Uislamu ni dini ambayo Allaah ameichagua kama mfumo sahihi wa maisha kwa Wanadamu wote na tokea Nabii wa kwanza Baba yetu Aadam (Peace be upon Him ) alikuwa Muislamu na Manabii wote Musa , Yesu , Nuhu , Ibrahimu , Yakubu nk (Amani iwe juu yao wote ) dini yao ilikuwa ni Uislamu na walilingania katika Uislamu .
Sheria tu zilitofautiana kutoka na zama lakini misingi mikuu ile ile ambapo msingi mkuu unawaunganisha wote kuwafanya wawe Waislamu ni Tawheed maana yake kumpwekesha Mola muumba pekee kwa kumuabudia yeye tu bila kumshirikisha . Ndio maana hakuna Nabii akiyekuja kudai kuwa yeye ni Mungu au kiabudiwe kingine kinyume na Mungu muumba (Allaah)
Manabii wote walikuja kukingania watu waachane na maovu , wafanye mema kwa kumtii mola wao huo ndio Uislamu . Uislamu maana yake ni kujisalimisha kwa Allaah mola muumba kwa kumuabudu yeye pekee bila kumshirikisha kufuata maarisho yake na kuacha makatazo kama jinsi alivyoolekeza kupitia Manabii na wajumbe wake.
Ndio maana tunasema Uislamu ukikuwepo tokea mwanzo na Manabii wote walikuwa Waislamu sababu walikuwa kwenye misingi hiyo , tofauti ipo kwenye baadhi ya Sheria tu sawa na Leo I phone zote ni I phone zina sifa za kipekee kuitwa I phone pamoja na kuwa na matoleo tofauti kutokana na maboresho ila sifa za kipee zinazofanya kuwa I phone lazima zitabaki kama msingi