia muda mfupi ujao..
 
Unashushaje matarajio kwa timu kama yanga labda uwe umerogwa

nyau sio ya kushusha matarajio, hutakiwi kuwa na matarajio kabisa

timu kama kombaini ya timu za shule kucheza umitashumita/umiseta
Katika total football, ubora wa Yanga upo kwenye formation yeyote ya ku-defence. Ni ngumu sana kuona Yanga hii ya Nabi inafungwa goli nyingi. Je, uta-score?

Shida yangu, Uta-score mwananchii?

Mnayama falsafa yake ni kushambulia. Ila akikutana na timu ambayo wanatumia mipira ya juu saana na wapo aggressive. Mnyama hana jipya.
Siwalaumu, ila ni nature ya wachezaji waliopo. Mpinzani tumia wings kushambulia(Huwa tunaona madhaifu ya kina Tshabalala), Wakimbize, Piga cross ya juu. Utakuta Manula haya yeye haelewi kilichotokea.

Ila ukisema utembeze boli chini. Mnyama ataku-outshine, Mnyama atakutesa sana.
 
Katika total football, ubora wa Yanga upo kwenye formation yeyote ya ku-defence. Ni ngumu sana kuona Yanga hii ya Nabi inafungwa goli nyingi. Je, uta-score?

Shida yangu, Uta-score mwananchii?

Mnayama falsafa yake ni kushambulia. Ila akikutana na timu ambayo wanatumia mipira ya juu saana na wapo aggressive. Mnyama hana jipya.
Siwalaumu, ila ni nature ya wachezaji waliopo. Mpinzani tumia wings kushambulia(Huwa tunaona madhaifu ya kina Tshabalala), Wakimbize, Piga cross ya juu. Utakuta Manula haya yeye haelewi kilichotokea.

Ila ukisema utembeze boli chini. Mnyama ataku-outshine, Mnyama atakutesa sana.
sema yooote ila nyau hakuna timu pale ukicheza mpira wa nguvu tu wanapotea wote
 
Hizi forum zetu kupata mtu mpya ni kazi sana.

Hebu fikiria hapa mtu kutoka malawi huko amejua kiswahili hapa ataelewa nini?

Ataona tunaongolea vitu ambavyo hawezi kupata rejea.

Sio TZ tuna dunia yetu hakika.
Napenda sana JF, Ni either ujifunze kwanza communication skills ndiyo ujinge, au jiunge JF ili ujifunze Communication Skills. Ila kwa namna yeyote ukiwa member humu, Utajifunza tu. Utake, Usitake.
 
Kuna mtu anaenda kupigwa kama dufu Tunisia niko pale nimekaa muda utasema.
Tukutane:

Stade Mustapha Ben Jannet​

 
Msimu wa Nabi atuachie timu yetu umefika
Bila kuathiri mafanikio ya Nabi, ila Nabi anafikirisha sana. Mechi ikiwa tough tu, huwa anachanganyikiwa. Ni ngumu sana kuja na mbinu mbadala kama tayari umechanganyikiwa.

Evidence: Angalia mechi ya Ihefu, sijui alitaka kufanya nini kwa Nkane.

Mechi moja ya kimataifa, alitaka kufanyiwa Sub yeye aingie mchezoni.
Napenda sana makocha hata kama ana-midadi kama Arteta, Guardiola, Robertinho ila tu ubongo wake uwe umetulia hasa wakati wa mechi zenye pressure.
 
Yanga ana ugeni wa kuwasha moto tu uwanjani kuliko ninyi Kolowizards [emoji2]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Napenda sana na Naogopa sana Yanga linapokuja suala la majadiliano au ubishani wa mpira hapa nchini.

Mashabiki wengi wa Yanga wanakitu kinaitwa "Know it all, Judgemental, Justification Ego".

-Wao katika mpira wanajua kila kitu.
-Wao hao hao wana mazuri ya kila baya, wao wana-mabaya katika kila zuri. Itategemea limefanyika upande gani.
-Wao wanasababu ya kufanya jambo fulani au kutofanya jambo fulani. Bahati mbaya sababu nyingi huwa si za kweli.

Napenda kuangalia mpira pale Board Room or B-Max pale sinza, katika nyakati tofauti nimeishuhudia Yanga ikiwa inashindwa ku-score goli zaidi ya moja, basi mashabiki hushangilia na kusema sisi hatutaki goli zaidi ya moja. You see, hapo wameshindwa ku-score ila wao wanasema tunataka moja moja. Yaani kufunga goli moja tu imekua ni sifa njema kwao. Inachekesha.

Mashabiki wa Yanga wanaipenda sana timu yao.
 
Ukiizoea kuishi kwa kukariri maisha lazima uferi pakubwa, kila siku sio jumapili wala jumamosi, Na kujifunza kutokana na makosa ndio chanzo cha mafanikio yako kwa maana iyo hawa Yanga wanaobezwa kwa mwendo wanaokwenda nao kimataifa kwa sasa ni wazi kuna kitu wanakitafuta na watawashangaza wengi, Mipango yao na dhamira yao inaonyesha wanataka kufyeka kile kichaka cha kuwabeza kuwa kimataifa awawezi, Na naona watakifyeka muda sio mrefu ni suala la muda tu
 
Hii ndiyo ile miezi ya manung'uniko pale msimbazi(Hawa jamaa hawana kelele sana kama wananchi). Naamini utakubaliana na mie, Simba linapokuja suala la kimataifa mentality yao ni kama Real Madrid, yaani ligi ya ndani anaweza kuwa wa kawaida ila kimataifa wana-spirit moja ya ajabu sana. Timu nyingi zina mengi ya kujifunza kutoka kwa Simba. Simba ikija kupata wachezaji bora, Nawaona fainali kabisa.
Nakubaliana na wewe umeandika bila kupelekeshwa na mihemko ya kishabiki lakini naomba nikupinge kidogo katika hii aya

Ni kweli miaka ya karibuni simba imekua na rekodi nzuri kimataifa ukilinganisha na timu zingine hapa nchini lakini bado haijafika hatua ya kusema they belong to that competition kumbuka simba imefanya ivyo kwa miaka takribani minne tu kwaiyo haijafika level za kusema nae ni kigogo uko umweke kwenye mzani mmoja na wakina al ahly, sundowns n.k ambao miaka nenda rudi wanasumbua uko hata ulaya kuna timu ambazo zinaibuka na kupotea mfano monaco, dortmund, porto n.k hawa huwezi kuwaweka kwenye mzani mmoja na real madrid, bayern munich n.k ambao wanapambania kombe miaka nenda rudi na pia tusisahau miaka sita au mitano nyuma simba alikua na kikosi bora sana huwezi kufananisha na hawa wakina kibu dennis pamoja na spirit na mentality ya timu pia kikosi bora kinachangia sana kupata matokeo chanya pia ukiangalia tangu simba anaondolewa na orlando pirates ubora na chati yake hapa nyumbani na kimataifa imekua ikishuka kutokana na kuuza wachezaji wazuri, kushuka viwango na umri kwenda kwa wachezaji waliopo na usajiri mbovu. Binafsi sitashangaa kama simba ikishika mkia kwenye kundi lake
 
Back
Top Bottom